Saturday, April 30, 2022

MWAMKO DUNI WA WAZAZI WAWAKOSESHA WATOTO CHAKULA SHULENI

Ofisa Elimu Msingi katika Manispaa ya Singida, Omary Maje akifafanua jambo kuhusiana na hali halisi ya mwamko wa wazazi juu ya  uchangiaji  chakula kwa wanafunzi.
Wanafunzi wakipata chakula moja ya shule za msingi.


Na Abby Nkungu, Singida


 MWAMKO duni wa wazazi kuwachangia chakula cha mchana watoto wao wanaosoma bado ni changamoto kubwa ambapo asilimia 66.1 ya shule za msingi za Serikali katika Manispaa ya Singida hazitoi huduma hiyo.

Hali hiyo inatajwa kuathiri usikivu, umakini, uelewa na ufaulu hasa kwa watoto wasiozidi miaka minane ambao bado wanahitaji lishe bora kwa ajili ya ukuaji wa ubongo ili waweze kufanya  vyema darasani.

Ofisa elimu Msingi Manispaa ya Singida, Omary Maje alisema kuwa kati ya shule 53 za msingi  za Serikali zilizopo halmashauri hiyo, 18 tu (sawa na asilimia 33.9) ndizo zinazotoa chakula cha mchana kwa  wanafunzi wake.

“Manispaa hii kuna jumla ya shule 71. Shule 53 ni za Serikali, 13 binafsi na 5 za awali tu. Wenzetu wa binafsi shule zote zinatoa chakula cha mchana  na uji  ndio maana hata ufaulu wao ni mzuri lakini sisi wa Serikali ni shule 18 tu ndizo zenye huduma hiyo” alifafanua  Maje.

Alisema kuwa tatizo  kubwa ni mwamko mdogo wa wazazi na walezi kushindwa kuchangia chakula cha mchana  kwa watoto  wao shuleni lakini akasisitiza kuwa idara hiyo inaendelea na juhudi za kuwapa wazazi hao ujumbe sahihi na kuwaeleza manufaa yake; ikiwa ni pamoja na kuwaongezea usikivu, umakini na uelewa kwenye masomo yao.

“Hata hivyo, tunashukuru kwani kuna ongezeko kubwa ikilinganishwa na ilivyokuwa Oktoba mwaka jana ambapo ni shule nne  tu za Serikali ndizo zilizokuwa zinatoa chakula. Baada ya kubanana na nyie vyombo vya habari kuandika-andika, hatimaye leo tumefikia shule 18 zenye huduma hiyo, sio jambo dogo” alieleza.

Alisema kuwa Manispaa ya Singida ni miongoni mwa halmashauri nchini zinazotekeleza Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ya miaka mitano (2021 -  2026 ) ambapo  suala la lishe mashuleni na hasa kwa watoto walio chini ya miaka minane linapewa kipaumbele.  

Mmoja wa walimu wanaofundisha shule ya awali ambaye hakupenda  jina lake litajwe alisema ni vyema juhudi hizo zikaharakishwa ili watoto wapate elimu bila kikwazo chochote.  

“Wanaoumia zaidi na changamoto  hii ni hawa watoto wadogo ingawa baadhi yao huwahi kuondoka shule lakini kwa wanaobaki ikifika saa 4:00 asubuhi huwa wanaanza kusinzia na  kupiga miayo  kwa njaa na uchovu hadi unawahurumia, wanapoteza usikivu kabisa” alisema.

Halima Omari, mzazi na mkazi wa Majengo na John Lameck mkazi wa Ginnery Manispaa ya Singida, pamoja na kukiri juu ya  adha ya njaa  hasa kwa watoto wa chekechea na madarasa ya chini, wanawatupia lawama viongozi na watendaji  wa Serikali wakidai wameshindwa kuhamasisha vya kutosha suala hilo.

"Mbona michango mingine tunatoa.....ujenzi wa madarasa, maabara, vyoo, Mbio za Mwenge, harusi na kipaimara. Iweje chakula tena cha mtoto wangu mwenyewe nisichangie? Tatizo ni viongozi  wetu" alisema John huku  akiungwa mkono na Halima ambaye ametaka  viongozi na watendaji kutimiza kikamilifu wajibu wao.

Kwa mujibu wa wataalamu wa lishe, ulaji duni au ulaji usiozingatia makundi matano ya chakula huathiri ukuaji wa ubongo wa mtoto hivyo kusababisha kutokufundishika kirahisi darasani na kuwa mzito kwenye kufikiri na kutoa uamuzi sahihi anapokuwa mtu mzima.


MAJI KUVING'ARISHA KIJIJI CHA STAHABU NA MIKUNGUNI WILAYANI PANGANI MKOA WA TANGA

Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Pangani, Mhandisi Willybroad Mungereza akiwa na Mkandarasi wa Mradi wa Maji Mikinguni, John Msafiri kukagua hatua ya ujnzi ulipofikia.
Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Wilaya ya Pangani mkoani Tanga, Ramadhan Hamad akielezea furaha aliyonayo kwa RUWASA kuwapelekea maji katika kijiji cha Stahabu
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Tanga, Mhandisi Pendo Omary akielezea waandishi wa habari namna fedha za ustawi zinavyotekeleza miradi ya maji mkoani humo.
Muonekano wa nyumba ya kuweka pampu ya Mradi wa Maji Mikinguni wilayani Pangani mkoani Tanga.
Muonekano wa tenki la maji kwenye Mradi wa Maji Mikinguni wilayani Pangani mkoani Tanga.
Mwananchi wa kijiji cha Stahabu Wilaya ya Pangani Mkoa wa Tanga Mwanaidi Almas akielezea furaha aliyonayo baada ya RUWASA kuwapelekea mradi wa maji.
Mwenyekiti wa kijiji cha Stahabu kata ya Mikinguni Mussa Mzee akielezea furaha yao kwa kitendo cha RUWASA kuwapelekea mradi wa maji.


Na Selemani Msuya, Pangani


WANANCHI wa Vijiji vya Stahabu na Mikunguni Wilaya ya Pangani Mkoa wa Tanga, wamesema mradi wa maji unatekelezwa kijijini kwao kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19 utang’arisha vijiji hivyo.

Mradi huo unatekelezwa kwa zaidi ya Sh.milioni 533 fedha za mkopo usio na riba wa Sh.trilioni 1.3 zilizotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuomba ili kuhakikisha Sera ya Maji inayotaka kila mwananchi anachota maji kwa umbali wa mita 400.

Akizungumzia ujio wa mradi huo wa maji kijijini kwao, Mwana mama Mwanaidi Almas amesema wanatarajia kung’aa bada ya maji hayo kutoka kwani walikuwa wanatumia maji kwa kupima kutokana na changamoto ya upatikanaji.

“Hadi sasa hatujafungua koki maji yakatoka, ila imani yangu siku chache zijazo tutafungua koki, hivyo Shahabu itaanza kung’aa kama maeneo mengine yenye maji safi na salama,”amesema.

Almas amesema wamepitia mateso makubwa wakati wa kutafuta maji usiku wa manene kwa kuvamiwa na watu wabaya, huku wakiwa hawana amani pale ambapo wanaacha watoto wa kambo na waume zao ambao baadhi yao walikuwa wanashindwa kuvumilia.

Naye Mawazo Shaban amesema. “Sisi tumefurahi sana kwa kutuliwa ndoo kichwani kwani tumesulubika vya kutosha, naomba Rais Samia na Serikali yake waendelee kutumikia Watanzania,” amesema.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Wilaya ya Pangani mkoa wa Tanga, Ramadhan Hamad (Diblo) amempongeza Rais Samia kuwaona Stahabu na kuweka bayana kuwa yoyote anayemuwazia mabaya kiongozi huyo Mwenyezi Mungu amuangamize.

“Mimi kama kiongozi wa CUF nitashirikiana na viongozi wa Serikali kuhakikisha mradi huu unalindwa ili uwe endelevu na kuing’anisha Stahabu na yoyote anayemtakia mabaya Rais Samia tunaomba asifanikiwe,” amesema.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mikinguni, Kaoneka Jumaa amesema mradi huo utawaondolea adha ya kunywa maji ya madimbwi ambayo yalikuwa yanatumiwa pia na mifugo na wanyama kama nguruwe.

Jumaa amesema pia changamoto ya maji Mikinguni  ilikuwa inasababisha wanafunzi kuchelewa kwenda shule kutokana na kutumia muda mwingi kutafuta maji.

“Mradi huu wa maji kata ya Mikinguni umekuja wakati muafaka kwani hitaji ni kubwa kwa wananchi wetu. Imani yangu ni ujio wa maji haya ubadilishe maisha yetu kuanzia usafi wa mazingira na maendeleo.

Rais Samia ameupiga mwingi katika hili la maji, na Waziri wetu wa Maji Dogo Jumaa Aweso amecheza kama Simba. Tunawashukuru sana,” amesema.

Mwenyekiti wa kijiji cha Stahabu kata ya Mikinguni Mussa Mzee amesema wana zaidi ya miaka 35 ya kufuata maji kwa umbali wa kilometa tatu, hivyo ni imani yao kuwa wanaenda kufurahi maji bombani kama Watanzania wengine.

“Tunamshukuru Rais Samia na RUWASA kwa kumtua ndoo mama kichwani, kwani amesaidia shughuli zingine kushika kasi,” amesema.

Mtendaji wa kijiji Stahabu Mwinyihamis Akida amesema mradi huu utachangia kumaliza migogoro kati ya wafugaji na wananchi kugombea maji kwenye madimbwi.

Akifafanua kuhusu mradi huo wa Maji Mikinguni, Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Pangani, Mhandisi Willybroad Mungereza amesema mradi huo utanufaisha zaidi ya watu 4,990 vya vijiji vyote viwili.

Amesema wamejenga tenki lenye uwezo wa kuhifadhi lita 135,000, kibanda cha pampu, mtandao wa kusambaza mabomba ya maji wenye urefu wa kilomita, vituo 21 katika vijiji vyote viwili na kinyoshea ng’ombe.

“Mradi huu unaotekelezwa na Kampuni ya NTU Business Network Limited,  unagharimu zaidi ya Sh.533 utanufaisha zaidi ya watu 4,990 wa vijiji vya Mikinguni  na Stahabu ambao wamekuwa wakiteseka kupata maji safi na salama. Lakini kukamilika kwa mradi huo kutaongeza asilimia ya upatikanaji maji wilayani Pangani hadi kufikia 70 kutoka asilimia 68 ya sasa,” amesema.

Akizungumzia miradi hiyo Meneja wa RUWASA Mkoa wa Tanga, Mhandisi Pendo Omary amesema miradi ya maji mkoani hapo inagharimu zaidi ya Sh.bilioni 6.7 na itanufaisha wananchi 80,000.

Mhandisi Omary amesema zaidi ya vijiji 21 vitanufaika na fedha hizo katika majimbo 12 ya uchaguzi ya mkoa huo, hivyo lengo la mkoa kufikisha maji vijijini asilimia 85 na mijini asilimia 95 litatimia ifikapo 2025.

Mkandarasi wa mradi huo, John Msafiri amesema wamejipanga kumaliza mradi huo kwa wakati na ubora unaokubalika.

Amesema hadi sasa mradi huo umefikia zaidi ya asilimia 75 ya utekelezaji na kuiomba Serikali kuendelea kuwapa nafasi wakandarasi wazawa kutekeleza miradi.

Naye Fundi Geofrey Mnonganile amesema uamuzi wa Serikali kuwawapatia wakandarasi wazawa miradi mbalimbali utachochea ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira kwa vijana.

Kwa upande wake Fundi Haji Abdallah ambaye pia ni Mkazi wa kijiji cha Stahabu amesema kupitia mradi huo amenufaika na kuiomba Serikali kuendelea kuwaletea miradi hiyo.

“Naujenga kwa nguvu zote kwa sababu ni mradi ambao unakuja kumaliza kero ya maji kijijini kwetu, tulikuwa tunafuata maji kijiji cha Sakura, Makarawe na Mtandu. Kusema kweli Rais Samia ametenda miujiza hapa kwetu,” amesema.


SHILINGI 500 MILIONI KUMALIZA KERO YA MAJI VIJIJI VYA LWANDE NA SAGASI KILINDI TANGA

Bibi Fatuma Lwande na Mjukuu wake Mwajuma Said wakisafusha ndoo ili kuchota maji Mto Kombe uliopo kijiji cha Lwande kwa matumizi ya nyumbani.
Bibi Fatuma Lwande wa kijiji cha Lwande akisafisha ndoo ili kuchota maji mto Kombe kwa matumizi ya nyumbani.
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilindi, Mhandisi Alex Odena akiangalia Jenereta ambayo itatumika kusukuma maji kuingia kwenye tenki la maji kijiji cha Lwande.
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilindi, Mhandisi Alex Odena akiangalia Jenereta ambayo itatumika kusukuma maji kuingia kwenye tenki la maji kijiji cha Lwande.
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilindi,Mhandisi Alex Odena akifafanua jambo kuhusu Mradi wa Maji Lwande.
Zainabu Mohamedi wa kijiji cha Sagasi akielezea furaha aliyonayo kwa kupelekewa maji na RUWASA.


Na Selemani Msuya, Kilindi


WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijiji (RUWASA) Wilaya ya Kilindi Mkoa wa Tanga umetumia Sh.milioni 504 za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19 kumaliza kero ya maji kijiji cha Lwande na Sagasi.

Fedha hizo ni sehemu ya mkopo usio na riba wa Sh.trilioni 1.3 zilizotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuomba ili kuhakikisha Sera ya Maji inayotaka kila mwananchi anachota maji kwa umbali wa mita 400.

Hayo yamesemwa na Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilindi, Mhandisi Alex Odena wakati akizungumza na waandishi wa habari walikuwa wanatembelea miradi ya maji inayotekelezwa kwa fedha za ustawi Sh.milioni 504.

Amesema RUWASA wamelazimika kupeleka mradi huo kwenye kijiji cha Lwande baada ya chanzo cha maji kilichopo kuwa na maji ya uhakika na salama.

Mhandisi Odena amesema mradi huo ambao ni kwanza tangu kijiji kuanzishwa utahusisha usambazaji wa bomba kilometa 15.5, ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita 100,000 na vituo saba ambavyo hadi sasa vimeshakamilika.

“Tumetumia zaidi ya Sh.milioni 500 kutekeleza mradi huu wa Lwande ambao utanufaisha wananchi 4,611 wa vijiji viwili vya Lwande na Sagasa na utaongeza upatikanaji wa maji Kilindi hadi kufikia asilimia 36.6 kutoka asilimia 35 iliyopo kwa sasa,” amesema.

Meneja huyo amesema pia baada ya mradi huo kukamilika Kilindi itaongeza vijiji vinavyopata maji safi na salama hadi kufikia 43 kati ya 102.

Mhandisi Odena amesema mradi huo unaenda kuwatua ndoo kichwani wakina mama hali ambayo itachochea shughuli za kilimo, biashara na kijamii kupewa kipaumbele.

Odena amesema mradi huo umetekelezwa kwa ushirikishaji wananchi wa Lwande ambao wamepata ajira za muda na wengine watapatab za kudumu kama kuendesha mtambo wa kupandisha maji.

Meneja huyo wa RUWASA Kilindi amesema ina changamoto ya vyanzo vya maji, hivyo wanaendelea kutafuta vyanzo vingine ili kuhakikisha dhamira ya Serikali vijijini maji kupatikana kwa asilimia 85 inatimia.

Akizungumzia miradi hiyo Meneja wa RUWASA Mkoa wa Tanga, Mhandisi Pendo Omary amesema miradi ya maji mkoani hapo inagharimu zaidi ya Sh.bilioni 6.7 na itanufaisha wananchi 80,000.

Mhandisi Omary amesema zaidi ya vijiji 21 vitanufaika na fedha hizo katika majimbo 12 ya uchaguzi ya mkoa huo, hivyo lengo la mkoa kufikisha maji vijijini asilimia 85 na mijini asilimia 95 litatimia ifikapo 2025.

Diwani wa kata ya Lwande Wilaya ya Kilindi Mkoa wa Tanga, Hassan Mwengo amesema mradi huo umekuja wakati muafaka na kuahidi kuulinda kwa nguvu zote ili uwe endelevu.

Mwengo amesema ukosefu wa maji safi na salama kupitia bomba kulikuwa kunawapa wakati mgumu kunadi sera zao kwa kuwa wananchi wengi walikuwa wanatumia muda mwingi kutafuta maji.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Lwande, Abdallah Gumbo amesema maendeleo ya kijiji chao yalikuwa yanadidimia kutokana na changamoto ya maji, hivyo ni imani yao kuwa maendeleo yatakuwa.

Mwananchi Ramadhani Kimweri wa kijiji cha Lwande amesema mradi huo wameupokea kwa shangwe kwa sababu tangu mwanzo wameshirikishwa, hivyo wanampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kuwakumbuka baada ya miaka 60 ya kupitia wakati mgumu kwenye eneo la maji.

“Wananchi wa Lwande ni wakulima na wafugaji, hivyo walikuwa wanatumia muda mrefu kutafuta maji, ila ujio wa mradi huu ni wazi kuwa tumekombolewa kiuchumi na kijamii.

Lakini pia kilichofanyika ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ibara ya 147 hadi 150, hivyo CCM imesafisha njia ya 2025,” amesema.

Kwa upande wake Bibi Fatumba Lwande (60) amesema changamoto ya maji inasababisha atumie muda wa saa mbili kufuata maji, hivyo uamuzi wa RUWASA kuwapelekea maji bombani ni wa kupongeza.

“Natuamia muda mwingi kufuata maji huku mtoni, unaona nimekuja huku na vitukuu, kwani siwezi kuwaacha, tunateseka sana,” amesema.

Mwajuma Said ambaye ni mjukuu wa Bibi Fatuma amesema kutokana na shida ya maji kijiji kwao analazimika kufuata maji mbali huku akiwa mjamzito, hali ambayo sio salama kwake na mtoto.

“Sina cha kusema tofauti na kumchukuru Rais Samia, kwani mateso haya ambayo mama wajawazito tumepitia naamini yanafikia mwisho,”amesema.

Naye Amina Mbezeni wa kijiji cha Sagasi amesema wanashukuru kupata maji safi na salama hali ambayo itawaondolea changamoto ya magonjwa mbalimbali.

Zainab Mohammed amesema matarajio yao ni kupitia mradi huo kijiji chao kitapata maendeleo kwa haraka, huku usafi wa mazingira ukiongezeka.

Naye Mkandarasi wa mradi huo, Enock Chengula amesema wanashukuru Serikali kuwapatia mradi huo ambao umewezesha wananchi zaidi ya 50 wamepata ajira.

SERIKALI YA AUSTRIA NA SHIRIKA LA C.I.P WAWEZESHA MAFUNZO YA LUGHA YA ALAMA WAZAZI WENYE WATOTO VIZIWI-SINGIDA


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Community Initiatives Promotion (CIP) la mkoani Singida, Afesso Ogenga akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya lugha ya alama yaliyowahusisha Wazazi na Walezi mkoani Singida jana.

Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika hilo Parinemas Mashanjara akizungumza katika hafla hiyo.
      Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Singida, Tumaini Christopher ambaye alikuwa mgeni rasmi akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Singida.
Afisa Elimu Maalum wa Manispaa ya Singida Philipina Mboya akizungumzia umuhimu wa elimu hiyo.
Afisa Elimu Kata ya Misuna, Nembris August akizungumzia mafunzo hayo na kutoa shukurani kwa shirika hilo kwa msaada mkubwa wanaotoa katika shule hiyo.

Mkuu wa Shule ya Msingi Tumaini Viziwi, Francis Edward akizungumzia historia ya shule  hiyo.

Hafla ya kufunga mafunzo hayo ikiendelea.

Mshiriki wa mafunzo hayo Mnkwimba John akielezea faida aliyoipata kwa kupata mafunzo hayo.
Wazazi wakiwa kwenye hafla hiyo.

Iddy Ramadhani mzazi alipata mafunzo hayo akielezea furaha aliyonao kwa kupata mafunzo hayo.

Hafla ikiendelea.
Wazazi wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wazazi walioshiriki mafunzo hayo wakisubiri kukabidhiwa vyeti vyao.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Lugha ya alama ikioneshwa.
Lugha ya alama wakionesha wahitimu wa mafunzo hayo.
Hafla ikiendelea.
Vyeti vikikabidhiwa kwa wahitimu wa mafunzo hayo.
Vyeti vikitolewa.

VIONGOZI WILAYA YA IKUNGI WAENDELEA NA MKAKATI WA KUNUSURU MSITU WA ASILI WA MINYUGHE

Mhifadhi Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Samuel  Matura (kulia) akimuonesha ramani Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ikungi mkoani Singida  ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo, Jerry Muro (kushoto) wakati wajumbe wa kamati hiyo, walipokuwa wakikagua Msitu wa Asili wa Minyughe ambao umevamiwa na kufanyika uharibifu mkubwa wa mazingira.

Wajumbe wa kamati hiyo wakipitia ramani ya msitu huo.
Majadiliano yakifanyika wakati wa ziara hiyo.
Safari ya ukaguzi wa msitu huo ikifanyika.
Muonekano wa baadhi ya maeneo ya msitu huo.
Muonekano wa mazao yaliyolimwa ndani ya msitu huo.
Muonekano sehemu ya msitu huo.
Magari yakichanja mbugu ndani ya msitu huo wakati wa ukaguzi.
Mashamba ya alizeti yakiwa yamelimwa ndani ya msitu huo.

Friday, April 29, 2022

WIZARA YA UWEKEZAJI VIWANDA NA BIASHARA YAIPONGEZA SUA KWA TAFITI ZAKE

  Naibu Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe akifungua Warsha hiyo

 Kiongozi wa Mradi huo wa  TRADE HUB nchini Tanzania Prof. Reuben Kadigi akizungumza na wadau lengo la warsha hiyo.

Mhadhiri Muandamizi wa Uchumi Kilimo na Masoko Dk. Fulgence Mishili akitoa  salamu kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo.

MATOKEO YA UTAFITI WA MAJI JIJI LA DODOMA

Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Profesa Japhet Kashaigili akifafanua jambo wakati wautoajiwa uwasilishwaji wa matoke ya utafiti wa miaka mitano wa chanzo cha maji cha Jiji la Dodoma Makutupora.

 Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji kutokaWizaraya Maji Dkt George Lugomela akitoa neno wakati akifungua Warsha hiyo ya siku moja ya kupokea matokeo ya utafiti wa mradi wa GroFutures Jijini Dodoma.

Mtafiti Mkuu wa Mradi huo Profesa. Richard Tayrol kutoka katika Chuo Kikuu cha jiji la London nchini Uingereza akichangia kwenye uwasilishaji wa matokeo hayo.

1Mmoja ya wakulima ambao wamepata nafasi ya kuhudhuria Warsha hiyo kwa niaba ya wa  kulima wengine Dkt. Huruma Msuya akizungumza na SUA MEDIA nje ya Warsha hiyo.

Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Cardiff cha nchiniUingereza Dkt. Adrian Healy  akizungumza wakati akiwasilisha sehemu ya utafiti wake.

Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi, Watafiti pamoja na wadau wengine kutoka sekta mbalimbali walioshiriki katika warsha hiyo ya kutoa matokeo ya utafiti huo.

1.     Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.

Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.

Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.

Washiriki kutoka Sekta mbalimbali wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya Utafiti huo uliofanyika Jijini Dodoma.