Wednesday, September 30, 2020

UN yamuunga mkono Magufuli kutokomeza ukatili wa mwanamke Ikungi

 

   Picha ya pamoja ya Mkuu wa mkoa wa Singida  Dk. Rehema Nchimbi(mwenye kilemba) na       wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo mara baada ya uzinduzi wa mradi
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Rehema Nchimbi(kulia) akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania, Zlatan Milisic baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi
 

 Na John Mapepele, Ikungi
 MKUU wa  Mkoa wa Singida Mhe, Dk. Rehema Nchimbi  leo amezindua  miongoni mwa miradi mikubwa iliyowahi kutekelezwa nchini, mradi wa  pamoja  baina ya Mashirika ya Kimataifa ya UN Women na UNFPA kupitia ufadhiri  wa  Shirika la KOICA wa Tuufikie usawa  wa jinsia kupitia kuwawezesha wanawake na wasichana utakaogharimu takribani bilioni 11.5 za kitanzania  ambao utatekelezwa  katika Wilaya ya Ikungi mkoani Singida na Msalala mkoani  Shinyanga katika kipindi cha  miaka mitatu kuanzia sasa.
 Dk. Nchimbi amesema lengo kuu la mradi huo ni kuchangia  katika kuwawezesha  wanawake na wasichana  kuwakwamua kiuchumi na kijamii katika mikoa ya Singida na Shinyanga  ili kufikia usawa wa kijinsia ambapo amewataka watendaji wote wa Serikali ambao watatekeleza mradi huo kuwa makini katika utekelezaji wa mradi ili  malengo ya mradi huo yaweze kufikiwa.

Amesisitiza kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali watendaji ambao  kwa namna moja au nyingine hawataendana na kasi ya utekelezaji wa miradi chini ya Serikali ya awamu ya Tano  inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli ambapo amesema  mrai huo  ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi  ili kuwaletea wananchi  maendeleo ya  kweli.

Kwa mujibu wa  Mkurugenzi wa  KOICA  Tanzania, Bi Jieun Mo,  walengwa wasio wa moja kwa moja takribani  wakazi 40,000 kutoka kwenye wilaya  ya Ikungi na Msalala na walengwa  wa moja  kwa moja 2350 wanawake na wasichana  kutoka katika wilaya hizo watanufaika na mradi huu ambapo pia  wanaume na wanawake 6000 wa Wilaya  ya Ikungi watanufaika kwenye eneo la muingiliano wa  hati za ardhi.

Mo ameainisha kuwa  shughuli za mradi katika kuwaweza wanawake  kwenye eneo la uchumi zitajikiza zaidi kwenye kuimarisha uwezo wa wanawake  na vijana   wakulima ili waweze kutumia  njia nzuri za kilimo na hali ya hewa katika uzalishaji wa alizeti na kilimo cha bustani, kukuza uuzaji wa pamoja, ujuzi wa ujasiriamali na wakala wa uchumi  wa wanawake  na kuimarisha  usalama wa ardhi na umiliki.

Amesisiza kuwa  shughuli hizo zitatekelezeka  kupitia kuunda  vikundi vya uzalishaji wa kilimo cha bustani kwa wanawake, kuunganisha  wanunuzi wa vikundi  vya wakulima vya wanawake,kusaidia ujenzi wa  ghala kubwa  moja la alizeti na kituo cha ukusanyaji kilomo cha bustani ili  kuboresha uuzaji wa pamoja na utunzaji baada ya kuvuna, kutoa mafunzo ya ujasiriamali, kutoa mafunzo ya ujasiriamali na ufikiaji wa habari za kifedha na kufuatilia ushauri wa usimamizi wa biashara na  fedha na kukuza  umiliki wa ardhi pekee na wa pamoja  wa wanawake kupitia utoaji wa  Hati za Haki za kimila za Makaazi(CCROs).

Mwakilishi wa UN Women  Bi, Hodan Addou ameishukuru Serikali  ya  Tanzania  kuwa ushirikiano wake katika kuhakikisha  kuwa mradi huu  hatimaye umeanza kutekelezwa ambapo amesema Shirika lake  linaunga mkono juhudi za Serikali za kumkomboa mwanamke ili kuondokana na  unyanyasaji wa kijinsia.

Bi Addou amesisitiza kuwa mradi utasaidia uwezeshaji kijamii kwa kuwawezesha  wanawake kusimamia haki zao, kujenga ujuzi wa ujasiiamali wa wanawake na wasichana kukabiliana  na unyanyasaji wa kijinsia na kuimarisha mifumo ya kuzuia na kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia kupitia kuanzisha na kuandaa vifaa katika madawati matatu ya  Polisi ya Jinsia na Watoto, kuanzisha  vituo vitatu vya  huduma  ya dharura katika  vituo vya wilaya, kuunda nafasi salama ya umma, kujenga uwezo  wa nambari ya msaada ya watoto kitaifa, kuunda na kuimarisha Klabu za Wasichana na kuunda Kamati za ulinzi na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania  Zlatan Milisic   ameipongeza Serikali kwa kuwa  na mradi huo na kuongeza kuwa mradi huo unaendana na malengo ya endelevu ya 2030 hususani lengo namba 5 kuhusiana kuwaendeleza wanawake  katika nyanja mbalimbali na kuongeza kuwa mwaka 2020 ni mwaka muhimu sana kwa kuwa tunaelekea  katika kutimiza miaka 25 ya azimio la wanawake la Beijing.

Ameeleza kuwa  malengo endelevu ya 2030 yameeleza kuwa ili kufikia maendeleo ya nchi kumtambua mwanamke ni jitihada muhimu sana  katika kuharakisha na kutimiza malengo yote ya maendeleo ambapo ameihakikishia Serikali ya Tanzania kuendelea kufanya kazi kwa karibu sana  ili kuhakikisha wanawake wanakuwa chachu ya maendeleo katika  nchi ya Tanzania.

Mwakilishi wa UNFPA, Dk. Winfred amesema kuwa uzinduzi wa mradi umelenga kutokomeza aina zote za unyanyasaji wa kijinsia  na kuimarisha usawa katika jamii ikiwa ni pamoja na  kuimarisha maisha ya wanawake ambapo amesisitiza kitovu cha matatizo ya kijinsia  ni wanaume na mila na desturi potofu zinazomtazama mwanamke kwa kumdharirisha hivyo juhudi za makusudi  zinatakiwa  kufanywa za kuwaweka wanaume mbele ili kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake.

Naye  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo  amesisitiza kuwa kazi nzuri zinazofanywa na  Rais John Pombe Magufuli katika Nyanja mbalimbali ndiyo zinazoyafanya  jumuiya za kimataifa  kuunga mkono kwa kutoa  misaada  kupitia miradi mbalimbali hapa nchini

Sunday, September 27, 2020

TARI YATOA MAFUNZO YA UPANDAJI BORA WA ZAO LA KOROSHO MPWAPWA DODOMA

Mtafiti  kutoka Tari- Naliendele Programu ya Zao la Korosho, Kasiga Ngiha, akitoa mafunzo ya jinsi ya kuandaa shamba, kulipima na upandaji wa zao la korosho kwa Maafisa Ugani na Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma jana katika shamba la Magereza la wilaya hiyo.
Afisa Kilimo kutoka Kata ya Lufu, Pascal Male (kushoto) na wenzake wakijifunza kutoka TARI namna ya kuweka alama wakati wa mafunzo kwa vitendo ya upimaji wa shamba la korosho kabla ya kupandwa zao hilo.
Maafisa Ugani na Wakulima wakijifunza kwa vitendo namna ya upimaji wa shamba la korosho kabla ya kupanda.

Mkulima kutoka Kata ya Lupeta, Yohana Mkasanga (Aliye chuchumaa akipima shamba kwa kamba katika mafunzo hayo ya vitendo. Kushoto (mwenye kofia) ni Mratibu wa Kitaifa wa Zao la Korosho kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele Mtwara, Dkt.Geradina Mzena akiwa kwenye mafunzo hayo.


Afisa Kilimo kutoka Wilaya ya Mpwapwa, Kongwa, Malizia Said (kulia), akijifunza kutoka TARI namna ya kuweka alama wakati wa mafunzo kwa vitendo ya upimaji wa shamba la korosho.
Afisa Kilimo kutoka Kata ya Ving'hawe, Bhoke Magere (kulia) na wenzake wakijifunza kutoka TARI namna ya kuweka alama wakati wa mafunzo kwa vitendo ya upimaji wa shamba la korosho.
Maafisa kilimo wakijadiliana jambo kwenye mafunzo hayo kwa vitendo. Kutoka kushoto ni Afisa Kilimo kutoka Kata ya Chuyu, Oscar Masamalo, Elirehema Elinisafi kutoka Kata ya Pwagi na Monica Malika kutoka Kata ya Ving'hawe.
Mratibu wa Kitaifa wa Zao la Korosho kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele Mtwara, Dkt.Geradina Mzena (katikati) akielekeza namna ya upimaji wa shamba kwenye mafunzo hayo.
Mtafiti  kutoka Tari- Naliendele Programu ya Zao la Korosho, Kasiga Ngiha, akitoa mafunzo ya jinsi ya kulipima ukubwa wa shimo kabla ya kuchimbwa na upandaji wa zao la korosho kwa Maafisa Ugani na Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwawa.
Mkulima  Mary Mahinyila kutoka Mpwapwa mjini, akishiriki mafunzo kwa vitendo kwa kuchimba mashimo katika shamba hilo la Magereza la wilaya hiyo.
Mkulima  Joseph Kodi kutoka Kata ya Mazai, Kijiji cha Kisokwe, akishiriki mafunzo kwa vitendo kwa kuchimba mashimo katika shamba hilo la Magereza la wilaya hiyo.
Mtafiti  kutoka Tari- Naliendele Programu ya Zao la Korosho, Kasiga Ngiha, akitoa mafunzo ya jinsi ya upandaji wa zao la korosho kwa Maafisa Ugani na Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwawa.
Maafisa Kilimo na Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wakiangalia mkorosho ambao upo kama kichaka kwa sababu ya kuto pogolewa na kuhufanya husistawi vizuri.
Mtafiti wa Kilimo kutoka  Tari Naliendele, Selemani Libaburu,  akitoa mafunzo ya jinsi ya kupogolea  mkorosho huo ambao umekuwa kama kichaka.
Muonekano wa mkorosho huo baada ya kupogolewa.
 

Friday, September 25, 2020

TARI YATOA ELIMU KUDHIBITI MAGONJWA YA ZAO LA KOROSHO

Mtafiti Mwandamizi na Mdhibiti wa Visumbufu vya Wadudu na Magonjwa kwenye zao la korosho, kutoka Tari- Naliendele  Mtwara, Dkt.Wilson Nene, akiwaeleza  Maafisa Ugani na Wakulima namna  ugonjwa wa Ubwiriunga unavyoathiri mikorosho wakati wa mafunzo kwa vitendo yaliyofanyika Shule ya Sekondari ya Mnyakongo wilayani Kongwa mkoani Dodoma jana..

Mtafiti wa Kilimo kutoka  Tari Naliendele, Selemani Libaburu,  akitoa mafunzo ya jinsi ya kupogolea  mkorosho ili uweze kustawi vizuri.
Maafisa Ugani na Wakulima wa Wilaya ya Kongwa wakiwa shambani wakijifunza namna ya kudhibiti magonjwa mbalimbali yanayoathiri mikorosho.




Mtafiti Mwandamizi na Mdhibiti wa Visumbufu vya Wadudu na Magonjwa kwenye zao la korosho, kutoka Tari- Naliendele  Mtwara, Dkt.Wilson Nene, akiwaeleza  Maafisa Ugani na Wakulima namna ya kudhibiti magonjwa mbalimbali ya zao hilo.


Moja ya mkorosho wilaya ya Kongwa ulivyoathiriwa na wadudu waharibifu.

Mtafiti wa Kilimo kutoka  Tari Naliendele, Selemani Libaburu, akionesha namna ya kutumia mashine ya kupulizia (Motorized Blower).


Mtafiti wa Kilimo kutoka  Tari Naliendele, Selemani Libaburu, akimfundisha Mwalimu wa Kilimo wa Shule ya Sekondary ya Mnyakongo, Rehema  Lighola namna ya kutumia mashine ya kupulizia kwenye shamba la korosho.
Mwalimu wa Kilimo wa Shule ya Sekondary ya Mnyakongo, Rehema  Lighola akijifunza namna ya kutumia mashine ya kupulizia viuatilifu kwenye shamba la korosho.
Mkulima wa Kata ya Songambele, Richard Sanyaji,  akijifunza namna ya kutumia mashine ya kupulizia viuatilifu kwenye shamba la korosho.
 


Na Godwin Myovela, Kongwa Dodoma

KITUO cha Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele hatimaye kimetoa majawabu ya namna ya kudhibiti visumbufu vya wadudu waharibifu na magonjwa, ikiwemo ugonjwa wa Ubwiriunga, ugonjwa wa Blaiti na Debeki ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa ni changamoto kwa ustawi wa zao la korosho ndani ya Wilaya ya Kongwa na kwingineko nchini

Athari nyingine zilizoonekana wazi ndani ya wilaya hiyo na kupatiwa ufumbuzi na Tari Naliendele ni pamoja na kukithiri kwa wadudu waharibifu wa zao hilo wakiwemo Mbu wa Mikorosho, Mbu wa Minazi na Vidung’ata ambao ni kikwazo kikubwa cha ukuaji mzuri wa zao la Korosho ambalo linatajwa kuwa ni zao lenye uchumi mkubwa na soko la uhakika

Akizungumza kwenye mafunzo ya Kilimo Bora cha Korosho yaliyotolewa jana wilayani hapa kwa wakulima na Maafisa Ugani, Mtafiti kutoka TARI Naliendele Programu ya Korosho, Kitengo cha Udhibiti wa Visumbufu vya Wadudu waharibifu na Magonjwa, Dk Wilson Nene, alisema ugonjwa wa ubwiriunga kama usipodhibitiwa hugeuka tishio kwa ustawi wa mkorosho na  hasara yake ni kuanzia asilimia 70 mpaka 100 (kwa maana ya kutoambulia mavuno yoyote)

“Hapa Kongwa kwenye mashamba tuliyokwenda kufanyia ‘field’ tumeona kuna changamoto ya magonjwa kwa mikorosho mingi kuwa na matatizo ya wadudu waharibifu hasa mbu wa mikorosho, mbu wa minazi na ugonjwa wa ubwiriunga,” alisema Nene

Alisema wadudu hao wakiwa wengi na kushambulia kwa kasi husababisha majani ya mkorosho husika kuathirika, na zaidi majani yake hubadilika na kuonekana yameungua au mfano wa kitu kilichoungua au kubabuliwa na moto au moshi

“Hali hiyo hutokana na wadudu hawa waharibifu mbu wa minazi na mbu wa mikorosho wanapokuwa wanafyonza kwenye majani ‘maeneo teketeke’…basi pale walipofyonza inatokea vidonda ambapo ndio sehemu kimelea hicho kinachosababisha ugonjwa unaoitwa ‘Debeki’ kinapoingilia. Ndio maana hapa Kongwa tumekuta baadhi ya mikorosho imeathiriwa na Debeki,” alisema

Dk Nene alisema kuna umuhimu mkubwa kwa wakulima wa Kongwa, na wengine waliopo mikoa yote 17 inayolima zao hilo nchini kwanza kutambua wadudu waharibifu na magonjwa ya mkorosho kabla athari hazijajitokeza lakini pia kuzingatia mafunzo ya namna ya kudhibiti kitaalamu yanayoendelea kutolewa na TARI kwa sasa

Alieleza kwamba kuna njia kuu tatu za kudhibiti ambazo ni njia za asili kwa maana ya usafi shambani, kuanzia katika upandaji-kupanda kwa nafasi, lakini pia mikorosho yako isisongamane ili kuweza kupogolea. Kwa kufanya hivyo mkulima atatengeneza mazingira yasiyo-rafiki kwa vimelea na wadudu hao waharibifu

Aidha, njia nyingine ni matumizi ya aina 54 ya mbegu bora zinazozalishwa na kituo cha utafiti wa kilimo Tari Naliendele, na kwa kufanya hivyo shamba la mkulima litakuwa na tija na ubora sambamba kuongezeka kwa kiwango cha uzalishaji bila kusahau matumizi sahihi ya viuatilifu na aina zake zote sanjari na matumizi bora ya mashine za kupulizia

“Kupitia elimu hii ambayo imekuwa na mwamko mkubwa tunaamini wilaya ya Kongwa na wakulima wengine za zao hili nchini sasa tutakwenda kuleta mchango mkubwa kwa kuongeza uzalishaji mara 4 kutoka kiwango cha sasa cha tani laki 3.15 kufikia tani milioni 1 kama shabaha ya taifa kufikia 2023.

Thursday, September 24, 2020

TARI YATOA MAFUNZO YA AGRONOMIA YA KOROSHO KWA MAAFISA UGANI NA WAKULIMA KONGWA

Mtafiti  kutoka Tari- Naliendele Programu ya Zao la Korosho, Kasiga Ngiha, akitoa mafunzo ya jinsi ya kuandaa shamba, kulipima na upandaji wa zao la korosho kwa Maafisa Ugani na Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa katika shamba la Shule ya Sekondari ya Mnyakongo.
Mtafiti  kutoka Tari- Naliendele Programu ya Zao la Korosho, Kasiga Ngiha, akitoa mafunzo ya jinsi ya upimaji wa shamba kabla ya kupanda korosho.
Afisa Kilimo kutoka Kata ya Songambele, Asha Malekela wa Wilaya ya Kongwa akipima shamba kwa kamba katika mafunzo hayo kwa vitendo. 

Maafisa Ugani na Wakulima wakijifunza kwa vitendo namna ya upimaji wa shamba la korosho kabla ya kupanda.
Mkulima Gasper Rupia kutoka Kijiji cha Ibwaga,  akijifunza namna ya kupima shamba wakati wa mafunzo kwa vitendo. Kulia ni Mkulima Raheli Esau kutoka kijiji hicho.

Afisa Kilimo, Said Kajagale  kutoka Kata ya Ngomai akijifunza kunyoosha mstari kwa kuelekeza kwa mkono katika mafunzo hayo ya vitendo. 

Afisa Kilimo kutoka Kata ya Mkoka, Marcelin Chingilile (kushoto) na wenzake wakiwa kwenye mafunzo hayo

Afisa Kilimo kutoka Wilaya ya Kongwa, Elias Chilemue (kushoto) na wenzake, wakijifunza kutoka TARI namna ya kuweka alama wakati wa mafunzo kwa vitendo ya upimaji wa shamba la korosho.
Afisa Kilimo kutoka Wilaya ya Kongwa, Dominica Swai (kushoto) akijifunza namna ya kuweka mambo wakati wa mafunzo kwa vitendo ya upimaji wa shamba la korosho.
Mratibu wa Kitaifa wa Zao la Korosho kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele Mtwara, Dkt.Geradina Mzena (kulia), akielekeza namna ya kunyosha mstari kwa kamba katika mafunzo hayo. 
Mkulima  Richard Sanyaji kutoka Kata ya Songambele ,  akishiriki mafunzo kwa vitendo kwa kuchimba mashimo katika shamba hilo la mfano la korosho la Shule ya Sekondari Mnyakongo.
Mkulima Gasper Rupia kutoka Kijiji cha Ibwaga,  akijifunza namna ya kuchanganya udongo na samadi kabla ya kupanda korosho.
Afisa Kilimo kutoka Kata ya Chitego, Michael Edward,  akishiriki mafunzo kwa vitendo kwa kuchimba mashimo katika shamba la mfano la korosho la Shule ya Sekondari Mnyakongo.
Mtafiti wa Kilimo kutoka  Tari Naliendele, Selemani Libaburu,  akitoa mafunzo ya jinsi ya kupanda korosho katika  shamba la mfano la korosho la Shule ya Sekondari Mnyakongo.

Wednesday, September 23, 2020

KONGWA YAANZA MKAKATI WA KILA KAYA KULIMA EKARI MOJA YA KOROSHO



Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Suleiman Serera akizungumza na Maafisa Ugani na Wakulima wakati akifungua mafunzo ya kilimo bora cha korosho yanayotolewa na Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele Mtwara, wilayani humo mkoani Dodoma. Kushoto ni Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Kongwa, Jackson Shija na Mratibu wa Kitaifa wa Zao la Korosho kutoka  TARI Naliendele, Dkt.Geradina Mzena.

Mratibu wa Kitaifa wa Zao la Korosho kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele, Dkt.Geradina Mzena, akitoa mada kwenye mafunzo ya kilimo bora cha korosho yaliyotolewa kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kwa Maafisa Ugani na Wakulima mkoani Dodoma. 

Mtafiti Mwandamizi na Mdhibiti wa Visumbufu vya wadudu na magonjwa kwenye zao la korosho, kutoka Tari- Naliendele  Dkt.Wilson Nene, akitoa mada kwenye mafunzo hayo.

Mtafiti  kutoka Tari- Naliendele Programu ya Zao la Korosho, Kasiga Ngiha, akitoa mada kuhusu 'Agronomia' ya korosho.

Meneja wa Bodi ya Korosho Kanda ya Kati na Magharibi, Ray Mtangi, akizungumzia masoko ya zao hilo.

Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo.
Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Kongwa, Jackson Shija, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo.
Afisa Kilimo wa Kata ya Mkoka, Marcelin Chingilile, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mkulima wa Korosho wa Kata ya Mkoka, Rajab Singo, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa Kilimo wa Kata ya Mlali, Markusi Wongo, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mkulima wa Korosho, Sospeter Chiwuyo, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa Kilimo wa Kata ya Songambele, Asha Malekela, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa Kilimo wa Kata ya Zoissa, Emmanuel Mongi, akizungumza kwenye mafunzo hayo.


Godwin Myovela na Doto Mwaibale, Kongwa 

WILAYA ya Kongwa ipo mbioni kuanza kutekeleza mpango wa kuhakikisha kila kaya 
inalima ekari moja ya zao la miche ya mikorosho bora azma ikiwa ni kuongeza kipato sambamba na kusaidia kurejesha hali ya uoto wa asili na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo yalibainishwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Suleiman Serera, wakati akifungua mafunzo ya Kilimo Bora cha Korosho yanayoendelea kutolewa na Kituo cha Utafiti wa Kilimo Tari Naliendele kwa wakulima na Maafisa Ugani wa Halmashauri wilayani hapa.

“Mkakati wa Wilaya ya Kongwa ni kuhakikisha angalau kila kaya inakuwa na ekari moja ya zao la korosho bora sababu ni zao la kudumu la kibiashara lenye manufaa kiuchumi, lakini tunataka kuikijanisha Kongwa yetu kupitia mbegu bora za mikorosho kutoka Tari Naliendele ,” alisema Serera.

Alisema ili kukamilisha mpango huo ambao hata hivyo tayari umeanza kutekelezwa kwa awamu itahitajika miche zaidi ya milioni 2 ili kuzifikia kaya zote 74,000 zilizopo ndani ya wilaya hiyo.

Serera alisema kilimo cha zao la Korosho katika Wilaya ya Kongwa kilianza rasmi msimu wa kilimo wa 2007l2008 na mpaka sasa kuna jumla ya mikorosho mikubwa 75,591 na midogo 231,295, hivyo kuwa na jumla ya mikorosho 306,886 sawa na ekari 10229.5.

“Naamini baada ya mafunzo haya maafisa ugani mtaendelea kutoa mafunzo ya kilimo bora cha korosho kwa wakulima kwenye maeneo yenu ili kuongeza tija na uzalishaji kwa ustawi wa wilaya yetu,” alisema Serera.

Kwa upande wake, Mratibu wa zao la Korosho Kitaifa kutoka Tari Naliendele, Dkt.Geradina Mzena alisema mafunzo hayo ya nadharia na vitendo yana lengo la kuongeza ujuzi kwa wakulima na maafisa ugani ili kuinua tija kwenye zao la korosho.

“Kwenye mafunzo haya pamoja na mambo mengine tutajikita katika kuangalia namna 
bora ya kuanzisha shamba jipya, ‘agronomia ya Korosho’ na namna bora ya kudhibiti wadudu na magonjwa ya zao hilo,” alisema Mzena.