Thursday, August 5, 2021

PROFESA KABUDI: SERIKALI KUJENGA MAHAKAMU KUU KATIKA MIKOA TISA

Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Viongozi wa Idara za Serikali na Mahakama  (hawapo pichani) wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo jana.

Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi (kulia) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Viongozi wa Idara za Serikali na Mahakama  wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wakati akikagua eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Ikungi.

Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akikagua jengo linalojengwa la Kituo cha Polisi Wilaya ya Ikungi. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu.
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Viongozi wa Idara za Serikali ya  Wilaya ya Ikungi  wakati akikagua jengo linalojengwa la Kituo cha Polisi wilaya humo. 


Na Dotto Mwaibale, Singida


SERIKALI kuanza ujenzi wa Mahakama Kuu katika mikoa tisa nchini iliyobaki ukiwemo Mkoa wa Singida  ili kuondoa tatizo la wananchi kusafari kwenda mikoa ya jirani kwa ajili ya kupata huduma za Kimahama.

Hayo yamesemwa jana  na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi wilayani Ikungi mkoani hapa katika ziara yake ya kukagua Mahakama za wilaya na za Mwanzo pamoja na kuzungumza na wadau wa masuala ya Sheria.

Kabudi alisema alisema mpango wa ujenzi wa mahakama hizo utaenda pamoja na ujenzi wa mahakama za wilaya hasa kwenye wilaya ambazo hazina mahakama.

" Wilaya ya Ikungi nayo itaingizwa kwenye mpango wa ujenzi wa mahakama ya wilaya kwa sababu mpaka sasa haina mahakama ya wilaya ambapo wananchi wanafuata huduma za kimahakama mjini Singida,". alisema Profesa Kabudi.

Aidha Waziri Kabudi amewapongeza viongozi wa Wilaya ya Ikungi kwa kutenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama ya wilaya na kusema jambo hilo ni nzuri na linapaswa kuigwa na wilaya nyingine.

Akizungumzia kuhusu ukarabati wa mahakama za mwanzo nchini, Profesa Kabudi alisema utafanyika kwa awamu na kipaumbele kitatolewa kwenye Mahakama za Mwanzo ambazo zinahudumia idadi kubwa ya wananchi.

Wednesday, August 4, 2021

WAZIRI KABUDI: WATUMISHI WAZEMBE, WAPENDA RUSHWA HATUTA WAVUMILIA


 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge (kushoto) akimpokea Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi  alipowasili mkoani hapa kwa ziara yake ya kikazi juzi ambapo tayari ametembelea wilaya ya Singida, Mkalama na Iramba. 


Na Dotto Mwaibale, Singida


WAZIRI  wa Katiba na Sheria Profesa  Palamagamba Kabudi amewaagiza Watumishi wa Mahakama kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma katika utendaji wao wa kazi wa kila siku hasa katika utoaji wa haki kwa wananchi. 

Kabudi ametoa kauli hiyo kwa Nyakati tofauti wakati akizungumza na Watumishi wa Mahakama na Wadau wa Sheria katika wilaya za Singida na Halmashauri ya Mkalama na kusisitiza kuwa wizara yake haitawavumilia watumishi wazembe na wapenda rushwa kwani wakiachwa bila kuwajibishwa wataipata matope Idara ya Mahakama.

Wizara yangu haitawavumilia watumishi wazembe na wapenda rushwa kwani wakiachwa bila kuwajibishwa wataipata matope Idara ya Mahakama ili ionekane kuwa haifanyi kazi zake vizuri kumbe hali hiyo inasababishwa na watumishi wachache," alisema Profesa Kabudi.

Akizungumzia kuhusu uhaba wa Watumishi wa Mahakama Kabudi alisema Serikali itahakikisha inaondoa changamoto hiyo haraka ili wananchi waweze kupata huduma bora na ya uhakika karibu na maeneo yao.

Aidha alisema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kufanyika kazi kwa Watumishi wa Mahakama ikiwemo kupatia vitendea kazi ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Monday, August 2, 2021

WAZIRI KABUDI AANZA ZIARA MKOANI SINGIDA, ATAKA UJENZI WA MAHAKAMA MANYONI UHARAKISHWE.

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge (kushoto) akimpokea Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi  alipowasili mkoani hapa katika ziara ziara yake ya kikazi jana. 

Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza katika kikao na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Viongozi wa Idara za Serikali na Mahakama  wa Mkoa wa Singida wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani hapa jana.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge, akizungumza kwenye kikao hicho.

Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida,Mkambazi Kazen akitoa taarifa ya hali halisi ya utoaji haki na utekelezaji wa sheria kwenye kikao hicho

Profesa Kabudi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waandamizi wanaohusika na utoaji haki ngazi ya mkoa wa singida mda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao kazi 
 


Na Godwin Myovela, Singida.


WAZIRI wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi ameagiza watendaji wa mahakama mkoani hapa kuharakisha mchakato wa kuandaa eneo litakalotumika kwa mradi wa ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Manyoni,  ambayo pamoja na mambo mengine, inatarajia kujikita  katika kushughulikia kesi za ujangili ili kuimarisha ulinzi wa mazingira

Hifadhi ya mto Kizigo uliopo kwenye msitu wa Rungwa wilaya ya manyoni mkoani hapa mbali ya kuwa na wanyama pia mto huo ni moja ya chanzo muhimu kinachopeleka maji kwenye mto Ruaha ambao ndio hutiririsha maji yake mpaka  kwenye bwawa la kufua umeme la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililopo Rufiji.

Profesa Kabudi alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani hapa jana, alipokutana na viongozi waandamizi wa mahakama na wadau wa utoaji haki, wakati akikagua hali halisi ya mwenendo wa utoaji haki na utekelezaji wa sheria hususani sheria ya msaada wa huduma za kisheria iliyopitishwa na Bunge mwaka 2017.

"Ujenzi wa mahakama hii ambayo itashughulikia kesi za ujangili, kulinda utajiri wa asili na mali za asili haukwepeki na upo kwenye mpango wa mwaka huu wa fedha,  nataka kufikia Ijumaa muwe mmeainisha eneo la ujenzi wake na mmeshughulikia hati husika nitafika kukagua," alisema.

Aidha, Profesa Kabudi akifafanua kuhusu dhana na chimbuko la kuanzishwa kwa sheria ya msaada wa huduma za kisheria alisema ni utekelezaji wa takwa la Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema kulingana na Ilani hiyo sura 6 ukurasa wa 161 hadi 181 inazungumzia ajenda ya Utawala Bora, Maadili kwenye Utumishi wa Umma, Rushwa, Demokrasia na Haki za Binadamu na kimsingi Wizara ya Katiba na Sheria ndio msimamizi katika kuhakikisha inapanua wigo kwa kuimarisha huduma hizo.

"Kabla ya kutungwa kwa sheria hiyo msaada wa kisheria ulikuwa unatolewa kwa wale tu wenye makosa ya jinai, na makosa yenyewe ni yale ambayo adhabu yake ni kifo. Lakini sasa sheria hii mpya imeruhusu na kupanua wigo kwa fursa hiyo kutolewa kwa wananchi wote," alisema.

Kwa mujibu wa Ilani ya CCM pamoja na mambo mengine, imesisitizwa kwamba huduma hiyo ya msaada wa kisheria inapaswa kutolewa kwa kila halmashauri ya wilaya na ulenge zaidi makundi ya wanawake, watoto na wajane.

Kupitia ziara hiyo alikumbusha juu ya takwa la Ilani kuhusu kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa haki za kupata elimu, afya, maji safi na salama na nyinginezo huku akiwataka watu kutambua kwamba hizo pia ni haki za msingi za binadamu na si zile za kisiasa pekee ambazo zimezoeleka na wengi.

Pia aliitaka jamii kuwa na mtazamo chanya katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani kujitokeza na kutoa ushahidi ili kurahisisha mwenendo wa mashauri hayo.

Kuhusu uendeshaji wa mashauri kwa kutumia lugha ya Kiswahili, Profesa Kabudi kupitia ziara hiyo alisema kwa sasa wapo kwenye hatua ya kutengeneza kamusi ya kiswahili cha kisheria itakayotafsiri sheria mbalimbali.

"Lugha hii ni fahari kwa taifa, na lengo hasa la kuendelea na hatua ya kutengeneza kamusi na kitabu cha kiswahili cha kisheria lengo hasa ni kuongeza 'access to justice' na tunatarajia mpaka ifikapo Juni 2022 kanuni za sheria mbalimbali zitakuwa zimetafsiriwa," alisema.

Kuhusu kukithiri kwa makosa ya kiuandishi kwenye kuandika kiswahili cha kiserikali Profesa Kabudi alisema anasikitishwa sana na namna watumishi walio wengi 'kubananga' (kuharibu) lugha hiyo na kujikuta wakiingiza na kutumia ofisini lugha za mitaani zisizo na fasihi stahiki.

"Nimekasirika, nimefadhaika, nimeghadhabika kuona ndani ya serikali baadhi ya watumishi wameanza kupoteza umahiri wa kuandika kiswahili cha kiserikali na badala yake kinatumika kile cha mtaani. Ifahamike serikali ina kiswahili chake," alisisitiza na kuongeza;

Miaka ya nyuma ilikuwa mtumishi hawezi kupanda daraja bila ya kufaulu mtihani wa kiswahili kigumu uliotungwa na chuo cha utumishi wa umma magogoni..ni lazima tuanze kujifunza na kuandika nyaraka na miongozo kwa kutumia kiswahili cha serikali.

Awali, Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Mkoa wa Singida, Mkambazi Kazen, alisema miongoni mwa changamoto zinazokabili sekta ya utoaji haki mkoani hapa ni kuwepo kwa Mahabusi wengi katika baadhi ya magereza.

Suala lingine ni kesi nyingi za ukatili wa kijinsia kama zile za ubakaji, ulawiti na kuwapa mimba wanafunzi zimekosa ufanisi kutokana na kupata ushirikiano mdogo kwa kukosa mashahidi wa kesi.

Pia Kazen alisema pamoja na changamoto nyingi zilizopo hasa kutokuwepo kwa Mahakama Kuu ndani ya mkoa, uhaba wa vitendea kazi, watumishi wanaohusika na utoaji wa haki jinai na baadhi ya wilaya kukosa mahakama za wilaya ni pigo na hali hiyo inafifisha ustawi wa utoaji haki.

Waziri Kabudi baada ya kukutana na viongozi waandamizi mkoani hapa, akiwemo Mkuu wa Mkoa Dk. Binilith Mahenge, pia anatarajia kukutana na viongozi na watumishi wote wanaohusika na utoaji haki jinai kwenye wilaya za Ikungi, Iramba, Singida, Mkalama na Manyoni.

TANESCO SINGIDA YATOA ELIMU KWA WANANCHI KULINDA MIUNDOMBINU YA NJIA YA MSONGO WA UMEME WA 400 KV

Afisa Usalama wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Singida, Davis Mkwiche, akionesha moja ya chuma  vinavyofunguliwa kwenye nguzo za chuma za njia ya msongo wa umeme mkubwa wa 400KV wa mradi wa usafirishaji wa umeme  kutoka Singida kupitia Manyara Arusha hadi Kenya katika mkutano wa hadhara wa kutoa elimu ulioandaliwa na Tanesco wenye lengo la kutoa elimu kwa wananchi ya kulinda miundombinu  hiyo baada ya kujitokeza kwa baadhi ya watu wasio waaminifu wa Kijiji cha Sagara Kata ya Itaja na maeneo nengine wilayani Singida kudaiwa kuanza kuiba vyuma vya nguzo za umeme wa mradi huo. 

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Singida katika mkutano huo Afisa Tarafa ya Mungumaji, Ally Mwendo, akizungumza kwenye mkutano huo.
       Mkaguzi wa Polisi Ninga Gewe akizungumza kwenye mkutano huo  kwa niaba ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Singida.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Itaja,  Philipo  Mbwambo, akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa Uhusiano na Huduma  kwa  Wateja wa Tanesco Mkoa wa Singida, Rehema Mwaipopo, akigawa vipeperusha kwa wananchi kwenye mkutano huo.
Wananchi wakisoma vipeperushi vya Tanesco  kwenye mkutano huo.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Wakina mama wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Diwani wa Kata ya Itaja, Paul  Abdallah, akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Itaja,  Swalehe Shabani, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Sagara,  Francis Langu, Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkazi wa Kijiji hicho, Michael Kasyani akiuliza swali.
Mkazi wa Kijiji hicho, Richard Amas akiuliza swali.
Mkazi wa Kijiji hicho, Charles Kitiku akiuliza swali.

 Mkazi wa Kijiji hicho, Hawa Hussein akiuliza swali.



 Na Dotto Mwaibale, Singida 


SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Singida kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi limetoa onyo kwa mtu yeyote atakayebainika akihujumu miundombinu ya njia kuu ya umeme wa 400 KV unaoanzia Singida kupitia Manyara hadi Namanga mkoani Arusha kwenda nchini Kenya.

Onyo hilo limetolewa katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Tanesco wenye lengo la kutoa elimu kwa wananchi ya kulinda miundombinu  hiyo baada ya kujitokeza kwa baadhi ya watu wasio waaminifu wa Kijiji cha Sagara na maeneo nengine wilayani Singida kudaiwa kuanza kuiba vyuma vya nguzo za umeme wa mradi huo. 

Akizungumza kwenye mkutano huo Afisa Usalama wa Tanesco Mkoa wa Singida, Davis Mkwiche alisema inasikitisha sana kuona mradi huo mkubwa unaotekelezwa na Serikali kwa fedha nyingi zinazotokana na kodi za wananchi ukianza kuhujumiwa na watu wachache kwa kuharibu miundombinu mbinu yake.

"Njia  ya mradi huu hivi sasa ipo katika hatua za mwisho za ujenzi na kama mambo yatakwenda vizuri miezi miwili ijayo itakabidhiwa kutoka kwa mkandarasi kuja kwetu lakini tukiwa katika hatua hizi za mwisho imebainika baadhi ya watu wachache wenye nia hovu wameanza kufanya vitendo vya hujuma kwenye njia ya kusafirisha umeme," alisema  Mkwiche.

Alisema watu hao wanafungua vyuma kwenye nguzo za chuma za msongo wa umeme wa 400KV vinavyo julikana kwa jina la kitaalumu miiba au vifaa vinavyowekwa kuzuia mtu asiyetakiwa, kuidhinishwa, asiye na utaalamu kuweza kupanda kwenye hizo nguzo.

Uchunguzi wa awali uliofanywa na shirika hilo umebaini kuwa vyuma hivyo vikishatolewa kwenye nguzo hizo vinaenda kutumika kwenye matumizi mbalimbali ikiwemo kuwekwa kwenye mikokoteni inayovutwa na wanyama, wengine wanaenda kutengenezea bangiri, utengenezaji wa mikuki hama mishale na wengine wanaenda kuviuza kwa wanunuzi wa vyuma chakavu.

Akizungumza kwenye mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Singida, Mkaguzi wa Polisi Ninga Gewe alisema kwa mujibu wa mwenendo wa makosa ya jinai Tanzania kuanzia kifungu cha 14 hadi 16 kinamruhusu raia au mwananchi mzalendo kumkamata mhalifu bila kumpiga na kumpeleka ofisi ya mtendaji wa kijiji au kituo cha polisi lakini awe ametenda kosa husika na siyo kwa kumuonea.

Alisema kosa lolote la kuharibu au kuiba miundombinu ya Tanzania ni kosa la kuhujumu uchumi wa nchi ambapo mtuhumiwa akikamatwa hakuna dhamana.

Gewe alitumia nafasi hiyo kutoa onyo kwa wananchi wa kijiji hicho na maeneo mengine kuacha mara moja vitendo hivyo vya kuhujumu miundombinu ya Serikali na jeshi la polisi alipendi kuona mwananchi hata mmoja akikamatwa kwa tuhuma za kuharibu miundombinu na kujikuta akifungwa kifungo cha maisha kwa sababu hiyo. 

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Singida katika mkutano huo Afisa Tarafa ya Mungumaji, Ally Mwendo alisema miradi hiyo ni lazima ilindwe kwa nguvu zote na kuwa mlinzi wa kwanza ni mwananchi mwenyewe na sio mtu mwingine.

Aidha ametoa maagizo kwa viongozi wote wa kijiji hicho kuwa walinzi wa mradi huo na mingine yote ambayo inatekelezwa na iliyokwisha kamilika.

Afisa Mkuu Usalama na Uzuiaji kutoka Makao Makuu ya Tanesco, Misana Gamba alisema wapo timu ya maafisa kutoka makao makuu, Mkoa wa Singida na Manyara katika ziara ya kutoa elimu ya utunzaji wa miundombinu hususani ya msongo huo mkubwa wa umeme unaoanzia Singida, Babati Manyara, Namanga hadi Kenya baada ya kuona unaanza kuhujumiwa.

Alisema idara ya usalama Tanesco makao makuu kwa kushirikiana na idara ya miradi, ofisi ya uhusiano na mameneja wa mikoa wataendelea kutoa elimu maeneo mbalimbali ya shirika hilo ili kuzuia vitendo hivyo na kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa kufuatia utoaji wa elimu hiyo kwani wananchi wamekuwa wakiuliza maswali mengi na kuahidi kutunza mradi huo.

Afisa Uhusiano na Huduma  kwa  Wateja  Tanesco Mkoa wa Singida, Rehema Mwaipopo, alisema ni wajibu wa kila mwananchi unapopita mradi huo kulinda miundombinu ya njia ya umeme huo ambapo alitoa namba kwa ajili ya kupiga ili kuwataja watu watakao bainika wakihujumu mradi huo kuwa ni 0755873035 na 0714477445.5.

Sunday, August 1, 2021

RC SINGIDA AHIMIZA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUPATA CHANJO YA CORONA

Kaimu Afisa Tarafa ya Ikungi Yahaya Njiku akizungumza kwa niaba ya Mkuu  wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hadhara Tukufu ya Mazazi ya Mtume Mohammad (S.AW) iliyofanyika Issuna  Wilaya ya Ikungi mkoani hapa jana ambayo iliandaliwa na  Jumuiya ya Kinamama wa kiislamu wilayani humo (JUWAKITA)

Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro, akizungumza na Waislamu mkoani hapa kupitia hadhara hiyo.
Katibu Mkuu Baraza Kuu la Waisalamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida Sheikh Burhan Mlau, akizungumza kwenye hadhara hiyo.
Shekhat wa Mkoa wa Singida Zeana Salum, akizungumza kwenye hadhara hiyo
 Hadhara hiyo ikiendelea.
Viongozi wakiwa meza kuu.
Kaimu Afisa Tarafa ya Ikungi Yahaya Njiku, akiteta jambo na Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro  kwenye hadhara hiyo.

Mdau Shabani Mukee (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu Baraza Kuu la Waisalamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida Sheikh Burhan kwenye hadhara hiyo.



Na Dotto Mwaibale, Ikungi


MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge amewaomba wananchi mkoani hapa kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya kujikinga na janga la wimbi la tatu la ugonjwa wa virusi vya Corona.

Ombi hilo limetolewa na Kaimu Afisa Tarafa ya Ikungi Yahaya Njiku kwa niaba ya Dkt.Mahenge ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hadhara Tukufu ya Mazazi ya Mtume Mohammad (S.AW) iliyofanyika Issuna  Wilaya ya Ikungi mkoani hapa jana ambayo iliandaliwa na  Jumuiya ya Kinamama wa kiislamu wilayani humo (JUWAKITA)

"Tumuunge mkono Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kujitokeza kupata chanjo hiyo ambayo aliizindua kwa kuchanjwa na kufuatiwa na viongozi wengine mbalimbali ambapo hapa mkoani kwetu itaanza kutolewa wakati wowote katika vituo vilivyoainishwa kwenye wilaya zote,". alisema Njiku.

Akizungumza na wakina mama hao Njiku alisisitiza kuzidi kuwa wacha Mungu na kujishughulisha na shughuli za ujasiriamali ili waweze kuinuka kiuchumi bila kusahau kuvaa mavazi ya stara ya kiislamu.

Aidha Njiku aliwahimiza wakina mama hao kuishi vizuri na waume zao na kuzingatia haki za ndoa na kutunza familia zao.

Njiku alipongeza ushirikiano uliopo baina ya Serikali na taasisi za dini jambo lililosaidia kuimarisha amani na mshikamano kwa wananchi kote nchini.

Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro amewaomba waislamu mkoani hapa kuendelea kuchukua tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa wa corona hasa huu wa wimbi la tatu ambao umeelezwa kuwa ni mkali kuliko wa awamu ya kwanza na wa pili.

Nassoro aliwataka waislamu kuendelea kumuomba Mungu kuwaepusha na ugonjwa huo na kueleza wasifanye mzaha katika jambo hilo.

Alisema Tanzania bado tuna fursa kubwa kutokana na kutokuwepo kwa zuio la kutotoka nje kutokana na janga ili la Corona kama ilivyo nchi zingine ambazo wananchi wake wanashindwa hata kwenda kuswali.

Shekhat wa Mkoa wa Singida Zeana Salum alisema jumuiya hiyo ya akina mama katika  wilaya hiyo imejiwekea mikakati ya kutembelea kata zote 28 na kuwa hadi sasa wametembelea kata 18 huku wakihamasisha kuwepo kwa madrasa za akina mama na watoto katika kila msikiti.

Katika hadhara hiyo walifanya harambee ili kupata fedha za kujenga ofisi yao ya wilaya ambapo walimuomba mkuu wa mkoa awasaidie ambapo mahitaji ya kukamilisha ujenzi huo  ni Sh.19,675,000. 

MBUNGE KINGU ACHANGIA MIFUKO 20 YA SARUJI, UTENGENEZAJI MADIRISHA KANISA LA KKKT

Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  (KKKT)  Dayosisi ya Kati, Mchungaji Dkt. Syprian Hilinti (kushoto) akizungumza katika harambee ya ujenzi wa nyumba ya Mchungaji wa Kanisa hilo Usharika wa Chungu lililopo Ihanja wilayani Ikungi mkoani Singida. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu


Wachungaji wa kanisa hilo wakiwa kwenye harambee hiyo.
Waumini wakiwa kwenye harambee hiyo.



Na Dotto Mwaibale, Ikungi


MBUNGE wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu amechangia saruji mifuko 20 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  (KKKT) Usharika wa Chungu lililopo  Ihanja wilayani Ikungi mkoani Singida.

Kingu ametoa msaada huo wakati wa harambee iliyofanyika katika kanisa hilo leo hii ambayo iliongozwa na Msaidizi wa Askofu wa Kanisa hilo  Dayosisi ya Kati, Mchungaji Dkt. Syprian Hilinti.

Aidha katika harambe hiyo Kingu alichangia kutengeneza madirisha yote ya nyumba ya mchungaji wa ushirika huo.

Akizungumza katika harambee hiyo Mchungaji Dkt.Syprian Hilinti alimshukuru Mbunge Kingu na kumuombea kwa Mungu kutokana na mchango wake huo mkubwa kwa kanisa.

Baadhi ya waumini wa kanisa hilo walimshukuru mbunge huyo kwa msaada huo na kumuelezea kuwa ni mtu anayejitoa kusaidia shughuli nyingi za kijamii na misaada ya ujenzi wa makanisa na misikiti katika jimbo hilo.

"Kingu amekuwa akijitoa sana kuchangia shughuli za maendeleo na kuchangia ujenzi wa makanisa na misikiti hakika Jimbo la Singida Magharibi tumepata mbunge,". alisema muumini wa kanisa hilo ambaye hakupenda kutaja jina lake.

SUA, NEMC WAJIPANGA KUTAFUTA SULUHISHO LA UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI NA MAZINGIRA BONDE LA MTO RUFIJI

Mkurugenzi wa Masomo ya Shahada za juu utafiti uhauwilishaji wa Teknolojia na Ushauri wa Kitaalamu SUA,   Prof. Esron Karimuribo akitoa salamu za Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wakati wa uzinduzi wa mradi wa “usimamizi endelevu wa madakio ya maji kupitia tathmini ya kuimarisha mtiririko wa maji kwa mazingira na utekelezaji wake katika kulinda Ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi iliyofanyika wilayani humo mkoani Mbeya juzi.
Meneja Tafiti za Mazingira kutoka NEMC ambaye pia ni Mtafiti Mkuu mwenza wa mradi huo, Rose Mtui akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu (NEMC) Mhandisi Dkt. Samuel Mafwenga.
Mratibu wa mradi Dkt. Winfred Mbungu akitambulisha mradi huo wa EFLOWS kwa wadau ili kujua utekelezaji wake,malengo yake na matarajio yake utakapokamilika.
Mtafiti Mkuu wa mradi huo wa EFLOWS Prof. Japhet Kashaigili ambeye pia ni Mratibu wa tafiti na machapisho SUA akieleza malengo la Warsha hiyo ya siku moja ya wadau.
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Reuben Mfume akifungua washara hiyo ya uzinduzi wa mradi wa utafiti wa EFLOWS.
Wadau wakifuatilia hotuba za ufunguzi wa mradi huo wa EFLOWS.
Warsha ikiendelea.
Picha ya pamoja ya wadau wa mradi huo na mgeni rasmi.
 


Na Calvin Gwabara,  Mbarali.

 

SERIKALI Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya imeahidi kutoa ushirikiano ili kufanikisha kupatikana kwa matokeo mazuri ya mradi wa utafiti na kuwezesha kupatikana kwa suluhisho la changamoto za uharibifu wa mazingira hasa katika vyanzo vya maji na dakio la mto rufiji na bonde lake lenye  mchango mkubwa katika maisha ya binadamu,mimea na viumbe vingine.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfume katika warsha ya uzinduzi wa mradi “usimamizi endelevu wa madakio ya maji kupitia tathmini ya kuimarisha mtiririko wa maji kwa mazingira na utekelezaji wake katika kulinda Ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi kutokana na athari za shughuli za kibinadamu Tanzania” iliyofanyika wilayani humo mkoani Mbeya.

‘’Mimi kama mkuu wa wilaya nina majukumu mengi lakini miongoni mwa majukumu hayo katika wilaya hii ni kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli za kiuchumi vizuri na kuboresha maisha yao lakini kuhakikisha nasimamia sheria na usimaizi wa sheria,kanuni na miongozo mbalimbali ya uhifadhi wa mazingira jambo ambalo sio rahisi sana maana wananchi wanahitaji bonde hili kuzalisha mali lakini pia nisimamie sheria ili kilimo chao kisiathiri mazingira vyanzo vya maji kwa hiyo ninapambana kuhakikisha nabalansi vitu hivyo viwili kwahiyo ujio wa mradi huu utanisaidia na kusaidia kusaidia kurahisisha kazi yangu’’  alisema Mfume.

Aidha, nawapongeza watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC)  kwa kuanzisha mradi huu wa utafiti na kuona kwamba masuala ya mazingira kama vile umwagiliaji, kilimo kandokando ya kingo za mito, ufugaji wa mifugo ndani ya kidakio cha mto Mbarali na Bonde la Rufiji pamoja na ongezeko la watu, vinasimamiwa kwa uhifadhi kamilifu wa eneo la Magharibi mwa Ukanda wa Bahari ya Hindi kwamba ni  muhimu zaidi kwa ajili ya mtiririko endelevu wa maji kuelekea Mradi wa Kufua umeme wa Mwalimu Nyerere (Julius Nyerere Hydro Power Project  - JNHPP).’’. 

Akizungumzia uharibifu huo Mfume alisema , kuna masuala mengi ndani ya dakio la Mbarali kama vile ukataji wa miti, kilimo ndani ya kingo za mto na vyanzo vya maji (Vinyungu), ongezeko kubwa la watu, ufugaji wa mifugo na skimu za umwagiliaji ambao una matokeo hasi kwenye mtiririko wa maji, uchafuzi wa mazingira, kupungua kwa ubora wa maji na kuongezeka kwa tope kunakokwamisha mtiririko endelevu wa maji kwa ajili ya mazingira. 

‘’Ni matumaini yangu kwamba mradi huu utakuja na ufumbuzi wa changamoto zilizobainishwa na kusaidia utekelezaji wa mtiririko endelevu wa maji kwa mazingira kwenye mto Mbarali kwa mara ya kwanza hapa Tanzania na Kama Serikali, tunawaahidi kutoa ushirikiano na msaada wowote unaohitajika katika kuhakikisha malengo ya mradi yanafikiwa kikamilifu na kwa mafanikio makubwa’’ alisema Mfume. 

Akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa (NEMC) Mhandisi Dkt. Samuel Mafwenga, Meneja Tafiti za Mazingira kutoka NEMC ambaye pia ni Mtafiti Mkuu mwenza wa mradi huo Rose Mtui alisema kufuatia majukumu ya utafiti mahususi ambayo yamefafanuliwa bayana katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira namba 191; NEMC kwa kushirikiana na taasisi za kitaaluma/utafiti zimekuwa zikitengeneza miradi/programu  na kufanya tafiti na mojawapo ni kama mradi huu unaozinduliwa leo ili kutatua matatizo mbalimbali ya kimazingira. 

‘’Tunajua mazingira na mifumo ikolojia na bioanuai zilizopo (nchi kavu na majini) na huduma zinazopatikana vinaendelea kupata changamoto kutokana na ongezeko la idadi ya watu, matumizi yasiyo endelevu, uchafuzi utokanao na kemikali n.k.. Hii ni muhimu kwa kuwa miradi na program zinalenga katika kuhakikisha rasilimali zote na mifumo ikolijia ambayo watu wanaitegemea kwa maisha inatunzwa’’ alifafanua Mtui. 

Akitoa salamu za Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Mkurugenzi wa Masomo ya Shahada za juu utafiti uhauwilishaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalamu SUA  Prof. Esron Karimuribo alisema hivi sasa nchi imeanza kuona matokeo ya uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji kama vile upungufu wa maji yanayotiririka mitoni hasa wakati wa kiangazi,mafuriko wakati wa masika,ubora hafifu wa maji kwaajili ya matumizi ya nyumbani lakini pia matokeo yanayoonekana kwenye ikolojia nyingine za nchi kavu na majini. 

‘’Kwa matokeo haya,hatuwezi kuendelea kuyafumbia macho haya yote ambayo yanaleta madhara kwa binadamu,Mifugo,wanyamapori na mazingira hivyo nipende kuwapongeza watafiti kutoka SUA na NEMC kwa kuwa na maono ya kuanzisha mradi huu ambao unakusudia katika utunzaji endelevu wa vyanzo vya maji’’ alisema Prof. Karimuribo. 

Prof. Karimuribo aliongeza kuwa SUA inatambua umuhimu wa kusimamia na kuhifadhi vyanzo vya maji na mazingira yake ili yapatikane maji kwa njia endelevu kwa ajili ya kizazi hiki na pia vizavi vijavyo na hivyo akatumia nafasi hiyo kuwakaribisha wale wote wenye sifa na nia ya kujiunga na mwaka huu wa masomo kuomba kusoma SUA na kuwaahidi kuwa hawata jutia hasa ukizingatia ubora wa elimu wanayoitoa Pamoja na umahiri wa watafiti wa chou hicho katika tafiti na kufundisha. 

Mtafiti Mkuu wa mradi huo wa utafiti wa EFLOWS Prof. Japhet Kashaigili ambaye pia ni Mratibu wa tafiti na machapisho SUA alisema lengo la warsha hiyo ni kuwafahamisha wadau madhumuni ya mradi huo wa utafiti na matokeo yake,Kujua matarajio ya wadau kutokana na matokeo ya utafiti,Kujua na kuyabainisha majukumu yatakayofanywa na kila mdau katika kuifikia na kuanisha maeneo ya ushirikiano ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa na kuleta matokeo chanya kwa taifa. 

‘’Kuna usemi unasema ukitaka kwenda kasi nenda peke yako lakini kama unataka kufika mbali nenda na wenzako usemi huu tunataka kuuzingatia kwa kilahali ili tuweze kupata yote kwa wakati mmoja kwa maana ya kwamba twende kasi ili tufike haraka lakini pia twende Pamoja ili tufike mbali ili utafiti huu uweze kuleta mchango kwa wadau wote kwa manufaa mapana ya taifa, alisisitiza Prof. Kashaigili. 

Akitambulisha mradi huo Mratibu wa mradi Dkt. Winfred Mbungu alisema mradi unalenga kufanya utafiti kwenye usimamizi endelevu wa madakio ya maji kupitia tathmini ya kuimarisha mtiririko wa maji kwa mazingira na utekelezaji wake katika kulinda Ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi kutokana na athari za shughuli za kibinadamu kwenye bonde hilo. 

‘’Mradi utajikita Zaidi kwenye kushirikiana na wadau wote ambao wanahusika kwenye bonde hilo kwanza kwa kutoa Elimu, kuibua mbinu bora za matumizi na usimamizi salama wa bonde na kuzipendekeza namna ya kuzitekeleza kwa Pamoja ili mwisho wa siku kila mmoja ashiriki na kuona thamani ya utunzaji huo wa vyanzo vya maji kwenye bonde hilo’’ alifafanua Dkt. Mbungu.

 Alisema lengo kuu ni kupunguza athari zinazotokana na shughuli za kibinadamu kuongeza uwezo wa kuthamini na kutathimini mtiririko wa mito kwa mazingira kwa kurejesha hali ya mtiririko wa maji ulio endelevu,kufanya tathimini ya mtitirko wa mito kwa mazingira katika Madakio ya mito ili kutoa muongozo wa  usimaizi endelevu wa mtiririko wa maji na pia utekelezaji wa mtitiriko uliopendekezwa kwa usimamizi endelevu wa rasilimali za maji. 

Dkt. Mbungu alisema mradi huu ni moja ya miradi mitano inayotekelezwa katika katika nchi tisa kufikia malengo manne ya mradi mama mkubwa ambao unaitwa WIOSAP ambao malengo yake ni usimamizi wa makazi maalumu ya viumbe,Kuboresha ubora wa maji ili ifikapo mwaka 2035 maji katika nchi hizo za mradi yafikie katika viwango vya kimataifa,Usimamizi endelevu wa mtiririko wa mito na utawala na ushirikiano wa kikanda.