Viongozi wa Wilaya ya Ikungi wakiwasili katika viwanja vya Shule Shikizi ya Namba 7 iliyopo Kata ya Mang'onyi kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 45 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyofanyika juzi katika kata hiyo kiwilaya. kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, Mika Likapakapa, Mkuuu wa Wilaya Jerry Muro, Diwani wa Kata hiyo Innocent Makomelo na Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo Stanley Shabani.
Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, Mika Likapakapa akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mkuuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akisisitiza jambo kwenye maadhimisho hayo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Mwanga (kulia) akizungumza kwenye maadhimisho hayo. Wengine wote ni madiwani wa wilaya hiyo.
Viongozi wakiwa meza kuu. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga, DC wa Ikungi Jerry Muro, Mwenyekiti wa CCM Mika Likapakapa, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mang'onyi Stanley Shabani na Katibu wa CCM wa Wilaya ya Ikungi, Stamili Dendego.
Baadhi ya wataalamu wa wilaya hiyo wakishiriki maadhimisho hayo.
Wanafunzi wa Shule ya Shikizi Namba 7 wakiwa mbele ya madarasa waliojengewa na Kampuniya Uchimbaji Madini ya Shanta.
Sherehe zikiendelea.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye sherehe hizo.
Wanafunzi na wazazi wao wakiwa kwenye sherehe hizo.
Taswira kwenye sherehe hizo.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Abubakari Muna akitoa salamu katika maadhimisho hayo.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Ally Rehani akitoa salamu kwenye maadhimisho hayo.
Diwani wa Kata ya Mang;onyi, Innocent Makomelo akizungumza kwenye hafla hiyo.
Diwani wa Viti Maalumu Kata hiyo Fatuma Makula akichangia jambo kwenye maadhimisho hayo.
Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Shanta Mhandisi Kundael Ntiro akitoa taarifa ya miradi iliyotekelezwa na kampuni hiyo wilayani humo.
Burudani zikitolewa.


