Wednesday, April 13, 2022

TANZANIA KUWA NCHI YA KWANZA AFRIKA KWA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI


Mkuu wa Mkoa Singida Dk.Binilith Mahenge akishiriki kujenga Shule Mpya ya Sekondari inayojengwa Kitongoji cha Kisubio Iguguno wilayani Mkalama mkoani hapa wakati wa ziara yake kikazi ya siku moja ya kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo inayoendelewa kutekelezwa  ya Sekta ya Afya, Maji na Elimu iliyofanyika jana.
Mkuu wa Mkoa Singida Dk.Binilith Mahenge akisisitiza jambo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa shule hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo na Kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkalama, Mhandisi Lameck Itungi.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo akishiriki kujenga Shule Mpya ya Sekondari inayojengwa Kitongoji cha Kisubio.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Selemani Msunga akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa halmashauri hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, James Mkwega.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Victorina Ludovick akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Gumanga.
Katibu Tawala Wilaya ya Mkalama, Elizabeth Rwegasira akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa Singida Dk.Binilith Mahenge akisisitiza jambo wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wilaya hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo.
Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Daniel Tesha akitoa taarifa ya utekelezaji wa baadhi ya miradi kwa mkuu wa mkoa.
Kikao cha kupokea taarifa kikifanyika.
Mkuu wa Mkoa Singida Dk.Binilith Mahenge akishiriki kuchimba msingi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Gumanga.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo akishiriki kuchimba msingi wa kituohicho cha Afya.
Wananchi wa Kata ya Gumanga wakimlaki Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge (kulia)
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Gumanga Mshamu Kalugula akitoa taarifa ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Gumanga.
Wananchi wa Kata ya Gumanga wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Gumanga.
Diwani wa Kata ya Gumanga, James Mkwega akizungumza kwenye mkutano huo.

Tuesday, April 12, 2022

MTENDAJI KATA DUNG'UNYI ATOA ONYO KALI KWA WAZAZI WANAORUBUNI WATOTO WAO WASIENDE SHULE

Afisa Mtendaji  wa Kata  ya Dung'unyi wilayani, Ikungi mkoani Singida  Yahaya Njiku, akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Munkinya wakati wa ziara yake ya kukagua miradi katika  kata hiyo aliyoifanya jana ambapo pia alipata fursa ya kuzungumza na Wazazi na Walezi wa wanafunzi hao.

Afisa Mtendaji  wa Kata  ya Dung'unyi wilayani, Ikungi mkoani Singida  Yahaya Njiku, akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanafunzi hao.
Wazazi na Walezi wakiwa kwenye mkutano huo.
Afisa Elimu wa Kata ya Dung;unyi, Ester Mkoma (kushoto) akizungumza na Wazazi na Walezi katika ziara hiyo.
Afisa Mtendaji  wa Kata  ya Dung'unyi wilayani, Ikungi mkoani Singida  Yahaya Njiku, akizungumza na Wazazi.
Afisa Mtendaji  wa Kata  ya Dung'unyi wilayani, Ikungi mkoani Singida  Yahaya Njiku, akizungumza na Wanafunzi wa shule hiyo. 

 

Na Dotto Mwaibale, Singida

 

AFISA Mtendaji wa Kata  ya Dung'unyi wilayani, Ikungi mkoani Singida  Yahaya Njiku ametoa onyo kali kwa Wazazi na Walezi wenye tabia ya kuwarubuni watoto wao waache kwenda shuleni huku wakitoa sababu mbalimbali ikiwemo ya kutaka kuwaoza. 

Njiku alitoa onyo hilo jana alipokuwa akizungumza na wazazi na wanafunzi  wakati wa ziara yake ya kukagua miradi katika Shule ya Sekondari Munkinya ilioyopo katika kata hiyo. 

" Hivi karibuni kumezuka tabia ya  baadhi ya wazazi kuwarubuni watoto wao waache shule ili wabaki nyumbani kufanya kazi mbalimbali ikiwemo kuwaoza  na wengine wanaambatana na watoto wao mpaka ofisi za Serikali za Vijiji na kata ambako wamekuwa wakitoa madai eti watoto wao hawataki shule hivyo wanaomba wafutwe" alisema Njiku. 

Njiku alisema mzazi au mlezi atakaye bainika akifanya hivyo hatamvumilia atamkamata na kumfikisha kwenye vyombo cha dola na katika jambo hilo hata kuwa na huruma na mtu.

Alisema ni jambo la ajabu kwa mzazi na mlezi kufanya jambo hilo kwani Serikali imetumia fedha nyingi kuboresha miundombinu mashuleni ili watoto wapate elimu katika mazingira bora alafu anatokea mzazi akidai anataka mtoto wake aachishwe shule. 

" Itakuwa Serikali ya ajabu ambayo itaukubali upuuzi huo nasema ole wake  mzazi tukakaye mbaini akifanya hivyo" alisisitiza Njiku kwa ukali. 

 Alisema ni wajibu wa wazazi na walezi kushirikiana na Serikali kuhakikisha watoto wanapata mazingira bora ya elimu wawapo shuleni na nyumbani lakini si kwa kuwarubuni kuacha shule. 

Njiku alitumia nafasi hiyo kumshukuru  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani kwa kuwapatia kiasi cha Sh. Milion 40 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili katika shule hiyo ambapo aliwasisitiza wanafunzi hao kusoma kwa bidii.

RC SINGIDA AITAKA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRAMBA KUKAMILISHA MIRADI

Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge akielekeza jambo wakati akikagua  ujenzi wa Wodi ya dharura (EMD) katika Hospitali ya Wilaya Kiomboi wilayani Iramba mkoani hapa katika ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kukagua miradi ya maendeleo  ya Sekta ya Elimu, Afya na Maji aliyoifanya leo.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda.

Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge akikagua  ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kisiriri wakati wa ziara hiyo. Kushoto ni Mhandisi wa Wilaya hiyo Profiri Modaha.

Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge na Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda wakiongoza ukaguzi wa Kituo cha Afya cha Kisiriri.

Mkuu wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge akielekeza jambo wakati akikagua  ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Maluga.

Thursday, April 7, 2022

CHAMA CHA TGGA CHATOA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA TABIANCHI MKOANI SINGIDA

      Afisa Mradi Msaidizi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira  kutoka Chama      cha Girl Guides Tanzania (TGGA) Praxeda Swai akizungumza wakati wa mafunzo ya wasichana na kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi yalioanza leo mjini Singida.

Kamishna wa TGGA Mkoa wa Singida, Rehema Sinda akizungumza kwenyemafunzo hayo.
Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Singida Anitha Msangi akiongoza mafunzo hayo.
Katibu wa Vijana wa chama hicho Mkoa wa Singida, Mary Gukwi akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakishiriki michezo mbalimbali ya kuchangamsha viungo.
Michezo ikiendelea.
Michezo ikiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.

 

Na Dotto Mwaibale,  Singida

 

CHAMA cha Girl Guides Tanzania (TGGA) kimetoa mafunzo kwa walimu kutoka shule za Sekondari na Msingi katika Halmashauri za wilaya  tatu mkoani Singida yaliyowalenga  wasichanaa na masuala ya mabadiliko ya tabianchi. 

Mafunzo hayo yaliwahusisha walimu na wanajamii kutoka katika Halmashauri za wilaya yaIkungi, Singida DC na Manispaa. 

Akizungumzia mafunzo hayo Afisa Mradi Msaidizi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira kutoka TGGA, Praxeda Swai alisema mafunzo hayo ya siku nne yamewalenga walimu hao na wasichana  ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na masuala ya tabia nchi na kugombea uongozi. 

“Baada ya kuwapatia mafunzo haya walimu na wanajamii ambao tumewakutanisha hapa wataenda kuwa mabalozi wa kuhamasisha jamii kuchukua hatua chanya cha kukabiliana na changamoto za tabianchi akitolea mfano Mkoa wa Singida  ambao ulikuwa ukikabiliwa na ukame kutokana na ukataji wa miti” alisema Swai. 

Alisema kazi kubwa watakayokuwa wakiifanya ni kuhamasisha jamii kupanda miti kwani wahanga wakubwa kunapokuwa na ukame ni wasichana na mama zao ambao wanakuwa wakiangaika kwenda kutafuta maji wakitumia muda mwingi na umbali mrefu na kuwa lengo lao ni kuifanya Singida kuwa ya kijani. 

Mafunzo hayo yalioanza leo katika Ukumbi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Singida yatafunguliwa kesho ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida mjini Mhandisi Paskas Muragili na yanatarajiwa kufikia tamati Aprili 10, 2022.

SINGIDA WAANZA KUTATUA CHANGAMOTO ZA ELIMU KWA WATOTO WADOGO

p>

Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk Binilith Mahenge akieleza mafanikio mbalimbali yaliyopatikana mkoani kwake katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Wanafunzi wa darasa la Awali wakifurahia mazingira ya kujifunzia katika darasa jipya lililojengwa hivi karibuni.

Wanafunzi wa darasa la Awali wakiwa katika harakati za kujifunza mambo mapya darasani



Na Abby Nkungu, Singida

 

MKOA wa Singida umefanikiwa kuongeza kiwango cha uandikishaji wanafunzi  elimu ya awali kwa zaidi ya asilimia tisa kwa kipindi cha mwaka mmoja ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha sekta hiyo kuanzia ngazi ya chini katika kumwezesha kila mtoto kupata haki ya msingi ya elimu. 

Mkuu wa mkoa, Dk Binilith Mahenge alibainisha hayo mjini hapa katika taarifa yake juu ya Mafanikio mbalimbali ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. 

Dk Mahenge alisema kuwa katika kipindi hicho, kiwango cha uandikishaji wanafunzi wa darasa la Awali kimeongezeka kutoka wanafunzi 43,801 sawa na asilimia 87 mwaka jana hadi 49,785 sawa na asilimia 96.6 ya lengo  kufikia mwezi Machi mwaka huu. 

Alieleza kuwa pamoja na sababu nyingine, kupanda kwa uandikishaji huo kumechangiwa  kwa kiasi kikubwa na kuanzishwa shule shikizi 77 kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huu katika kuwaondolea wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu kufuata shule. 

Naye Ofisa elimu mkoa wa Singida, Maria Lyimo alifafanua kuwa shule hizo shikizi zina wanafunzi wa chekechea takriban 8,700 ambao wanaendelea na masomo kama kawaida.

“Wewe unajua  Singida  ni miongoni mwa  mikoa inayotekeleza Programu Jumuishi ya Taifa ya  Malezi, Makuzi na Maendeleo ya  Awali ya Mtoto ( PJT- MMMAM). Kwetu sisi, hii ni sehemu ya  utekelezaji wa Programu hiyo ambayo uzinduzi wake ulifanyika Dodoma mwaka jana” alisema Ofisa elimu huyo. 

Mmoja wa walimu katika shule shikizi Mwembe Mmoja nje kidogo ya mji huu, Fatuma Yusufu alisema kuwa shule hizo zimesaidia kupunguza utoro, kuongeza usikivu darasani na kuwafanya watoto kupenda elimu. 

“Wapo watoto katika baadhi ya shule wanatoka  mbali na wanatembea zaidi ya kilomita 14 kwenda shule na kurudi nyumbani. Hebu fikiria, mtoto wa chini ya miaka minane anayesoma  chekekechea anafika shuleni kachoka, anapiga miayo tu kwa njaa na uchovu  kisha anachapa usingizi darasani hivyo hasomi chochote" alieleza Mwalimu huyo. 

Nao baadhi ya wazazi na walezi wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zilizosaidia katika ujenzi wa shule hizo shikizi ili kuondoa adha; hasa kwa watoto wanaosoma Chekechea.

“Watu wamekuwa wakijiuliza kwa nini wazazi wengi wanapenda kupeleka watoto wao  wadogo shule binafsi za Awali. Sababu ni kama hiyo.....mazingira ya shule zetu  nyingi za Serikali hayakuwa rafiki kwa watoto wadogo. Kwa kweli Mama ameupiga mwingi kwenye elimu, sekta hii itapanda sana” alisema Ntandu Mumwi, mkazi wa Utemini.

Rehema Ali mkazi wa Mandewa pamoja na kumshukuru Rais  Samia kwa kutoa fedha za madarasa hayo, alisema bado kuna haja ya kuboreshwa zaidi mazingira; hasa kwa watoto wadogo ambao hupenda michezo mbalimbali jambo ambalo pia linaungwa mkono na Wataalam wa masuala ya watoto. 

Tanzania ni Nchi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki kuifanya elimu ya Awali kuwa ya lazima kwenye Sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 ili kuijumuisha elimu ya Awali katika elimu ya msingi kwa kuzitaka shule zote za msingi kuwa na darasa la Awali kwa watoto walio chini ya miaka mitano.  

Tuesday, April 5, 2022

SHIRIKA LA SPRF LAIBUA TUKIO LA BABA KUKOJOLEA UNGA NA MBOGA ILI KUIKOMOA FAMILIA YAKE MKOANI SINGIDA


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Jiokoe na Umaskini yaani Stars of Poverty Rescue Foundation (SPRF) Dk. Suleiman Muttani akizungumza katika kikao cha Watekelezaji wa Sheria kilichoketi kwa ajili ya kuhimiza utekelezaji wa mkakati wa kushughulikia kesi za ukatili wa kijinsia kilichofanyika hivi karibuni wilayani Ikungi mkoani Singida.

Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Ikungi, Mrakibu wa Polisi (SP)  Stephen Chaula akizungumzia jinsi wanavyo yapokea matukio ya ukatili wa kijinsia kutoka katika vituo saba vya polisi vilivyopo katika kata mbalimbali wilayani humo kabla ya kuyapeleleza na kufungua kesi ili zipelekwe mahakamani.

Saturday, April 2, 2022

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ATOA ZAIDI YA SH. 2 BILIONI KUWATUA NDOO WANAWAKE TARAFA YA KISIRIRI IRAMBA

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda  (wa pili) akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa  jengo la Wagonjwa Mahututi (ICU) linalojengwa Hospitali ya Wilaya Kiomboi mkoani Singiga juzi. Kulia ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya Kiomboi Abel Mafuru.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kiomboi Abel Mafuru akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo.
Wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya huo wakiwa kwenye ukaguzi wa jengo hilo.


Mhandisi wa Wilaya hiyo, Profiri Modaha akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akizungumzia ujenzi huo wakati wa ukaguzi.
Wajumbe wa kamati hizo wakikagua matengenezo ya barabara ya Old Kiomboi-Kisinda na Doromoni.
Meneja wa TARURA Wilaya ya Iramba Mhandisi Evance Kibona akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo.
Mjumbe wa kamati hiyo, Edward Makala akichangia jambo wakati wa ukaguzi wa barabara ya Kiomboi-Ruruma-Uwanza.
DC wa Iramba Suleiman Mwenda akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa barabara hiyo. Kulia ni Meneja wa TARURA Wilaya ya Iramba, Mhandisi Venance Kibona.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, David Madelu akichangia jambo wakati wa ukaguzi wa mradi wa upelekaji umeme Kijiji cha Tutu.
Muonekano ya vyumba vya maabara katika Shule ya Sekondari ya New Kiomboi.
Ukaguzi wa ujenzi wa Maabara Shule ya Sekondari ya New Kiomboi ukifanyika.
Mkuu wa Sekondari ya New Kiomboi Amadeus Kiduu akitoa taarifa ya ujenzi wa vyumba viwili vya maabara.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda (kulia) akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya New Kiomboi wakati wa ukaguzi wa vyumba vya maabara.
Ukaguzi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kisiriri ukifanyika.
Kamati hiyo ikipokea maelezo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kisiriri kutoka kwa Mganga Mkuu wa Wilaya Iramba Hussein Sepoko (kulia)
Muonekano wa kituo cha Afya cha Kisiriri.
Ukaguzi wa Mradi wa Maji Kijiji cha Kisiriri ukifanyika.
Meneja wa Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Iramba Mhandisi Ezra Mwacha akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo.