Saturday, July 11, 2020

JPM AMWAGA KIWANDA KIKUBWA CHA KUKU NA KLINIKI YA KISASA YA MIFUGO SINGIDA



Waziri wa Mifugo na Uvuvi (mwenye kofia nyeusi) Luhaga Mpina akishiriki katika zoezi la uchanjaji wa mifugo kitaifa pamoja na wataalam wa mifugo lililofanyika leo kwenye kijiji cha Kinyangiri wilayani Mkalama mkoani Singida ambapo Serikali imeahidi kuwezesha kujenga kiwanda kikubwa cha machinjio ya kisasa kitakacholisha Tanzania na nchi mbalimbali duniani.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi (mwenye kofia nyeusi) Luhaga Mpina wa kwanza kulia akifuatiwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Injinia Jackson Masaka na Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida ndugu Beatus Choaji wakiwa kwenye sherehe za uzinduzi wa uchanjaji wa mifugo kitaifa pamoja na wataalam wa mifugo lililofanyika leo kwenye kijiji cha Kinyangiri wilayani Mkalama mkoani Singida.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi (mwenye kofia nyeusi) Luhaga akionyeshwa kifaa maalum cha kuchanjia mifugo wakati wa zoezi la uchanjaji wa mifugo kitaifa pamoja na wataalam wa mifugo lililofanyika leo kwenye kijiji cha Kinyangiri wilayani Mkalama mkoani Singida.

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi (mwenye kofia nyeusi) Luhaga akihutubia umati wa wadau wa mifugo wakati wa zoezi la uchanjaji wa mifugo kitaifa pamoja na wataalam wa mifugo lililofanyika leo kwenye kijiji cha Kinyangiri wilayani Mkalama mkoani Singida.
Umati wa wadau wa mifugo wakati wa zoezi la uchanjaji wa mifugo kitaifa pamoja na wataalam wa mifugo lililofanyika leo kwenye kijiji cha Kinyangiri wilayani Mkalama mkoani Singida.



Na John Mapepele, Singida

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amesema Serikali inakusudia kuwezesha kujenga kiwanda kikubwa cha kisasa cha kuchaka nyama ya kuku kwenye Mkoa wa Singida kitakacholisha Tanzania na nchi mbalimbali duniani ambacho kitakuwa kinafanya uzalishaji ifikapo Desemba mwaka huu ili kuinua hali za wafugaji wa kuku wa Singida na kuongeza pato la taifa.

Mbali na kiwanda hicho, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inatarajia kujenga Kliniki bora ya kisasa ya mifugo kwenye Halmashauri ya Mkalama.

Kliniki hiyo ni miongoni mwa Kliniki 30 ambazo zinazijengwa nchi nzima na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwenye Halmashauri mbalimbali.

Waziri Mpina ameyasema haya kwenye hotuba yake ya uzinduzi wa Kampeni ya Chanjo za Mifugo Kitaifa kwenye kijiji cha Kinyangiri katika Wilaya ya Makalama mkoani Singida ambayo imelenga kutokomeza magonjwa mbalimbali ya mifugo (hususan magonjwa 13 ya kipaombele) ambayo yamekuwa kikwazo katika uzalishaji na biashara ya mifugo ndani na nje ya Tanzania.

“Tumeona hapa uzalishaji mkubwa sana wa kuku Singida, sasa ninaagiza mambo makubwa mawili Bodi ya Nyama na Dawati la linaloshughulikia Sekta Binafsi katika Wizara yangu kuwezesha kujenga kiwanda cha kuchakata nyama ya kuku na tutakizindua kikiwa kinatoa huduma ifikapo Desemba mwaka huu"Alisema

"Lakini la pili ninamuagiza Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko na Dawati la Sekta Binafsi kuunda vikundi na kuwaletea vitotoleshi vya kisasa ili kuongeza kasi ya uzalishaji wa kuku ili kuwezesha upatikanaji wa malighafi za kiwanda kwa uhakika” alisisitiza Waziri Mpina.

Mpina amesema magonjwa mengi ya mifugo ni yale ya kuambikiza hususani yanayotokea kwa mlipuko na kusabisha vifo na hasara kubwa kwa wafugaji na kufafanua kuwa hadi sasa tayari, Serikali imekiimarisha kiwanda cha chanjo cha Tanzania Vaccine Institute (TVI) na kinazalisha aina sita (6) ya chanjo za kipaumbele na kitaanza kuzalisha aina nyingine tatu kufikia mwezi Desemba, 2020.

Mbali na Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuanza kutengeneza chanjo sita Mpina amesema mapinduzi na mageuzi makubwa yamefanyika ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Mifugo inatoa mchango mkubwa katika uchumi wa nchi na kwa mwananchi mmoja mmoja tofauti na awali ambapo sekta hiyo na wafugaji walidharaulika sana.

Ametaja baadhi ya mambo yaliyoboreshwa kwenye eneo la chanjo hapa nchini kuwa ni pamoja na Wizara yake kupitisha Mpango wa Ununuzi wa Chanjo za Mifugo kwa Pamoja (Vaccine Bulk Procurement Plan);

Serikali kutangaza Bei Elekezi ya chanjo aina 13 za magonjwa ya kipaumbele ambapo chanjo zimepungua bei kwa zaidi ya asilimia 60;

Amebainisha kuwa, Katika mwaka 2019/2020, Serikali katika kiwanda cha TVI imezalisha jumla ya dozi 53,851,850 za chanjo za magonjwa ya mlipuko na yanayovuka mipaka na chanjo hizi zote zimechanja mifugo.

Pia, Wizara imevutia wawekezaji na kiwanda kikubwa cha Hester Biosciences Africa Limited kinajengwa na kitakapokamilika kitakuwa kinazalisha aina 37 ya chanjo za wanyama.

Ameongeza kuwa katika mwaka 2019/2020, utoaji wa chanjo umeimarika ambapo Halmashauri 103 kati ya 185 sawa na asilimia 56 zimeshiriki kikamilifu katika kutoa chanjo kwa mifugo

Aidha Mpina amesema kutokana na mikakati ya Wizara yake ya kudhibiti utoroshaji wa mifugo kutoka nchni kwenda nchi za nje na udhibiti wa uingizaji holela wa bidhaa za mifugo nchini kupitia “Operesheni Nzagamba” Serikali ya awamu wa Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliweza kukusanya zaidi ya bilioni 50 kwa mwaka ukilinganisha na Shilingi bilioni 9.5 zilizokuwa zikikusanywa katika kipindi cha nyuma kwa mwaka.

Akitoa maelekezo kwa wataalam Waziri Mpina amewataka wataalmu wote wa mifugo ngazi ya Wizara, Mikoa, Wilaya na Kata kuhakikisha uchanjaji wa mifugo unatekelezwa kikamilifu kulingana na kalenda ya chanjo kwa kuwa ni suala la kisheria ambapo amemtaka Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo (DVS) kuhakikisha unasimamia jukumu hili na yeye kupatiwa ripoti ya chanjo hizo kila mwezi.

Pia amewataka Wataalamu wote wa mifugo kuhakikisha wanatoa elimu ya chanjo kwa wafugaji ili watambue umuhimu na faida za kuchanja mifugo yao na kwamba, Serikali imeshaandaa mazingira wezeshi ya upatikanaji wa chanjo kila mahali na kwa bei elekezi.

Amesema kulingana na Kalenda ya chanjo kitaifa, mwezi Juni mpaka Augosti, 2020 ni msimu wa chanjo za Homa ya Mapafu ya Ng'ombe, Homa ya Mapafu ya Mbuzi, Sotoka ya Mbuzi na Kondoo, Ugonjwa wa kutupa mimba na Ugonjwa wa Miguu na Midomo.

Hivyo, ametoa wito kwa madaktari wa mifugo wote nchini kuhakikisha kwamba chanjo hizi zinatolewa kikamilifu.

Aidha ameziagiza Halmashauri zote ambazo hazitowi huduma ya chanjo kwa mifugo yao kufanya hivyo mara moja kuanzia mwezi huu wa Julai, 2020.

Ripoti ya idadi ya mifugo na aina ya chanjo inayotolewa iwe inaletwa kwa Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo (DVS) kila wiki

Thursday, July 2, 2020

SPORTPESA YAIPA SIMBA SC SH MILIONI 100 KWA KUTWAA TAJI LA LIGI KUU TANZANIA BARA

Wadhamini wakuu wa klabu ya Simba SC, Sport Pesa Tanzania wakiwakabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni 100, Nahodha wa klabu hiyo, John Raphael Bocco baada ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululzo. Fedha hizo zimetolewa kama sehemu ya makubaliano ya mkataba wa udhamini uliosainiwa mwaka 

DC WA SINGIDA AJA NA OPERESHENI TOKOMEZA CORONA


Mkuu wa Wilaya ya Singida MhandisiPaskasi Muragili akiwa ndani ya basi la Kampuni ya Kiazi Kitamu akiwaelezaabiria mbinu za kujikinga na Virusi vya Corona (COVID-19) alipokuwa kwenye Operesheni maalum ya Tokomeza Corona Katika Manispaa ya Singida kwenye Kituo Kikuu cha mabasi. (Picha na. Peter Kashindye).
  Madereva na Mawakala wa mabasi kwenye
Kituo Kikuu cha mabasi ya Mkoa wa Singida (Misuna) wakionyesha jinsi ya kutumia
vitakasa mikono ili kukabiliana na ugonjwa wa Corona (COVID-19) kwa Mkuu wa Wilaya
ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili (Hayupo pichani) alipofanya Operesheni Maalum
ya Tokomeza Corona Katika Manispaa ya Singida kuona utekelezaji wa maagizo ya
Serikali ya kujikinga na ugonjwa huo (Picha na. Peter Kashindye).

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi PaskasiMuragili (aliyenyanyua mkono) akihoji uelewa wa kujikinga na virusi vya Corona (Covid-19) mahali pa kazi kwenye maduka ya kuuzia nyama alipofanya Operesheni Maalum ya Tokomeza Corona Katika Manispaa ya Singida kwenye Soko Kuu la Singida Mjini. (Picha na. Peter Kashindye).

DKT. NCHIMBI AMPA TANO RAIS KWA KUIINGIZA TZ KATIKA UCHUMI WA KATI


 Mkuu wa MKoa wa Singida Dkt. Rehema
Nchimbi akifunga  mafunzo maalum ya  siku sita kwa wadau zaidi ya 300 kutoka katika mikoa mbalimbali nchini  yaliyokuwa yameandaliwa na Baraza la Taifa  la watu wanaoishi na  virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kupitia “Mradi wa Hebu Tuyajenge” unaotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano 2019-2024, unaofadhiliwa na  Shirika la Marekani  la  Maendeleo ya Kimataifa (USAID) katika mikoa 22 Tanzania Bara. kushoto Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa, Kulia Mkurugenzi wa Utatifi wa NACOPHA  Pantaleo Shoki

>Awataka wenye virusi kufanya kazi bila hofu
                                       >Awaonya wanaomchokoza,asisitiza hatatia nia


Na John Mapepele
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amempongeza Rais Magufuli kwa kuvunja rekodi ya  maendeleo kabla ya mwaka 2025 na kuifanya Tanzania kuingia kwenye nchi za uchumi wa kati duniani Julai Mosi mwaka huu.  
Huku akiwahimiza watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI nchini  kufanya kazi kwa  bidii bila kuwa na hofu sambamba na kumtanguliza Mungu na kutumia fursa za mikopo inayotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano ili  ku kuinua hali za maisha na kuongeza pato la taifa kwa ujumla

Dkt. Nchimbi ameyasema hayo leo katika Mji Mdogo wa Manyoni mkoani  Singida alipokuwa akifunga  mafunzo maalum ya  siku sita kwa wadau zaidi ya mia 3 kutoka katika mikoa mbalimbali nchini  yaliyokuwa yameandaliwa na Baraza la Taifa  la watu wanaoishi na  virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kupitia “Mradi wa Hebu Tuyajenge”.
Mradi huo unaotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano 2019-2024,unaofadhiliwa  na  Shirika la Marekani  la  Maendeleo ya Kimataifa (USAID) katika mikoa 22 Tanzania Bara.

Amesema kwa sasa Serikali ya Awamu ya Tano imepiga hatua kubwa ya kupiga vita unyanyapaa dhidi ya watu wanaishi na virusi vya UKIMWI na kwamba watu wote wana haki na fursa sawa  mbele ya Serikali yao hivyo hakuna sababu ya  wao kuendelea kujinyanyapaa  wenyewe  na badala yake wawe walimu wa kuwaelimisha wengine kwenda kupima na kutambua hali zao  na kuendelea kuchapa kazi ili kuinua uchumi wan chi yetu.

“Kubwa ndugu zangu hapa ni  kumtanguliza  Mungu mbele, kutoa hofu na  kuachana  na mambo yote ambayo yanapelekea  kudhoofu kwa afya zetu kama vile unywaji wa pombe  hata kama wake zetu wanapika  kwa ajili ya biashara na badala yake tutumie juisi lishe za matunda ya asili kama vile  Sasati, Ubuyu na Ukwaju” amesisitiza Dkt. Nchimbi

Umewaelekeza  Wataalam wa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Singida kuangalia namna  ya kuja na mikakati madhubuti ya kiuendelevu ya kuwakopesha wanaoishi na UKIMWI  ili kuwaletea maendeleo huku akisisitiza kuwa  Mkoa wake utaendelea kutekeleza mikakati iliyojiwekea ya kuinua maisha  ya wanainchi wake ikiwa ni pamoja na mkakati wa kuwavusha salama mama na mtoto.

Aidha ameweka msimamo wake wa kutokuonesha nia yeyote ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge katika uchaguzi wa mwaka huu huku akiwaonya watu ambao wamekuwa wakianza kudanganya kuwa atagombea ambapo alisisitiza kuwa nafasi hiyo ya ukuu wa Mkoa aliyopewa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli ni ya heshima kubwa.

“Naomba niliseme  hili, na tayari nimeshalisema mara kadhaa  hata hivi karibuni nilipokuwa nyumbani kwangu, kijijini Matufa,  Babati Manyara nilipo hudhuria mazishi ya mtoto wa Kaka yangu aliyefariki kwa ajali ya Pikipiki kwamba nilikwenda kuungana na familia yangu katika msiba wa kijana wetu na si vinginevyo. Ninaridhika sana na nafasi hii niliyo nayo ya ukuu wa Mkoa” alisema Dkt. Nchimbi huku akishangiliwa na umati wa  wadau wa mafunzo hayo

Baadhi ya waombolezaji wamesikika kupongeza msimamo wa kiongozi huyo, huku wakisema  kuwa Msimamo huo unapaswa kuigwa na viongozi wengine  kwa kuwa umejikita katika kuwaletea maendeleo wananchi badala ya kuwa na tamaa za madaraka.

“Binafsi nampongeza sana Mama Nchimbi  kwani kwa muda wote amekuwa aking’ang’ana na kuwaunganisha watu wote bila kujali dini wala rangi kwa, hata sisi leo ametutia moyo sana kiasi kwamba  baada ya kutoka hapa tumekuwa na nguvu mpya  ya kuchapa kazi na kushirikiana na Serikali yetu ya  kujiletea maendeleo Zaidi ili tutoke katika nchi za uchumi wa kati na kwenda katika nchi tajiri duniani na tuna imani kubwa chini ya Rais wetu Magufuli tutafika” amesema Amina  Huredi ambaye ni Mshiriki wa mafunzo hayo kutoka Singida

Mkurugenzi wa Utatifi wa NACOPHA  Pantaleo Shoki  amemshukuru Mkuu wa Mkoa na kumhakikishia kuwa  wataendelea kushikiana na Serikali ili kuhakikisha kuwa malengo ya Mradi huo yanatimia kama yalivyopangwa.
Shoki  amesema Mradi  unalenga kufikia Mkakati wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na UKIMWI(UNAIDS) wa 95-95-95 yaani  asilimia 95 ya watu wote wanaoishi na maambukizi ya VVU wawe wamepima na kugundua afya zao,asilimia 95 ya watu wote waliopimwa na kukutwa na maambukizi wawe wameanza tiba na asilimia 95 walio kwenye tiba wawe wamefubaza virusi hivyo ifikapo 2030