Sunday, August 15, 2021

WAKURUGENZI HALMASHAURI YA MANYONI WAKABIDHIANA OFISI


Mkururgenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Melkzedeki Humbe na Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya hiyo  Charles Fussi (ushoto) wakikabidhiana ofisi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Jumanne Mlagaza (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi hao.

Wakurugenzi Melkzedeck Humbe (kushoto) na Charles Fussi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya ofisi.

Mkurugenzi Charles Fussi (wa pili kulia) na Afisa Kilimo Fadhili Chimsala na Mkaguzi wa Ndani, Rweikiza wakimuonesha mashamba ya korosho Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya  Manyoni, Melkzedeck Humbe.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Jumanne Mlagaza akitoa shukrani kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Charles Fussi kwa kuweza kukabidhi ofisi kwa mkurugenzi aliyechukua nafasi yake.

Wakuu wa Idara na vitengo wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi na Mwenyekiti wa Halmashauri baada ya sherehe hiyo ya makabidhiano.


Na  Alinikyisa Humbo, Manyoni 


ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni  Charles Fussi amemkabidhi ofisi Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Halmashauri hiyo Melkzedeck Humbe katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika jana wilayani humo.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Halmashauri hiyo Melkzedeck Humbe alisema anategemea ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi wa Halmashauri hiyo, wakuu wa idara na watumishi wote.

Humbe alisema kwamba bila ushirikiano hakuna kitakachoweza kufanyika ambapo alitumia nafasi hiyo kumpongeza  aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Charles Fussi kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa kipindi chote alichoweza kuhudumu hasa katika usimamimizi wa shughuli zote za maendeleo na ubunifu wa mradi wa kilimo cha korosho.

"Sijaja hapa kuanzisha kazi bali nimekuja kuendeleza kazi iliyoachwa na mtangulizi wangu Fussi na kwamba kama ambavyo kauli ya Rais Samia Suluhu isemavyo kwamba kazi iendelee basi ndivyo ninavyotamani Manyoni iendelee kazi alizokuwa akiifanya mwenzangu ziendelee". alisema Humbe.

Alisema amefika Manyoni kuendeleza yale yote ambayo Fussi aliweza kuyaibua ikiwa ni utekelezaji wa ilani na si vinginevyo.

Kwa upande wake Fussi amewashukuru watumishi wote na kuahidi kwamba ataendelea kutoa ushirikiano pale watakapoona inafaa ili kuleta tija ya maendeleo kwa wananchi wa Wilaya ya Manyoni.

Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Jumanne Mlagaza alitoa shukrani kwa Fussi kwa kipindi chote walichoweza kufanya kazi pamoja na kuwa anaamini Mkurugenzi aliyekabidhiwa ofisi ataendeleza ushirikiano wa utendaji kazi kati ya Ofisi ya Mkurugenzi na ofisi yake.

Makabidhiano hayo yamehudhuriwa na Wakuu wa Idara na Vitengo vyoe na,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na baada ya makabidhiano ya ofisini ya nyaraka basi waliweza pia kutembelea mradi mama wa kilimo cha korosho katika maeneo yote yalipo mashamba hayo wilayani humo.

Friday, August 13, 2021

DK. MABULA AWAPONGEZA NHC KWA KUWA NA MIKAKATI YENYE TIJA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula, akizungumza juzi na watumishi wa idara za ardhi na wadau mbalimbali wa Mkoa wa Singida katika ziara yake ya siku moja ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi. Kutoka kulia ni Mwakilishi wa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida Mjini, Eva Jeremia na Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida, Shamim Hozza.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula, akimkabidhi hati za Viwanja Afisa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Mkoa wa Singida, Vicent Mboya.
Meneja wa NHC Mkoa wa Singida, Judith Mwalongo akisoma taarifa ya utekelezaji katika kikao hicho.

Muonekano wa Jengo la NHC Mkoa wa Singida.


Na Dotto Mwaibale, Singida.

NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amelipongeza Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) Mkoa wa Singida kwa kuwa na mikakati endelevu na yenye tija.

Mabula alitoa pongezi hizo mkoani hapa wakati akizungumza na watumishi wa idara za ardhi na wadau mbalimbali katika ziara yake ya siku moja ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi kwenye kikao kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida juzi.

"Nimeisoma taarifa yenu nawapongeza sana kwa mikakati yenu yenye tija na kazi nzuri mnayoifanya" alisema Mabula.

Akitoa taarifa ya utekelezaji na jinsi walivyojipanga kuongeza mapato Meneja wa shirika hilo Mkoa wa Singida Judith Mwalongo alisema  mwaka huu wa fedha 2021/2022 wamepanga kubadilisha miundo ya baadhi ya majengo yaliyopo mjini ili waweze kupata wapangaji wengi zaidi kwenye maeneo hayo.

Alitaja mkakati mwingine kuwa ni kufuatilia kwa ukaribu makao makuu ya Shirika hilo ili waweze kupata fedha za kuweza kuendeleza na kuboresha nyumba ambazo zimekoma kuingiza kodi sababu ya uchakavu na hivyo kuhitaji ukarabati mkubwa.

Mwalongo alisema wanatarajia kufanya uhakiki wa vipimo kwa nyumba zote za Shirika hilo zilizopangishwa ili kubaini nyumba zenye tozo ndogo kulingana na matumizi ya wakati huu ya wapangaji na kuhakikisha wapangaji wote wanalipa kodi ya kila mwezi kwa wakati kwa kuwafuatilia kwa karibu ili kufanikisha malengo waliojiwkea ya kuwa na bakaasifuri (Nil balance).

Alitaja malengo yao mengine kuwa ni kuongeza wigo wa matangazo ya sehemu zilizo wazi kwenye vyombo vya habari vya ndani ya mkoa na nje ya mkoa pamoja na mitandao ya kijamii.

Aidha Mwalongo alisema wamelenga kulishawishi shirika hilo liweze kuendeleza viwanja vyao vilivyo wazi kwa kujenga nyumba za makazi jambo litakalosaidia kuongeza mapato kwenye shirika na wananchi kupata huduma za nyumba kwa urahisi zaidi.

Alisema wanatarajia kukarabati Jengo la Hotel ya Lake Hill na nyumba zingine za zamani ambazo zilijengwa kwa udongo na kuwa nyumba zote hizo ziko katikati ya mji na zikifanyiwa matengenezo zitaongeza pato ndani ya Shirika na vilevile kupendezesha mji.

Mwalongo aliongeza kuwa mkakati wao mwingine ni kutafuta zabuni za ujenzi wa nyumba au majengo mapya yanayopangwa kujengwa na kuendelezwa na taasisi mbalimbali mkoani hapa ili waweze kuongeza mapato ya Shirika kwa ujumla.

Alisema kwa mwaka wa Fedha 2020/2021 mkoa ulijiwekea lengo la kukusanya kodi kiasi cha Shilingi 587,338,398.74 a hadi wanafunga mwaka huo wa Fedha walifanikiwa kukusanya Shilingi 533,874,759.00 ambayo ni sawa na Asilimia 90.9 (90.9%).

Alisma kwa mwaka huu 2021/2022 wamejiwekea malengo ya kuweza kukusanya kodi kwa kiwango cha asilimia mia (yani kuwa na bakaasifuri). Pia wataendelea kufanya ufuatiliaji wa madeni ya zamani ili kuhakikisha madeni yote ya zamani yashirika yanalipwa. 

DK. MABULA AWAPONGEZA NHC KWA KUWA NA MIKAKATI YENYE TIJA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula, akizungumza juzi na watumishi wa idara za ardhi na wadau mbalimbali wa Mkoa wa Singida katika ziara yake ya siku moja ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi. Kutoka kulia ni Mwakilishi wa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida Mjini, Eva Jeremia na Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida, Shamim Hozza.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula, akimkabidhi hati za Viwanja Afisa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Mkoa wa Singida, Vicent Mboya.
Meneja wa NHC Mkoa wa Singida, Judith Mwalongo akisoma taarifa ya utekelezaji katika kikao hicho.

Muonekano wa Jengo la NHC Mkoa wa Singida.


Na Dotto Mwaibale, Singida.

NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amelipongeza Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) Mkoa wa Singida kwa kuwa na mikakati endelevu na yenye tija.

Mabula alitoa pongezi hizo mkoani hapa wakati akizungumza na watumishi wa idara za ardhi na wadau mbalimbali katika ziara yake ya siku moja ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi kwenye kikao kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida juzi.

"Nimeisoma taarifa yenu nawapongeza sana kwa mikakati yenu yenye tija na kazi nzuri mnayoifanya" alisema Mabula.

Akitoa taarifa ya utekelezaji na jinsi walivyojipanga kuongeza mapato Meneja wa shirika hilo Mkoa wa Singida Judith Mwalongo alisema  mwaka huu wa fedha 2021/2022 wamepanga kubadilisha miundo ya baadhi ya majengo yaliyopo mjini ili waweze kupata wapangaji wengi zaidi kwenye maeneo hayo.

Alitaja mkakati mwingine kuwa ni kufuatilia kwa ukaribu makao makuu ya Shirika hilo ili waweze kupata fedha za kuweza kuendeleza na kuboresha nyumba ambazo zimekoma kuingiza kodi sababu ya uchakavu na hivyo kuhitaji ukarabati mkubwa.

Mwalongo alisema wanatarajia kufanya uhakiki wa vipimo kwa nyumba zote za Shirika hilo zilizopangishwa ili kubaini nyumba zenye tozo ndogo kulingana na matumizi ya wakati huu ya wapangaji na kuhakikisha wapangaji wote wanalipa kodi ya kila mwezi kwa wakati kwa kuwafuatilia kwa karibu ili kufanikisha malengo waliojiwkea ya kuwa na bakaasifuri (Nil balance).

Alitaja malengo yao mengine kuwa ni kuongeza wigo wa matangazo ya sehemu zilizo wazi kwenye vyombo vya habari vya ndani ya mkoa na nje ya mkoa pamoja na mitandao ya kijamii.

Aidha Mwalongo alisema wamelenga kulishawishi shirika hilo liweze kuendeleza viwanja vyao vilivyo wazi kwa kujenga nyumba za makazi jambo litakalosaidia kuongeza mapato kwenye shirika na wananchi kupata huduma za nyumba kwa urahisi zaidi.

Alisema wanatarajia kukarabati Jengo la Hotel ya Lake Hill na nyumba zingine za zamani ambazo zilijengwa kwa udongo na kuwa nyumba zote hizo ziko katikati ya mji na zikifanyiwa matengenezo zitaongeza pato ndani ya Shirika na vilevile kupendezesha mji.

Mwalongo aliongeza kuwa mkakati wao mwingine ni kutafuta zabuni za ujenzi wa nyumba au majengo mapya yanayopangwa kujengwa na kuendelezwa na taasisi mbalimbali mkoani hapa ili waweze kuongeza mapato ya Shirika kwa ujumla.

Alisema kwa mwaka wa Fedha 2020/2021 mkoa ulijiwekea lengo la kukusanya kodi kiasi cha Shilingi 587,338,398.74 a hadi wanafunga mwaka huo wa Fedha walifanikiwa kukusanya Shilingi 533,874,759.00 ambayo ni sawa na Asilimia 90.9 (90.9%).

Alisma kwa mwaka huu 2021/2022 wamejiwekea malengo ya kuweza kukusanya kodi kwa kiwango cha asilimia mia (yani kuwa na bakaasifuri). Pia wataendelea kufanya ufuatiliaji wa madeni ya zamani ili kuhakikisha madeni yote ya zamani yashirika yanalipwa. 

Tuesday, August 10, 2021

SERIKALI KUKABIDHIWA RASMI DARAJA LA MSINGI SINGIDA OKTOBA 30,2021

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Singida, Mhandisi Matari Masige (katikati) akimuonyesha jana Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge (kushoto) ujenzi unaoendelea wa mradi wa daraja la Msingi linalo jengwa wilayani Mkalama mkoani humo, ambalo ujenzi wake umegharimu Sh.10.9 Bilioni. 

Viongozi mbalimbali wakiwa eneo la mradi wa ujenzi huo.


Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Singida, Mhandisi Matari Masige (katikati) akimuonyesha jana Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge (kushoto) ujenzi unaoendelea wa mradi wa daraja hilo la Msingi\ Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo.

Diwani wa Kata ya Msingi, Amri Gyuda, akizungumzia daraja hilo.
Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge (kushoto) akizungumza na Mhandisi wa ujenzi wa daraja hilo Method Mwalongo (kulia) wakati akipokea taarifa ya ujenzi wa mradi huo. Katikati mwenye Kombati nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo.
Muonekano wa daraja hilo linalojengwa.
Mafundi wa Kampuni ya Gemen Engineering Company Ltd,  inayojenga daraja hilo wakiwa kazini.
Wananchi wakiwa eneo la mradi wa ujenzi huo.

Muonekano wa daraja la chuma linalotumika kwa sasa.




Na Dotto Mwaibale, Singida


MKANDARASI Gemen Engineering Company Ltd,  anayejenga Daraja la Msingi lililopo Wilaya ya Mkalama mkoani Singida amesema daraja hilo litakabidhiwa rasmi Serikalini Oktoba 30 mwaka huu baada ya ujenzi wake kukamilika.

Hayo yalisemwa na Mhandisi wa ujenzi wa daraja hilo Method Mwalongo wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge katika ziara yake ya siku moja ya kukagua daraja hilo aliyoifanya jana.

"Mheshimiwa mkuu wa mkoa ujenzi wa daraja ili unaendelea vizuri na tunatarajia kulikabidhi serikalini Oktoba 30 mwaka huu,". alisema Mwalongo.

Akipokea taarifa ya ujenzi wa daraja hilo   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge, aliwashukuru viongozi wa Wilaya ya Mkalama, Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Singida kwa ushiriki wao mkubwa wa ujenzi wa daraja hilo ambalo ni tegemeo kubwa kwa uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Dk. Mahenge alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha ujenzi wa daraja hilo na kumtaka mkandarasi kumaliza haraka ujenzi kama alivyoahidi kabla ya mvua hazijaanza kunyesha.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa daraja hilo Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Singida, Mhandisi Matari Masige alisema daraja hilo ambalo limegharimu Sh. 10.9 Bilioni ni kiungo muhimu kati ya Mkoa wa Singida na Mkoa wa Simiyu kupitia Barabara ya Mkoa ya Ulemo, Gumanga na Sibiti. 

" Daraja hili pia ni kiungo muhimu kuunganisha makao makuu ya Wilaya ya Mkalama na Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, kupitia daraja la Sibiti, hadi Mkoa wa Mara," alisema Masige. 

Masige alisema mradi huo ni ahadi ya Hayati Dk. John Magufuli, aliyekuwa Rais wa Tanzania aliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. 

Alisema daraja hilo linajengwa takribani umbali wa meta 10 upande wa juu toka lilipo daraja la sasa likiwa na urefu wa meta 100 zilizogawanywa sawa katika sehemu nne zenye urefu wa meta 25 kila sehemu (spans). 

Alisema daraja hilo lina jumla ya upana wa meta 10.2 zinazojumuhisha upana wa meta 7.6 ikiwa ni sehemu ya njia za kupitisha magari mawili kwa wakati mmoja na sehemu iliyosanifiwa kupita kwa watembea kwa miguu yenye upana wa meta 1.3 kila upande. 

" Ujenzi wa daraja hili pia unahusisha ujenzi wa barabara za maingilio (approach roads) kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilometa 1 (yaani meta 300 upande wa Ulemo na meta 700 upande wa Gumanga) pamoja na kalvati moja lenye ukubwa wa meta 4x2.5 (upana x kimo) upande wa Ulemo".alisema Masige.

Alisema madhumuni ya daraja hilo ni pamoja na kuwaondelea wananchi kero ya usafiri wa barabara waliokuwa wanaipata kutokana na daraja la vyuma la zamani lililokuwa la muda (temporary) kuwa jembamba na ambalo pia nguzo zake zilititia kutokana na kuchimbwa na mkondo wa maji hivyo kuwa hatarishi kwa watumiaji wa barabara na wananchi kwa ujumla. 

Aidha Masige alisema kuwa daraja hilo linajengwa kwa zege na litakuwa la kudumu zaidi ya miaka mia moja. Pia magari zaidi ya Tani 50 yatapita baada ya kukamilika daraja hili. 

Alisema matarajio yao baada ya ujenzi kukamilika ni kuwa hali ya usafiri na usafirishaji kati ya Mkoa wa Singida na Mikoa ya kanda ya ziwa hasa Mkoa wa Simiyu na Mara itaboreka zaidi. Vilevile Wananchi wa Wilaya za Mkalama na Iramba wataboresha hali zao za uchumi kwa kuwa kutakuwa na uhakika wa usafiri wakati wote. 

Alitaja changamoto kuwa kutokana na mvua kubwa zilizonyesha mwanzoni mwa mwezi Novemba, 2019 hadi mwezi Mei, 2020 sehemu kubwa ya kazi za daraja zilisimama kutokana mto kujaa maji hivyo kushindwa kuendelea na kazi, hata hivyo Mkandarasi aliendelea na kazi ya kuinua tuta la barabara kadri hali ya hewa ilivyoruhusu.

Alisema mategemeo yao baada ya mradi huo kukamilika wananchi wa pande zote zinazounganishwa na daraja hilo wataweza kusafiri na kusafirisha mazao yao kwa urahisi zaidi na hivyo kujiongezea kipato na kuinua uchumi wao na wa Taifa kwa Ujumla na vivile kutaunganisha Mkoa wa Singida na ukanda wa Ziwa kupitia daraja la Mto Sibiti ambalo tayari limekamilika.  

Mkuu wa Wilaya ya  Mkalama, Sophia Kizigo aliishukuru Serikali kwa ujenzi wa daraja hilo ambalo litakuwa mkombozi kwa wananchi wa eneo hilo ambao amewataka kuilinda miundombinu yake. 

Sunday, August 8, 2021

SERIKALI YAKAMILISHA UJENZI MRADI WA MAJI WA SH. 192.7 MILIONI IKUNGI.

Wananchi wa Kijiji cha Dung'unyi wilayani Ikungi mkoani Singida wakichota maji jana baada ya Serikali kukamilisha mradi wa maji uliogharimu zaidi ya Sh.192.7 Milioni ambao utahudumia watu 4946 wa Vijiji vya Dung'unyi na Munkinya.
Mhandisi wa Maji Victor Kamate, akizungumza na wananchi wakati alipokuwa akikagua mradi huo.
Afisa Mtendaji Kata ya Dung'unyi, Yahaya Njiku, akimtwika maji Mmoja wa Wananchi wa Kijiji cha Dung'unyi.
Muonekano wa mradi huo wa maji.

 Tenki la kuhifadhia maji la mradi huo.



Na Dotto Mwaibale, Singida


SERIKALI imekamilisha ujenzi wa mradi wa maji wenye gharama ya zaidi ya Sh.192.7 Milioni uliotekelezwa katika Vijiji vya Dung'unyi na Munkinya wilayani Ikungi mkoani Singida.

Akizungumza na waandishi wa Hmhabari jana Afisa Mtendaji Kata ya Dung'unyi, Yahaya Njiku alisema kukamilika kwa mradi huo kutawaongezea kasi ya maendeleo wananchi wa vijiji hivyo ambao walikuwa wakitumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kufanya kazi za uzalishaji.

Alisema mradi huo utawanufaisha wananchi zaidi 4946 wa vijiji hivyo ambao sasa wameondokana na adha waliyokuwa wakiipata ya kukosa maji.

Akizungumzia ujenzi wa mradi huo Njiku alisema unahusisha tenki la maji lenye ujazo wa lita 50,000 ambalo limejengwa kwenye mnara wa mita 12. 

Alisema chanzo cha maji cha mradi huo ni kisima chenye uwezo wa kutoa 4,800 lita kwa saa, mtandao wa mabomba unaofikia kilomita 5.6 huku kukiwa na jumla ya vituo saba vya kutolea maji.

"Mradi huu umekamilika kwa asilimia 100 na wananchi hivi sasa wameanza kupata huduma ya maji wakati tukisubiria uzinduzi wake rasmi,". alisema Njiku.

Njiku ameipongeza Serikali kwa kumaliza mradi huo kwa wakati na akatumia nafasi hiyo kumshukuru  Meneja wa Wakala wa Maji Safi na Mazingira (RUWASA) Wilaya ya Ikungi Mhandisi Hoppeness  Liundi kwa kuwashirikisha viongozi  wa Serikali na wananchi katika kutekeleza mradi huo ambao ni mmoja kati ya miradi mikubwa wilayani humo.

Njiku amewataka wananchi wa vijiji hivyo kulinda na kutunza miundombinu ya mradi huo na kumshukuru  Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupeleka fedha za miradi katika wilaya hiyo.

Njiku ametoa onyo  kwa mtu yeyote atakaebainika anahujumu miundombinu ya mradi huo na kuwa  Serikali haitasita kumchukulia hatua kali za kisheria.

Aidha Njiku amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Singida  Mashariki, Miraji Mtaturu kwa kuwasemea bungeni wananchi wa Kata ya Dung'unyi  jambo lililosaidia kupatikana kwa mradi huo katika vijiji hivyo na Kijiji cha  Kipumbuiko.

Wakazi wa vijiji hivyo wakiongea kwa nyakati tofauti wameishukuru Serikali kwa kuwakamilishia mradi huo na kueleza kuwa walikuwa na changamoto kubwa ya maji  kwani walilazimika kwenda kuchota kwenye visima vya kienyeji  na madimbwi ya maji ya mvua.

Theresia Mghesi Mkazi  wa Kijiji cha Dung'unyi alisema wanawake ndio waliokuwa wakihangaika usiku na mchana kufuata maji umbali mrefu wa zaidi ya kilometa saba  hali iliyosababisha wakati mwingine ndoa zao  kutetereka.

CHUO CHA AFYA HERMAGIS CHA MOROGORO KUPUNGUZA UHABA WA WAFAMASIA NCHINI

    Kiongozi wa mbio za  Mwenye wa Uhuru Kitaifa 2021  Luteni Josephine  Mwambashi akitoa salamu na ujumbe wa Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2021 kabla ya kuzindua Jengo la Mababara ya Chuo cha Hermagis. Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero Hakima Okash na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Chuo hicho Prof.Robinson Mdegela.

Kiongozi wa Mbio za  Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021  Luteni Josephine  Mwambashi akivuta pazia  kuashiria uzinduzi wa jengo la maabara na maabara ya Chuo cha Afya Hermags mkoani Morogoro.
Mlezi na Mshauri wa Chuo cha Afya Hermagis  Askofu Mtaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa Dkt. Owdenburg Mosses akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye uzinduzi huo..
Mkurugenzi wa Chuo cha Afya Hermags Prof. Robinson Mdegela  akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi huo wa maabara uliofanywa na Mbio za Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2021.
Mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Afya Hermags Prof. Yonica Ngaga akieleza mikakati ya Bodi yake kwa chuo hicho pamoja na maono ya Bodi kitaaluma kwa wanafunzi mara baada ya kumaliza uzinduzi wa jengo hilo la maabara.
Meneja wa Benki ya CRDB Mkoa wa Morogoro, Stephen Mapunda ambao ndio wafadhili wa shule hiyo akieleza sababu za CRDB kusaidia upanuzi wa Chuo hicho.
Kiongozi wa Mbio za  Mwenye wa Uhuru Kitaifa2021  Luteni Josephine Mwambashi akikagua maabara hiyo akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Halima Okash kabla ya kuzindua rasmi maabara hiyo.
Kiongozi wa Mbio za  Mwenye wa Uhuru Kitaifa 2021  Luteni Josephine  Mwambashi akiangalia namna Wanafunzi wa Chuo hicho wakitengenza madawa mbalimbali ikiwemo vitakasa mikono yaani SANITIZER.
Wanafunzi wa Chuo cha Hermagis wakionyesha kazi wanazozifanya chuoni hapo kwa vitendo hasa wakati wa utengenezaji wa madawa mbalimbali.

 Picha ya pamoja ya baadhi ya Wanafunzi,Wafanyakazi na viongozi wa Chuo hicho mara baada ya kuondoka kwa Mwenge wa Uhuru chuoni hapo.


Na Calvin Gwabara, Morogoro.


KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021 Luteni Josephine  Mwambashi ameupongeza uongozi na Mmiliki wa Chuo Cha Afya Hermagis kwa kusaidia kuwezeshamvijana wa Kitanzania kupata Elimu ya Famasia hasa utengenezaji wa dawa na kujiajiri.

Pongezi hizo amezitoa wakati akizindua Jengo na Maabara ya kisasa  (Compound Lab) ya chuo hicho kilichopo wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

"Napongeza jitihada hizi kubwa zilizofanywa na wenzetu wa sekta binafsi kuanzisha chuo hiki muhimu kinachozalisha wataalamu wa famasia nchini kwetu maana mambo haya yalikuwa ya afanywa nje ya nchi ndio unaoana dawa zinaletwa nchini lakini sasa kupitia sayansi na teknolojia tunaona na sisi tuna uwezo was kuzalisha sawa hapahapa kupitia wataalamu wetu hii ni hatua kubwa na sasa nitamke kuwa mwenye wa uhuru unazindua Maabara hii" alieleza Mwambashi.

Akitoa taarifa ya Mradi huo wa ujenzi wa Maabara mkuu wa chuo hicho Benedict Lugarisha alisema kupitia maabara hiyo ya kisasa imewezesha wanafunzi kusoma kwa vitendo lakini pia kuzalisha madawa mbalimbali kama vile sabuni na vitakasa mikono yaani Sanitizer.

"Mhe. Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru  Kitaifa mwaka 2021 jengo hili limeshakamilika na linavifaa vyote muhimu vinavyohitajika kwaajili ya Wanafunzi kujifunza na lina miundombinu yote muhimu hivyo tunayo heshima kubwa kukukaribisha uweze kulitembelea, kuona namna wanafunzi wetu wanavyolitumia na vifaa vyake na kisha utuzindulie jengo hili" alisema Lugarisha.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Askofu Dkt. Owdenburg Mosses amepongeza ushirikiano mkubwa ambao Serikali ya Tanzania unautoa kwa sekta binafsi katika kuanzisha Vyuo vya Afya na huduma zingine na hivyo kuwezesha kuongeza ufanisi wa wataalamu katika utoaji wa huduma.

Alisema afya ni suala nyeti na muhimu kwa maendeleo watu na taifa lolote lile Duniani hivyo chuo hicho kitasaidia kupata wataalamu wengi ambao watakwenda kusaidia jamii na taifa katika kutoa huduma sahihi za afya zinazozingatia taratibu na kanuni zinazowaongoza.

"Tunajua sote kuwa huko mtaani karibu nchi nzima kuna vyuo vingi lakini wengi wao ni wajanjawajanja tu kwenye utoaji wa taaluma kwa watoto wetu hivyo kuwepo kwa chuo chenye miundombinu bora na ushahdi tumeuona kwa wanafunzi wenyewe wanavyotengeneza madawa mbalimbali vizuri wakitoka hapa hawawezi kusubiria ajira bali wanakwenda kujiajiri wenyewe" alisema Askofu Mosses.

Mkurugenzi wa chuo hicho Prof. Robinson Mdegela ameishukuru Serikali ya Mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Mvomero na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa kukubali mwenge kumulika kwenye Chuo hicho na kuahidi kuhakikisha wanaendelea kupunguza uhaba wa Wafamasia nchini hasa kutokana na umuhimu wa kada hiyo ya afya.

" Sisi hatufundishi tuu watoto kupata elimu na vyeti bali tumejikita kwenye kufundisha vya vitendo ili kila mhitimu wa Chuo chetu akitoka hapa aende kujiajiri kwenye kutengeneza madawa au akaajiriwe kwenye maeneo ambayo yana uhitaji wa Kada ya Famasia kwakuwa watakuwa wahitimu wa tofauti kutokana na Elimu bora waliyoipata hapa" alisisiza Prof. Mdegela.

Alisema kwa sasa Chuo kinatoa Mafunzo ya Famasia kwa ngazi ya Astashahada (Certificate) na  Stashahada (Diploma) kwa wanafunzi wayne ufaulu wa kuanzia alama "D" kwenye masomo ya Kemia na Baiolojia na kina mpango wa kuongeza kozi nyingine muhimu ambazo sina soko kubwa la ajira kwa wahitimu na mchango mkubwa kwa taifa.

Akielezea mikakati ya chuo hicho cha Afya Hermagis,  Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Prof. Yonica Ngaga alisema ni kuhakikisha wanasimamia ubora wa elimu itolewayo Chuoni hapo ili ibaki kuwa ya vitendo na kuzalisha Wahitimu watakaokuwa na mchango kwa jamii hasa kwenye sekta muhimu ya afya.

" Naomba nitumie nafasi hii kuwa shauri Wazazi, Walezi na vijana wenye sifa za kujiunga na Chuo hiki wajiunge maana hawatajutia kusoma au kumsomesha mtoto kwenye Chuo huki, Tunasomesha watoto wetu ili wapate kazi za kufanya kwa kuajiriwa au kujiajiri hivyo hapa ni mahali sahihi na mimi watoto wangu wasingekuwa wamemaliza Ngazi za juu ningewaleta hapa maana ninauhakika hatokosa kazi za kufanya" alisema Prof. Ngaga.

Alisisitiza kuwa wao kama bodi ya chuo wanataka mwanafunzi  anayetoka chuo hicho kama ni mfamasia awe na Elimu ya nadharia na vitendo na aweze kutengeneza baadhi ya dawa kwenye jamii na ajipatie fedha kupitia mtaji mdogo tu kulingana na uwezo wake au uwezo wa mzazi.

Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 unaendelea na ziara yake Mkoani Morogoro ambapo leo unepokelewa kwenye Wilaya ya Mvomero kutoka Wilaya ya Kilombero ambapo unafungua miradi mbalimbali ya maendeleo ya kusambaza ujumbe wa mwenge kitaifa kwa mwaka huu unaosema " TEHAMA ni Msingi wa Taifa endelevu, Itumie  kwa usahihi na uwajibikaji".

TANZANIA KUUZA NYAMA NCHINI SAUDI ARABIA

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akiongea na Ujumbe kutoka nchini Saudi Arabia alipokutana nao jijini Dar es Salaam jana. Kushoto kwake ni Mkaguzi, Mamlaka ya Dawa na Chakula, Saudi Arabia, Ahmed Alhajouj. 

 

Na Mbaraka Kambona, 


Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel amekutana na Ujumbe kutoka nchini Saudi Arabia kwa lengo la kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara ya nyama na nchi hiyo.

Prof. Ole Gabriel alikutana na Ujumbe huo kutoka Saudi Arabia ulioongozwa na Mkaguzi,  Mamlaka ya Dawa na Chakula, Saudi Arabia, Ahmed Alhajouj jijini Dar es Salaam jana.

Kwa mujibu wa Prof. Gabriel kabla ya kukutana nao, ujumbe huo ulipata fursa ya kukagua maeneo mbalimbali yanayohusika na uchakataji wa mazao ya mifugo ikiwemo Machinjio, Maabara na Shirika la Viwango Tanzania(TBS) ambapo kote wamejirisha na kutoa mapendekezo kadhaa ya kuboresha ili biashara hiyo iweze kufanyika kwa viwango vinavyohitajika na nchi hiyo. 

Alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameielekeza Wizara hiyo kutafuta masoko nje ya nchi hivyo Wizara inaendelea kufanya jitihada ikiwemo hatua hiyo ya kutafuta soko katika nchi Saudi Arabia.

"Haya masoko ya nje ya nchi ni mazuri kwa sababu yanatupatia fedha za kigeni lakini pia yanawahakikishia wafugaji wetu soko la uhakika kwa mazao ya mifugo yao," alisema Prof. Ole Gabriel

Aidha, Prof. Gabriel alitoa rai kwa Wafugaji nchini kuchukulia hatua hiyo kama ni fursa kubwa na hivyo wahakikishe wanaboresha ufugaji wao kuwa wa kisasa zaidi ili kukidhi soko hilo la kimataifa.

"Serikali ni rahisi kutafuta masoko lakini je, mifugo iliyopo inakidhi soko hilo? hivyo niwaombe wafugaji na Wafanyabiashara watumie fursa hii vizuri ili kuboresha uchumi wao na wa Taifa pia," aliongeza Prof. Ole Gabriel

Alisema Sekta ya Mifugo kwa sasa inachangia katika pato la Taifa kwa asilimia 7.4 lakini lengo la Wizara ni kufikia asilimia 15 ifikapo mwaka 2025 na hilo linawezekana kama milango ya masoko nje ya nchi  ikianza kufunguka kwa uhakika.

Prof. Ole Gabriel aliongeza kuwa wao kama wizara watatoa ushirikiano kwa kila mdau anayechangia katika mnyororo wa thamani wa mazao ya mifugo kuhakikisha kunakuwa na mazao bora kwa ajili ya soko la ndani na la nje.

Naye, Msajili wa Bodi ya Nyama, Dkt. Daniel Mushi alisema anaishukuru Serikali kwa jitihada mbalimbali inazozifanya kwa kushirikiana na wadau kufungua masoko mengine nje ya nchi ili kuuza nyama katika masoko yanayolipa bei nzuri.

Aliongeza kuwa ujio wa ujumbe huo umewapa changamoto kwani kuna mambo wanapaswa kufanya ili nyama ya Tanzania iweze kukubalika katika masoko ya nje. 

Aliendelea kusema kuwa ili waweze kufikia masoko hayo ni lazima kuboresha lishe ya mifugo ili wanyama waweze kukua kwa haraka na ambao watakuwa na nyama nyingi yenye ubora.

Itakumbukwa hivi karibuni, Rais Samia alikutana na Mtoto wa Mfalme wa Saudi Arabia ambapo miongoni mwa maeneo yaliyoangaliwa ni pamoja na Sekta ya Mifugo na aliielekeza Wizara kutafuta masoko nje ya nchi ikiwemo nchi ya Saudi Arabia.