Friday, March 4, 2022

JAJI MSOFFE AIPONGEZA MENEJIMENTI YA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA KWA KUTOA MAFUNZO YA KUJIANDAA KUSTAAFU

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria, Wawakilishi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na afya Tanzania(TUGHE)ngazi ya Taifa na Mkoa wakiwa katika picha ya pamoja  baada ya ufunguzi wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT ) Tawi la Mbeya leo hii.
Wajumbe hao wakiwa katika picha ya pamoja.
Mgeni rasmi katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Jaji Mstaafu January Henry Msoffe akihutubia wajumbe wakati wa ufunguzi wa kikako hicho kilichofanyika mkoani Mbeya Ukumbi wa  Benki Kuu ya Tanzania (BOT.).  Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Bwana Khalist Luanda.

Jaji Mstaafu January Msoffe (katikati) akisisitiza jambo kwenye kikao hicho.

DC SINGIDA AOMBA KUTOFANYA MAKOSA ZOEZI LA ANWANI ZA MAKAZI

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Mulagiri akizungumza  wakati akifunga mafunzo ya uhabarisho wa anwani za makazi na postikodi kwa wadau mbalimbali yaliyofanyika wilayani hapa jana.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Singida Mjini, Lucia Mwiru akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa Tarafa  Mungu Maji, Ally Mwendo akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa Dini mbalimbali Mkoa wa Singida Hamis Kisuke akichangia jambo kwenye mafunzo hayo
Meneja wa Mfuko wa  Pensheni kwa Watumishi wa Umma,   (PSSSF ) Mkoa wa Singida, Beda Mgonja akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Wadau wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Singida, Oscar Kalimilwa akichangia jambo kwenye mafunzo hayo. Kulia ni Meneja wa PSSSF Mkoa wa Singida, Beda Mgonja. 
Mchungaji Yona Mbogo wa Kanisa la Moravian Singida akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Afisa Miliki kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoa wa Singida Israel Ngapona akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
  Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) Mkoa wa Singida Burhan Mlau akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.



Na Dotto Mwaibale, Singida


MKUU wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Mulagiri amewaomba viongozi mbalimbali na wananchi wilayani hapa kutofanya makosa na kuichafua heshima waliyopewa ya kushiriki moja kwa moja zoezi la uandaaji anwani za makazi na postikodi.

Muragili alitoa ombi hilo wakati akifunga mafunzo ya uhabarisho wa anwani za makazi na postikodi kwa wadau mbalimbali yaliyofanyika wilayani hapa jana.

Wadau walioshiriki mafunzo hayo ni 275 wakiwemo watendaji wa kata, mitaa, maafisa elimu wa kata,wakuu wa shule, walimu wakuu, wenyeviti wa mitaa, vijiji, viongozi wa dini, wazee maarufu, wakuu wa idara na vitengo pamoja na madiwani.

"Tunapokwenda kutekeleza mambo yote tuliyojifunza hapa nawaomba tukayasimamie vizuri ili tuweze kufanikiwa na si vinginevyo" alisema Muragili.

Muragili alisema zoezi la uandaaji anwani za makazi na postikodi linahitaji ushirikishwaji wa hali ya juu katika ngazi zote hasa inayomuhusu mwananchi moja kwa moja ambapo aliwataka washiriki kuwa makini na kuziepuka dosari zote ambazo zinaweza kuharibu utekelezaji wa zoezi hilo.

Alisema kutokana na mafunzo hayo waliyopata na kuwepo kwa viongozi mbalimbali walioshiriki mafunzo anaamini zoezi hilo litakwenda kufanyika kwa mafanikio makubwa.

Aidha Muragili alisema ili zoezi hilo liweze kufanyika vizuri na kuweza kuonekana katika kiwango kinachohitajika linagharama kubwa ambazo haziwezi kuepukwa kwani zipo gharama ambazo zitabebwa na Serikali Kuu,Halmashauri na zipo gharama ambazo zitabebwa na wananchi hivyo wasiogope kuzipokea.

Alisema gharama hizo zikishuka kwenye ngazi ya mwananchi zinakuwa sio kubwa bali ni ndogo zaidi akitolea mfano wa kubandika vibao vidogo vya mitaa na vya namba za nyumba ambavyo vipo ndani ya uwezo wao ukilinganisha na kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya kutoa mafunzo na mambo mengine.

Alisema kazi hiyo ya kuweka vibao hivyo vya mitaa lipo ndani ya uwezo wao na Serikali haiwezi kuweka vibao hivyo kila sehemu hivyo aliomba vibao hivyo vyenye rangi njano na maandishi meusi na nguzo zake viwekwe na watu wa mtaa husika kwa kuzingatia utaratibu watakao elekezwa na Manispaa ili viwekwe kwa mpangilio na kuwa na mandhari nzuri.

Baadhi ya wadau mbalimbali waliokuwepo kwenye mafunzo hayo wakitoa maoni yao akiwepo Meneja  wa Mfuko wa  Pensheni kwa watumishi  (PSSSF ) Mkoa wa Singida, Beda Mgonja akizungumza kwenye mafunzo hayo.    PSSSF Mkoa wa Singida Beda Mgonja alisema mpango wa anwani za makazi na postikodi una manufaa makubwa hapa nchini hasa katika mashirika yao ambayo yanafanya kazi na jamii.

"Sisi tunafanya kazi na jamii hasa wastaafu ambao mara kwa mara tumekuwa tukionana nao kwa ajili ya kuwalipa fedha zao hivyo mpango huu wa anwani za makazi utatusaidia kuwafikia kiurahisi kwenda nyumbani kwao na kuwapunguzia adha ya kuja ofisini kwetu ukizingatia wastaafu wengi ni wazee na wanakuwa hawana uwezo wa kutembea" alisema Mgonja. 

Akitoa mchango wake Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) Mkoa wa Singida Burhan Mlau alisema Anwani za makazi na postikodi zitawasaidia wageni wanaofika mjini hapa kuwapata jamaa na ndugu zao maeneo wanayoishi kwa kuwaelekeza boda boda mtaa na namba ya nyumba walipo tofauti na sasa ambapo hakuna majina ya mitaa wala namba za nyumba.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu alisema Manispaa imetambua umuhimu wa wadau mbalimbali kushirikishwa katika zoezi la uwekaji anuani za makazi na postikodi na kuwa watasaidia kutekeleza kwa wakati mpango huo ambao kwa wilaya hiyo ili kuifanya kazi hii kuwa shirikishi na hivyo kuleta wepesi katika utekelezaji ambapo kwa mkoa wa Singida wanatakiwa kukamilisha zoezi hilo Aprili 15 mwaka huu na kitaifa mwezi Mei.

Alisema Mpango huu una manufaa mengi  ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi  katika utawala bora kwa kutambua makazi ya raia wote nchini, kuimarisha usalama, kuboresha utoaji huduma za Jamii na kuongeza pato la taifa kwa kuboresha ukusanyaji wa kodi mbalimbali.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Singida Mjini, Lucia Mwiru alimpongeza Ofisi ya Mkurugenzi kupitia kamati ya kurat

HALMASHAURI YA JIJI LA ILALA 'DAR ES SALAAM' YATOA TUZO KWA SHULE ZA MSINGI ZA SERIKALI NA BINAFSI

Baadhi ya washiriki katika hafla ya utoaji tuzo kwa shule 20 binafsi na Serikali pamoja na walimu wakuu wakiwa katika hafla iliyoandaliwa na Halmashauri ya Jiji la Ilala Idara ya Elimu Msingi iliyofanyika juzi.
Washiriki wakionesha tuzo zao baada ya kukabidhiwa.


Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya shughuli hiyo,  Godrick Rutayungururwa akizungumzia tuzo hizo ambazo zimetolewa kama motisha kwa walimu ili kuinua chachu ya ufundishaji.
Hafla ikiendelea.

Thursday, March 3, 2022

SUA NA MKEMIA MKUU WA SERIKALI WAWAJENGEA UWEZO WAGANGA WA TIBA ASILI NCHINI

Mkuu wa Mradi wa VASPHARD Dk. Faith Mabiki akizungumza kwenye mafunzo kwa Waganga wa Tiba Asili   ya siku moja ya watengenzaji wa dawa za asili kutoka mikoa mbalimbali yaliyofanyika mkoani Morogoro jana

Mhadhiri wa  Idara ya Sayansi ya mazao ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Dk. Richard Madege akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.

HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI MKOA WA SINGIDA YAZIDI KUNG'ARA KITAALUMA

Afisa Elimu Taaluma  Mkoa wa Singida,Eva Mosha akizungumza  kwenye kongamano la siku ya Taaluma na kujadili mbinu za kuongeza ufaulu kwa wanafunzi lililofanyika wilayani Ikungi hivi  karibuni  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Haika Masawe akizungumza kwenye kongamano hilo.
Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Margaret Kapolesya akitoa taarifa kwenye kongamano hilo.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu akizungumza kwenye kongamano hilo.
Afisa wa Benki ya NMB Wilaya ya Ikungi, Grace Kasege akizungumzia shughuli mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.
Afisa Elimu Mstaafu wa Mkoa wa Singida,  Hamis Maulid akichangia jambo kwenye kongamano hilo.
Taswira ya kongamano hilo.
Burudani zikitolewa.
Burudani zikitolewa kwenye kongamano hilo.
Afisa Mahusiano ya Jamii wa Kampuni ya Shanta, Mukein Habib akizungumza kwenye kongamano hilo.
Meneja Maendeleo ya Biashara wa Benki ya NBC Tawi la Singida Olairiuani Elirehema akizungumza na wadau na wananchi kwenye kongamano hilo.
Afisa wa Benki ya CRDB Tawi la Singida Musa Walwa akielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.

Burudani ikiendelea.
Makamu Mwenyeki wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Stephen Mtyana akichangia jambo.

Wednesday, March 2, 2022

ASASI ZA KIRAIA ZAKARIBIA KUTOKOMEZA UKEKETAJI WATOTO MKOANI SINGIDA

Mmoja wa Waelimishaji kutoka Dawati la Jinsia  ( aliyeshika kipaza sauti kushoto) akitoa elimu juu ya madhara ya ukeketaji kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kijota, Wilaya ya Singida vijijini hivi karibuni.

Baadhi ya zana zilizokuwa zikitumika kuwakeketa watoto wa kike zikioneshwa.

Tunda la Ndulele, moja ya zana mpya inayotumika kukeketa watoto wachanga wa kike. 



Abby Nkungu, Singida. 


JUHUDI za Asasi za kiraia kutokomeza vitendo vya ukeketaji mkoani Singida huenda zikazaa matunda hivi karibuni baada ya kufanikiwa kubaini mbinu mpya zinazotumiwa na baadhi ya wazazi na walezi kuwasugua sehemu za siri watoto wao wachanga wa kike kwa kutumia ndulele, majivu au kuwafinya kwa kucha.

Mradi wa kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia; ikiwemo ukeketaji, unaotekelezwa na mashirika ya Action Aid na MEDO mkoani Singida umebaini kuwa baada ya Serikali na wadau wake kusimamia ipasavyo sheria ya kuzuia vitendo hivyo, wazazi na walezi wamebuni mbinu mpya za kuwafanyia mila hiyo potofu watoto wao wachanga wa kike kabla hawajajitambua.

Hayo yalibainika katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kijota Singida Vijijini chini ya mashirika hayo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) ya miaka mitano 2021/22 - 2025/26.

Katika mkutano huo, baadhi ya wazazi Doricas Manase mkazi wa Ilongero, Singida na Rahel Nkindwa mkazi wa Nduu walisema licha ya juhudi kubwa za Serikali na wadau wake kupinga ukeketaji, wanaoendeleza mila hiyo wamekuja na mbinu mpya kukwepa mkono wa sheria. 

“Hili jambo sasa linafanyika kwa siri kubwa, mama akikaribia kujifungua anaomba ruhusa kwenda kwa shangazi yake na akishajifungua mtoto wa kike wanakifinya kwa ukucha kichanga hicho sehemu zake za siri hadi damu itoke na wakati mwingine wanamsugua kwa majivu au ndulele” alieleza Doricas.

Naye Rahel alisema ukatili huo sasa unafanyika bila wanaume kujua kwani wengi wao wameelimika; hivyo akaomba Serikali kutoa kibali cha watoto wote wa kike kukaguliwa na waatalamu wa afya waendapo kliniki na wataobainika kukeketwa, wazazi au walezi wao wachukuliwe hatua kali.  

Afisa Muuguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Singida, Neema Mlowe alipendekeza kuwa pamoja na kuchukua hatua za kisheria ni vyema jamii ikaendelea kuelimishwa juu ya madhara ya ukeketaji. 

“Hii mila pamoja na kuwa  kinyume cha sheria na kukiuka misingi ya haki za binadamu, kiafya pia ina madhara kwani mwanamke aliyekeketwa huvuja damu nyingi wakati wa kujifungua na hata kupoteza maisha” alifafanua. 

Hata hivyo, Naibu Mkuu wa Kituo kikuu cha Polisi Singida Inspekta Athumani Muna alisema pamoja na ukeketaji kuendelea, juhudi za mashirika hayo zimesaidia  kubaini mbinu mpya za wazazi na walezi hivyo kuwa rahisi kwa mpango huo kuzaa matunda ya kukomesha vitendo hivyo. 

“Tumeshajua mbinu yenu na sisi kama Jeshi la Polisi na dawati la jinsia tunaenda kujipanga upya na kuja na mbinu yetu. Lazima tushirikiane wadau wote kutokomeza mila hii potofu ambayo pia ni ukatili wa hali ya juu kwa watoto” alisema Insepkta Athumani. 

Takwimu za idara ya afya mkoani Singida zinaonesha kuwa wastani wa asilimia 20 ya wanawake wanaokwenda kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya wamekeketwa, wakati ripoti ya hali ya ukeketaji nchini ikionesha mkoa wa Singida unashika nafasi ya tano ukitanguliwa na Manyara, Dodoma, Arusha na Mara. 

Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) imekuja kama mwarobaini wa kuhakikisha vitendo kama hivyo vinadhibitiwa kwa watoto walio umri wa miaka 0 hadi 8 kwa kushirikisha sekta mbalimbali ili kuleta ulinzi na usalama kwa kundi hilo muhimu.  


WAZIRI WA MAJI JUMAA AWESO AZINDUA MRADI WA UHIFADHI VYANZO VYA MAJI KARATU


Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa uhifadhi na utunzaji chanzo cha maji cha chemchem za Qang'dend na mito ya Baray na Mang'ola wilayani Karatu mkoani Arusha juzi. Kushoto ni  Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Musa Matoroka.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipanda kwenye tengi la maji kwa ajili ya kulikagua baada ya kuzindua  mradi wa uhifadhi na utunzaji chanzo cha maji cha chemchem za Qang'dend na mito ya Baray na Mang'ola wilayani Karatu mkoani Arusha juzi.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikagua birika la kunyweshea mifugo wakati akizindua mradi wa uhifadhi na utunzaji chanzo cha maji cha chemchem za Qang'dend na mito ya Baray na Mang'ola wilayani Karatu mkoani Arusha juzi.

Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji, Dk.George Lugomela, akitoa taarifa ya mradi huo.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Wanyenda Philip Kutta, akitoa taarifa fupi wakati wa uzinduzi huo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Musa Matoroka akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA) Mkoa wa Arusha, Cecilia Paleso, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Dadi Kolimba, akichangia jambo kwenye uzinduzi huo.