Wednesday, October 6, 2021

DKT. MAHENGE: TUTATUMIA KILA MBINU WANANCHI WAPATE CHANJO YA UVIKO 19 SINGIDA

Mkuu wa Mkoa Singida Dkt.Binilith Mahenge akizungumza kwenye kikao cha kamati ya afya ya msingi ya jamii  (PHC) Mkoa wa Singida kilicho keti leo kuhusu utekelezaji wa mpango shirikishi na harakishi kwa ajili ya utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhaj Juma Kilimba na Mganga Mkuu Mkoa wa Singida Victorina Ludovick.
Mganga Mkuu Mkoa wa Singida Victorina Ludovick akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akizungumza kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI) Idara ya Jamii  na Lishe, Dinah Atinda (kulia) na Richard Magodi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiwa kwenye kikao hicho. 

Viongozi wa dini wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Mratibu wa Health Promotion Mkoa wa Singida, Habibu Mwinory akichangia jambo kwenye kikao hicho.
            Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili akichangia jambo kwenye kikao

          Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo akichangia jambo kwenye kikao

Mwakilishi kutoka Shirika la Sema na Mjumbe wa Taifa wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Singida Peter Lissu akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mratibu wa TASAF Mkoa wa Singida, Patrick Kasango akichangia jambo kwenye kikao hicho.
    Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Joseph Kyense akichangia jambo kwenye kikao hicho

 


Na Dotto Mwaibale, Singida


MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge amesema watatumia kila mbinu ili kuona wananchi wa mkoa huo wanapata chanjo ya Uviko-19.

Dkt.Mahenge ameyasema hayo leo kwenye kikao cha kamati ya afya ya msingi ya jamii  (PHC) Mkoa wa Singida kilicho keti kuhusu utekelezaji wa mpango shirikishi na harakishi kwa ajili ya utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19.

"Tumekwisha anza kuona matokeo mazuri ya watu kujitokeza kupata chanjo, hii inatokana na kazi nzuri na mbinu mbalimbali za uhamasishaji naomba tusimame hapo na twende tukaeneze hizo juhudi ninachohitaji ni kuona watanzania wengi wanapata chanjo,". alisema Mahenge.

Alisema zitatumika kila mbinu katika kukamilisha kazi hiyo kwani kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani hivyo ni wajibu wetu tufanye kila liwezekanalo ili wabaki mamba na kuachana na hao kenge ambao wanazohofisha jitihada hizo.

Alisema kazi hiyo inawezekana hasa baada ya hizi siku chache kuongezeka kwa idadi ya wananchi kujitokeza kupata chanjo hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo alisema muitikio wa wananchi kupata chanjo hiyo ni mkubwa zaidi maeneo ya vijiji tofauti na mijini ambapo alitolea mfano wa Singida Mjini ambayo imepitwa na Singida Vijijini hivyo akaomba uhamasishaji katika maeneo ya mijini uongezewe nguvu.

Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Joseph Kyense aliiomba Serikali iendelee kuleta chanjo nyingi zaidi ili kila mwananchi aweze kuchagua chanzo atakayoipenda badala ya kuwa na moja tu.

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili alisema kupitia mpango huo Shirikishi na Harakishi wananchi wamekuwa na muitikio hasa baada ya kueleweshwa umuhimu wa chanjo hiyo.

 Mwakilishi kutoka Shirika la Sema na Mjumbe wa Taifa wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Singida Peter Lissu alisema kesho kwa kushirikiana na Civil Society Foundation watakuwa na kikao na Mashirika 50 ya mkoani hapa kwa ajili ya kuona mchango wao wa uhamasishaji wananchi kujitokeza kupata chanjo hiyo.

Mwenyekiti wa Dini mbalimbali Mkoa wa Singida Sheikh Hamisi Kisuke alisema zoezi la kwenda kuhamasisha nyumba kwa nyumba ili watu wajitokeze kupata chanjo  limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuongeza idadi ya watu tofauti na mwanzo.

Tuesday, October 5, 2021

MACHIFU HAMASISHENI MICHEZO YA JADI – DKT ABBASI

 Na John Mapepele, Dodoma 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi amewataka Machifu na Viongozi wa Kimila kushirikiana na Serikali kuhamasisha michezo ya jadi ili michezo hiyo iwe na tija kwenye mashindano ya kombe la taifa yanayoanza kurindima hivi karibuni. 

Dkt. Abbasi amesema hayo leo wakati akitoa maazimio ya kikao cha pamoja baina ya Wizara, Machifu na Viongozi wa Kimila kuhusu utoaji wa maoni ya kuhuisha Sera ya Utamaduni leo Oktoba 05, 2021 katika ukumbi wa African Dreams jijini Dodoma. 

"Serikali imeamua kufufua na kuboresha mashindano ya Kombe la Taifa ambapo tumeijumuisha michezo ya jadi kutokana na umuhimu wake hivyo natoa wito kwenu kuhamasisha michezo hii ambayo inaanzia kwenye ngazi za vijiji ili iweze kuwa na athari chanya kwenye mashindano ya Taifa ya mwaka huu". Ameongeza Dkt. Abbasi 

Amefafanua kuwa miongoni mwa maazimio ya kikao hicho ni Machifu kuendelea kushirikiana na Serikali katika kulinda amani na ustawi wa jamii ya wananchi wa Tanzania. 

Ametoa siku saba za kuendelea kutoka maoni ya kuboresha Sera hiyo ambapo amesema baada ya hapo zoezi hilo litaendelea katika ngazi za juu. 

Pia ametoa siku 30 kwa Machifu kuwasilisha maeneo ya kimila na kiutamaduni ili Serikali iweze kuyatambua na kuyafanyia kazi. 

Makamu Mwenyekiti wa (UMT) ambaye pia ni Chifu wa Unyanyembe Tabora Chifu Msagata Fundikila ameipongeza Serikali kwa kuwashirikisha Machifu katika kikao hicho.Amesema kikao hiki kimekuja katika wakati mwafaka kwa kuwa utamaduni wa taifa umekuwa ukiharibiwa na utandawazi. 

Makamu Katibu Mkuu wa Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) nchini Amani Lukumai amesema kuna haja kwa Serikali kuendelea na utoaji wa elimu wa umuhimu na uzuri wa utamaduni na mila. 

Aidha, ameongeza kuwa ni muhimu kwa Serikali kufanya utafiti wa namna gani nchi mbalimbali duniani kama China wamefanikiwa kuulinda utamaduni wao. 

Kikao hiki kinafuatia maelekezo aliyoyatoa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika Tamasha la Utamaduni lilioandaliwa na Umoja wa Machifu Tanzania (MUT) Septemba 8, 2021 jijini Mwanza. 

Rais Samia aliitaka Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo iwashirikishe Machifu katika kuhuisha Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997. 

Zaidi ya Machifu na Viongozi wa Kimila 105 kutoka mikoa yote nchini wamehudhuria.

Katibu Mkuu Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akihutubia Machifu na Viongozi wa Kimila katika Kikao kilichoandaliwa na Wizara hiyo kujadili na kuchukua maoni ya Viongozi hao katika kuboresha Sera ya Taifa ya Utamaduni, Kikao kilichofanyika Oktoba 5, 2021 Jijini Dodoma ambapo Dkt. Abbasi amekuwa Mgeni Rasmi katika Kikao hicho.



Katibu Mkuu Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi (aliyekaa katikati) akiongoza mjadala wa kukusanya maoni kutoka kwa Machifu na Viongozi wa Kimila ambao wamekutana leo Oktoba 5, 2021 kujadili na kuchukua maoni ya Viongozi hao katika kuboresha Sera ya Taifa ya Utamaduni. Viongozi wengine kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, Dkt. Emmanuel Temu na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania, Msagata Fundikila.


Baadhi ya Machifu na Viongozi wa Kimila walioshiriki katika Kikao kilichoandaliwa na Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kujadili na kuchukua maoni ya Viongozi hao katika kuboresha Sera ya Taifa ya Utamaduni, Kikao kilichofanyika Oktoba 5, 2021 Jijini Dodoma ambapo Dkt. Abbasi amekuwa Mgeni Rasmi katika Kikao hicho.


Katibu Mkuu Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akizawadiwa fimbo kutoka kwa Kiongozi wa Kimila wa Jamii ya Wamasai baada ya kumalizika kwa Kikao kilichoandaliwa na Wizara hiyo kujadili na kuchukua maoni ya Viongozi hao katika kuboresha Sera ya Taifa ya Utamaduni, Kikao kilichofanyika Oktoba 5, 2021 Jijini Dodoma ambapo Dkt. Abbasi amekuwa Mgeni Rasmi katika Kikao hicho.

SHIRIKA LA SPRF LAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI MBINU BORA ZA KUTOKOMEZA UKATILI SINGIDA

Wanafunzi wa Shule za Sekondari ya Siuyu na Munkinya wilayani Ikungi Mkoani Singida wakiwa katika kikao cha majadiliano kupata ufumbuzi na mbinu bora za kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ambao umekithiri mkoani hapa. Kikao hicho cha siku moja kilihusisha Kamati za Vijiji za Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), kikishirikisha Majukwaa ya vikundi vya Sauti ya Mwanamke, Sauti ya Wanafunzi na Jukwaa la Wanaume Washawishi. Kikao hicho kilichofanyika mwishoni mwa wiki kiliandaliwa na Shirika la SPRF lenye makao yake makuu mkoani Singida.

Mkurugenzi Mtendaji wa  Shirika  la Jiokoe na Umaskini yaani Stars of Poverty Rescue Foundation (SPRF) nchini, Dkt.Suleiman Muttani, akizungumza kwenye kikao kilicho wakutanisha wadau mbalimbali  wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kujadili   mbinu bora za kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Baadhi ya wadau wakiwa kwenye kikao hicho.

Mshauri wa Masuala ya Sheria wa shirika hilo na Mratibu Msaidizi wa mradi huo , Paul Kigeja akizungumza kwenye kikao hicho.
Usikivu katika kikao hicho ukiendelea.
Wanafunzi wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Majadiliano katika vikundi yakiendelea.


Majadiliano katika vikundi yakiendelea.
Majadiliano katika vikundi yakiendelea.
Maofisa wa SPRF wakijadiliana jambo kwenye kikao hicho. Wa pili kushoto ni Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Ikungi, Haroun Yunus Haroun.
Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Ikungi, Haroun Yunus Haroun akizungumza kwenye kikao hicho.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ikungi  Mariam Mwandikile akizungumza kwenye kikao hicho.
Baadhi ya wadau wakiwa kwenye kikao hicho.
Mwalimu Ester Robert wa Siuyu Sekondary  akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwanafunzi Anna Yona wa Shule ya Sekondari ya Siuyu, akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwanafunzi Gasper Moris kutoka Sekondari ya Munkinya, akizungumza kwenye kikao hicho.
Mama Marietha Kibao kutoka Sauti ya Mwanamke Kijiji cha Munkinya akizungumza kwenye kikao hicho
Mwalimu Ngogo Paul kutoka Sekondari ya Munkinya  akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Katibu wa Jukwaa la Wanaume Ferdnand Holota akizungumza kwenye kikao hicho.
 

Picha ya pamoja.



Na Dotto Mwaibale, Singida


SHIRIKA  la Jiokoe na Umaskini yaani Stars of Poverty Rescue Foundation (SPRF) kupitia mradi wa ‘AWARE 2020’ limewakutanisha wadau mbalimbali  wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida kwa ajili ya kujadili na kupata ufumbuzi na mbinu bora za kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Wadau waliokutanishwa na shirika hilo katika kikao hicho ni Kamati za Vijiji za Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), Majukwaa ya vikundi vya Sauti ya Mwanamke, Sauti ya Wanafunzi na Jukwaa la Wanaume Washawishi ambao wanapinga vitendo vya ukatili (kama ubakaji, ulawiti, ukeketaji, ndoa za utotoni) , vipigo kwa wanawake na ukatili kwa watoto katika vijiji vinne vya mradi  ndani ya wilaya hiyo. 

Vijiji hivyo vya mradi ni Siuyu na Unyankhanya vilivyopo Kata ya Siuyu, Munkinya na Damankia kutoka Kata ya Dung’unyi.

Kikao hicho cha wadau kilichofanyika mwishoni mwa wiki wilayani humo kililenga  kufanya majadiliano ili kupata ufumbuzi na mbinu bora za kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ambao umekithiri mkoani hapa.

Mkurugenzi Mtendaji wa SPRF nchini, Dkt.Suleiman Muttani alisema shirika hilo chini ya ufadhili wa Foundation for Civil Society (FCS) limekuwa likitekeleza mradi wa AWARE katika kata 5 za Wilaya ya Ikungi kwa kufanya utetezi wa haki za wanawake na mtoto wa kike dhidi ya athari zitokanazo na mila na desturi kandamizi.

Mshauri wa Masuala ya Sheria wa shirika hilo na Mratibu Msaidizi wa mradi huo , Paul Kigeja alisema lengo la kikao hicho ilikuwa ni kuwakumbusha majukumu yao ya msingi ya kutekeleza kazi zao katika ngazi za vijiji lakini pia kwa pamoja waweze kujadili na kufikia hitimisho la kupata njia bora zaidi za kukomesha vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.

"Lakini kwa umuhimu zaidi lengo letu lilikuwa ni namna ya kuweza kuratibu juhudi za pamoja kwani hivi ni vikundi mbalimbali ambavyo vina viongozi wa dini, vijiji, watendaji na kuna baadhi ya kamati zinafanya kazi nzuri lakini hazipati ushirikiano na kamati zingine hivyo tukaona kupitia kikao hiki tuweze kuwakutanisha ili wawe na juhudi na sauti ya pamoja,".alisema.

Mwanafunzi Gasper Moris kutoka Sekondari ya Munkinya alisema Shirika hilo lina mchango mkubwa kwani limemsaidia kujua mambo mbalimbali ambapo aliweza kumsaidia mwanafunzi mwenye ulemavu aliyekuwa akifanyiwa ukatili wa kijinsia  kwa kupigwa na kuchaniwa nguo zake na kuchanjwa chanjwa na wembe.

Mwanafunzi Naina Selemani wa Shule ya Sekondari ya Siuyu ambaye ni kiongozi wa Klabu ya kupinga ukatili shuleni hapo alisema amekuwa akitoa taarifa ya matukio ya ukatili wa kijinsia kwa walimu walezi ambao nao waliyapeleka ngazi za kata jambo lililosaidia kuwafanya wanafunzi kuacha kujihusisha na vitendo hivyo.

Katibu wa Jukwaa la Wanaume Ferdnand Holota ambaye alijiunga na shirika hilo mwaka jana alisema baada ya kupata mafunzo ya kupinga ukatili na wao kwenda kuelimisha jamii sasa na wanaume ambao wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia wameanza kujitokeza hadharani ili wasaidiwe.

"Shirika la SPRF limetuletea mabadiliko makubwa wanaume walikuwa wakiona aibu kujitokeza kuelezea madhira waliyokuwa wakiyapata kutoka kwa wake zao lakini sasa hivi wanayaeleza na kupatiwa msaada,"alisema Holota.

Mama Marietha Kibao kutoka Sauti ya Mwanamke Kijiji cha Munkinya alisema shirika hilo limeleta mabadiliko makubwa katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuzipa ujasiri kamati za kupinga vitendo hivyo.

"Mambo ya unyanyasaji wa watoto na wanawake vikiwemo vitendo vya ukeketaji mimba za utotoni na ubakaji vimeanza kupungua baada ya mashirika haya kutoa elimu naamini Serikali na wafadhili wengine wakiendelea kuyawezesha vitendo hivi vitakwisha kabisa,".alisema Kibao. 

Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Ikungi, Haroun Yunus Haroun alisema mfumo wa mawasiliano uliopo sasa umesaidia kwa kiwango kikubwa kuwabaini watuhumiwa na kuibua vitendo hivyo vinavyofanyika kwa siri ambapo vimepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na siku za nyuma.

Saturday, October 2, 2021

MAJONZI, VILIO, SIMANZI VYATAWALA MISA YA KUMUAGA MWANAHABARI DORIS NTALIAGA MEGHJI MKOANI SINGIDA

Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mwanahabari Doris Ntaliaga wakati wakitoka katika Misa Takatifu ya kumuaga iliyofanyika Kanisa Katoliki Jimbo la Singida jana.

Marehemu Doris Ntaliaga Meghji enzi za uhai wake.

Askofu wa Jimbo Katoliki Singida Mhashamu Edward Mapunda aliyeongoza Misa hiyo akiweka msalaba kwenye kaburi la marehemu Doris Meghji wakati wa mazishi yake.
Mama wa marehemu Doris Meghji, Margareth Malecela akiwa na huzuni kwenye misa hiyo.
Baba wa marehemu Doris, Mzee Meghji akiwa na huzuni kwenye misa hiyo.
Ni vilio na huzuni kwenye misa hiyo.
Misa ikiendelea.
Misa ikiendelea.
Ni huzuni kwenye misa hiyo. Hawa jamaa hawaamini kama mpendwa wao Doris amefariki na hawata muona tena.
Utoaji sadaka ukifanyika.
Misa ikiendelea.
Zoezi la kuaga na kutoa heshima mbele ya mwili wa marehemu likifanyika.
Mama wa marehemu Doris Meghji, Margareth Malecela akimuaga mwanaye.
Ni vilio na huzuni wakati wakitoka kwenye misa hiyo.
Mazishi yakifanyika.
Maafisa Tarafa kutoka Tanga, Singida na mikoa mingine wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi la mwenzao Doris.

Baadhi ya Wanahabari wa Mkoa wa Singida wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi la mwanahabari mwenzao Doris Meghji.

Baba na Mama wa marehemu wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mpendwa mtoto wao Doris Ntaliaga Meghji.


Na Dotto Mwaibale, Singida


SIMANZI, Vilio na Majonzi  vilitawala katika Misa Takatifu ya kumuaga marehemu Mwanabahari Doris Meghji iliyofanyika Kanisa Katoliki Jimbo la Singida.

Akiongoza misa hiyo jana Askofu wa Jimbo Katoliki Singida Mhashamu Edward Mapunda alisema  Kanisa hilo limempoteza mwanahari huyo ambaye alikuwa mtangaji wa Radio Maria ambayo inasimamiwa na kanisa hilo.

" Namfahamu Doris kama mlivyosikia yeye ndiye alikuwa mtangazaji wa kwanza wa Radio Maria tulipotangaza nafasi ya kazi Doris alijitokeza na kuwa mwakilishi wa Radio yetu ,". alisema Askofu Mapunda.

Mapunda alisema walimkubalia kufanya kazi baada ya kujiridhisha kwamba alikuwa ni mwandishi wa habari mzuri na kuwa hata baada ya kupata nafasi hiyo alifanya kazi yake vizuri ya kutangaza neno la Mungu kupitia radio hiyo.

Alisema Doris alitangaza injili kupitia radio hiyo kwa kuwa alikuwa akihifahamu vizuri imani ya Kanisa Katoliki hivyo kutokana na kazi hiyo tunampongeza sana.

Alisema Doris alimuaga kuwa amepata nafasi nyingine ya kazi TBC ambapo alimpa baraka zote ili apate nafasi nyingi zaidi za kulitumikia Taifa baada ya kupata uzoefu mkubwa katika Radio Maria.

Alisema anaamini na  TBC aliwawakilisha vizuri kabla ya kupata nafasi nyingine ya kulitumikia Taifa kwa nafasi ya Afisa Tarafa mkoani Tanga ambayo aliifanya hadi umauti wake."Tuendelee kumuombea kwani kifo cha Doris ni cha baraka, neema na ni mlango wa kuingia mbinguni.. kumuona Mungu," . alisema Askofu Mapunda.

 Wakizungumza wakati waakitoa salamu za rambirambi katika Misa hiyo watu mbalimbali waliokuwa wakimfahami Doris walisema alikuwa mchapa kazi na alimuheshimu kila mtu bila ya kujali jinsia yake, cheo chake na umri wake.

Walisema mkoani Tanga alikokuwa akifanya kazi alichaguliwa kuwa kiongozi wa maafisa Tarafa wote wa mkoa huo hivyo inaonesha ni jinsi gani alivyokuwa akishirikiana na wenzake vizuri katika kazi.

Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Singida Elisante John alisema chama hicho kimempoteza mwanahabari mahiri licha ya kuwa alikuwa akifanya kazi nyingine ya Afisa Tarafa.

"Doris alikuwa mwenzetu na tulifanya naye kazi vizuri tukiwa wote hapa Singida na mimi ndiye niliyempokea na alikuwa mchapa kazi mzuri,". alisema John.

Marehemu Doris Meghji alizaliwa Septemba 15, 1977 mkoani Tabora wakiwa watoto wa kwanza na pacha wake Dorica Meghji ambaye naye ni marehemu.

Marehemu Doris alipata elimu ya Msingi Shule ya Msingi Utemini na baadae Shule ya Sekondari ya Margaret iliyopo mkoani Kilimanjaro.

Baada ya hapo Marehemu alisoma kidato cha Tano na cha Sita Shule ya St.Joseph iliyopo Arusha na baada ya hapo alijiunga na Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT) jijini Mwanza ambapo alisomea Uandishi wa Habari Ngazi ya Cheti na kuendelea na masomo zaidi ya fani hiyo hadi kupata Shahada.

Enzi za Uhai wake marehemu alifanya kazi sehemu tofauti tofauti kama Sibuka FM, EFM, Gazeti la Tanzania Daima, Mtangazaji wa Radio Maria, TBC, Standard FM, Azam TV na Afisa Tarafa Ngamiani mkoani Tanga.

Mazishi ya Mwanahabari huyo yalihudhuriwa na viongozi kutoka  Serikalini, vyama vya siasa, madiwani, Meya wa Manispaa ya Singida  na wananchi kutoka sehemu mbalimbali wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Singiga mjini Ramadhan Mussa Sima.

Friday, October 1, 2021

DC HANANG ATATUA MGOGORO WA ARDHI KWA MASAA MANNE WANAWAKE WAKESHA SIKU TISA

Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, Janeth Mayanja, akizungumza juzi na Wananchi wa              Kijiji cha Mogitu kilichopo Kata ya Mogitu  wakati akitatua mgogoro wa ardhi ambao uliwafanya  wanawake wa kijiji hicho wa kabila la Barbaiq kukesha siku tisa wakishinikiza kurudishiwa eneo lao la kuabudia lililouzwa.

Wananchi wa Kijiji cha Mogitu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya , Janeth Mayanja (hayupo pichani) wakati akitatua mgogoro huo.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja, akiwa amekaa na Wananchi wa Kijiji cha Mogitu baada ya kutatua mgogoro wa ardhi.
Wananchi na Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja wakiwa kwenye eneo lililokuwa na mgogoro.


Na Mwandishi Wetu, Hanang


MKUU wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, Janeth Mayanja  ametatua mgogoro wa ardhi kwa muda wa masaa manne na kuwashangaza wananchi na wanawake wa kabila la Barbaiq waliokesha siku tisa wakishinikiza kurudishiwa eneo lao la kuabudia katika Kijiji cha Mogitu kilichopo Kata ya Mogitu wilayani humo.

Wakiongea mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye alifika juzi katika kijiji hicho kwa ajili ya kutatua mgogoro huo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wanawake hao walisema eneo hilo wamekuwa wakilitumia kwa kuabudia tangu enzi na enzi.

Walisema walilazimika kukesha wakishinikiza kurejeshewa eneo hilo baada ya mwanakijiji mwenzao waliyemtaja kwa jina la Gembe Nono kudaiwa kuwauzia wananchi wengine wawili wa kijiji hicho.

Afisa Mtendaji wa kijiji hicho  Linda Darema alisema wanawake hao walilala nje kwa siku tisa kuonesha hasira zao kufuatia eneo lao hilo la kuabudia kumegwa na kuuziwa  watu kinyume na imani za kabila hilo ambalo lilitengwa kwa ajili ya kuabudia na si mashamba wala makazi ya watu.

Akitatua mgogoro huo kwa njia ya mkutano wa hadhara uliowahusisha muuzaji wa eneo hilo na wanunuzi pamoja na wananchi  mkuu wa wilaya hiyo Mayanja  alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haina dini ila watu wake wanadini na kuwa inaheshimu mila na desturi.

Mayanja alimtaka muuzaji wa eneo hilo Gembe Nono kuelezea uhalali wa kuuza eneo hilo ambapo alikiri kuliuza kimakosa ambapo aliwarejeshea fedha aliowauzia.

"Wanunuzi wa eneo hilo walieleza kwamba walinunua bila ya kujua kama lilikuwa likitumika kwa ajili ya kuabudia ambapo tayari wamebomoa nyumba walizokuwa wamejenga baada ya kurejeshewa fedha zao,". alisema Mayanja.

Aidha mkuu wilaya hiyo Janeth Mayanja amelikabidhi eneo hilo kwa viongozi wa kijiji  na kuagiza liendelee kutumika kama jamii ilivyokua inalitumia awali na kuhimiza jamii kuendelea kulinda maeneo hayo ili kudumisha mila na desturi.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho aliyetambulika kwa jina moja la Safari  amemshukuru mkuu wa wilaya kwa kufika kwa wakati na kutatua mgogoro huo ndani ya masaa manne jambo ambalo hawakulitegemea hasa baada ya wanawake kukesha siku tisa wakishinikiza waliouziwa eneo hilo waondoke.

"Tunachukua nafasi hii kumshukuru na kumpongeza sana mkuu wetu wa wilaya kwa kutatua mgogoro huu kwa wakati na maagizo yake yote alioyatoa tutayatekeleza,". alisema Safari.