Sunday, September 25, 2022

REA YAWANOA WABUNGE KUHUSU MRADI WA KUSAMBAZA NISHATI SAFI YA KUPIKIA VIJIJINI

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azan Zungu, akifungua Semina ya kuwajengea uwezo Wabunge Wanawake kuhusu Mradi wa kusambaza nishati safi na salama ya kupikia vijijini, iliyofanyika Dodoma, Septemba 22, 2022. Semina hiyo iliandaliwa na REA.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Dunstan Kitandula, akizungumza wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo Wabunge Wanawake kuhusu Mradi wa kusambaza nishati safi na salama ya kupikia vijijini, iliyofanyika Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy akizungumza wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo Wabunge Wanawake kuhusu Mradi wa kusambaza nishati safi na salama ya kupikia vijijini, iliyofanyika Dodoma.
Mgeni Rasmi katika Semina ya kuwajengea uwezo Wabunge Wanawake kuhusu Mradi wa kusambaza nishati safi na salama ya kupikia vijijini, ambaye ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Azzan Zungu (katikati) akifuatilia Mada zilizokuwa zikiwasilishwa. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Dunstan Kitandula, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy, Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG) Mhe. Shally Raymond na Mwakilishi kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Edson Ngabo. Semina hiyo iliandaliwa na REA.
Sehemu ya Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia Semina ya kuwajengea uwezo Wabunge Wanawake kuhusu Mradi wa kusambaza nishati safi na salama ya kupikia vijijini, iliyofanyika Dodoma.
Semina ikiendelea.
Semina ikiendelea.
Sehemu ya Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia Semina ya kuwajengea uwezo Wabunge Wanawake kuhusu Mradi wa kusambaza nishati safi na salama ya kupikia vijijini, iliyofanyika Dodoma.

Mkurugenzi wa Uendelezaji Masoko na Teknolojia kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Advera Mwijage akiwasilisha Mada wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo Wabunge Wanawake kuhusu Mradi wa kusambaza nishati safi na salama ya kupikia vijijini, iliyofanyika Dodoma, Septemba 22, 2022. Semina hiyo iliandaliwa na REA.

Sehemu ya Wajumbe wa Menejimenti na Wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakifuatilia Semina ya kuwajengea uwezo Wabunge Wanawake kuhusu Mradi wa kusambaza nishati safi na salama ya kupikia vijijini, iliyofanyika Dodoma.


Na Issa Sabuni - REA

 

WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) umeendesha Semina ya kuwajengea uwezo Wabunge Wanawake kuhusu Mradi wa kusambaza nishati safi na salama ya kupikia vijijini.

Akifungua Semina hiyo iliyofanyika Dodoma, Septemba 22 mwaka huu, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azan Zungu aliwahamasisha Washiriki kuwa mfano kwa wananchi katika maeneo yao, namna gani wanaweza kupikia nishati ambayo ni salama.

“Tuzingatie na tusaidiane kupeleka nishati mbadala kwenye maeneo yetu na hasa sisi wabunge, tuanze kuonesha mfano.”

Aidha, alizungumzia suala la uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa ambapo alisema pamoja na mambo mengine, umeathiri Mlima Kilimanjaro ambacho ni kivutio cha utalii nchini.

Akifafanua, alisema utafiti unaonesha kuwa hewa ya moto ambayo hupaswa kupozwa na miti hususan katika mikoa ya Pwani, Dar es Salaam na Tanga, inakwenda kwenye Mlima Kilimanjaro jambo linalochangia kupoteza barafu yake.

Naibu Spika alisisitiza kuwa Wabunge Wanawake wana nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko chanya kwenye eneo la nishati safi na salama na kuokoa afya za watumiaji wa kuni na mkaa hususan akina mama na watoto.

“Tumeambiwa na Wataalam kuwa Mama akipika kwenye moshi kwa saa moja ni sawa na kuvuta sigara mia tatu. Kwa hali hii atakuwa ameathirika kwa kiwango kikubwa na kwa wenye ujauzito itamuathiri hata mtoto aliye tumboni.”

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba, akizungumza kupitia video fupi iliyorekodiwa na kuchezwa katika Semina hiyo, aliomba ushirikiano kutoka kwa Wabunge Wanawake katika kufanikisha mkakati huo maalum unaotekelezwa na Wizara kupitia REA, ili kuleta mapinduzi katika nishati ya kupikia hususan vijijini.

Waziri Makamba ambaye hakuweza kushiriki katika Semina husika kutokana na majukumu mengine ya kitaifa, alibainisha kupitia video hiyo fupi kuwa athari za matumizi ya kuni na mkaa ni kubwa hasa kwa akina mama na watoto lakini hazisemwi sana kwani kundi linaloathirika zaidi halina sauti.

Akitoa takwimu, alisema kuwa utafiti unaonesha takribani watu 33,000 hupoteza maisha kila mwaka hapa nchini kutokana na kuvuta hewa ya ukaa inayosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa katika kupikia.

Alisema kuwa kutokana na madhara makubwa yanayosababishwa na matumizi ya nishati zisizo salama, Wizara kupitia REA imeamua kuweka juhudi za makusudi kuhakikisha inawakomboa akina mama hususan waishio vijijini kutoka katika madhara ya kiafya pamoja na kupunguza athari kwa mazingira.

Akizungumza katika Semina hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Dunstan Kitandula, alipongeza kazi kubwa iliyofanywa na REA katika kupeleka nishati ya umeme vijijini na kuongeza kuwa kazi ya kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala kwa kupikia vijijini ni kubwa zaidi hivyo Wakala unapaswa kuungwa mkono katika utekelezaji wake.

“Kwahiyo Wabunge wenzangu, tulichukue jambo hili, tulisemee kwa nguvu kubwa kwa umoja wetu ili tuweze kupata matokeo chanya ambayo wote tunayatarajia,” alisisitiza.

Mwakilishi wa Wizara ya Nishati katika Semina hiyo, Mhandisi Edson Ngabo alisema kuwa katika kuhakikisha upatikanaji wa nishati bora ya kupikia, Serikali imeanza utekelezaji awamu kwa awamu ambapo katika Mwaka huu wa Fedha (2022/23) Shilingi Bilioni Tano zimetengwa kwa ajili ya kusambaza gesi asilia kwa ajili ya kupikia katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.

Awali, akitoa salamu za Ukaribisho, Mwenyeji wa Semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy, alisema kuwa, kwa kutambua kwamba kuna madhara ya kuendelea kutumia nishati isiyo salama, Serikali imekuja na Mpango Maalum wa kuwezesha upatikanaji wa nishati bora ya kupikia vijijini.

Alieleza zaidi kuwa, katika Mpango huo, kuna maeneo kadhaa ya kipaumbele ikiwemo kujenga ufahamu, hasa kwa wananchi kuhusu upatikanaji na kuhamasisha matumizi ya bidhaa na teknolojia za nishati bora vijijini.

Mkurugenzi Mkuu alifafanua kuwa, baadhi ya watu hawafahamu kama kuna majiko hivi sasa yanayotumia kiwango cha nishati inayotumika kupikia mlo mmoja na kutumia kiwango kilekile kupikia mlo zaidi ya mmoja.”

“Kwahiyo, tutawajengea ufahamu kuhusu upatikanaji wake na kuhamasisha pia matumizi yake, tukiwalenga zaidi wananchi wa vijijini,” alibainisha Mhandisi Saidy.

Akiwasilisha Mada katika Semina hiyo, Mkurugenzi wa Uendelezaji Masoko na Teknolojia kutoka REA, Mhandisi Advera Mwijage, alitaja baadhi ya madhara yatokanayo na matumizi ya nishati isiyo bora na salama kwa kupikia kuwa ni pamoja na kupoteza nguvu kazi ya Taifa.

Mhandisi Mwijage alibainisha kuwa vifo vitokanavyo na uvutaji wa hewa ya ukaa majumbani ni asilimia 8.5.

Semina hiyo kwa Wabunge Wanawake ilihudhuriwa pia na Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge, Wabunge Vinara, Menejimenti ya REA, Mwakilishi kutoka TPDC pamoja na Wadau mbalimbali wanaojishughulisha na uendelezaji wa teknolojia mbadala za nishati ya kupikia.

 

Tuesday, September 20, 2022

TANZANIA YAJIPANGA KULINDA MAJI NA MAZINGIRA UKANDA WA MAGHARIBI MWA BAHARI YA HINDI

  Mkuu wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya,   Reuben Mfune akifungua mafunzo hayo ya kimataifa ya kujengea uwezo wataalamu wa Tathimini ya Maji kwa  Mazingira, Pembeni yake ni Mkuu wa Mradi wa wa Utafiti wa  EFLOWS Prof. Japhet Kashaigili kutoka SUA.
 Mtafiti Mkuu wa Mradi huo kutoka (SUA) Prof. Japhet Kashaigili akieleza malengo ya Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wataalam wa masuala ya Maji kwa Mazingira na tathimini yake kutoka nchi nzima na nchi zingine 11 za magharibi mwa bahari ya Hindi.
Meneja wa Programu ya Mazingira ya Bahari (WIOMSA) ambao ndio wafadhili wa mafunzo hayo, Dk Mathias Igulu akitoa salamu za Taasisi yao umuhimu wa mafunzo hayo kwa nchi wanachama.
Mratibu wa Mradi wa Tathimini ya maji kwa mazingira EFLOWS Dk. Winfred Mbungu akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi mara baada ya kufungua mafunzo hayo ya siku tano.
  Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo hayo kutoka Taasisi mbalimbali nchi nzima ambazo zinahusiana na Sekta ya Maji,Mazingira,Misitu na Kilimo.
 Washiriki wa ma mafunzo hayo wakifuatilia hotuba za ufunguzi na uwasilishwaji wa mada mbalimbali kwenye mkutano huo Wilayani Mbarali.
Mafunzo yakiendelea.
 Washiriki wa ma mafunzo hayo wakifuatilia hotuba za ufunguzi na uwasilishwaji wa mada mbalimbali kwenye mkutano huo Wilayani Mbarali.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
 Washiriki wa ma mafunzo hayo wakifuatilia hotuba za ufunguzi na uwasilishwaji wa mada mbalimbali kwenye mkutano huo Wilayani Mbarali.
Mafunzo yakiendelea.


Na Amina Hezron, Mbarali
 

CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia ufadhili wa Taasisi inayojishughulisha na tafiti za utunzaji wa Bahari (WIOMSA) wameendesha mafunzo ya Kimataifa ya kuwajengea uwezo Wanasayansi, Mameneja na wadau wengine namna ya kuendesha na kufanya tathimini ya Maji kwa Mazingira katika ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi.

Akifungua mafunzo hayo jana Septemba 19, 2022 Wilayani Mbarali mkoani Mbeya, Mkuu wa Wilaya hiyo Reuben Mfune amewataka wadau waliopata mafunzo hayo kuhakikisha wanakwenda kuyafanyia kazi na kuwafundisha wengine kwenye ofisi wanazotoka ili kutimiza malengo ya mafunzo hayo ambayo yanataka kuwepo na utiririkaji wa maji safi na salama kwenye mito kuelekea baharini mwaka mzima.

 “Wale ambao wako ukanda wa juu ya mto unakoanzia wanatakiwa kujua fika shughuli za uharibifu wanazozifanya kule ndizo zinazoleta athari kwenye mabwawa ambayo yanajaa tope ambalo linakwenda mpaka Baharini na kuaathiri viumbe vilivyomo katika Mito, Maziwa na Bahari”, alisema Mfune.

Mfune amewapongeza SUA na WIOMSA kwa kuandaa mafunzo hayo  kwakuwa yanaendana na kazi inayoendelea ya kurejesha afya ya Mito na kupunguza madhara yanayotokana na uchafuzi wa Mazingira katika mito, kwani ni jambo jema kufanyika na litakuwa msaada mkubwa kwa Taifa.

Aidha alisema zipo shughuli nyingi za kibinadamu zinazofanywa kwenye vyanzo vya maji na kandokando ya mito kama vile ukataji miti hivyo,ufugaji usionzingatia ukubwa wa eneo hivyo amewataka Wananchi kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na serikali katika kusimamia sheria na kanuni zilizowekwa ili kuhifadhi mito na mazingira kwa faida ya kizazi hiki na kijacho.

“Maji haya yana umuhimu kwa taifa zima kama bwawa la Nyerere ambalo linajengwa kwa gharama kubwa. Iwapo litashindwa kufanya kazi kutokana na ukosefu wa maji maana yake serikali itakuwa imepoteza fedha hizo bure, lakini pia tuna bwawa la umeme la Mtera na  Kidatu haya yote yasipoweza kufanya kazi tutakuwa tunapunguza uwezo wa kuwa na Tanzania ya viwanda”, alisema Mfune.

Aidha amewataka wadau wengine kuendelea kujitokeza kusadia jitihada za Serikali na wadau waliopo sasa ili kuhakikisha Mito inaendelea kutiririka mwaka mzima na hivyo kuwataka Wananchi kuheshimu Sheria zilizowekwa kwakuwa zipo kwa manufaa ya watanzania wote.

Akizungumzia mafunzo hayo Mtafiti Mkuu wa Mradi huo kutoka (SUA) Prof. Japhet Kashaigili alisema lengo kubwa la mafunzo hayo ni kujenga Wataalamu na utaalamu wa kuweza kufanya tathimini ya maji kwa mazingira ili kusaidia wanapofanya maamuzi katika kugawana maji iwe kwa ajili ya maendeleo endelevu.

“Ni mafunzo ya kujenga uwezo ambayo yana vitendo ndani yake. wataona shughuLi zinazofanyika kama sehemu ya kuhifadhi mazingira na kilichopelekea shughuLi hizo zifanyike pamoja na sababu za msingi za kuwezesha kwanini hiyo tathimini ya maji kwa mazingira ifanyike na shughuli gani zifanyike kwenye maeneo hayo. Hivyo mahari kwingine watafanya wao wenyewe kama sehemu ya mazoezi”, alisema Prof. Kashaigili.

Prof. Kashaigili amefafanua kuwa tathimini hiyo ya maji kwa mazingira itawezesha kuhusanisha madhara yanayotokana na shughuli mbalimbali zinazozifanywa na kwa kiasi gani zinapelekea kuathiri  Ukanda wote wa Bahari  ili kuweza kujua chanzo cha tatizo, hatua  tatizo lilipofikia, madhara na namna ya kutatua.

“Hii itasaidia nchi kutekeleza Sera ya maji pamoja na Sheria ya maji ya mwaka 2009 ambayo imeainisha katika kugawana maji kwa vipaumbele ni kwa ajili ya matumizi ya Binadamu, Mazingira na kwa shughuli nyingine, hivyo maji kwaajili ya mazingira ilikuwa ni sehemu ambayo haina utaalamu na hakukuwa na jinsi ya kufanya hivyo bila kujenga utaalamu sasa utaalamu upo hivyo ni lazima tujenge sasa Wataalamu wengi “, alisema Prof. Kashaigili.

Meneja wa Programu ya Mazingira ya Bahari (WIOMSA) ambao ndio wafadhili wa mafunzo hayo, Dk. Mathias Igulu amesema kuwa kuna mahusiano makubwa kati ya Bahari na Mito, lakini jambo hilo halijaongelewa sana ndio maana WIOMSA wameona ni vyema kuanzisha mjadala na kuwaleta pamoja Wanasayansi na wadau wengine  kwa maslahi mapana ya uhifadhi wa Bahari, Mito na Mazingira.

“Kwa kushirikiana na chuo chetu kikubwa cha SUA ambacho wote tunajua wana Wataalamu wabobevu kwenye maswala ya Sayansi za Kilimo, Maji na Mazingira, Ufugaji wa Samaki na Sayansi zingine zinazoendana na hizo tumeona ni muda muafaka kushirikiana nao kuwaleta pamoja wadau muhimu nchini na nje ya Tanzania kwa kuwa wanao uwezo mkubwa wa kusimamia” alisema Dk. Igulu.

Ameongeza kuwa maswala ya Bahari na mito ni mambo yanayogusa maisha ya watu kila siku na ni swala la kiusalama pia maana jamii inahitaji kutumia maji katika kuzalisha, hivyo ni jambo muhimu na lazima liangaliwe kwa umakini kwa faida ya nchi zote zinazoguswa na mambo haya.

Alisema, wataalamu wa mambo hayo ya tathimini ya maji kwa mazingira ni wachache sana nchini na hii ni kutokana na kutokuwa na chuo kinachotoa Wataalamu mahususi kwa fani hiyo na hivyo amekiomba Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kuona umuhimu wa kuanzisha mitaala ya masuala ya tathimini ya maji kwa mazingira kwakuwa wanao uwezo na Wataalamu wabobevu.

Akizungumza mmoja ya washiriki wa mafunzo hayo, Mtafiti Msaidizi kutoka Taasisi ya Utafiti ya Uvuvi (TAFIRI) Wendo Lukwambe alisema mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwao kwakuwa yatawasaidia kujua jinsi mtiririko wa maji unavyoenda na namna ya kutunza maji kwa mazingira kwakuwa isipofanyika hivyo itasababisha kuathirika kwa maji hayo.

“Tunajitahidi sana tujue mawazo na teknolojia za mtiririko wa maji na mazingira kwasababu zitatusaidia hata katika mambo ya samaki kwenye uvuvi. Kuna baadhi ya samaki huwa wanapotea kutokana na mazingira jinsi yalivyobadilika ukija kuangalia chanzo utakuta kinatoka kwenye Maji na Mazingira, hivyo kama tukitunza chanzo cha Maji vizuri kinaweza kutusaidia hata sisi kwenye Bahari na Samaki pia kwa kuepusha vifo na kutoweka kwa aina za samaki”, alisema Lukwamba.

Mafunzo hayo ya siku tano yamewahusisha washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Utafiti katika sekta za Maji, Mazingira, Misitu  na washiriki wengine kutoka nchi za ukanda wa magharibi mwa Bahari ya Hindi ikiwemo  Afrika Kusini, Kenya, Mauritius, Msumbiji, Visiwa vya Shelisheli, Somalia, , Visiwa vya  Comoro, Madagasca na Visiwa vya Reunion ambao wameshiriki kwa njia ya Mtandao (Zoom).

 

Monday, September 19, 2022

MFUKO WA MAENDELEO WA MUFTI WAZINDULIWA RASMI SINGIDA


Mufti  wa Tanzania Sheikh Dk. Abubakar Zubeir Ally Mbwana (katikati) akizungumza wakati akiongoza maelfu ya Waislam mkoani Singida katika hafla ya kuzindua Mfuko wa Maendeleo wa Mufti katikahafla iliyofanyika leo Septemba 19, 2022 Stendi ya zamani mjini haaapa. Kushoto ni Katibu wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) Nuhu Jabir Mruma na kulia ni Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issah Nassoro Issah.
Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issah Nassoro Issah. akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu akizungumza kwenye uzinduzi wa mfuko huo.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akizungumza.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mfuko huo.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo wa Mufti akizungumzia umuhimu wa mfuko huo na jinsi utakavyokuwa ukifanya kazi.

Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Bakwata Taifa, Sheikh Ally Hamisi Ngorike akizungumza.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Bakwata Taifa, Sheikh Hamis Mataka akizungumza.
Dua ikifanyika.
Bi. Salha Amir mkazi wa Iramba, akimkabidhi Mufti Zubeir taarifa ya Hospitali yake aliyoikabidhi kwa Mfuko huo wa Maendeleo wa Mufti.
Mufti Zubeir akionesha taarifa hiyo.

 Mjumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida kutoka Kata ya Ihanja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Bakwata Mkoa wa Singida, Ahmed Misanga akimkabidhi Mufti Zubeir Sh. 300,000 kwa ajili ya kuchangia mfuko huo.
Sehemu ya Taswira ya uzinduzi huo.
Mufti Zubeir akiagana na viongozi mbalimbali baada ya kuzindua mfuko huo.

Sunday, September 18, 2022

MUFTI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA OFISI YA BAKWATA MKOA WA SINGIDA

Mufti wa  Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir (wa pili kushoto) akiongoza kuomba dua baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Baraza Kuu la Waislam  Mkoa wa Singida (BAKWATA) inayojengwa katika msikiti wa Masjid Taqwa mjini hapa katika hafla iliyofanyika leo Septemba 18, 2022. Kutoka kulia Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Sheikh Burhan Mlau, Sheikh wa Mkoa wa Singida Issah Nassoro na Rais wa Taasisi wa Majmaul Ahbaab, Sharif Muhamad Bin Said Al-Beidh.

Mufti wa  Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir (kushoto) akiwa na viongoziwengine katika hafla hiyo. Kutoka kulia ni  Sheikh wa Mkoa wa Singida Issah Nassoro na Rais wa Taasisi wa Majmaul Ahbaab, Sharif Muhamad Bin Said Al-Beidh.
Mufti wa  Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir akizungumza na Waislam wakati alipotembelea   Taasisi wa Majmaul Ahbaab..
Mufti wa  Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir akionesha Tuzo ya heshima baada ya kutunukiwa  na Rais wa Taasisi wa Majmaul Ahbaab, Sharif Muhamad Bin Said Al-Beidh (kushoto).

Vijana wa Skauti wakiwa katika ziara hiyo ya Mufti.
Wanawake wa kiislam wakimsikiliza Mufti wa  Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir wakati alipotembelea Taasisi ya Majmaul Ahbaab.
Hafla ikiendelea.
Vijana wa Qaswida wakiwa nadhifu wakati wa hafla hiyo .
...............................................

Dotto Mwaibale, na Philemon Mazalla-Singida

MUFTI wa  Tanzania sheikh Dk.Abubakar Zubeir leo Septemba 18, 2022 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Baraza Kuu la Waislam  Mkoa wa Singida (BAKWATA) inayojengwa katika msikiti wa Masjid Taqwa mjini hapa.

Azungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe hilo la msingi alisema amefurahishwa na ridhishwa na hatua iliyochukuliwa ya kuanzisha ujenzi huo kwani hayo ndiyo maendeleo yanayotakiwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)

"Mimi na msafara wangu masheikh wote waliofika katika kutekeleza mambo yetu hapa Singida tumefurahishwa sana na jambo hili na haya ndio mambo yetu ya bakwata tunayoyazungumza sana kuhusu maendeleo" alisema Mufti Zuberi.

Mufti Zuberi alisema changamoto zote zilizotolewa katika hafla hiyo alisema baraza na viongozi wapo hivyo wanaona namna ya kuzishughulikia na kuwekana sawa kwani kila jambo lina taratibu zake namna ya kuzitatua.

Aidha Mufti Zuberi alisema jambolililokubwa ni kwa waislam mkoani hapa kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu awawezeshekufanya mambo yao vizuri na kuondosha magomvi baina yao.

Taarifa ya ujenzi huo ikitolewa mbele ya Mufti ilieleza kuwa Mwezi Marchi 2022 Sheikh wa Mkoa wa Singida na Baraza la Masheikh waliunda kamati maalumu ili kuongeza nguvu ya ufuatiliaji wa eneo la ujenzi  na kufanikiwa kuipata ndani ya Masjid Taqwa kwa idhini ya uongozi wa msikiti huo.

Ujenzi wa ofisi hiyo hivi sasa umefikia hatua ya linta kwa gharama ya Sh.8.2 mILIONI na kaziiliyobakia ni upauaji na umaliziaji ambapo fedha zilizokadiriwa kumalizia kazi hiyo ni Sh.14 Milioni.

 Mufti akiwa njiani kwenda Singida mjini alisimama  wilayani Ikungi na kuomba dua kwenye eneo ambalo waislam wa wilaya hiyo wanatarajia kujenga Kituo cha afya na baada ya uwekaji wa jiwe hilo la msingi la ofisi ya Bakwata alikwenda kutembelea  Taasisi ya Majmaul Ahbaab iliyopo eneo la Unyakhindi Manispaaya Singida ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanawake wa kiislam na kutunukiwa Tuzo ya heshima ya Kimataifa na Rais wa Taasisi hiyo Sharif Muhamad Bin Said Al-Beidh.

Saturday, September 17, 2022

PROFESA NDALICHAKO AKAGUA MRADI WA VIJANA, KITALU NYUMBA MANISPAA YA SINGIDA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako (wa pili kulia) akipata maelezo leo Septemba 17, 2022 kutoka kwa Kiongozi wa Wanufaika wa mradi wa Kitalu Nyumba, Emmaculatha Nkumbi (katikati) wakati wa ziara yake ya siku moja ya kukagua mradi huo wa kilimo  cha mbogamboga na matunda wenye thamani ya Sh. 30 Milioni unaotekelezwa Manispaa ya Singida.Kutoka kushoto ni mnufaika wa mradi huo,  David Nyitika, Madania Juma na Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Singida, Ally Mwendo.
Wanufaika wa mradi huo Madania Juma na David Nyitika (kulia) wakiwajibika katika Kitalu Nyumba.

Friday, September 16, 2022

MAAFISA AFYA SINGIDA WAPONGEZWA KWA KUTEKELEZA KAMPENI YA USAFI WA MAZINGIRA

 Mganga Mkuu Mkoa wa  Singida Dk.Victoria Ludovick. akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida na Maafisa Afya kutoka halmashauri zote za wilaya mkoani hapa  wakati wa kikao kazi kilichofanyika leo Septemba 16, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Kushoto ni Afisa Afya Mkoa wa Singida, Mgeta Sebastian na kulia ni Afisa Afya Mazingira na Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Afya Mkoa wa Singida, Evaristo Mwinuka.
Afisa Afya Mkoa wa Singida, Mgeta Sebastian akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu wa Afya Mkoa wa Singida, Vedastus Kiwango akizungumza kwenye kikao hicho.
Mratibu wa Malaria Mkoa wa Singida, Dk. Abdallah Balla akizungumza kwenye kikao hicho.
 Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Singida, Habibu Mwinory akisisitiza jambo kwenye kikao hicho.
Maafisa Afya wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Maafisa Afya wakiwa kwenye kikao hicho.
Taswira ya kikao hicho.
Afisa Afya wa Wilaya ya Manyoni  Seif Swedi akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Afisa Afya Wilaya ya Iramba, Salome Mwaipopo akizungumza kwenye kikao hicho.
Afisa Afya Singida DC, Hilda Masele, akizungumza kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.

 

Na Dotto Mwaibale, Singida.


KATIBU Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko amewapongeza Maafisa Afya mkoani hapa kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutekeleza kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira katika maeneo yao.

Mwaluko,ametoa pongezi hizo leo Septemba 16, 2022 wakati wa kikao kazi cha Maafisa Afya kutoka halmashauri za mkoa wa Singida katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mganga Mkuu wa Mkoa wa  Singida Dk.Victorina Ludovick.

Mnafanya kazi nzuri ya kutekeleza kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira lakini lazima mhakikishe  fedha inayotolewa na serikali matokeo yake yanaonekana na si vinginevyo” alisema Mwaluko.

Aliongeza kuwa Wakurugenzi wa Halmashauri,Waganga Wakuu, Maafisa Afya na Watendaji wa vijiji na kata wasimamie ili kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo bora.

Alisema taarifa zilizopo hadi 31 Julai, 2022 kaya zenye vyoo katika Mkoa wa Singida ni asilimia 99.2 na zisizokuwa na vyoo ni asilimia 0.8, zenye vyoo bora ni asilimia 62.1 kutoka asilimia 27.6 mwaka 2015.

"Mimi kama Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, sitavumilia kuona magonjwa ya aibu kama vile kipindupindu yakitokea katika mkoa wangu hivyo mjipange katika hili," alisema.

Aidha, alisema Maafisa Afya watambue kuwa wao kama wasimamizi na wafuatiliaji Wakuu wa shughuli za chanjo, ukaguzi wa dawa, ukaguzi wa vyakula na ukaguzi wa vituo vya kutolea huduma za Afya mashuleni na taasisi zote waongeze bidii kusimamia hayo.

Alisema serikali ya awamu ya sita inathamini sana suala la usafi wa mazingira kwani ndio mhimili mkubwa wa Afya ya Watanzania na ukuaji wa uchumi.

"Tumieni sheria ya Afya ya Jamii ya mwaka 2009 na kanuni Zake,sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 pamoja na sheria ndogo za miji kuhakikisha maeneo ndani ya Mkoa wa Singida hayachafuliwi hovyo ikiwemo barabara kuu,stendi,masoko,mitaro,maeneo ya wazi,makazi na makaburi," alisema.

Mwaluko alisema maeneo ya masoko na biashara wananchi waweke vyombo vya kuhifadhia taka vyenye ukubwa wa kutosha kulingana na uzalishaji wa taka kwa lengo la kupunguza taka kuzagaa ovyo mitaani.

"Kuna maeneo ambayo tumeona hadi yanarushwa kwenye mitandao, Manispaa (Singida) ndio kioo chetu cha Mkoa wa Singida tuhakikishe usafi unafanyika maeneo yawe safi," alisema.

Alisema yapo baadhi ya magari ya abiria yanasimama maporini na abiria kuchimba dawa (kujisaidia) vichakani jambo ambalo halikubariki hivyo Maafisa Afya wahakikishe wanachukua hatua.

Afisa Afya Mkoa wa Singida, Mgeta Sebastian, alisema maeneo mengi ya mijinj hata yale ambayo wanapita viongozi wakuu ni machafu sana na kwamba wakati sasa umefika kwa Maafisa Afya kuhakikisha wanasimamia ili kuweka mazingira safi.

Sebastian alisema katika suala la usimamizi wa afya atakuwa mkali na kwamba afisa afya asiyetekeleza majukumu yake kama inavyotakiwa atachukuliwa hatua ikiwamo kumripo kwa wakuu wake.

Aidha Sebastan aliwataka maafisa hao kujenga tabia ya kutoa taarifa za mara kwa mara za utendaji kazi wao jambo litakalosaidia ufanisi wa kazi na hakuna sababu ya kusukumana katika jambo hilo.