Sunday, May 2, 2021

RC NCHIMBI AUNGANA NA RAIS SAMIA KUWATIA MOYO WAFANYAKAZI SINGIDA

Wafanyakazi kutoka Vitengo, Idara, Taasisi na Mashirika mbalimbali ya Umma na Binafsi kutoka wilaya zote za Mkoa wa Singida wakiingia kwa maandamano maalumu kwenye uwanjawa Liti,huku wakionesha mabango yenye jumbe mbalimbali zinazohusiana na siku ya wafanyakazi kwa mwaka huu.

Wafanyakazi wakifurahia Mei Day 2021.
Mkurugenzi waHalmashauri ya Ikungi Justice Kijazi akionesha cheti baada ya Halmashauri hiyo kuibuka mshindi kwa nafasi yaMwajiri Bora wa mwaka kupitia sherehe hizo. Kushotoni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.
Mamlaka ya Maji  Safi na Mazingira Singida (SUWASA) wakishiriki sherehe hizo kikamilifu.
Wafanyakazi wakiimba wimbo  wa Mshikamano.

Mkuu  wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia wafanyakazi kupitia sherehe hizo zilizofanyika kwa ngazi ya mkoa.

Katibu wa TUGHE Mkoa waSingida, Ethel Kahuluda akisoma risala iliyo sheheni mafanikio, changamoto na mapendekezo ya wafanyakazi kwa niaba ya wafanyakazi wote wa mkoa.

Wafanyakazi wa Shirikalisilo la kiserikali la Maendeleo mkoani hapa SEMA wakionyesha juzi na stadi zinazotokana na matundayakazi yao, hususani kwenye eneo la karakana.

Sherehe zikiendelea
Sherehe zikiendelea
Mkurugenzi wa Ikungi Justice Kijazi (kushoto) na mmoja wa watendaji wa halmashauri hiyo wakifurahia zawadi mbalimbali walizokabidhiwa.

Wafanyakazi wakifuatilia matukio mbalimbali  kwenyesherehe hizo.

sherehe zikiendelea.
matukio mbalimbali yakiendelea.
Sherehe zikiendelea.
sherehezikiendelea
sherehezikiendelea
Wafanyakazi wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye sherehe hizo.
Zawadi zikitolewa kwa wafanyakazi bora.
Zawadi zikiendelea kutolewa.
Mgeni rasmi wa sherehe hizo akiendelea kukabidhi zawadi kwa washindi.
Zawadi zikiendelea kutolewa.
Zawadi zikiendelea kutolewa.
Kikundi cha Ngoma na Burudani kikitumbuiza.

Maandamano yakiingia uwanjani.

Sehemu ya Itifaki ya Maandamano kuingia uwanjani.


 Singida Manispaa wakishiriki sherehe hizo kikamilifu. 



Godwin Myovela, na Dotto Mwaibale, Singida


MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema tunu, fahari, tuzo na kila aina ya sifa iliyo nayo Tanzania kuanzia Awamu ya Kwanza ya uongozi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mpaka Awamu hii ya Sita chini Rais SamiaSuluhu Hassan, ni matunda ya kazi za wafanyakazi.

Nchimbi alitoa kauli hiyo wakati akihutubia sherehe za siku ya Mei Mosi kimkoa, mkoani hapa juzi, ambazo kwa mwaka huu zimebeba Kauli Mbinu isemayo ‘Maslahi Bora, Mishahara Juu-Kazi Iendelee.’ 

“Jeuri yote tuliyonayo kama taifa, msimamo, kujivunia kwetu, uwezo wa kuthubutu, kasi ya maendeleo na ukuaji wa Tanzania hii kiuchumi ni kwa-sababu ya wafanyakazi,” alisema.

Aliwasihi wafanyakazi kuitazama kizalendo na kuibeba kiuaminifu dhamana hiyo kubwa waliyonayo bila ya manung’uniko wala kubaguana kwa namna yoyote ile, lengo hasa ni kuongeza tija na ufanisi, ili kazi iendelee. 

“Niwaombe sana tunapoadhimisha Mei Mosi hii tukiri kwa umoja na pamoja kwamba popote alipo Rais wetu Samia na sisi wafanyakazi tupo...na tutamuunga mkono. Na katika hili naomba kila mmoja kwa nafasi na dhamana aliyonayo amfanye Rais wetu wa Awamu ya Sita aonekane,” alisisitiza Nchimbi na kuongeza:

Tunataka Mkoa wa Singida uwe ni nyumba ya amani kwa wafanyakazi na wanaofanyiwa kazi…nyumba ya furaha, usalama, na daima tuchape kazi ili kuonesha na kudhihirisha kweli sisi wafanyakazi wa mkoa huu ni watu ambao tunastahili maslahi bora, ili utumishi wa tija uendelee.

Awali akiwasilisha risala ya wafanyakazi mkoani hapa, pamoja na mafanikio kadhaa yaliyofikiwa chini ya Shirikisho la Vyama hivyo (TUCTA), Katibu wa TUGHE Mkoa wa Singida, Ethel Kahuluda, alieleza changamoto kadhaa zinazokwamisha ustawi wa wafanyakazi mahali pa kazi, ikiwemo suala la maslahi duni na kukosekana nyongeza ya mshahara.

Alisema changamoto nyingine ni kucheleweshwa kwa madai ya fedha za likizo, uhamisho, na malimbikizo ya mishahara sambamba na ucheleweshaji wa Pensheni  kwa wastaafu.

“Tunaomba serikali ilipe madeni ya watumishi kwa wakati ili kurudisha imani ya watumishi kwa serikali yao. Na suala hili la uhamishwaji watumishi tunaomba liendane na ulipwaji wa stahiki zao,” alisema Kahuluda.

Aidha, kwa niaba ya wafanyakazi mkoani hapa aliomba mamlaka husika kuzingatia kwa wakati suala la upandishaji wafanyakazi madaraja pamoja na marekebisho yake, sanjari na kupunguza kodi kwenye mishahara ili kuongeza ari ya utendaji.

Zaidi Kahuluda alipendekeza Waajiri wa Sekta Binafsi watoe mikataba ya kudumu, likizo na kima cha chini cha mishahara kizingatiwe kulingana na takwa la sheria No 5 ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004.

Pendekezo lingine lililowasilishwa ni kutaka ‘Mabaraza yaWafanyakazi’ yafanyike kwa wakati na malipo ya posho yatolewe kwa mujibu wa sheria na sio kwa hisani ya wakurugenzi.

Hata hivyo, waliomba pia wafanyakazi wote wanaolipwa kwa mapato ya ndani ‘GF’ walipwe mishahara yao kwa wakati na wawekwe kwenye akiba katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na wapatiwe Bima ya Afya.

“Baadhi ya waajiri hawawasilishi michango ya bima ya afya kwa wakati na hivyo kupelekea waajiriwa kujigharamia ikiwa ni sawa na kulipa mara mbili,” alisema Kahuluda.

Hata hivyo, kupitia hotuba ya kitaifa ya kilele cha sherehe za wafanyakazi kwa mwaka huu iliyotolewa na Rais Samia jijini Mwanza juzi, tayari serikali imeanza kuchukua hatua za utekelezaji, ikiwemo kushusha PAYE kutoka asilimia 9 hadi 8.

Aidha Samia alisema suala la utegemezi wa ukomo wa bima ya afya kwa umri wa watoto limeongezwa kutoka miaka 18 mpaka 21, huku akiagiza madeni yote ya watumishi yaanze kulipwa.

Kuhusu makato ya HESLB aliagiza kufutwa kwa asilimia 6 ya juu na kubakiza asilimia 15 ya mshahara, huku suala la stahiki kwa watumishi wa darasa la saba waliositishiwa ajira zao lizingatiwe.

Hata hivyo kuhusu suala la nyongeza ya mshahara wafanyakazi wametakiwa kusubiri kwanza mpaka ifikapo mwezi Mei mwakani.

Saturday, May 1, 2021

DANIEL CHONGOLO NA SHAKA H.SHAKA WATAKIDHI KIU YA WANA CCM NA WANANCHI

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida Dkt. Denis Nyiraha 


Na Dotto Mwaibale


MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM) Mkoa wa  Singida,  Dkt. Denis Nyiraha amesema Katibu Mkuu wa chama hicho aliyechaguliwa juzi Daniel Chongolo na Katibu wa Itikadi na Siasa, Shaka H.Shaka kuwa ni viongozi ambao watakidhi kiu ya wana CCM na wananchi kwa ujumla.

Nyiraha aliyasema hayo juzi baada ya kumalizika kwa  mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika jijini Dodoma.

" Viongozi hawa ni wazoefu katika chama chetu na kazi zao zilikuwa zikionekana kwa kukitumikia chama chetu na Serikali hivyo kuchaguliwa kwao kutakidhi kiu za wananchi." alisema Nyiraha.

 Dkt. Nyiraha alisema kuwa viongozi hao watashusha kiu ya wananchi katika majukumu yao ya kila siku na kuongeza ari ya utendaji kwa kuwa wanauzoefu na uwezo na kuwa wamekuja wakati sahihi.

Nyiraha amewahikishia wananchi  kuwa chama kimepata viongozi sahihi chini ya Mwenyekiti wao wa Taifa Rais Samia Suluhu Hassan na akaomba wapewe ushirikiano.

WAFANYAKAZI WA I&M BANK WAJITOLEA DAMU KUOKOA MAISHA YA WATANZANIA WAKISHIRIKIANA NA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

 

Meneja masoko na mawasiliano benki ya I&M Tanzania kushoto Bi.Anitha Pallangyo akiwa na wafanyakazi wenzie katika kampeni ya uchangiaji dau
         Damu ikiendelea kutolewa kutokana na hamasa iliyoletwa na wafanyakazi wa Benki ya I&M
    Bi.Lencer Odhiambo kutoka kitengo cha huduma kwa wateja cha benki ya I&M akiwa anajitolea damu katika kampeni ya kuchangia damu   
    Mkuu wa kitengo cha mikopo Bw.Clemence Kagoye wa benki ya I&M akiwa anatoa damu katika kampeni ya kuchangia damu ilioandaliwa na benki hiyo

Mwandishi Wetu

Benki ya I&M Tanzania, Ijumaa tarehe 30 Aprili 2021, walifanya Kampeni ya utoaji Damu ili kuokoa maisha ya watanzania chini ya mpango wao wa ‘IM FOR YOU’ katika jitihada za kurudisha kwa jamii. Kampeni hiyo ilifanyika Makao Makuu ya Benki hiyo yaliopo Maktaba Square jijini Dar es salaam.

Zaidi ya wafanyakazi 30 walishiriki na kujitolea Damu ili kuiwezesha Serikali kukabiliana na upungufu wa Damu kupitia hospitali ya taifa ya Muhimbili ambayo ilishirikiana na Benki hiyo katika zoezi la utoaji damu.

Kwasababu uhitaji wa damu bado upo, Benki ya I&M kupitia mpango wake wa ‘IM FOR YOU’ ambao wafanyakazi wake hujitolea kwa jamii wameamua kufanya kampeni hii ya uchangiaji damu kama njia ya kurudisha kwa jamii.

Akiongea wakati wa zoezi hilo la kujitolea damu, Bi. Anitha Pallangyo, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya I&M alisema,”tumefurahishwa sana na muitikio ambao wafanyakazi wenzetu wameonyesha katika zoezi hili la kipekee. Tunawashukuru sana hospitali ya Taifa  Muhimbili kwa muitikio wao walioonyesha kwa kukubali kushirikiana nasi katika zoezi hili la utoaji damu ili kuokoa maisha ya watanzania wengi wenye uhitaji wa damu.”

 Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kitengo cha Uboreshaji huduma za Benki Bi. Deepali Ramaiya, , Alisema “Hii ni moja ya mipango mikakati ya aina yake ambayo huanzishwa  na wafanyakazi wenyewe wa Benki ya I&M, kwa kujitolea huduma bure kwa jamii kama vile kutoa Elimu ya Ujasiriamali bure kwa wafanyabiashara kupitia Vikundi mbalimbali na sasa wamejitolea damu kupitia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

 Naye Afisa muhamasishaji damu kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,John Daniel Bigambalaye alisema, “sisi kama wawakilishi wa Muhimbili kitengo cha damu, tumehamasika na kampeni hii iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Benki ya I&M kwa jitihada hizi za kusaidia hospitali ya Taifa na watanzania wenye uhitaji wa damu kwa ujumla. Tunashauri na taasisi nyingine ziwe mstari wa mbele katika kuhamasisha wafanyakazi wake kujitolea kwa jamii”

 Benki ya I&M kupitia wafanyakazi wake wameweza kufanya kampeni mbalimbali za kusaidia jamii kama vile kujitolea kufundisha Wanawake, Vijana na Wajasiriamali, kujitolea damu  na mengine mengi kwenye sekta ya Afya, Elimu na Mazingira.

 Licha ya wafanyakazi wa Benki ya I&M kujitolea damu pia walialika Taasisi mbalimbali na kampuni zilizo karibu na Makao Makuu ya Benki ili kushiriki.

WANAONYONYESHA WAOMBA MAREKEBISHO SHERIA YA LIKIZO

Mama akiwanyonyesha watoto wake mapacha  huku akiwa anafurahia na kutafakari jambo lake moyoni. 


Na Abby Nkungu, Singida


WAKATI leo dunia inaadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu kama “Mei Mosi”, wanawake waliopo kwenye utumishi wa umma na sekta binafsi wameiomba Serikali kuvifanyia marekebisho baadhi ya vipengele vya Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini ili  kutoa  haki na kukidhi mahitaji ya  kiafya kwa malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto.

Wakizungumza na Mwandishi wa Blog hii kwa nyakati tofauti, baadhi yao walisema kuwa Sheria hiyo  imekuwa kikwazo  katika utekelezaji wa  miongozo, kanuni na taratibu nyingine za kiafya;  hivyo kuathiri suala zima la malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto.

Walisema kuwa wakati miongozo ya afya inataka mtoto mchanga anyonyeshwe  maziwa ya mama pekee  kwa miezi sita mfululizo bila kumchanganyia chakula kingine, Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini inatoa siku 84 tu za likizo ya uzazi ambazo hazizidi miezi mitatu na ni hatari kiafya kwa mtoto mchanga.

“Hebu fikiria Serikali hiyo hiyo kupitia Wizara ya Afya inatutaka tunyonyeshe miezi sita mfulilizo halafu Utumishi wanatupa likizo ya miezi  mitatu tu, hii sio sawa. Ni kumnyima haki mtoto na mzazi wake lakini pia  inaweza kuathiri makuzi ya mtoto” alisema Halima John  mkazi  wa Mwenge  mjini Singida.

Neema Omari,  mkazi wa Ginnery mjini hapa alisema kutokana na siku za likizo kuwa chache huwa wanalazimika kukamua maziwa  yao na kuyahifadhi kwenye chupa ya chai ili mtoto aweze kupewa na yaya au mtu mwingine anayebaki nyumbani pindi yeye awapo kazini.

Kaimu  Mganga Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk Ernest Mugeta alisema kuwa ingawa  mtindo huo umezoeleka kwa akinamama watumishi wanaonyonyesha, njia hiyo sio sahihi kwani mbali na maziwa hayo kupungukiwa baadhi ya virutubisho yanapohamishwa kutoka kwa mama kwenda kwenye chombo kingine pia inatenganisha mahusiano mema baina  ya mama na mtoto.

“Usafi wa maziwa hayo baada ya kutoka kwenye titi la mama ni wa kutiliwa shaka. Pia, joto na ladha ya maziwa yanayotoka moja kwa moja kwenye titi la mama kwenda kwa mtoto haiwezi kulinganishwa na joto la chombo chochote cha kuhifadhia maziwa hayo… iwe chupa ya chai au vinginevyo” alieleza Dk Mugeta na kuongeza;

Kimsingi, uhusiano wa karibu wa mama na mtoto hutokana na mtoto kunyosha titi la mama, anazoea harufu ya mama na ndio maana mtoto humjua mama zaidi kuliko baba. Hivyo, inashauriwa pale inapowezekana mama apewe ruhusa ya kwenda kunyonyesha hata baada ya likizo yake ya uzazi kumalizika”.

Kutokana na hali hiyo, akinamama walisema kuwa kuna haja kwa Serikali kuvifanyia marekebisho baadhi ya vipengele vya Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini  ili kutoa muda zaidi wa likizo kwani kumruhusu mama mzazi kwenda nyumbani kunyonyesha kisha kurudi kazini inaleta usumbufu na haitekelezeki mahali pengine kama Dar es Salaam.

Kwa Mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini Namba 6 ya mwaka 2004, mtumishi hupewa siku 84 za  likizo kwa anayejifungua mtoto mmoja, siku 100 kwa anayejifungua mapacha na siku tatu kwa baba wa mtoto huyo.

Ofisa Kazi Mfawidhi mkoa wa Singida, Bibi Eunice Mmari anasisitiza kuwa likizo hiyo inatosha kwa mama kumlea mtoto na kuweka mazingira mazuri ya usalama na ulinzi wake baada ya  yeye kuanza kazi likizo inapomalizika; hiyo ikizingatia pia kutoathiri tija mahali pa kazi. 


BODI YA MAJI BONDE LA KATI YAZINDUA JUMUIYA ZA WATUMIA MAJI BWAWA LA SONGWA NA NHUMBU MKOANI SINYANGA

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa  wa Shinyanga, Joackim Otaro (kulia) kwa niaba ya mkuu wa mkoa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa jumuiya za watumia maji wa Bwawa la Songwa na Nhumbu yaliyopo mkoani  Shinyanga, akikabidhi pikipiki mbili kwa  viongozi wa jumuiya hizo katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shinyanga hivi karibuni.

Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Kati, William Mabula, akizungumza katika hafla hiyo.

Afisa Maendeleo  ya Jamii Mkuu Bodi ya Maji Bonde la Kati, Halima  Faraji, akizungumza katika hafla hiyo.

Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi, Bodi ya Maji Bonde la Kati, Nelea Bundala, akielezea mchakato wa uundaji wa jumuiya hizo mbili.


Wana jumuiya za watumia maji wa Bwawa la Songwa na Nhumbu wakiwa kwenye hafla hiyo.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, William Jijimya, akizungumza katika hafla hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Emmanuel Johnson na kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese.


Pikipiki zilizotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Kati kwa  watumia maji wa Bwawa la Songwa na Nhumbu kwa ajili ya matumizi ya kutunza vyanzo vya maji.



Uzinduzi ukiendelea.

Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Kati, William Mabula, akisisitiza jambo kwenye uzinduzi huo Kulia ni .Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi, Bodi ya Maji Bonde la Kati, Nelea Bundala. 

Wana jumuiya za watumia maji wa Bwawa la Songwa na Nhumbu wakiwa kwenye hafla hiyo.

Uzinduzi ukiendelea.

Watendaji wa kata na wenyeviti wa vijiji wakiwa kwenye hafla hiyo.


Watendaji wa kata na wenyeviti wa vijiji wakiwa kwenye uzinduzi huo.


Watendaji wa vijiji wanaohusika na Jumuiya ya watumia maji wa Bwawa la Nhumbu na Songwa wakiwa kwenye uzinduzi huo.

Madiwani wakiwa kwenye hafla hiyo.

Wana jumuiya za watumia maji wa Bwawa la Songwa na Nhumbu wakiwa kwenye hafla hiyo.

Uzinduzi ukiendelea.
Wana jumuiya za watumia maji wa Bwawa la Songwa na Nhumbu wakiwa kwenye hafla hiyo.
Uzinduzi ukiendelea.
Uzinduzi ukiendelea.

Afisa Maendeleo  ya Jamii Mwandamizi wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, Hhau Sarwatt, akizungumza katika hafla hiyo.

Mhandisi kutoka Kampuni ya Williamson Diamonds Limited, Raphael Matola (kulia) akiwa na Mhasibu Mkuu wa Bodi ya Maji  Bonde la Kati, Elibariki Shanguya.

Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Kati, William Mabula, akisisitiza jambo kwa viongozi wa jumuhiya hizo kuhusu matumizi ya pikipiki walizo kabidhiwa.

Makabidhiano ya vitendea kazi yakiendelea.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese, akizungumza katika hafla hiyo.

Wanajumuhiya wakiserebuka katika uzinduzi huo.

Viongozi wa Jumuiya ya watumia maji wa Bwawa la Nhumbu na Songwa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi wa Bodi ya Maji ya Bonde la Kati.



Na Dotto Mwaibale, Shinyanga


WANANCHI  mkoani Shinyanga wameombwa kutumia rasilimali za maji vizuri kwa kuwa ndio tegemeo katika ustawi wa kiuchumi, kijamii na kimazingira.

Ombi hilo limetolewa hivi karibuni na Kaimu Katibu Tawala wa mkoa huo, Joackim Otaro kwa niaba ya mkuu wa mkoa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa jumuiya za watumia maji wa Bwawa la Songwa na Nhumbu yaliyopo mkoani humo.

"Ndugu zangu wana Shinyanga niwaombe tutumie rasilimali zetu za maji vizuri maana maji hayana mbadala, maji ni uhai na ndio tegemeo letu katika ustawi wa kiuchumi, kijamii na kimazingira." alisema Otaro.

Otaro alisema madhumuni ya kuzindua Jumuiya za Watumia maji wa Bwawa la Nhumbu na Bwawa la Songwa ambazo zimeundwa kwa ufadhili wa Bodi ya Maji ya Bonde la kati  kwa sheria namba 11 ya mwaka 2009 na Sera ya maji ya mwaka 2002 ni kutunza vyanzo vya maji. 

Alisema Jumuiya za watumia maji ni chombo cha chini katika ngazi ya jamii kinachoundwa kwa lengo la kuiwezesha na kuiunganisha jamii ya watumia maji wa chanzo husika kwa pamoja, ili kujadili changamoto zao na kuandaa mipango ya usimamizi na uhifadhi wa chanzo chao cha maji kwa lengo la kupunguza vitendo vya uchafuzi, uharibifu wa miundo mbinu, migogoro ya matumizi ya maji. 

"Suala la usimamizi na uhifadhi wa vyanzo vya maji ni jukumu la kila mtu si jukumu la Serikali peke yake, hivyo linahitaji nguvu ya pamoja katika kupanga na kusimamia mipango mbalimbali ya kuendeleza uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya maji." alisema Otaro.

Aidha,  Otaro aliongeza kuwa Bodi ya Bonde la Kati kama chombo chenye dhamana na Usimamizi wa Rasilimali kwenye eneo la bonde lake, waendelee kutoa hamasa, elimu na hata kuunda jumuiya za watumia maji kwenye maeneo mengine yenye changamoto za namna hiyo hususan katika mkoa huo wa Shinyanga na alieleza juhudi hizo walizozianzisha ziwe endelevu pamoja na kuhakikisha kuwa vyanzo vya maji vinatambuliwa, kuwekewa mipaka na kuhifadhiwa vizuri ili visiharibiwe na kuchafuliwa na shughuli zozote za kibinadamu. 

Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Kati, William Mabula alisema kuna umuhimu mkubwa mno wa jumuiya hizo kwa ajili ya kutunza vyanzo vya maji.

Alisema tukisiliza sekta ya maji inavyojadiliwa katika ngazi ya kimataifa na hata ngazi za Serikali kumekuwa na msisitizo kwenye lile tone la maji linalotoka lakini si habari ya chanzo chake na jinsi yanavyohifadhiwa.

"Serikali imeendelea kuhimiza utunzaji wa vyanzo vya maji kama tulivyomsikia hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihimiza utunzaji wa vyanzo hivyo kuanzia ngazi za chini na ndio kama hizi jumuiya tulizozianzisha." alisema Mabula.

Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi, Bodi ya Maji Bonde la Kati, Nelea Bundala, alisema mchakato wa uundaji wa jumuiya hizo mbili ulianza Septemba mwaka 2020 baada ya maagizo ya kamati ya Taifa ya ufungaji migodi ya kuitaka Bodi ya maji Bonde la Kati kutembelea mabwawa yote ya Williamson na kuangalia changamoto zilizopo zinazopelekea kuharibika kwa ubora wa maji na kupungua kwa wingi wa maji. 

Alisema Bodi ilitekeleza agizo hilo na ilitembelea na kutathmini hali ya vyanzo hivyo na ilionekana kwamba kuna umuhimu wa kutoa elimu kwa watumia maji wa mabwawa hayo yote, pamoja na kuwezesha kuunda chombo cha kijamii yaani Jumuiya za watumia maji kwa Mujibu wa  sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za maji namba 11 ya mwaka 2009 inavyoelekeza. 

" Katika mchakato huo mikutano ilifanyika kila kijiji na wawakilishi wa kila kijiji walipewa mafunzo yatakayowawezesha kusimamia vyanzo hivyo vya maji vizuri." alisema Bundala.

Bundala alisema kwa Jumuiya ya Nhumbu vijiji vinavyohusika ni Mwamalili, Bushora, Songwa, Buchachi, Buganika, Mwigumbi, Seseko na Mpumbura na kwa Bwawa la Songwa jumuiya inahusisha vijiji vya Songwa, Buganika, Buchambi, Mwigumbi, Maganzo, Ikonongo na Masagala. 

Aidha Bundala alisema kuwa wawakilishi hao walitengeneza katiba ambayo ndani yake kuna sheria ndogondogo ambazo zitatumika kuzuia uharibifu mbalimbali unaoendelea katika mabwawa hayo, ikiwemo kulima karibu na mabwawa, kunywesha mifugo kiholela bwawani, uvuvi haramu, uchenjuaji madini bwawani, kuosha vyombo, kufua ndani ya vyanzo vya maji. 

Alisema mambo hayo yote yanayoharibu ubora na wingi wa maji na kuwa madhara ya uharibifu huo ni makubwa kwani kina cha maji kinapungua siku hadi siku na matokeo yake yanakua ni mafuriko. 

Katika uzinduzi huo Bodi ya Maji Bonde la Kati ilitoa pikipiki mbili aina ya Yamaha, simu za mkononi, katiba na baadhi ya vifaa vya ofisini kwa ajili ya kusaidia jumuiya hizo katika kazi  za kila siku za kutunza vyanzo vya maji.

TAHA YAPELEKA MAJI IKUNGI MKOANI SINGIDA KUWAKOMBOA WANAWAKE

Mtambo wa uchimbaji wa visima wa Kampuni ya Ahia General Supplies, ukiwa kwenye eneo la shamba la ekari mbili la mradi wa kilimo cha mbogamboga katika Kata ya Kipumbwiko wilayani Ikungi mkoani hapa. Mradi huo unaendeshwa na  Asasi kilele ya sekta binafsi inayojihusisha na kuendeleza tasnia ya horticulture hapa nchini ijulikanayo kama TAHA.
Mshauri na Msimamizi wa uchimbaji wa visima vya mradi huo ambavyo vinachimbwa na Kampuni ya Ahia General Supplies, Hezron Philip, akizungumzia manufaa ya mradi huo na mchakato mzima wa uchimbaji wa kisima hicho.
Mtaalamu wa Kilimo wa TAHA Mkoa wa Singida, Mohamed Bakari, akiwaelekeza jambo wataalamuwa uchimbaji wa visima wa Kampuni ya Ahia General Supplies. Kushoto ni Mratibu wa Mradi wa UN WOMEN, Glory Prosper.
Wananchi wa Kata ya Kipumbwiko, wakisaidia kuweka matawi ya miti barabarani ili kuwezesha gari lenye mtambo wa uchimbaji wa kisima liweze kupita.
Gari lenye mtambo wa uchimbaji wa kisima likielekea kwenye eneo la mradi.
Mtambo wa uchimbaji wa kisima ukitoa maji.
Muonekano wa shamba la mradi.
Fundi wa mtambo wa uchimbaji wa kisima wa Kampuni ya Ahia General Supplies, akiwa kazini.



Na  Dotto Mwaibale, Singida 



 ASASI kilele ya sekta binafsi inayojihusisha na kuendeleza tasnia ya horticulture hapa nchini ijulikanayo kama TAHA imeanza mchakato wa kuchimba kisima cha maji katika Kata ya Kipumbwiko wilayani Ikungi mkoani hapa kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kuanza kilimo cha mbogamboga.

 Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa  mshauri na msimamizi wa uchimbaji wa visima vya mradi huo ambavyo vinachimbwa na Kampuni ya Ahia General Supplies, Hezron Philip alisema kisima hicho chenye urefu wa mita 100 kwenda chini kikikamilika kitakuwa mkombozi wa kiuchumi kwa wananchi wa kata hiyo hasa wanawake.

"Baada ya kukamilika kwa kisima hiki kitakacho wanufaisha wanawake wa vikundi vinne vilivyopo ndani ya mradi  katika  Kijiji cha Kipumbwiko kwa uzalishaji wa mboga mboga kwa njia ya kilimo cha umwagiliaji kitawapa wananchi matumaini ya maisha" alisema Philip.

Alisema maji yatakayopatika katika kisima hicho ni kuanzia lita 5000 kwa saa hivyo kuwa na uhakika wa kuendesha kilimo hicho. 

"Kisima hiki ambacho tutakijenga kwa ubora wa hali ya juu kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kuwepo zaidi ya miaka 100 hivyo  wanakikundi watarajie mafanikio makubwa kwani maji yatakuwepo ya kutosha kwa masaa 24." alisema Philip.

Philip alitoa mwito kwa wananchi kutunza chanzo cha maji ambacho ndio maendeleo na kuwa kisima hicho kitakuwa shamba darasa ambapo wananchi watajifunza kuwa na maji wataweza kuwa na maisha bora na maendeleo katika jamii.

 Mradi wa kilimo hicho unaendeshwa na TAHA kwa kushirikiana na UN WOMEN pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi lengo likiwa ni kuwakomboa wanawake  kiuchumi.

 TAHA inaendesha kazi zake katika mikoa 25 ya Tanzania ikiwemo Arusha, Mwanza, Manyara, Kilimanjaro,Tanga, Dodoma, Morogoro, Iringa, Njombe, Pwani, Dar es salaam, Lindi, Mtwara, Mara, Simiyu, Mbeya, Songwe, Unguja

 ( Unguja Kaskazini, Unguja Kusini na mjini Magharibi ) na Pemba  ( Pemba Kaskazini na Pemba Kusini )  Ikungi-Singida na  Msalala-Shinyanga.

 Asasi hiyo yenye makao makuu yake jijini Arusha imejikita zaidi kuwawezesha wadau katika mnyororo wa thamani wa mazao ya mboga mboga, matunda, maua, viungo na mazao ya mizizi. 

Wadau wanao wezeshwa katika mnyororo huo wa thamani ni wasambazaji wa pembejeo, wakulima, wasindikaji, wafanyabiashara, wasafirishaji na makampuni yanayofanya usafirishaji nje ya nchi na wanawawezesha kwa vitendo.

Kazi kubwa zinazofanywa na TAHA ni nne kwanza  ni kuwaunganisha wakulima na masoko, kuwawezesha wakulima katika suala zima la kilimo na kuwaonesha teknolojia mbalimbali ambazo wanaweza kuzitumia kulingana na uwezo na mazingira waliopo. 

Tatu ni kutengeneza mazingira wezeshi ya biashara na kufanya kazi hiyo kwa kushirikiana kwa karibu na serikali kuu kwa maana ya kushawishi na kutetea sera

zile ambazo zinamuumiza mzalishaji, mfanyabiasha na mdau yeyote katika mnyororo wa thamani.

Kazi ya nne na ya mwisho ni kuwaunganisha wadau katika mnyororo wa thamani na vyombo vya fedha baada ya kuwafundisha elimu ya fedha.