Tuesday, May 30, 2023

DC IRAMBA AGUSWA NA ADHA YA WANANCHI KIJIJI CHA MSAI KUKOSA ZAHANATI

Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda (katikati) akishiriki kufyatua matofali wakati wa mfululizo wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo aliyoifanya Kata ya Shelui na Mtoa wilayani humo jana May 29, 2023 akiwa ameongoza na wataalam, watendaji wa Kata na Tarafa pamoja  na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama.

...................................................... 

Na Mwandishi Wetu, Iramba

MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda amesema atafanya mawasiliano na wahusika wa sekta ya afya ili ziweze kupatika fedha za kumalizia ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Msai

Kupatikana kwa fedha hizo na kukamilika kwa ujenzi wa zahanati hiyo kutawaondolea adha wananchi ya kutembea umbali mrefu kwenda kupata huduma za matibabu maemo mengine.

Mwenda ameyasema hayo  wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Kata yaMtoa na Shelui pamojana kusikiliza kero za wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi.

Akiwa katika Zahanati ya Msai inayojengwa kwa nguvu za wananchi wakisaidiwa na fedha za Mfuko wa Jimbo zinazo simamiwa na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Dkt. Mwigulu Nchemba aliombwa na wananchi kupatikana kwa fedha za kumalizia ujenzi wa jengo hilo la zahanati hiyo Ili ianze kutoa huduma na kuwaondolea kero wakazi wa kijiji hicho hasa Wajawazito na watoto.

"Nimesikia maombi yenu napenda kuwasiliana na wahusika ili kuwaomba tupate fedha za kumalizia ujenzi wa zahanati iweze kukamilika na kuanza kutoa huduma haraka iwezekanavyo," alisema Mwenda.

Alisema kijiji hicho ni kikubwa na kuna wananchi wengi lazima ujenzi wa zahanati hiyo ukamilike haraka ili wananchi wasiendelee kwenda mbali kupata huduma za afya.

Aidha,Mwenda akiwa kwenye ziara hiyo aliwasisitiza wasimamizi wa miradi yote inayotekelezwa katika wilaya hiyo kuhakikisha inakamilika kabla ya June 10,2023.

Katika hatua nyingine Mwenda amewaomba wananchi kuendelea kujitolea nguvu kazi kwa kushirikiana na wataalam na viongozi katika kutekeleza  miradi yote  inayofadhiliwa na  serikali na kuhakikisha inamalizika kwa wakati  na viwango kulingana  na thamani ya fedha walizozipokea 

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda, akipokea taarifa wakati wa ziara hiyo.
Kazi za utekelezaji wa miradi zikiendelea.
Ziara ikiendelea.
Ziara ikiendelea.
 

RC SINGIDA :UKAMILISHAJI WA MIRADI YA MAENDELEO NI JAMBO LA KUFA NA KUPONA


 Mkuuwa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akizungumza na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida wakati alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mkhandi kilichopo wilayani humo leo May 30, 2023. Kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Mhandisi Paskas Muragili na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Omari Mande.

........................................................ 

Na Dotto Mwaibale, Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida,Peter Serukamba amesema kazi ya kumalizia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya zote mkoani hapa ni la kufa na kupona na kuwa kazi hiyo ifanyike usiku na mchana kutokana na umuhimu wake.

Serukamba ameyasema hayo leo May 30, 2023 wakati alipokuwa katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea na kukagua ukamilishaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida na kuhimiza miradi yote iwe imekamilika kabla ya Julai 1, 2023 kwa viwango vinavyotakiwa na kulingana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa.

" Mkurugenzi, Mkuu wa wilaya, Madiwani, Mhandisi na timu yenu nzima msikae ofisini nendeni ilipo miradi na hakikisheni ukamilishaji wake unakuwa ndani ya siku 20 kuanzia leo na si vinginevyo kwani fedha zote zitakazo salia kabla ya kuikamilisha zitarudishwa serikalini mwisho wa mwaka wa fedha wa 2022/ 2023 ambapo zimebaki siku 20 tu  kuanzia leo,” alisema Serukamba.

Serukamba alisema hatapenda kuona fedha hizo zikirudi bila ya kumaliza kazi iliyokusudiwa ya kumaliza ujenzi wa miradi hiyo yakiwemo madarasa, zahanati na mabweni kwani kurudi kwa fedha hizo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliyezitoa hatakuwa ajatendewa haki pamoja na wananchi ambao ndio walengwa wa miradi hiyo.

Aidha, Serukamba alisisitiza vituo vya afya na zahanati zinazoendelea kujengwa ujezi wake uwe umekamilika kabla ya Julai na Julai Mosi, 2023 zizinduliwe rasmi na kuanza kutoa huduma za afya kwa wananchi.

Alisema agizo la kukamilisha miradi hiyo kabla ya Julai, 1, 2023 kwa halmashauri zote nchini zimetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Angellah Kairuki na ndio maana wapo katika ziara ya kuhimiza kukamilika kwa miradi hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Omari Mande akizungumza kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo alisema maagizo yote aliyoyatoa Mkuu wa Mkoa watayatekeleza kama walivyoagizwa na kuwa hakuna mradi hata mmoja ambao hautakamilika ndani ya muda huo.

Miradi aliyoitembelea leo ni ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Makhandi ambayo ujenzi wake ulianza mwaka 2019 kwa nguvu za wananchi kwa ushirikiano wa vijiji viwili vya Makhandi na Idd Simba, ujenzi wa bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari ya Maghojoa ambapo Mkuu wa Mkoa Serukamba aliomba halmashauri hiyo itumie fedha zake za ndani kwa ajili ya kuingiza umeme na maji.

Mradi mwingine uliokaguliwa ni ujenzi wa Zahanati ya Kijijicha Sagara, ujenzi wa bwalo la chakula katika Shule ya Sekondari ya Itaja, Ujenzi wa vyoo katika Shule ya Msingi ya Mwighanji, ujenzi wa bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari ya Mughanga, ujenzi wa bweni kupitia mradi wa elimu maalum.

 katika Kijiji cha Mgori, ujenzi wa darasa katika Shule ya Msingi Mughamo na ujenzi wa nyumba ya walimu katika Shule ya Msingi Ngaramtoni.

Katika ziara hiyo Serukamba aliongoza na wakuu wa idara, maafisa watendaji wa kata na Tarafa, wataalam na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo.

Kesho Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba anatarajia kuendelea na ziara yake hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni  na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuhimiza ukamilishwaji wake kwa wakati.

Mkuu wa wilaya hiyo, Mhandisi Paskas Muragili, akisisitiza jambo wakati wa ukaguzi wa Zahanati ya kijijihicho.

Muonekano wa zahanati ya kijiji hicho.
RC Serukamba akisisitiza jambo kwenye ziara hiyo.
Muonekano wa zahanati ya Kijiji cha Sagara wakati wa ziara hiyo.
Ukaguzi wa Zahanati ya Kijiji cha Sagara ukifanyika.
RC Serukamba akielekeza jambo baada ya ukaguzi wa zahanati ya Kijiji cha Sagara.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, akizungumza wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Bwalo la Shule ya Sekondari ya Itaja.
Muonekano wa ujenzi wa Bwalo hilo.
RC Serukamba akiwa ameongoza na Diwani wa Kata ya Itaja, Paul Himida wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Bwalo hilo
Ukaguzi wa ujenziwa vyoo vya Shule ya Msingi,Mwighanji ukifanyika.
Muonekano wa vyoo vya Shule ya Msingi, Mwighanji ambavyo vilikuwa vikitumika.
Ukaguzi wa ujenzi wa nyumba ya walimu katika Shule ya Msingi Ngaramtoni ukifanyika.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Omari Mande akielekeja jambo wakati wa ukaguzi wa ujenzi nyumba hiyo ya walimu.
Muonekano wa bweni la wanafunzi wasichana wa Shule ya Sekondari ya Mughanga ambao ujenzi wake umekamilika. RC Serukamba ameomba washirikishwe wazazi ili waweze kununua vitanda na vifaa vingine ikiwa ni pamoja na kuingiza maji ili wanafunzi hao waanze kulitumia bweni hilo.
Ukaguzi wa bweni kwa ajili ya watoto maalum linalojengwa Kijiji cha Mgori ukiendelea.
Muonekano wa bweni hilo ambalo ujenzi wake upo mwishoni kukamilika.
Ukaguzi wa ujenzi wa darasa katika Shule ya Msingi Mughamo ukifanyika.
 

Saturday, May 27, 2023

WACHIMBA MADINI KUANZISHA BENKI KWA LENGO LA KUKOPESHANA

Rais wa Shirikisho la Vyama Vya Wachimbaji Madini Tanzania ( FEMATA) John Bina (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa shirikisho hilo katika kikao cha siku mbili kilicho anza leo May 27, 2023, Ukumbi wa Hotel ya Aqua Mjini Singida ambacho kitafikia tamati kesho. Kulia ni mgeni rasmi wa kikao hicho Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Singida, Chone Malembo na kushoto ni Mwenyekiti wa Wanawake wachimbaji madini Taifa, Martha Kayaga.

...........................................................

Na Dotto Mwaibale, Singida

SHIRIKISHO la Vyama vya Wachimba Madini Tanzania (FEMATA) linatarajia kuanzisha benki yao ambayo itatumika kuwakopesha wachimbaji kwa lengo la kuinua sekta hiyo muhimu kiuchumi nchini.

Hayo yamesemwa na Rais wa FEMATA,  John Bina wakati akizungumza katika kikao cha siku mbili cha Kamati Tendaji ya shirikisho hilo  ambacho kimeanza leo May 27, 2023 na kufikia tamati kesho May 28, 2023 chenye lengo la kukamilisha mchakato wa kuandika katiba mpya ambayo itaendana na wakati wa sasa pamoja na kujadili mambo mengine.

Bina alisema wamefikia hatua ya kuanzisha benki hiyo kwa ajili ya kuwasaidia wachimbaji ili waweze kukopeshwa fedha za mitaji ya kuendesha shughuli za uchimbaji baada ya kuwepo changamoto za kukopeshwa fedha na mabenki yaliyopo hapa nchini.

"Wachimbaji tumekuwa na changamoto kubwa katika sekta yetu hii muhimu katika kuinua uchumi wa nchi, tumekuwa tukitumia zana duni na kufanya kazi kwa kiwango cha chini kutokana na kuwa na mitaji midogo na kibaya zaidi hata tukienda katika mabenki yaliyopo kuomba mkopo tumekuwa hatukopeki ndio maana tukaona ni vizuri tukaanzisha ya kwetu," alisema Bina.

Alisema ili shirikisho hilo liendelee kuwa imara ni lazima liwe na katiba inayoendana na wakati wa sasa, baadae, wakati uliopo na ujao.

Alisema FEMATA ilianzishwa mwaka 1986 na katiba inayotumika ni ya tangu mwaka huo hivyo wamekubaliana katika vikao tofauti na kufikia maazimio hayo kwenye kikao walicho keti Musoma mkoani Mara na Tanga ambapo imeendelea kuandikwa na sasa wamefika mwisho wa kupata katiba hiyo.

Katika hatua nyingine Bina alitumia nafasi hiyo kuwahamasisha wananchi wa Mkoa wa Singida kuchangamkia fursa ya uchimbaji wa madini mengi ya aina mbalimbali yaliyopo mkoani hapa.

"Singida ina akiba ya madini ya kutosha lakini changamoto iliyopo ni ya rasilimali watu mimi kwetu ni hapa Singida lazima niwaambie acheni uzembe fanyeni kazi wenzetu wasukuma ndio wanaofanya kazi ya uchimbaji wa madini katika migodi iliyopo, dhahabu iliyoyopo Geita inaweza kuwa ni nyingi lakini Singida inaweza kuwa nyingi zaidi  shida hapa ni rasilimali watu sisi wanaSingida tumekalia kubishana badala ya kufanya kazi," alisema Bina.

Bina aliwaomba viongozi wa vyama vya wachimba madimi Mkoa wa Singida kuwaeleza wananchi umuhimu wa madini na faida zake jambo litakalowasaidia kuamka na kuanza kufanya kazi hiyo ikiwa pamoja na kupata ajira na kuinua maisha yao kiuchumi badala ya kuwaachia fursa hiyo ichangamkiwe na watu wengine kutoka nje ya mkoa huo.

Aidha, Bina alizungumzia tozo wanazotozwa wachimbaji kwenye Halmshauri za Wilaya wanapotunga sheria wawe wanawashirikisha viongozi wa FEMATA kwani  zimekuwa nyingi na kuwa kero kwao.

Alisema changamoto nyingine iliyopo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuja na mfumo wa kuwatoza kodi kwa asilimia mbili wakati wao wana asilimia saba na kwamba hawakatai kulipa kodi kwani kulipa kodi ndio msingi wa maendeleo na kuiomba mamlaka hiyo iangalie namna ya kuiondoa kodi hiyo ambayo imekuwa kero.

Bina aliomba TRA wakae pamoja na wachimbaji  kujadili kodi hiyo iliyoanza kutozwa ili kuona namna bora ya kuliweka sawa jambo hilo pasipo kuumiza upande wowote.

Afisa Mkazi wa Madini Mkoa wa Singida, Chone Malembo, ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema katiba iliyopo imeweza kuwafikisha hapo walipo lakini katibu mpya kwa sasa ni ya muhimu kwani itasaidia kuwapeleka mbele zaidi na kujibu changamoto mbalimbali zilizokuwa zikijitokeza mwanzo.

"Hivi sasa dunia imebadilika ikiwa ni pamoja na sekta yenyewe hivyo naamini katiba mpya italeta tija na maendeleo sambamba na kuondoa changamoto mlizokuwa mkikabiliana nazo," alisema Chone.

Aidha, Chone aliomba shirikisho hilo kufungua milango ya kuwaita wachimbaji wengine kutoka mikoa mingine kuja kuwekeza mkoani Singida kwani Tanzania ni yetu sote.


Afisa Madini Mkazi, Mkoa wa Singida, Chone Malembo akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho.
Naibu Katibu Mkuu FEMATA, Peter Kabepela, akizungumza katika kikao hicho.


Mhazini Mkuu wa FEMATA, Gregory Kibusi, akizungumza kwenye kikao hicho.


Katibu wa Wachimbaji wadogo Mkoa wa Singida, Innocent Makomelo, akizungumza kwenye kikao hicho

Wajumbe wakiomba dua kabla ya kuanza kikao hicho.
Dua ikifanyika kabla ya kikao hicho.
Dua ikiendelea kufanyika.
Sala ikifanyika kabla ya kuanza kwa kikao hicho.
Sala ikifanyika.
Viongozi meza kuu wakishiriki kuomba kabla ya kuanza kwa kikao hicho.

Taswira ya kikao hicho.
Mwenyekiti wa Wachimbaji wadogo Mkoa wa Singida, Robert Malando akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Wachimbaji Mkoa wa Mbeya, Leonard Wangesha akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mchimbaji Yusuph Mwandami, akiomba vyama vyote vya uchimbaji mikoani viitwe, FEMATA vinavyoitwa  hivi sasa zinakuwa kama vinawatenganisha.
Mwenyekiti wa Wachimbaji Madini Wilaya ya Ikungi,, Selemani Dule, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mhimbaji Madini kutoka Mbeya, Happyness Mabula akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Wanawake wachimbaji madini Taifa, Martha Kayaga. akizungumza kwenye kikao hicho.
Picha ya pamoja.
 

Thursday, May 11, 2023

DC MWENDA AZINDUA ZAHANATI YA KIJIJI CHA MASAGI ILIYOJENGWA KWA MIL.99/-

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akikoroga uji wa Lishe ulikuwa unagawiwa kwa Watoto waliofika kwenye uzinduzi wa Zahanati ya Kijiji cha Masagi iliyopo Kata ya Mtoa Tarafa ya Shelui wilayani hapa iliyojenga kwa zaidi ya Sh.Milioni 99 katika hafla iliyofanyika juzi.

Na Mwandishi Wetu, Iramba

MKUU wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Suleimani Yusuph Mwenda,  amezindua rasmi Zahanati ya Kijiji cha Masagi Kata ya Mtoa Tarafa ya Shelui wilayani hapa iliyojenga kwa zaidi ya Sh.Milioni 99 ambayo  itahudumia wananchi  3,117 wa  kijiji hicho..

 Akizungumza baada ya kuzindua zahanati hiyo,  Mwenda, amewataka wananchi hao kuhudhuria kikamilifu na kupata matibabu katika zahanati hiyo kwani kwa sasa changamoto ya kufuata matibabu kwa mwendo mrefu umeisha.

Alisema  kuzinduliwa kwa Zahanati hiyo kutaondoa  kabisa vifo vya akina Mama na watoto  ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu kufuata  matibabu Shelui au Mtoa  na katika Hospitali ya Wilaya.

"Vifo vya akina mama vitapungua kwa asilimia kubwa  kutokana na kukamilika kwa Zahanati nyingi katika vijiji Wilayani Iramba, lakini pia pindi vituo vya Afya vya Mtoa, na Shelui vitakapokamilika vitafanya vifo vya mama na mtoto kuwa ni historia katika wilaya yetu," alisema.                            

Aliongeza kuwa Sh. Milioni 280 zimeletwa kumalizia ujenzi wa Kituo cha Afya Mtoa, ambapo Sh. Milioni 120 zimeingia tayari kwa ajili ya Kukamilisha Kituo Cha Afya Shelui na Sh.Milioni ni 200 zimeletwa Kukamilisha ujenzi wa  Zahanati ya Kinambeu  lengo kusogeza huduma za matibabu karibu kwa wananchi..

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba Dkt. Hussein Sepoko, alisema  Zahanati ya Masagi  imekamilika na tayari imepewa  vifaa tiba vyenye thamani ya Sh.  Milioni 24 huku wahudumu wa afya wawili tayari wamefika  kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.

Aidha, wananchi wa Kijiji hicho wameishukuru serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuwajengea zahanati karibu ambayo itawafanya sasa wasitembee umbali mrefu kufuata huduma za matibabu.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda, akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa zahanati hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akipata maelezokutoka kwa mmoja wa wazee wakati wa hafla hiyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mhe. Innocent Msengi akizungumza katika hafla hiyo.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Dr. Hussein Sepoko akisoma taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa Zahanati ya Masagi.

UjiLishe ukiandaliwa.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akigawa uji lishe kwa wananchi waliokuwepo kwenye uzinduzi huo.
DC Mwenda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mhe. Innocent Msengi akigawa uji wa lishe  kwa wananchi waliokuwepo kwenye uzinduzi huo.