|
Diwani Winjuka Songelaeli Mkumbo akiwa katika pozi enzi za uhai wake. |
Vijana wa Green Gurd wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iramba mkoani Singida wakiwa wamebeba jeneza lenye Mwili wa Diwani wa Viti Maalum wa Tarafa ya Kinampanda, Winjuka Songelaeli Mkumbo wakati wakiupeleka kwenye ibada ya mazishi iliyofanyika Kijiji cha Simbalugwala Kata ya Mukulu jana. Diwani Winjuka alifariki dunia kwa ajali ya gari Agosti 17, 2022 baada ya Basi la Tanzanite lenye namba za usajili T 916 DNU alilokuwa akisafiria kutoka Singida kwenda Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka Mlima Saranda uliopo Wilaya ya Manyoni na kusababisha vifo vya watu watano na wengine kujeruhiwa.
Marehemu Winjuka Songalaeli Mkumbo enzi za uhai wake.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wakiwa wamejipanga tayari kwa kuelekea ibada ya mazishi ya mwenzao Winjuka Songalieli Mkumbo yaliyofanyika jana Kijiji cha Simbalugwala.
Madiwa hao wakiwa tayari kwa ajili ya ibada hiyo iliyoongozwa na Askofu wa Kanisa la Assemblies of God Singida Kaskazini, Noel Lameck.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Michael Matomora akiongoza msafara wa madiwa kwenda kwenye ibada hiyo.
Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa tayari mbele ya eneo maalum ilipofanyika ibada hiyo.
Mme wa marehemu, Winjuka, John Lyanga akiwa na huzuni kubwa wakati wa ibada hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Mkoa wa Singida, Prisca Maleta anayeishi Manyoni ambaye alishuhudia ajali hiyo akizungumzia tukio hilo
Vijana wa Green Gurd wa CCM wakiwa tayari kwa lolote wakati wa ibada hiyo.
Huzuni wakati wa ibada hiyo.
Mjomba wa marehemu ambaye ni mwanzilishi wa Taasisi ya Ndugu ya Sweden Mzee Amoni Gyunda akifarijiana na baadhi ya ndugu wakati wa ibada hiyo.
Ni huzuni tupu.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea.
Ni huzuni tupu ya kuondokewa na mpendwa wao. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Singida, Diana Chilolo na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Martha Gwau.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, James Mkwega.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iramba, Samuel Ashery wakati wa ibada hiyo.
Ibada ikiendelea.
Ni huzuni tupu katika ibada hiyo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Iramba, Mwalimu Ephrahim Kolimba akiwaekeleza masuala ya itifaki vijana wa Green Gurd wakati wa ibada hiyo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Iramba, Mwalimu Ephrahim Kolimba (kulia) akiwa na Katibu Mwenezi wa CCM wa wilaya hiyo, Abbas Michael wakati wa ibada hiyo.
Chakula kikiwa tayari wakati wa ibada hiyo.
Taswira ya ibada hiyo.
Baadhi ya wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Iramba ambao walikuwa wakiwezeshwa na marehemu Winjuka kupitia Taasisi ya Ndugu ya Sweden wakiwa kwenye ibada hiyo. Watoto zaidi ya 900 walikuwa wakisaidiwa na taasisi hiyo.
Katibu wa Kanisa la T.A.G Singida Kaskazini, Mchungaji Danford Mlumba, akisali wakati akiuombea mwili wa marehemu kabla ya kufanyika ibada hiyo.
Waombolezaji wakiwa wamejipanga foleni wakati mwili wa marehemu ukipelekwa kwenye ibada hiyo.
Mwangalizi wa kanisa hilo , Joel Masinsi akiongoza itifaki za ibada hiyo.
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) wilayani humo, Glory Chubwa akiongoza wimbo maalum katika ibada hiyo.
Ibada ikendelea.
Samson Shila akisoma wasifu wa marehemu.
Katibu wa Kanisa la T.A.G Singida Kaskazini, Mchungaji Danford Mlumba, akizungumza katika ibada hiyo.
Askofu Noel Lameck akiongoza ibada hiyo.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko, akitoa salama za rambirambi za mkoa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Michael Matomola akizungumza katika ibada hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, akizungumza kwenye ibada hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akitoa salamu za rambirambi.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Martha Gwau akitoa salamu za rambirambi.
Mbunge wa Iramba Magharibi na Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk.Mwigulu Nchemba akitoa salamu za rambirambi.
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Boniphace akitoa salamu za rambirambi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah akizungumza kwenye ibada hiyo.
Mjomba wa marehemu Mzee Amon Gyunda ambaye ni mwanzilishi wa Taasisi ya Ndugu ya Sweden akizungumza kwenye ibada hiyo.
Mwanfamilia ya marehemu, Evaline Lyanga, akitoa neno la shukurani.