Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida Dkt.Denis Nyiraha, akizungumza na vijana wa chama hicho wa Wilaya ya Iramba baada ya kuanza ziara ya kikazi na kamati ya utekelezaji jana.
Thursday, May 6, 2021
UVCCM SINGIDA YAANZA ZIARA YA KIKAZI WILAYA YA IRAMBA
Monday, May 3, 2021
REPSSI TANZANIA WATOA MAFUNZO YA MSAADA WA KISAIKOLOJIA , NJOMBE, IRINGA NA MBEYA
Viongozi wa REPSSI Tanzania wakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Kanoni Lauteli (kushoto) kabla ya kuanza mafunzo.
Viongozi wa REPSSI Tanzania wakiwa nje ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe.
Na Mwandishi Wetu, Njombe
SHIRIKA la Regional Psychosocial Support Initiative (REPSSI) kwa kushirikiana na Tamisemi limetoa mafunzo juu ya namna ya kutoa msaada wa kisaikolojia kwa jamii, wakati wa majanga.
Mafunzo hayo yaliyotolewa kwenye mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya yamezishirikisha kamati za ulinzi na usalama za mama na mtoto katika kila halmashauri kwenye mikoa hiyo.
Akizungumza kwenye mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa REPSSI Tanzania, Edwick Mapalala amesema licha ya huduma nyingi ambayo huwa zinatolewa kwenye majanga kama moto, mafuriko, ajali na mengine, msaada wa kisaikolojia ni muhimu.
Amesema wanawake, watoto na watu wenye ulemavu huwa wahanga zaidi wa majanga hayo hiyo mafunzo yaliyotolewa yanaziandaa kamati husika kuweza kutoa msaada huo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Kanoni Luteni ameshukuru mafunzo hayo na kwamba, msaada wa kisaikolojia ni muhimu kutolewa kwa kila jamii.
Mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo, kamati hizo zilifanikiwa kuandaa mpangokazi wa kila halmashauri katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
I&M Holdings PLC Completes Acquisition of Orient Bank Limited in Uganda
Nairobi/Kampala, 3rd May, 2021: I&M Holdings PLC has announced the majority acquisition of Orient Bank Limited (OBL) from 8 miles LLP and Morka Holdings Limited. OBL is the 12th largest bank and a licensed and established commercial bank in Uganda.
I&M Holdings PLC and Orient Bank Limited signed an agreement in July 2020 for I&M Holdings PLC to acquire 90 percent shareholding of the Ugandan entity. The acquisition was completed on 30th April 2021 after receiving the necessary approvals from the Central Bank of Kenya, Bank of Uganda, Capital Markets Authority of Kenya and the COMESA Competition Authority.
The move underscores I&M Group’s commitment to its growth and expansion strategy in Eastern Africa, where Uganda was the missing link in the Group’s strategic effort to set up its presence in all East African countries. A key focus of this strategy is to seek opportunities to invest at a local and regional level enabling the Bank to serve the needs of all customers, while promoting trade flows within the region.
This development supports the Group’s Business Growth initiatives through diversification of revenue streams by entry into new markets and extension of its Corporate, Business, Personal Banking, as well as Treasury and Trade Finance solutions, to all its customers operating in Uganda.
Commenting on the acquisition, I&M’s Group Executive Director, Sarit Raja Shah noted, “I&M Group aspires to be Eastern Africa’s leading financial partner for growth. The acquisition of OBL will place I&M Bank in an advantageous position to capitalise on the growth in the Eastern African economies and thereby ultimately increasing shareholder value.”
“This acquisition is expected to give the Group greater capacity to grow profitably, through extending our network to our Regional customers. Further it demonstrates our continued leadership role in the industry across East Africa”, Sarit Raja Shah added.
Dr. Ketan Morjaria, a founding member of OBL and continuing shareholder and Director said “This acquisition marks a great milestone in the history of Orient Bank. We are proud to be integrating into a regional group like I&M Holdings PLC and this synergy will allow our customers to benefit from more seamless and superior banking products whilst continuing our tradition of trust.”
Kumaran Pather, CEO of OBL said “The acquisition of OBL into I&M Holdings PLC will see the new entity rise to greater heights and allow us to broaden our market reach and penetration. The management of OBL are excited to be part of a large and
fast growing Group and look forward to serving new and existing customers alike with better products, digital platforms and regional services.”
Through the acquisition, I&M Group has acquired additional net loan assets of approximately KES 7.7 Billion, deposits of KES 18.2 Billion, a customer base of close to 70,000, a staff component of 340 employees and a network of 14 branches and 22 ATMs across the country.
A clear plan for the integration of OBL has been developed and through its execution the Group expects to gain considerable business and operational synergies.
I&M Group has made significant investments in its robust infrastructure as part of its digital transformation journey. Through this acquisition, OBL customers will now benefit from this technologically driven infrastructure, which will give them a wide suite of market driven financial solutions aimed at meeting their financial and lifestyle requirements.
The I&M Group will continue to focus on mergers and acquisitions as part of its growth strategy, as we continue to enhance our shareholders’ value and to provide our customers with a wide network of banking solutions across the region.
The transaction with OBL adds to a list of previous strategic alliances that the Group has effectively completed such as the acquisition of Giro Commercial Bank Limited in Kenya, I&M Burbidge Capital Limited in Kenya and Uganda, CF Union Bank in Tanzania, BCR Bank in Rwanda and First City Bank in Mauritius. We believe that our aspiration in becoming Eastern Africa’s leading financial growth partner is well on course.
In his concluding remarks, Mr. Sarit Raja Shah, noted, “Uganda has made great strides in improving access to financial services across the country. The partnership with Orient Bank Limited is very timely since the Group plans to play a significant role in the growth of the banking sector in Uganda, as it has done in other East African markets.”
NDAHANI AWASHAURI VIONGOZI WA DINI KUSAIDIA VIJANA KUANZISHA MIRADI YA KIUCHUMI
Kaimu Afisa Maendeleo Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani (kulia) akiwa na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Aloyce Gonzaga-Minga Singida, Padri Festo King'wai baada ya kutembelea parokia hiyo na kuzungumza na baadhi ya vijana.wa Parokia hiyo,.
Sunday, May 2, 2021
MRADI MPYA WA MACHO SINGIDA KUNUFAISHA ZAIDI YA WATOTO LAKI MOJA.
Katibu
Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina Lutambi akizungumza kabla ya kuzindua Mradi
wa Afya ya Macho kwa Watoto unaojulikana kama ‘Mtoto Angaza.’ Mradi huo
unaoratibiwa na Shirika la Sight Savers chini ya Ufadhili wa USAID unatarajia
kuwafikia watoto wenye matatizo mbalimbali ya macho katika wilaya nne mkoani hapa-wapatao 150,000, sambamba na
kuendesha huduma za upasuaji zitokanazo na maradhi ya afya ya macho kwa watoto wapatao
100 ndani ya kipindi cha mradi 2021-2023
Katibu
Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina Lutambi akikata utepe kuzindua rasmi utekelezaji
wa andiko la mradi wa ‘Mtoto Angaza.’ Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
Sight Savers, Godwin Kabalika.
Mganga Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt .Victorina Ludovick akizungumza kwenye tukio la uzinduzi
huo.
Mratibu wa
Macho Mkoa wa Singida, Dkt. Upendo Mwakabalile akieleza namna walivyojipanga
kufikia walengwa waliokusudiwa ndani ya kipindi chote cha mradi.
Mratibu wa
Huduma za Macho kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Charles Kalidushi,
akizungumza kwenye tukio la uzinduzi huo.
Katibu
Tawala Mkoa wa Singida Dkt .Angelina Lutambi akimkabidhi Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Ikungi, Justice Kijazi nakala ya andiko la mradi huo kwa
utekelezaji. Wilaya nyingine zilizopokea nakala hiyo ni Manyoni, Iramba na
Singida DC.
Tukio la Uzinduzi wa Mradi wa Afya ya Macho kwa Watoto ujulikanao kama Mtoto Angaza likiendelea.
Picha ya pamoja
ya Viongozi mbalimbali wa Serikali na Maafisa Watendaji Waandamizi kutoka Sight
Savers muda mfupi baada ya kumalizika kwa tukio la uzinduzi wa mradi huo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
WATOTO wapatao 150,000 mkoani hapa wanatarajia kufikiwa na Mradi wa Afya ya Macho kwa Watoto ujulikanao kama ‘Mtoto Angaza,’ huku kati yao idadi ya takribani watoto 100 watafanyiwa huduma za upasuaji unaotokana na maradhi mbalimbali ya afya ya macho katika kipindi chote cha mradi kuanzia 2021 hadi 2023.
Akizindua mradi huo jana, Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt Angelina Lutambi, mbali ya kupongeza ujio wake, pia aliwataka watendaji wote wanao husika katika utekelezaji wa mradi husika kujitoa kikamilifu kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake, ili kuufanya mradi huo kuwaendelevu na wenyetija.
“Nawashukuru sana Shirika la Sight Savers kwa kutushika mkono kupitia mradi huu wa Mtoto Angaza ambao mnauratibu chini ya ufadhili wa USAID, niwasihi watendaji wote tuupe kipaumbele ili uwe na matokeo chanya,” alisema.
Hata hivyo, alihimiza elimu juu ya masuala yote yahusuyo lishe bora yazingatiwe katika kipindi chote cha mradi ili kuimarisha afya ya macho na kuzuia kabisa tatizo la uoni hafifu.
Pia Lutambi alimwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa kuweka utaratibu mzuri wa Mpango Kazi utakaoleta ufanisi katika utekelezaji wa shughuli zote zilizopangwa kufanyika ndani ya kipindi cha mradi, ili kuufanya kuwa mradi endelevu, sambamba na kuhakikisha watendaji wa mkoa wananufaika na fursa ya mafundisho yatakayotolewa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Sight Savers, Godwin Kabalika, alisema mradi huo umelenga kuboresha utoaji wa huduma ya Afya ya Macho kwa watoto wenye umri wa kuanzia mwaka 0 hadi 16 mkoani hapa ndani ya Wilaya 4 za Iramba, Manyoni, Ikungi na SingidaVijijini.
Aliongeza kuwa mradi huo utakaogharimu Dola za Kimarekani 350,000 utatekelezwa kwa kuhusisha ushiriki wa jopo la wataalamu kutoka Hospitali yaTaifa ya Muhimbili ambao watakuwa na jukumu la kushirikiana na wataalamu wenyeji kwenye utoaji wa huduma mbalimbali, zikiwemo za upasuaji na utoaji ujuzi wa kitaalamu kwenye eneo la macho.
“Lengo kubwa ni kuboresha huduma za macho ndani ya mkoa wa Singida. Na kupitia mradi huu wa miaka miwili tunatarajia kuwafikia watoto laki moja na nusu, na kati yao watoto wapatao mia moja watafanyiwa huduma za upasuaji,” alisema Kabalika.
Daktari Bingwa na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Macho kutoka Hospitali yaTaifa Muhimbili, Dkt Paul Nyaluke, alibainisha ushiriki wao katika mradi huo kuwa pamoja na mambo mengine, Muhimbili watashiriki kwenye eneo la kitaalamu kwa watoto watakao onekana wanamahitaji ya kufanyiwa upasuaji.
Aidha, Nyaluke alisema pia watajikita katika kuratibu usimamizi wa majukwaa yote yatakayo pangwa, huku akisisitiza kwamba kwenye eneo nyeti la upasuaji-hospitali hiyo itakuja na jopo la wataalamu mbalimbali kwa mfululizo wa ziara zisizopungua sita katika kipindi chote cha mradi.
Hata hivyo, akielezea ukubwa wa tatizo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Victorina Ludovick, alisema tatizo la macho kwa mkoa limefikia asilimia 2.8 huku wilaya ya Iramba ikionyesha kuwa na changamoto kubwa zaidi ikilinganishwa na wilaya nyingine.
Alisema serikali kwa kushirikiana na Sight Savers wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali za kukabiliana na tatizo la uoni unaozuilika na lile la uonihafifu-hasa eneo la changamotoya ‘Mtoto wa Jicho’ ambapo zaidi ya wananchi 3000 wamefikiwa na kupatiwa matibabu.
Kitaalamu, imeelezwa walengwa hasa watakaofanyiwa upasuaji ni wale wenye matatizo ya uoni hafifu ambao hutokana na sababu kadhaa, ikiwemo mtoto wa jicho. Tatizo hili ni matokeo ya lenzi ambazo zipo ndani ya macho kupata ukungu na hivyo kutoruhusu mwanga kupita na kuingia eneo la ndani la macho.
Pia kundi lingine litakalotazamwa kwa upekee ni watoto wenye changamoto ya uonihafifu ‘Low Vision’ ambao hata wanapopewa miwani huwa haiwasaidii kutokana na kukumbwa na tatizo la kuwa na kovu sehemu ya kuonea ambayo inapatikana sehemu ya nyuma ya jicho.
Kundi hili litapatiwa vifaa maalumu vya kuwasaidia kuona ‘Visual Aids.’
“Hivyo mradi huu umelenga kuwaibua huko walipo ili waweze kupatiwa huduma za kitiba dhidi ya tatizo la uoni hafifu unaozuilika kwa lengo la kurekebisha uoni wao,” alisema Dkt. Ludovick.
WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI AKOSHWA NA UTENDAJI KAZI WA BRELA
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Utalii yanayofanyika katika katika Viwanja vya Rock City Mall, Jijini Mwanza jana. Kushoto kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja akifuatiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Godfrey Nyaisa.
Maofisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wakihudumia wadau mbalimbali waliofika katika banda lao katika maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Utalii kwenye Viwanja vya Rock City Mall, Jijini Mwanza jana.
Kikao kikiendelea
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki aliyekuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Utalii, amefurahishwa na utendaji kazi Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).
Ndaki alionesha kufurahishwa na hatua hiyo ya utendaji kazi wa taasisi hiyo alipotembelea Banda lao la maonesho katika Viwanja vya Rock City Mall, Jijini Mwanza jana.
Afisa Usajili kutoka Brela, Gabriel Girangay akielezea mafanikio ya taasisi hiyo alisema imeboresha huduma inazotoa kwa wadau wake ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa kukamilisha usajili kwa kadri inavyowezekana lakini pia kuwahudumia wateja wote kwa ukaribu kupitia kituo cha miito.
“Kwa sasa muda wa usajili wa jina la biashara ni siku moja (1) na si zaidi ya siku tatu (3) za kazi, Usajili wa kampuni ni siku tatu (3) na si zaidi ya siku tano (5) za kazi. Usajili wa Alama za Biashara na huduma ni kipindi cha siku tisini (90) (kutokana na takwa la kisheria).
Maombi ya kupata Hataza ni siku mia moja na ishirini (120) (kutokana na takwa la kisheria), kupata Leseni ya Kiwanda au Leseni ya Biashara kundi A ni siku moja (1) na si zaidi ya siku tatu (3) za kazi”. alibainisha Girangay.
Aidha, akisoma hotuba ya ufunguzi wa maonesho hayo Ndaki amewataka wafanyabiashara na wajasiriamali wa Mkoa wa Mwaza kutumia fursa ya uwepo wa taasisi hiyo katika maonesho hayo kutatua changamoto zao na kupata elimu.
“Changamoto zinazosemekana zipo katika urasimishaji biashara sasa ndio muda wake kuzimaliza na bahati nzuri Brela wapo katika maonesho haya, fikeni katika banda lao la maonesho, pateni elimu, wasilisheni changamoto zenu hapo na rasimisheni biashara papo kwa hapo”. alisema Mhe. Ndaki.
Brela inashiriki maonesho haya ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kuwafikia wadau wake katika maeneo yao kwa lengo la kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kurasimisha biashara, taratibu za urasimishaji biashara na gharama zake, kutatua changamoto na kufanya usajili wa papo kwa hapo.
Maonesho ya Biashara Uwekezaji yanafanyika kwa siku tatu kuanzia Aprili 30 hadi leo.
RC NCHIMBI ATAKA MANUFAA YA CHANJO YATANGAZWE
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amewataka Wataalamu wa Afya mkoani hapa kuchanganua na kuainisha hadharani ni kwa namna gani chanjo zinazotolewa zimekuwa na tija kwa jamii ili kuleta msukumo kwa watu kuzipenda, kuzithamini, kuziheshimu na kuendelea kuchanjwa.
Akizindua ‘Wiki ya Chanjo’ kimkoa, kwenye viwanja vya Kata ya Muhintiri, Wilaya ya Ikungi mkoani hapa jana, Nchimbi pamoja na mambo mengine, aliwataka wataalamu hao kufuatilia na kutangaza hadharani matokeo na mazao ya chanjo hizo katika uhalisia wa maisha ili watu wajue.
“Wataalamu msikae kimya tuelezeni mara kwa mara manufaa ya hizi chanjo ni kwa namna gani zimekuwa chanzo cha afya bora na akili timamu kwa ukuaji stahiki wa watoto wetu, vijana, jamii na taifa…tuelezeni zinavyochangia ongezeko la ufaulu mashuleni na manufaa yake kwa ukuaji wa uchumi,”alisema Nchimbi na kuongeza;
“Mkieleza vizuri ubora wa chanjo hizi kwa jamii na tukawaelewa-basi- ubora huo ndio utakuwa msukumo katika kuchochea zaidi kasi ya ongezeko la watumiaji wake.”
Hata hivyo alisisitiza haitakuwa na maana yoyote kama chanjo zinazotolewa hazitaenda sambamba na lishe bora, huku akitumia nafasi hiyo kuhamasisha jamii kuzingatia vyote kwa pamoja, ili kuleta ustawi wa afya ya jamii kwa matokeo ya Taifa bora.
Nchimbi alisema Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kuhakikisha juhudi zilizopo za utoaji wa chanjo zinakwenda sambamba na maboresho katika utoaji wa huduma nyingine za afya-ili kupunguza vifo visivyo vya lazima na kumlinda kila mtanzania dhidi ya maradhi ambukizi.
Katika hilo, aliwahimiza wazazi kuhakikisha watoto wao wanapata dozi nzima ya chanjo zinazotolewa kwenye Vituo vya Afya, kwa kuzingatia chanjo ni chanzo cha afya bora na kinga madhubuti dhidi ya magonjwa hatarishi.
Awali, akiwasilisha taarifa ya mkoa juu ya hali halisi ya utoaji wa huduma za chanjo kwa mwaka 2020, Kaimu Mganga Mkuu mkoani hapa, Ernest Mgeta alisema licha ya mafanikio katika utoaji wa huduma hiyo lakini bado kuna changamoto, ikiwemo ya wengi kutokamilisha dozi.
Mgeta alibainisha kuwa idadi kubwa ya watumiaji wa chanjo huanza vizuri lakini hawakamilishi chanjo. Mathalani katika kipindi cha Januari hadi Disemba 2020, jumla ya akinamama 8,646 hawakupata au kukamilisha chanjo dhidi ya ugonjwa wa Pepopunda.
Ugonjwa huo ni rahisi kumpata mtoto atakayezaliwa kupitia mama ambaye hana kinga yake, na maambukizi hutokea ndani ya siku 28 tangu kuzaliwa kupitia kovu la kitovuni. Watoto wote ambao hupata vimelea vya Pepopunda huishia kufariki.
Mgeta alitaja changamoto nyingine kuwa ni kasumba hatarishi ya wazazi kuendelea kujifungulia nyumbani ambayo hupelekea watoto kukosa huduma za afya za awali, ikiwa ni pamoja na kupata chanjo dhidi ya Kifua Kikuu na Polio.
Suala lingine lililojitokeza ni watoto kusitishwa kuhudhuria kliniki mapema na kushindwa kukamilisha dozi ya mwisho ya chanjo dhidi ya Surua, mathalani, katika kipindi cha mwaka jana jumla ya watoto 18,583 hawakufika kukamilisha dozi ya pili ya Surua-hali inayoleta tishio la mlipuko wa ugonjwa huo miongoni mwa jamii ya wana-Singida.
Akizungumzia kinga dhidi ya Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa wanawake hususani kwa wasichana wenye umri wa miaka 14, Kaimu Mganga Mkuu alisema serikali tayari ina chanjo ya kuzuia ugonjwa huo unaosababisha kifo iliyoanza kutolewa tangu mwaka 2018, lakini hata hivyo bado mwitikio ni mdogo.
“Chanjo hii licha ya Serikali kuinunua kwa gharama kubwa lakini huduma zake kwa wananchi hutolewa bure kupitia vituo vyake vyote vya afya...hakuna malipo yoyote,” alisema Mgeta.
Hata hivyo, aliwahamasisha wazazi kujitokeza kuwapeleka watoto kwenye vituo vya afya, hususani wiki hii ya maadhimisho ya chanjo ili kuhakikisha zingatio la mahitaji ya kidozi linafikiwa kwa matokeo chanya ya kiafya, sambamba na kuepuka maradhi na vifo.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu yanasema “Chanjo Hutuweka Huru Pamoja, Kapate Chanjo” ikiwa na maana ya kama tutazingatia ipasavyo upatikanaji wa huduma hiyo basi ni dhahiri itatuweka huru bila ya kuwa na wasiwasi wa kuambukizana magonjwa.
Imeelezwa, kwa aliyechanja akakamilisha dozi yupo huru kutopata magonjwa ambayo yanasababishwa na milipuko na ambayo yanakingwa kwa chanjo.



















