Tuesday, November 30, 2021

RC SINGIDA AKABIDHI BASI HOSPITALI YA MANDEWA KWA AJILI YA KUSAFIRISHIA WAFANYAKAZI

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge.
Basi namba STL 9908 lililokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge kwa ajili ya wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.


Na Mwandishi Wetu, Singida.


MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amezindua Rasmi  na kukabidhi basi aina ya Coaster kwa ajili ya kusafirishia wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mandewa iliyopo mkoani hapo kama kitendea kazi kitakachowasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

Akizungumza na wafanyakazi akiwa Hospitalini hapo baada ya kuwakabidhi basi Mkuu wa Mkoa amewapongeza watumishi kwa namna ambavyo wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu  na wengi wao wakitumia bodaboda kufika kazini lakini pia hawakukata tamaa.


RC Mahenge amemtaka Afisa usafirishaji wa Hospitali ya Mkoa wa Singida kuhakikisha basi hilo linatunzwa na kuzingatia muda wa  kufanyia huduma (service) kila inapofika muda wake ili kulifanya lidumu kwa muda mrefu na kuendelea kuwasaidia watumishi.

Amewataka madaktari katika hospitahi hiyo ambayo ni Tawi la Hospitali ya Mkoa wa Singida  kuboresha huduma zao na kuzifanya ziwe za kibingwa  ili kuifanya Singida kuwa kimbilio la  mikoa ya jirani (center of excellence )

Aidha ameitaka bodi ya Hospitali hiyo kuanza kufikiria namna ya kujenga nyumba za watumishi kupitia vyanzo vyao vya ndani au kupitia  mashirika mbalimbali  kwa kuwa kukaa karibu na hospitali kunaongeza ufanisi katika kazi.

Akimalizia hotuba yake mkuu wa mkoa amewataka madaktari hao pamoja na bodi kuyafanya majengo ya zamani kuwa hospitali ya Wilaya halafu majengo ya Hospitali ya Mandewa yatumike kama hospitali ya mkoa.

Awali Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa  Dkt. Deogratius Banuba akisoma hotuba yake alisema gari hilo lina thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 236 ambazo zilitokana na makusanyo ya ndani.

Hata hivyo amemhakikishi RC kwamba gari hilo litatumika kubeba watumishi kuwaleta kazini na kuwarudisha na pia kutumika katika shughuli za kijamii kwa watumishi

VIJANA NCHINI WATAKIWA KUJIVUNIA MIAKA 60 YA UHURU

 Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani (wa pili kutoka kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa na wilaya wa  Taasisi ya Vijana ya Sisi ni Tanzania baada ya kumaliza kikao chao kilichofanyika Manispaa ya Singida mwishoni mwa wiki.

DC IKUNGI AOMBA KUMUOMBEA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

 

 Afisa Mtendaji wa Kata ya Dung'unyi Yahaya Njiku (katikati) akikata utepe kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro, kuashiria uzinduzi wa Album ya Kwaya ya Malezi ya Vijana Usharika wa Emanueli Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Singida juzi.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Dung'unyi Yahaya Njiku (katikati) akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro, katika uzinduzi wa Album hiyo.

MSTAHIKI MEYA JIJI LA ARUSHA MGENI RASMI KONGAMANO LA FURSA SEKTA YA MUZIKI

Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Maximillian Iranghe.
Katibu Mkuu wa TAMUFO Stella Joel.

Monday, November 29, 2021

WAZIRI BASHUNGWA -TAMASHA LA KIHISTORIA LATUA MBEYA

 




Na. John Mapepele, WUSM

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Innocent Bashungwa amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Filamu nchini inatarajia kwa mara ya kwanza tangu Tanzania kupata uhuru wake kufanya tamasha kubwa la kihistoria la utoaji wa tuzo mbalimbali za filamu ambalo litafanyika Disemba 18, 2021 jijini Mbeya.

Akizungumza na kwenye Mkutano wa Waandishi wa   wa habari jijini Mbeya, Novemba 29, 2021 Mhe. Bashungwa amesema sababu kubwa ya kufanyia kilele cha tuzo hizi jijini Mbeya ni kutambua uwepo wa wanatasnia ya filamu pamoja na wasanii katika mikoa na maeneo mengine nje ya Dar es Salaam ili kuamsha ari ya kufanya kazi za sanaa na hatimaye kujipatia ajira na kipato kitakacho boresha maisha yao.

  “Tamasha hili linakwenda kufungua milango ya fursa mbalimbali zilizoko maeneo hayo katika uwanja huu wa filamu na Sanaa kwa ujumla kupitia idadi kubwa ya wapenzi wa filamu watakaokuwa wanafuatilia tukio hili ndani na ncje ya nchi yetu.”. Amefafanua

Aidha amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, imedhamilia kuleta mapinduzi makubwa kwenye tasnia ya sanaa na Filamu ndyo maana imekuwa na miokakati mbalimbali ya kuboresha tasnia hiyo  ikiwa ni pamoja na kutoa tuzo za filamu kwa wanatasnia ya filamu hapa nchini kwa lengo la kutambua mchango wa wahatasnia hao.

“Kwa mwaka huu wa fedha, Mhe. Rais ametenga kiasi cha Sh. Bilioni 1.5 kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni ambao niliuzindua tarehe 22 Novemba 2021. Mfuko huo utatoa mikopo na kuwezesha programu mbalimbali za kuendeleza Sanaa nchini ikiwemo filamu” amefafanua Mhe. Bashungwa

Akifafanua zaidi Mhe. Bashungwa amesema  katika  kuboresha  kazi za sanaa na Filamu nchini Novemba 22,  2021, alizindua  Mfumo wa kidijitali utakaokuwa unatumiwa na Taasisi za BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA, ambazo ziko chini ya Wizara yake.

Ametaja baadhi ya faida za mifumo hiyo kuwa ni pamoja na kurahisha utendaji wa Taasisi hizo katika kuwahudumia wasanii kwa kutia huduma kwa haraka,kuwarahisishia wasanii wote nchini na hata nje ya nchi kupata huduma kokote walipo bila kufika katika ofisi hizo, ambazo ni BASATA, BODI YA FILAMU na COSOTA na kutunza kumbukumbu za wasanii na kuleta wepesi wa kuwatambua kokote walipo ili kurahisisha utoaji huduma kwao kama vile mafunzo mbalimbali ya Sanaa ambayo Taasisi hizi zimekuwa zikiyatoa.

“Huu ni wakati muafaka wa kuonyesha nguvu na mchango mkubwa wa Tasnia ya Filamu katika kuchochea ukuaji wa Uchumi. Sekta ya burudani inayohusisha filamu imefanya vizuri katika nyanja za Kiuchumi, kwa mfano, mnamo mwaka 2018 Sekta hii iliongoza kwa ukuaji wa kasi ya zaidi ya 13%, ambapo ilishika nafasi ya tatu mwaka 2019 kwa ukuaji wa kasi ya 11%. “ amesisitiza Mhe. Bashungwa

Sunday, November 28, 2021

JAJI WARIOBA AONGOZA MAHAFALI YA 38 YA CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO SUA MOROGORO.




Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokine cha Kilimo (SUA) Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba akimtunuku Shahada ya Uzamivu mmoja wa wahitimu katika mahafali ya 38 ya chuo hicho yaliyofanyika jana mkoani Morogoro.

Kiongzi Rasmi wa shughuli za Mahafali ya 38 ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)  Mlau Profesa Kalunde Sibuga akiongoza msafara wa Mkuu wa chuo kuingia kwenye ukumbi wa mahafali yaliyofanyika jana mkoani humo. 
 Mlau Profesa Kalunde Sibuga akitoa neno la ukaribisho wakati wa ufunguzi wa mahafali hayo.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.

Saturday, November 27, 2021

DC HANANG' AONGOZA SHUGHULI MBALIMBALI MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA UHURU

Mkuu wa Wilaya ya Hanang' mkoani Manyara, Janeth Mayanja akipanda mti ikiwa ni moja ya shughuli zilizofanyika katika Maadhimisho ya Kumbukizi ya Miaka 60 ya Uhuru yaliyofanyika leo  katika Viwanja vya Shule ya Msingi ya Katesh.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang' mkoani Manyara, Janeth Mayanja akiwa na viongozi mbalimbali kwenye maadhimisho hayo.

Friday, November 26, 2021

WAZIRI NDAKI AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA OMAN

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Desert Cold Store kutoka Oman, Dkt. Munawar Pardhan  alipokutana na Wawekezaji kutoka nchini Oman jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (katikati) akibadilishana mawazo na sehemu ya Wawekezaji waliomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam Novemba 26, 2021. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Desert Cold Store kutoka Oman, Dkt. Munawar Pardhan.

DC SAME AONGOZA MAOMBI MAALUMU YA KUIOMBEA NCHI IPATE MVUA

Mkuu wa Wilaya ya Same Edward Mpogolo akizungumza katika mkutano wa maombi maalumu wa kuliombea Taifa lipate mvua uliofanyika wilayani humo.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Viongozi wa Dini wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya Same Edward Mpogolo akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Same Isaya Mngulu, akizungumza wakati wa maombi hayo.
Askofu Mstaafu Jimbo Katoliki la Same Jacob  Koda akizungumza kwenye mkutano huo.



Mkutano ukiendelea.
Mkuu wa Wilaya ya Same Edward Mpogolo (katikati waliokaa) akiwa na viongozi wa Dini na Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kufanya maombi maalumu ya kuombea nchi ipate mvua.


Na Mwandishi Wetu, Same.


MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Edward Mpogolo ameongoza maombi maalumu ya kuiombea nchi ipate mvua ili kunusuru maisha ya watu na wanyama.

Maombi hayo muhimu yaliwahusisha, viongozi wa dini, wazee pamoja na wananchi.

Kati ya maeneo ambayo yanatajwa kuathirika zaidi na mabadiliko ya tabia ya nchi na kukosekana kwa mvua ni pamoja na wilaya hiyo ambayo wakazi wake ni wafugaji na wakulima.


Akizungumza jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa maombi hayo,  Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Mpogolo alisema changamoto kubwa iliyopo kwa sasa ni ukame unaoyakabili maeneo mbalimbali ya tambarare ndani ya wilaya hiyo huku wahanga wakubwa wakiwa ni wafugaji, wakulima pamoja na wanyama.

Mpogolo alisema Serikali wilayani hapo imeunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuwataka viongozi mbalimbali kuungana na viongozi wa dini na wa kimila katika kuliombea Taifa ili Mungu aweze kushusha mvua ya wastani kwa mahitaji ya wananchi ikiwa ni pamoja na kutunza vyanzo vya maji na kumhimiza utunzaji wa mazingira.

"Nimewaita wazee wangu pamoja na viongozi wa dini ili tuweze kujadili kwa pamoja nini tunaweza kufanya na kuokoa maisha ya wananchi wetu pamoja na mifugo, "alisema Mpogolo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazee Wilaya ya Same (JUWASA), Deoglas Msangi alisema mabadiliko ya tabia ya nchi yanayojitokeza sehemu mbalimbali hapa nchini yamesababishwa na uhalibifu wa mazingira ambao unafanyika katika maeneo mengi.

Msangi alisema kwa sasa kumekuwapo na uvunaji miti kiholela katika maeneo mengi kitu ambacho kinasababisha maeneo hayo kuwa makame na kukausha vyanzo vya maji.

"Zamani kulikuwa na misitu mingi ya asili ambayo wazee wetu waliitunza kwa lengo la kutunza mazingira sambamba na utunzaji wa vyanzo vya maji na mafanikio yake yalionekana kwa jamii lakini hivi sasa misitu mingi haipo na ukame umezidi hivyo inatupasa tubadilike," alisema Msangi.

Baadhi ya viongozi wa dini wakiongozwa na  Askofu Mstaafu Jimbo Katoliki la Same Jacob  Koda, Askofu Msaidizi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  (KKKT) Dayosisi ya Pare, Ibrahim Ndekia, Askofu Kanisa la TAG Paulo Ponda, Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Same, Idd Juma Ally wamesema ili taifa lifunguliwe ni lazima kufanyika Sala ya Toba kwa wananchi kwani kwa kiasi kikubwa jamii imemkosea Mungu.

Viongozi hao walijumuika pamoja na Serikali na waliongoza kuliombea Taifa Ili Mungu aweze kushusha mvua ya wastani kwa mahitaji ya Wananchi, wakulima na wafugaji huku wazee hao wakiiomba Serikali iwajengee mabwawa yatakayotumika kuvuna maji ya mvua yatakayosaidia wafugaji na wakulima kipindi cha ukame. 

Thursday, November 25, 2021

MKUU WA WILAYA TANDAHIMBA AIPONGEZA REA KWA KAZI NZURI

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Patrick Sawala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius Kalolo (wa tatu-kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy (wa tatu-kulia) na wataalam kutoka REA na TANESCO jana. Ujumbe wa REA ulikuwa katika ziara ya kazi.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Patrick Sawala akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius Kalolo na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy (hawapo pichani). Viongozi hao wa REA walimtembelea Mkuu wa Wilaya ofisini kwake jana.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Patrick Sawala (katikati) akionesha vijiji vya wilaya hiyo vilivyofikiwa na umeme na ambavyo havijafikiwa kwa kutumia ramani ya mkoa wa Mtwara kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Wakili Julius Kalolo (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy (kushoto). Viongozi hao wa REA walikuwa katika ziara ya kazi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara, Yusuf Nannila (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius Kalolo (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy (kushoto). Viongozi hao wa REA walikuwa katika ziara ya kazi.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Patrick Sawala (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Wakili Julius Kalolo, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy pamoja na watalaam kutoka REA na TANESCO. Viongozi hao wa REA walikuwa katika ziara ya kazi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius Kalolo (wa pili-kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy (wa tatu-kushoto), wakikagua shimo lililoandaliwa kwa ajili ya kusimika nguzo ya umeme katika kijiji cha Mtunungu, wilayani Masasi, Mkoa wa Mtwara. Viongozi hao wa REA walikuwa katika ziara ya kazi.
Kazi ya kusimika nguzo za umeme ikiendelea katika kijiji cha Mtua, wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi. Taswira hii ilichukuliwa wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius Kalolo na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy (hawapo pichani)
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Patrick Sawala (kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius Kalolo, Kitabu kinachoelezea utamaduni wa eneo hilo. Wakili Kalolo alimtembelea Mkuu wa Wilaya akiwa katika ziara ya kazi.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Patrick Sawala (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy Kitabu kinachoelezea utamaduni wa eneo hilo. Mhandisi Saidy alimtembelea Mkuu wa Wilaya akiwa katika ziara ya kazi.

 Kazi ya kusimika nguzo za umeme ikiendelea katika kijiji cha Mtua, wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius Kalolo (mwenye fulana ya mistari) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy (fulana ya njano)



 Na Veronica Simba, REA  - Mtwara


Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Patrick Sawala ametoa pongezi kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kutokana na kazi nzuri inayofanyika kupeleka umeme vijijini.

Alitoa pongezi hizo ofisini kwake wakati akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo na Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy, waliokuwa katika ziara ya kazi jana wilayani humo.

“Tunawapongeza na kuwashukuru REA kwa kushirikiana na TANESCO. Tunatambua kazi kubwa mnayoifanya  tunafarijika sana,” alisema Kanali Sawala.

Aidha, Mkuu wa Wilaya alipongeza kasi ambayo REA imeanza nayo katika kutekeleza Mradi wa REA Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Pili wilayani humo na kusisitiza kuwa iendelee hivyo ili vijiji vilivyosalia vipate umeme kwa wakati uliopangwa.

Vilevile, alipongeza maelekezo yaliyotolewa na Uongozi wa REA kwa mkandarasi anayetekeleza miradi ya umeme vijijini wilayani humo, kuandaa Mpango Kazi na kuuwasilisha katika ofisi yake, ofisi ya mbunge, diwani na serikali za mitaa akisema kuwa itarahisisha ufuatiliaji wa utendaji kazi hatua kwa hatua.

Akifafanua zaidi, Kanali Sawala alisema kuwa wananchi wanapaswa kufahamu kinachofanyika, namna watakavyonufaika na mradi husika na kwa wakati gani kwani kwa namna hiyo watatoa ushirikiano nzuri katika utekelezaji wake.

Pia, alitoa rai kwa Wakala kutekeleza kwa haraka kazi ya kupeleka umeme katika vijiji vya wilaya hiyo vilivyoko mpakani mwa nchi ili kuwezesha uimarishaji zaidi wa ulinzi na usalama wa nchi.

Katika hatua nyingine, viongozi hao wa REA walimtembelea Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara, Yusuf Nannila na kuzungumza naye kuhusu utekelezaji wa Ilani ya CCM hususan katika sekta ya nishati vijijini.

Mwenyekiti huyo wa CCM alieleza kuwa Uongozi wa Chama unafarijika kuona maelekezo yaliyotolewa katika Ilani kuhusu sekta ya nishati vijijini, yanatekelezwa kwa vitendo.

“Leo tunashuhudia kwamba Ilani yetu haikuwa maneno matupu bali ni matendo kama inavyojidhihirisha sasa,” alisema.

Hata hivyo, Nannila alitoa wito kwa watendaji wa serikali kuendelea kuchapa kazi kwa bidii ili vijiji vyote vifikiwe na umeme ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba, 2022 kama ilivyoelekezwa katika Ilani ya CCM.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mwenyekiti wa Bodi, Wakili Kalolo na Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Saidy, walimhakikishia Mkuu wa Wilaya na Mwenyekiti wa CCM kuwa watatekeleza maagizo yote waliyowapatia.

Walieleza kuwa REA imejipanga kuhakikisha inatekeleza azma ya serikali kufikisha umeme katika vijiji vyote ifikapo mwishoni mwa Desemba, 2022.

Aidha, walieleza kuwa Wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini nchini, wameshajulishwa kuwa hakutakuwa na ongezeko la muda wa kukamilisha miradi hiyo, hivyo wanapaswa wajipange kuhakikisha miradi inakamilika kwa muda uliopangwa.

Wakili Kalolo alimwomba Mwenyekiti wa CCM kufikisha salamu za shukrani kutoka REA kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kuendelea kuwezesha utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini na kwamba REA inaahidi haitamwangusha.

Akifafanua zaidi kuhusu utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili mkoani Mtwara, Mhandisi Saidy alieleza kuwa umelenga kuvifikishia umeme vijiji 402 vilivyosalia.

Mwenyekiti Bodi ya Nishati Vijijini, Wakili Julius Kalolo na Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy wako katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara, Lindi na Pwani.

Wednesday, November 24, 2021

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI KASEKENYA AWAPONGEZA TANRODS SINGIDA UJENZI WA DARAJA LA MSINGI

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya  (katikati) akizungumza na wataalamu wakati akikagua Daraja la Msingi lenye thamani ya Sh.Bilioni 10.9 linalojengwa wilayani Mkalama mkoani Singida wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja aliyoifanya hivi karibuni.
Meneja wa Wakala wa Barabara  Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Singida Mhandisi Matari Masige (kulia) akimuelekeza jambo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya

Tuesday, November 23, 2021

WANANCHI NALASI MASHARIKI KUWASHIWA UMEME WA REA

p>

Kazi ya kuchimba mashimo kwa ajili ya kusimika nguzo za umeme ikiendelea katika kijiji cha Likuyu Mandela, wilayani Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma, wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy, jana.

Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa REA Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Pili wilayani Namtumbo (kushoto) akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini Wakili Julius Kalolo (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy (kofia nyeusi), walipokuwa kwenye ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.

WATAALAMU UHIFADHI MISITU WA SERIKALI WATAKIWA KUCHAPA KAZI

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack akizungumza juzi na waandishi wa habari ( hawapo pichani) ambao walikuwepo mkoani humo katika ziara ya kujifunza kuhusu utekelezaji wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu ambayo iliratibiwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu (MJUMITA) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswis (SDC)
Mkutano na waandi wa habari ukiendelea,

Afisa Uhusiano wa TFCG Bettie Luwuge akizungumza kwenye mkutano huo.

Afisa Sera na Majadiliano wa TFCG Elida Fundi  akizungumza kwenye mkutano huo.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack akizungumza na maofisa wa Mashirika ya TFCG na MJUMITA baada ya mkutano na waandishi wa habari. Afisa Uhusiano wa TFCG Bettie Luwuge na Afisa Sera na Majadiliano wa TFCG Elida Fundi.

Picha ya pamoja baada ya mkutano huo.
Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.


Na Dotto Mwaibale,  Lindi.


WATAALAMU wa Uhifadhi misitu Serikalini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii badala ya kuyategemea mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambayo yanafanya kazi hizo kwa mkataba.

Hayo yamesemwa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao walikuwepo mkoani humo katika ziara ya kujifunza kuhusu utekelezaji wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu ambayo iliratibiwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu (MJUMITA) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswis (SDC)

RC Telack alifikia hatua ya kuyasema hayo baada ya maofisa wa mashirika hayo kumuambia wamebakiza mwaka mmoja wa kutoa elimu na kuhamasisha utunzaji wa misitu katika katika mkoa huo baada ya mkataba wao kukaribia kumalizika.

"Nichukue nafasi hii kuwataka wahifadhi wa misitu wa serikali kufanya kazi kwa bidii kwani serikali iliwasomesha kwa ajili ya shughuli hiyo na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kila mwaka kinatoa wahitimu wa uhifadhi wa wanyamapori na misitu hivyo katika suala hilo hakuna wasiwasi" alisema.

Alisema wahitimu hao mafunzo yao wakiwa shuleni ni mepesi na laini kwani naye amesoma katika chuo hicho na sasa kazini kwao ni mkoani Lindi hivyo licha ya mashirika hayo kumaliza muda wao wataalamu hao waliosomeshwa na serikali watafanya kazi hiyo.

Alisema kazi ya wahifadhi hao ni kuisaidia Serikali na kuwa misitu ikiachwa ipotee kilimo kinachosemwa ndio uti wa mgongo hakitakuwepo kwani misitu ni chanzo cha mvua na kuwa  mikoa yenye misitu mingi ndiyo yenye mvua za kutosha. 

Alisema kwa Mkoa wa Lindi ambao bado una misitu mimgi ya kutosha wenye wajibu wa kuhakikisha inatunzwa ni wataalamu hao na akawataka waamuke sasa na kuelekeza nguvu zao kwenye suala zima la uhifadhi wa misitu.

Aidha Telack aliyaomba mashirika hayo kwa muda huo wa mwaka mmoja uliobaki kutoa elimu hiyo ya uhifadhi wa misitu waitumie mkoani humo kwani Tanzania ni yetu wote hivyo kila mtu anajukumu la kuilinda. 

Alisema yeye kama kiongozi mkuu wa mkoa kwa kushirikiana na watendaji wake watasimamia suala zima la uhifadhi wa misitu ili kumsaidi Rais Samia Suluhu Hassan na hatakubali kuona uhalibifu wa misitu ukifanyika.

Mashirika hayo yanatekeleza mradi huo katika Wilaya za Kilosa, Mvomero, Morogoro, Liwale, Nachingwea, Kilolo na Ruangwa katika Kijiji cha Malolo.

MBUNGE MATTEMBE SINGIDA AENDELEA KUGAWA MBEGU ZA ALIZETI KWA MAKUNDI MBALIMBALI YA WANAWAKE

Mbunge wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Aysharose Mattembe (katikati) akigawa mbegu bora za alizeti kwa Vikundi mbalimbali vya Wanawake mkoani Singida jana, ikiwa ni mwendelezo wa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhamasisha kilimo cha zao hilo.

Mbunge wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Aysharose Mattembe (kuliai) akigawa mbegu bora za alizeti kwa Vikundi mbalimbali vya Wanawake mkoani Singida jana..
Zoezi la ugawaji mbegu likiendelea.
Mbegu zikipokelewa.
Vikundi mbalimbali vya akimama Wilaya ya Singida mjini wakionyesha mifuko ya mbegu bora za alizeti muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Mbunge Mattembe.
Katibu wa CCM Wilaya ya Singida Mjini Shaban Karage akikabidhi baadhi ya mifuko ya mbegu hizo kwa wanawake wa wilaya hiyo kwa niaba ya Mbunge.
Baadhi ya Wanawake wakitazama mbegu hizo wakati wa zoezi la makabidhiano.

Mbunge Mattembe akizungumza kwenye tukio hilo, kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Shee.

Zoezi likiendelea.
Mbunge akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanawake wa Mkoa wa Singida 
Ugawaji wa mbegu ukiendelea.
Mbunge akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanawake wa Mkoa wa Singida. 
 


Na Godwin Myovela, Singida


MBUNGE wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe amekabidhi msaada wa mbegu bora za kisasa za alizeti zaidi ya Tani 10 zenye thamani ya shilingi milioni 35 kwa Vikundi vya Wanawake wa mkoa wa Singida-ikiwa ni mwendelezo wa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuongeza tija ya kilimo cha zao hilo.

Mattembe akiwa kwenye ziara ya kuhamasisha tija ya kilimo hicho sambamba na kugawa mbegu hizo kwa nyakati tofauti ndani ya wilaya za Mkalama, Manyoni, Iramba, Ikungi, Wilaya ya Singida na Singida Manispaa, pia aliwataka wanawake kutobweteka na badala yake kila mmoja kujipanga ipasavyo kwa kuhakikisha anatumia fursa mbalimbali zitokanazo na kilimo katika kujikwamua na umasikini.

Zoezi hilo liliambatana na mafunzo kutoka kwa wataalamu mbalimbali wa kilimo juu ya namna bora ya kumwezesha mkulima kuongeza tija na uzalishaji wa zao la alizeti katika muktadha chanya wa kuongeza kipato cha mtu mmoja, sanjari na kuchagiza ongezeko la uzalishaji wa mafuta ya kula nchini kwa azma ya kupunguza gharama kubwa za takribani bilioni 474 ambazo hutumiwa na serikali kila mwaka kuagiza mafuta hayo kutoka nje.

Wakizungumza baada ya tukio hilo, baadhi ya wanawake mbali ya kumpongeza Mattembe, waliahidi kutumia mafunzo na mbegu hizo katika kuhakikisha wanajiimarisha kiuchumi-kwa mantiki ya matumizi ya kila kilo 6 za mbegu zilizotolewa na Mbunge huyo kwa kila mwanamke sasa ni dhahiri baada ya mavuno zinakwenda kuzalisha zaidi ya gunia 36 ambazo ni wastani wa fedha zaidi ya milioni 2.5.

“Kilo mbili za mbegu hiyo ya alizeti kama zitapandwa kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo huzalisha kati ya gunia 12 hadi 16, hivyo kwa idadi ya kilo 6 zilizotolewa na Mattembe kwa kila mmoja wetu zinakwenda kuzalisha magunia 36 ambayo bei ya soko kwa sasa ni zaidi ya milioni mbili,” alisema mmoja wa wanawake hao ambaye pia ni Diwani Viti Maalum Singida Mjini, Margaret Malecela.

Mjumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake Wilaya ya Singida Mjini na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo, Shaban Karage, alisema mbali ya msaada wa mbegu hizo katika nyanja ya kilimo, kumekuwa na jitihada za makusudi za Mbunge Matembe katika kuleta hamasa na  ustawi kwenye maeneo mengine mbalimbali ya kijamii ikiwemo afya, elimu na ujasiriamali.

Karage alisema ameridhishwa na Mattembe na wabunge wenzake wa mkoa wa Singida kwa namna wanavyotekeleza kwa vitendo maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan na Ilani ya CCM juu ya dhamira na takwa la uwajibikaji wa viongozi kwa masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo na ustawi wa watu.

“Ni mattembe huyu huyu aliyetupatia gari la wagonjwa ‘ambulance,’ mashuka na vitanda vya wagojwa,  pia ni Mattembe huyu huyu aliyetupatia mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na vifaa vya TEHAMA kwenye maeneo mbalimbali, ikiwemo pale shule ya Sekondari Mwanamwema na mengine mengi. Leo sote tunashuhudia namna alivyojitoa kwa dhati kwenye eneo la kilimo,tunamshukuru sana kwa moyo wake,” alisema Karage.