Sunday, July 31, 2022

WANANCHI WAZUIA MSAFARA WA WAZIRI WA MAJI, WALIA KERO YA MAJI



Waziri wa Maji Jumaa Aweso (kulia) akiwasikiliza Wananchi wa Mto wa Mbu wilayani Monduli mkoani Arusha ambao waliusimamisha msafara wake jana wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi wakilalamia kukosa maji.
Wananchi wakiwa na ndoo za maji na matawi ya miti wakati walipozuia msafara wa Waziri wa Maji Jumaa Aweso.

Saturday, July 30, 2022

WAZIRI AWESO ATAKA MABONDE YA MAJI KWENDA KUJIFUNZA BONDE LA KATI UFANISI WA UTENDAJI KAZI

Waziri wa Maji Jumaa Aweso (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa wa ujenzi wa ofisi ya maabara ya bodi ya maji Bonde la Kati, mjini Singida leo Julai, 30, 2022. Kutoka kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu, Afisa wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, Mhandisi Danford Samson, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Mulagiri, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida, Lusia Mwiru na Mjumbe wa Siasa Mkoa wa Singida, Diana Chilolo.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizindua jengohilo lililopo Kata ya Utemini mjini Singida.

Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji Nchini Dk. George Lugomela akitoa taarifa ya mradi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Taifa, Mhandisi Mbogo Futakamba akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, William Mabula akizungumza kwenye hafla hiyo.
Waziri wa Maji Juma Aweso (katikati) akitoka kukagua maabara ya maji. 
 Afisa wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, Mhandisi Danford Samson akiwatambulisha viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo.

Hafla hiyo ikiendelea.

Kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Mkoa wa Singida ikitoa burudani.

Mjumbe wa Siasa Mkoa wa Singida, Diana Chilolo. akizungumza kweny hafla hiyo kwa niaba ya mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Singida.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu, akizungumza kwenye uzinduzi huo.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida, Lusia Mwiru , akichangia jambo kwenye hafla hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Bonde la Kati aliyemaliza muda wake. Mhandisi Samson Mabala akizungumza kwenye hafla.

Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Mulagiri akizungumza kwenye hafla hiyo.
Wajumbe wa Bodi ya Maji Bonde la Kati waliomaliza muda wao wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, William Mabula akionesha zana za kazi baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Maji Jumaa Aweso.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso (kushoto) akikagua ujenzi wa mradi wa maji, Dareda, Singu, Sigino na Bagara unaotekelezwa Mkoa wa Manyara ambao utagharimu Sh.12 Bilioni.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Manyara (BAWASA) Idd Msuya (katikati) akimuelezea Waziri wa Maji Jumaa Aweso kuhusu mradi huo.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso (kushoto) akipata maelezo ya ujenzi wa mradi ya ofisi ndogo ya Bodi ya Maji Bonde la Kati inayojengwa Babati mkoani Manyara ambao ujenzi wake utagharimu zaidi ya Sh.700 Milioni. Katikati ni Afisa Maji Bodi ya Maji Bonde la Kati, Mhandisi Danford Samson.

 

Na Dotto Mwaibale ,Singida

 
WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso,amezindua jengo la ofisi kuu ya Bonde la Kati zilizopo mjini Singida na maabara za ubora wa maji na kuyataka mabonde mengine kwenda kujifunza utendaji mzuri wa kazi unaofanya na viongozi wa bonde hilo.

Akizungumza leo Julai 30, 2022 mara baada ya kuzindua jengo hilo ambalo ujenzi wake umegharimu zaidi ya Sh.bilioni 2.9 hadi kukamilika kwake, alisema Bonde la Maji Kati litakuwa kama chuo kwa mabonde mengine kwenda kujifunza kutokana na jinsi wanavyofanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

Aweso alisema Wizara ya Maji ina jukumu la kuhakikisha nchi inakuwa na maji ya kutosha
hivyo Bodi za Maji nchini ziache kuweka bei za kuwakandamiza watumiaji wa maji ili wapate nguvu za kuendelea kutunza vyanzo vya maji.

Aidha, alisema baada ya kukamilika kwa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi kukamilika, mabonde yote tisa ya maji nchini yarejewe takwimu za upatikanaji wa maji nchini.

Aweso alisema Bodi za Maji zihakikishe zinawatambua na kuwashirikisha watumiaji wa maji kwani wapo baadhi wanatumia maji bila kuwa na vibari lakini hawatambuliwi.

"Moja ya changamoto ya mabonde yetu yanatumika tu kwa ajili ya 'ambush' tu, washirikisheni, watambuweni wadau wenu wa maji na msiweke bei za kuwakandamiza, wekeni bei rafiki," alisema.

Aweso alisema wakurugenzi na maafisa wa mabonde ya maji watambue wajibu wao kwa kutoka maofisini kutoa elimu sahihi ya juu uanzishwaji wa mabonde ya maji.

"Wakati mwingine anapoambiwa mtu kuna taasisi ya bonde anajua pengine ni kimlima kidogo kidogo, maafisa wa bonde mtoke muwaelimishe wananchi," alisema.

Aweso alisema haiwezekani unajiita afisa bonde halafu hata vyanzo vya maji huvijui na hata watu wanapokuwa na changamoto ya maji hauna ufumbuzi wa tatizo hilo.

Alisema zifanyike jitihada za kuongeza rasilimali za maji kwani haiwezekani mvua zinanyesha halafu maji yote yanapotea kwenye bahari.

Waziri Aweso alisema ni muda mwafaka rasilimali za maji kwa maana ya mvua isiwe kama laana bali iwe baraka na fursa kwa maji ya mvua kuvunwa kwa kujenga mabwawa ya kimkakati ili maji hayo yatumike kwa matumizi ya kunywa.

Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji Dk.George Lugomela alisema Bodi ya Maji Bonde la Kati iliyomaliza muda wake imejitahidi kufanya kazi ambapo imeongeza ukusanyaji wa mapato kutoka Sh.Milioni 300 zilizokiwa zikikusanywa awali na kufikia Sh.mil.800.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Pakas Mlagiri, alisema Bonde ndio injini ya maji sababu wao ndio wanaovisimamia vyanzo vyote vya maji.

Alisema kutokana na umuhimu huo wa mabonde ya maji, kufanyike utafiti wa kuainisha vyanzo vyote vya maji kuanzia ngazi ya kijijjj na kata kufanya hivyo kutasaidia upatikanaji mkubwa wa maji.
Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu, alisema upatikanaji wa maji katika manispaa hiyo umefikia kiwango za asilimia 80.

Kiaratu alishauri Bonde la Maji Kati kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Singida kutunga sheria ndogo kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji.

Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, William Mabula alisema wamejipanga kufanya vizuri zaidi kwa kusimamia rasilimali za maji na kuongeza mapato kutoka Sh.milioni 800 hadi kufikia Sh. Bilioni 1.

 

Friday, July 29, 2022

MREMA ATOA NENO UTEUZI WAKUU WA MIKOA ULIOFANYWA NA RAIS SAMIA

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha TLP, Augustino Mrema.

 

Na Thobias Mwanakatwe

 

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha TLP, Augustino Mrema, amesema uteuzi na mabadiliko ya wakuu wa mikoa uliofanya na Rais  Samia Suluhu Hassan iwe chachu kwa walioteuliwa kufanya kazi kwa bidii kumsaidia rais katika kuleta maendeleo makubwa ya kiuchumi nchini.

Akizungumza jana kwa simu akiwa jijini Dar es Salaam, alisema rais anapofanya mabadiliko ya viongozi dhamira yake kuu ni kutaka kuona wasaidizi wake wanamsaidia katika kuleta maendeleo kwa wananchi.

Mrema ambaye ni mwanasiasa mkongwe ambaye amewahi kushika nyadhifa kadhaa ikiwano ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, alisema rais tuliyenaye anapenda kuona wasaidizi wake wanaleta mabadiliko ya kimaendeleo katika maeneo aliyowateua.

"Viongozi waliobahatika kuteuliwa cha msingi wakishaanza kutekeleza majukumu yao wachape kazi kuwaletea maendeleo wananchi maana dhamira ya rais ni kuiona Tanzania inakuwa nchi yenye watu wake wenye maendeleo makubwa," alisema Mrema.

Mrema aliongeza kuwa mara nyingi watu wanapoteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi wanafurahia badala ya kwenda kufurahia unapokuwa umesaidia kuleta mabadiliko ya maendeleo kwenye eneo ulilopangiwa.

Alisema walioachwa katika uteuzi huu hawana sababu ya kujisikia wanyonge kwani mchango wao walioutoa wakiwa viongozi unatambulika kwani uongozi ni kupokezana vijiti.

"Mimi nilikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani leo hii si niko benchi nafasi ameishika mwingine, na kwenye hizi kazi ukifanya vizuri utakumbukwa daima kwa uwajibikaji uliotukuka na heshima utakuwa nayo mbele ya jamii kama ikivyo kwangu mimi," alisema Mrema.

Mrema alisema moja ya majukumu ya Mkuu wa mkoa ni pamoja na kuhakikisha mkoa wako unakuwa na makusanyo ya mapato na kuzuia rushwa na upotevu wa mapato kwenye halmashauri zilizopo kwenye mkoa husika.

Aliongeza kuwa katika siku za karibu tumekuwa tukishuhudia na hata katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) halmashauri nyingi zikikumbwa na kashfa ya ubadhirifu wa mapato na wakuu wa mikoa wapo lakini hawachukui hatua kwa watendaji wao wa chini.

Mrema alisema sio jambo lenye afya kiongozi wa kitaifa anapofanya ziara katika mkoa wako na kuibua suala la ubadhirifu wa mapato wakati wewe kama Mkuu wa Mkoa upo na haukufanya jambo lolote kuchukua hatua kudhibiti haki hiyo.

 

MADEREVA BAJAJ, BODABODA KUWA MABALOZI WA TANESCO SINGIDA

Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika  la Umeme Tanzania i (TANESCO) Mkoa wa Singida, Rehema Mwaipopo akisisitiza jambo wakati akizungumza na madereva wa bajaj na bodaboda  katika Ukumbi wa Vatican uliopo eneo la Mwenge mjini hapa juzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Madereva na Wamiliki Pikipiki na Bajaj Tanzania (CHAMWAPITA) Mkoa wa Singida, Ahmed Mohamed, akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Diwani wa Kata ya Minga, Ibrahim Mrua.

Thursday, July 28, 2022

SERIKALI, LIONS CLUB YAKABIDHI CHUO CHA UFUNDI MSANDAKA MKOANI KILIMANJARO

Majengo ya Chuo cha Ufundi Msandaka yanvyoonekana baada ya ufunguzi uliofanywa na Mkurugenzi wa Elimu Mahitaji Maalum Tanzania Dkt. Magreth Matonya.
Mkurugenzi wa Elimu Mahitaji Maalum Tanzania Dkt. Magreth Matonya akishuhudia wanafunzi viziwi wenye ujuzi katika fani ya ushonaji wanavyofanya.

WAZAZI WATAKIWA KUHAKIKISHA WATOTO WENYE ULEMAVU WANAHESABIWA

 Mratibu wa Sensa Mkoa wa Singida, Naing'oya Kipuyo, akizungumza na Wakufunzi wa Makarani wa Sensa ya Watu na Makazi baada ya kuhitimu mafunzo hivi karibuni yaliyofanyika Chuo cha Ufundi VETA mkoani hapa.

Wednesday, July 27, 2022

DK. MWIGULU: UJENZI WA MIRADI YA BARABARA ILINGANE NA THAMANI YA FEDHA ZINAZOTOLEWA

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Mwigulu Nchemba ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi, akizungumza katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa, kilichofanyika leo Julai 27, 2022 katika Ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge ambaye alikuwa Mwenyekiti akiongoza kikao hicho
Makamu Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Mbunge wa Singida, Kaskazini, Ramadhan Ighondo akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimba akizungumza kwenye kikao hicho ambapo aliwapongeza wabunge wa mkoa huo kwa kazi nzuri wanayifanya.
Wabunge wa Mkoa wa Singida wakiwa kwenye kikao hicho.
kikao kikiendelea.

Tuesday, July 26, 2022

TFRA YATOA WITO KWA WAKULIMA KUJISAJILI ILI WANUFAIKE NA RUZUKU YA SERIKALI.



 Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania –TFRA Dkt Stephan Ngailo akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam akitoa taarifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan kuzindua mpango wa utoaji wa ruzuku ya mbolea kwa wakulima.

……………………….

NA MUSSA KHALID

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania -TFRA imewataka wakulima nchini kujitokeza kujiandikisha na kujisajili kwenye Ofisi za serikali za vijiji vyao ili waweze kunufaika na mpango wa serikali wa kuwapunguzia makali ya bei ya Mbolea kupitia Ruzuku.

Kauli hiyo imetolewa  jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA Dkt Stephan Ngailo wakati akitoa taarifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan kuzindua mpango wa utoaji wa ruzuku ya mbolea kwa wakulima.

Dkt Ngailo amesema kutokana na kupanda kwa bei za mbolea katika soko la Dunia na hapa nchini serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 150 kugharamia ruzuku ya mbolea itakayotolewa kwa wakulima wote nchini kwa lengo la kupunguza makali ya bei za mbolea na kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo.

Amesema kuwa Serikali imeamua kutumia Mfumo wa kidigitali kutekeleza mpango wa ruzuku ya Mbolea ili kuongeza ufanisi,kupunguza mianya ya udanganyifu Pamoja na Muda na gharama za Usimamizi.

Aidha Dkt Ngailo amesema kuwa Mbolea zitakazohusika kwenye Ruzuku ni za kupandia na kukuzia ambapo DAP kwa ajili ya kupandia na Urea kwa kukuzia ambazo zote ni takriban Asilimia 50 ya matumizi yote ya Mbolea Nchini.

Dkt Ngailo ameeleza kuwa Mfumo huo utafanya kazi kwa mkulima aliyesajiliwa ataenda kwa mfanyabiashara wa Mbolea aliyesajiliwa Kwa ajili ya kununua Mbolea na kuonyesha namba ya utambulishe aliyopewa wakati wa usajili.

“Ili kuhamasisha matumizi ya Mbolea zinazozalishwa nchini,zinazozalishwa na viwanda vya ndani zitaingia kwenye mpango wa ruzuku kulingana na mahitaji ya soko”amesema Dkt Ngailo

Amesema uuzaji wa mbolea kwa wakulima na malipo ya ruzuku ya mbolea mfumo huo utafanya na makampuni yataingiza na kuzalisha mbolea nchini na kuifungasha katika mifuko yenye uzito wa kilo 25 na 50 ambayo itaandikwa ‘MBOLEA YA RUZUKU’na itachapwa QR Code itakayotolewa na TFRA.

Amesema utekelezaji wa mpango wa ruzuku ya Mbolea utahusisha wadau mbalimbali wakiwemo Wizara ya Kilimo,Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea TFRA,Kamati Tendaji ya Ruzuku,Sekratieti za mikoa,Mamlaka ya serikali za mitaa,WAINGIZAJI/wazalishaji wa Mbolea,Mawakala wa Mbolea,Taasisi za Fedha na wakulima.

Pia ameziomba serikali za vijiji,viongozi,watendaji na mabalozi sambamba na maafisa ugani kushiriki kikamilifu katika zoezi la usajili wa wakulima na utoaji wa ruzuku ili kuhakikiha mkulima anafaida jambo litakaloisaidia kukuza uchumi wanchi

TANESCO SINGIDA YAANZISHA UTARATIBU WA KUWASIKILIZA WANANCHI ILI KUJUA CHANGAMOTO ZAO KUHUSU UMEME

Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Singida, Mhandisi Florence Mwakasege akizungumza na Wananchi wa Kata ya Iguguno wilayani Mkalama  leo Julai 26, 2022  wakati akisikiliza mahitaji na ushauri wao kuhusu sekta ya nishati.
Afisa Mtendaji Kata ya Iguguno,  Josia Pangazi akizungumza kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Meneja wa Tanesco Wilaya ya Mkalama, Mhandisi, Benedict Ryeimamu, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Singida, Mhandisi, Florence Mwakasege na Mwenyekiti wa Kijiji cha Iguguno Kiula Solomon.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Iguguno, Kiula Solomon akizungumza kwenye mkutano huo.

Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Tanesco Mkoa wa Singida, Rehema Mwaipopo akizungumzia huduma mpya ya maombi ya kuunganishiwa umeme kwa njia ya mtandao  iitwayo NIKONEKT  ambayo inafanyika kwa kutumia simu ambapo muombaji anaomba akiwa nyumbani bila ya kufika ofisi za shirika hilo.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Iguguno Mashariki, Nicolaus Ernest akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwananchi wa kata hiyo, Elisante Stephano akizungumzia changamoto ya gharama za kufungiwa umeme kuwa kubwa.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwananchi wa eneo hilo Modesta Masasi akiomba eneo wanaloishi kupelekewa umeme.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.

Monday, July 25, 2022

KAMATI YA SENSA MKOA WA SINGIDA YAWATEMBEA WAKUFUNZI 216 WATAKAO HITIMU MAFUNZO KESHO

 Mratibu wa Sensa Mkoa wa Singida, Naing'oya Kipuyo, akizungumza wakati Wajumbe wa Kamati ya Sensa ya Watu na Makazi mkoani hapa walipowatembelea leo Julai 25, 2922 Wakufunzi wa Makarani wa Sensa wanaotarajiwa kuhitimu kesho Julai 26, 2022 katika ukumbi wa VETA mjini hapa ambapo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge anarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Mjumbe wa kamati hiyo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Lucas Mwakatundu akijitambulisha kwa wakufunzi hao.

OFISI YA ARDHI MKOA WA SINGIDA YAANZA KUSIKILIZA KERO ZA MIGOGORO YA ARDHI

Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida, Shamim Hoza akizungumzia kuhusu ofisi ya Ardhi Mkoa wa Singida ilivyoanza leo Julai 25,2022 kusikiliza kero za migogoro ya ardhi ya wananchi kwa kila halmashauri ili ziweze kutatuliwa.

Wananchi wa Mkoa wa Singida wakiandika majina baada ya kufika Ukumbi wa Zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida kupeleka kero zao zinazohusu ardhi.

Friday, July 22, 2022

MBUNGE MULUGO AWAPIGA TAFU WAVUVI KUNUNUA INJINI YA BOTI

Mbunge wa Jimbo la Songwe, Philip Mulugo.

MAAFISA ARDHI MKOA WA SINGIDA WATAKIWA KWENDA KUTOA USHAHIDI BARAZA LA ARDHI

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza  kwenye kikao kazi cha watumishi wa sekta ya ardhi mkoa kilichofanyika mjini hapa leo Julai 22, 2022 katika Ukumbi wa ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG). Kushoto ni Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida, Shamim Hoza.

Afisa Utumishi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Salum Issa akizungumza kwenye kikao hicho.