Tuesday, April 9, 2024

MSD YAKUTANA NA WADAU WAKE KANDA YA IRINGA, RC RUVUMA ATAKA WELEDI SEKTA YA AFYA

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali. Ahmed Abbas Ahmed (kushoto) akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji wa Bohari ya Dawa (MSD), Victor Sungusia wakati wa mkutano mkuu wa MSD na  wadau wake wa Mkoa wa Ruvuma uliofanyika Aprili 8, 2024, 

Na Mwandishi Wetu, Ruvuma

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali. Ahmed Abbas Ahmed, amewataka watumishi wa sekta ya afya Mkoani Ruvuma, kuzingatia weledi na kutoa huduma bora kwa wananchi, ili kuakisi maboresho na uwekezaji mkubwa uliofanywa kwenye sekta ya afya, chini ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita.

Kanali Ahmed amesisitiza kuwa, serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa fedha nyingi kwa ajili ya maboresho na ujenzi wa miundombinu ya afya mathalani majengo, ununuzi wa bidhaa za afya

 na kuwezesha ajira za kutosha,  lengo likiwa kuinua hadhi ya huduma zinazotolewa nchini, hasa zinazomgusa mtanzania wa kawaida.

Kanali Ahmed ametoa rai hiyo hii leo, wakati wa akifungua kikao kazi baina ya MSD Kanda ya Iringa na wadau wake kutoka halmashauri saba za mkoa wa Ruvuma (Madaba Tc, Madaba Dc, Songea MC, Songea DC, Nyasa DC, Mbinga TC na Mbinga DC), kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ruwiko, ulioko Manispaa ya mji wa Songea.

Mkuu huyo wa Mkoa amewakumbusha viongozi hao wa sekta ya afya Mkoani humo, kufanya maoteo yao ya bidhaa za afya kwa usahihi, umakini na kwa wakati ili kuiwezesha Bohari ya Dawa (MSD) kutekeleza majukumu yake ya ugavi wa bidhaa za afya kwa weledi.

Mhe. Ahmed amewataka pia watendaji hao kusimamia ukusanyaji wa mapato, na kutumia vyema vyanzo vyao vingine vya mapato katika kulipa madeni ya MSD, huku akiwakumbusha pia kuhakiki taarifa sahihihi za utunzaji na utoaji wa bidhaa za afya, ili kuepuka upotevu wa bidhaa hizo.

Katika hatua nyigine, Mkuu huyo wa mkoa ameipongeza MSD kwa utendaji wake katika kuboresha hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya, huku akiwapongeza kwa kuitisha mkutano huo wa wadau kwani utasaidia kuboresha mahusiano na mawasiliano.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ugavi na uendeshaji wa MSD Victor Sungusia, amebainisha maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanywa na MSD katika nyanja mbalimbali kupitia majukumu yake makuu ya uzalishaji, ununuzi, utunzaji na usambazaji.

Bw. Sungusia amebainisha jinsi MSD ilivyojizatiti katika utekelezaji wa majukumu yake kupitia mifumo ya kisasa ya kidigitali, ugatuzi wa majukumu ya Kanda, ujenzi wa viwanda mbalimbali vya dawa na vifaa tiba, maboresho ya mfumo wa usambazaji wa bidhaa, upanuzi wa maeneo ya uhifadhi na kuwajengea uwezo watumishi wake.

Naye Meneja wa MSD Kanda ya Iringa Bw. Robert Lugembe akiwakiribisha wajumbe wa kikao hicho, alibainnisha kuongezeka kwa uwezo wa MSD kuwahudumia wateja wake na kukidhi mahitaji, sambamba na maboresho ya upatikanaji wa bidhaa za afya mathalani vifaa tiba, mkoani humo.Meneja wa MSD Kanda ya Iringa Bw. Robert Lugembe akizungumza kwenye mkutano huo.

Wadau wa MSD wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wadau wa MSD wakiwa kwenye mkutano huo.
Picha ya pamoja na viongozi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali. Ahmed Abbas Ahmed  akiwakabidhi vyeti wadau wa MSD kwa kutambua mchango wao.
Picha ya pamoja na viongozi waliohudhuria mkutano huo.
Vyeti vikiendelea kutolewa.
Vyeti vikiendelea kukabidhiwa kwa wadau wa MSD.
Vyeti vikiendelea kukabidhiwa kwa wadau wa MSD.