Tuesday, June 7, 2022

WAZIRI NDAKI: BANDARI YA UVUVI KILWA ITAIMARISHA UCHUMI WA BLUU NCHINI


  Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Anayesimamia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah (kushoto) na Meneja Mkuu, Kampuni ya ujenzi ya CHEC, Cheng Yongjian (kulia) wakisaini nyaraka za makubaliano ya ujenzi wa bandari ya uvuvi ya Kilwa katika hafla fupi ya utiaji saini iliyofanyika jijini Dodoma Juni 7, 2022. Katikati ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki. Kushoto kwa Waziri ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt. Christina Ishengoma.

 Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Anayesimamia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah (kushoto) akipeana mkono na  na Meneja Mkuu, Kampuni ya ujenzi ya CHEC, Cheng Yongjian (kulia) ikiwa ni ishara ya makubaliano baada ya kusaini nyaraka za makubaliano ya ujenzi wa bandari ya uvuvi ya Kilwa katika hafla fupi ya utiaji saini iliyofanyika jijini Dodoma Juni 7, 2022.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki akitoa hotuba katika hafla fupi ya utiaji saini wa nyaraka za makubaliano ya ujenzi wa Bandari ya Uvuvi ya Kilwa baina ya Serikali na Kampuni ya Ujenzi ya China Habour Engineering Company (CHEC) iliyofanyika jijini Dodoma Juni 7, 2022. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt. Christina Ishengoma na kushoto ni  Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, anayesimamia sekta ya Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah. 

Monday, June 6, 2022

VIONGOZI WANAOTENGENEZA MAKUNDI WAIPASUA CCM WILAYA MUSOMA MJINI


 

 

Na Thobias Mwanakatwe

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Musoma  mkoani Mara kimesema makundi  yanayotengenezwa na baadhi ya viongozi ndio chanzo cha kutokea malumbano yasio na tija kwenye uchaguzi unaoendelea ndani ya chama ngazi ya matawi.

Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Musoma, Abubakari Nyamakato, alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kufuatia taarifa zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari kwamba Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma, Magiri Benedictor anadaiwa kupigana ngumi na Katibu wa Wazazi wilaya, Zainabu David wakati wa uchaguzi wa  chama tawi la Nyasho.

Nyamakato alisema kimsingi tukio hilo halikutokea bali limepikwa na baadhi ya viongozi ambao wamekuwa vinara wa kutengeneza makundi ndani ya chama na kuwajengea chuki wengine kutokana na hofu ya kuja kuangushwa katika uchaguzi mkuu wa 2025.

"Katika Wilaya yetu hii viongozi wawili (anawataja majina) ndio wamekuwa ni tatizo na mabingwa wa kutengeneza makundi ndani ya chama na hata katika tukio hili la uchaguzi tawi la Nyasho wamehusika kutokana na maslahi yao ya kisiasa," alisema.

Nyamakato alisema kilichojitokeza ni kwamba baada ya kutokea malumbano yaliyotokana na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa tawi kuonekana sio wakazi wa tawi la Nyasho jambo hilo lilipofika wilayani ilitolewa agizo uchaguzi katika tawi hilo uahirishwe ili kuorodhesha upya wajumbe halali wa tawi ndipo uchaguzi ufanyike.

"Kimsingi hakuna ugomvi wala kupigana Mwenyekiti na Katibu wa Wazazi kilichotokea wajumbe walikuwa wanabishana baada ya kubainika kulikuwa na wajumbe ambao sio wakazi wa tawi la Nyasho," alisema.

Aliongeza kuwa baada ya kutokea malumbano hayo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ambaye ndiye msimamizi mkuu wa chama alifika eneo hilo na kuagiza uchaguzi uahirishwe kwanza ili kuepusha vurugu zaidi zisitokee.

"Kudai kwamba Mwenyekiti wa CCM amepigana na Katibu wa Wazazi huku ni kutaka kuchafua Mwenyekiti aonekane hafai kwasababu wapo viongozi waliojipanga kutaka kumchafua ili malengo yao ya kisiasa yaweze kutimia," alisema.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma, Magiri Benedictor, alisema yeye ni mkongwe katika mambo ya  siasa hivyo kamwe hawezi kufanya tukio la kupigana na Katibu wa Wazazi wilaya na kwamba kinachofanyika ni baadhi ya viongozi wasiompenda kutaka kumchafua kisiasa.

" Mimi katika uongozi wangu nimekuwa na misimamo isiyoyumba ambapo katika kukiongoza chama nazingatia kanuni na taratibu za chama sasa hilo ndilo linalowaumiza mahasimu wangu wa kisiasa na sasa wananitengenezea mizengwe kunichafua," alisema.

Benedictor alisema kama kweli alihushika kumpiga Katibu wa Wazazi suala hilo lingekuwa limefikishwa polisi lakini hadi sasa halijapelekwa kokote zaidi ya kuandikwa kwenye vyombo vya habari.

Aliongeza kuwa pamoja na mipango michafu inayofanywa na mahasimu wake wa kisiasa kumchafua haitamkatisha tamaa katika harakati zake za kukipigania chama na kukiongoza katika maadili ili kiendelee kuwa kimbilio la wananchi katika kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

DC IKUNGI AWATAKA WAKULIMA KUHIFADHI MAZAO YAO ILI WAYAUZE KWA BEI YENYE TIJA

Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na Wadau wa maendeleo wakiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro (kulia) wakivuta pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi la Mradi wa ujenzi wa Ghala la Kisasa la kuhifadhi zao la Alizeti lililojengwa Kijiji cha  Mnang;ana, Kata ya Sepuka katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki wilayani humo mkoani Singida.
Uzinduzi huo ukifanyika.Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi. Mwenyekiti wa wilaya  hiyo, Ally Mwanga,kushoto ni Diwani wa Kata ya Sepuka, Halima Ng'imba na Mwakilishi wa Shirika la Wanawake na Jinsia la Umoja wa Mataifa (UN-WOMEN), ambaye pia ni Mtaalam wa Kitengo cha kuwawezesha wanawake kiuchumi,  Lilian Mwamdanga.
Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Wilaya ya Ikungi, Gurisha Msemo akiwa kwenye hafla hiyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga akizungumza kwenye hafla hiyo.

Mwakilishi wa Shirika la Wanawake na Jinsia la Umoja wa Mataifa (UN-WOMEN), ambaye pia ni Mtaalam wa Kitengo cha kuwawezesha wanawake kiuchumi,  Lilian Mwamdanga akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro, akisalimiana na wananchi waliofika kuhudhuria hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ghala hilo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi.
DC Jerry Muro akisalimiana na wazee waliofika kwenye hafla hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo wakikagua Ghala hilo.
DC Jerry Muro akiwa na viongozi wa wilaya hiyo wakati wakikagua Ghala hilo.
Wazee wakiwa kwenye hafla hiyo.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ikungi, Haika Masawe akizungumza kwenye hafla hiyo.

WAZIRI NDAKI AWATAKA WAFUGAJI, WAVUVI KUHIFADHI MAZINGIRA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (wa pili kulia) akisaini kitabu cha mahudhurio ya Wageni alipotembelea banda la maonesho la Wizara ya Mifugo na Uvuvi  yaliyokuwa yakifanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete, jijini Dodoma. Maonesho hayo yalikuwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake ni Juni 5, 2022. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Sekta ya Uvuvi,  Bw. Melton Kalinga. Wengine kushoto ni Maafisa, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Sekta ya Uvuvi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (kulia) akipatiwa maelezo kuhusu uandaaji na uhifadhi wa malisho ya mifugo na Afisa Mifugo Mkuu, Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani (Sekta ya Mifugo), Bw. Deograsias Ruzangi alipotembelea banda la maonesho la Wizara ya Mifugo na Uvuvi  yaliyokuwa yakifanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

Sunday, June 5, 2022

IKUNGI KUWA NA JENGO LA KURATIBU UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO NA WANAWAKE




Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro (kushoto) akifurahia ramani ya Jengo la kuratibu vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIWOHEDE, Mama Justa Mwaituka.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Jerry Muro (kushoto) akionesha kwa Waandishi wa habari muonekano wa Jengo litakalojengwa wilayani mwake kwa ajili ya kuratibu vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake. Kushoto ni Mkurugenzi.
Pichani ni mtoto ambaye amepitia ukatili wa hali ya juu kwa watoto. Inaaminika kuwa asilimia 90 ya Vitendo vya Ukatili dhidi ya watoto husababishwa na wanafamilia.

Huyu ni mmoja wa watoto wanaopitia Ukatili dhidi ya watoto.


 

Na Abby Nkungu, Singida

 

WILAYA ya Ikungi mkoani Singida inakusudia kutumia zaidi ya shilingi milioni 110 kwa ajili ya  utekekezaji wa shughuli za mradi wa ujenzi wa kituo maalum cha kupinga vitendo mbalimbali vya ukatili wa kijinsia kwa  watoto  na wanawake katika  kipindi cha mwaka ujao wa fedha wa 2023/24.

Mkuu wa Wilaya hiyo Jerry Muro alisema kuwa ujenzi wa  kituo hicho ni sehemu ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa kuhusu Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT - MMMAM) inayoendelea hadi 2026.

Alisema kuwa lengo la hatua hiyo ni kudhibiti vitendo vya ukatili wa kijinsia ambapo takwimu zinaonesha kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi Juni mwaka huu, jumla ya watoto 36 wenye umri wa chini ya miaka minane (0 - 8), wamefanyiwa vitendo mbalimbali vya ukatili wa kijinsia.

DC Muro alifafanua kuwa watoto hao wamefanyiwa ukatili wa kingono, kimwili, kihisia au utekelezaji hivyo kuwasababishia madhara ya kisaikolojia, magonjwa, ulemavu, kupoteza ndoto zao na haki ya elimu na kuleta ongezeko la watoto waishio mazingira magumu na hatarishi.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa wilaya, kesi 9 zipo mahakamani, moja ilifungwa kituo cha polisi, nyingine iko rufaa Ustawi wa Jamii na zilizobaki watuhumiwa hawakuweza kupatikana. 

Alisema kuwa pamoja na shughuli hiyo kuwemo kwenye utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa, mradi huo mkubwa wa aina yake umetokana na maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan yanayoelekeza kila wilaya kukomesha matukio na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake.

 "Mradi huu unafadhiliwa na Shirika lisilo la kiserikali la KIWOHEDE. Mimi na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Mama Justa Mwaituka tumekamilisha mazungumzo na kwa pamoja tumekubaliana ujenzi wa jengo litakaloitwa MKONO SHUFAA na miundombinu muhimu, uanze mara moja. Jengo hilo litajengwa katika hospitali ya Wilaya yetu" alieleza DC Muro.

Alisema kuwa  pamoja na ujenzi wa kituo  hicho,  pia  wanaendelea kutoa elimu kwenye Jamii na shuleni juu ya namna ya kupinga ukatili wa kijinsia, kuanzisha  kamati za ulinzi wa mwanamke na mtoto kwa kushirikisha jamii na wadau mbalimbali na kuendeleza utoaji wa elimu ya Malezi na Makuzi kwa wazazi na Jamii kwa kushirikisha Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa KIWOHEDE, Justa Mwaituka alieleza kuvutiwa na jinsi ambavyo wilaya hiyo inapambana katika kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii na kuahidi kuendelea kutoa misaada mbalimbali ya hali na mali ili kutokomeza vitendo hivyo.

Hata hivyo, baadhi ya wadau wanasema pamoja na hatua hizo bado kuna haja ya kutoa   elimu zaidi kwa jamii juu ya umuhimu wa kuzuia  na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo yao.

“Jamii yetu bado haina elimu ya kutosha. Unakuta mtu mtoto wake amefanyiwa ukatili wa kingono kwa kulawitiwa au kubakwa lakini wanamaliza suala hilo kifamilia. Hii haisaidii kukomessha vitendo hivyo” alieleza Patrick Mdachi Ofisa Maendeleo ya Jamii mstaafu na kuungwa  mkono na Rehema Daniel aliyetaka viongozi wa Mitaa na Vijiji kuacha kumaliza masuala hayo ngazi za chini bali wayafikishe kwenye vyombo vya sheria.

Walisema kuwa iwapo hatua za kisheria zitachukuliwa kikamilifu dhidi ya wahusika wa vitendo  vya ukatili kijinsia kwa watoto,  itasadia kutoa funzo na kuogofya watu wengine wenye nia ovu katika jamii yote.

Daktari Bingwa Mshauri wa magonjwa ya Wanawake na Watoto katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Singida, Dk. Suleiman Muttani anasema kuwa ukatili wa kijinsia kwa watoto umekuwa  na madhara makubwa kwa kundi  hilo na kuleta athari za kiafya na kisaikosojia kwa muda mrefu na mfupi.

Dk. Muttani ameshauri kuwepo mikakati madhubuti kwa ajili ya kudhibiti vitendo hivyo katika jamii kwa kuwa baadhi yake vina athari kubwa kwa afya ya mtoto hata baada ya mtoto huyo kuwa mtu mzima. 


 

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII DK.PINDI CHANA AZINDUA MPANGO KAZI WA KITAIFA WA USIMAMIZI WA MISITU YA JAMII NCHINI

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Pindi Chana (wa tatu kushoto) akikata utepe kuashiria kuzindua Mpango Kazi wa Kitaifa wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii Tanzania katika hafla iliyofanyika jana Mei 5, 2022 katika Ukumbi wa Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Mpango huu umetayarishwa na Wizara ya Maliasili na Utalii Idara ya Misitu na Nyuki kwa Ufadhili wa Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswiss ( SDC). Kutoka kushoto ni Mratibu wa Sekta Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Mwichaga, Kansela  Heini Vihemaki kutoka Ubalozi wa Finland anayeshughulikia Maliasili,  Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Emmanuel Mwakalukwa, Mkurugenzi Msaidizi TFCG, Emmanuel Lyimo, Afisa kutoka Wizara hiyo,  Emma Nzunda na Mkurugenzi wa Utawala wa Wizara hiyo, Prisca Nzunda. 

Thursday, June 2, 2022

RAIS SAMIA AZITAKA HALMASHAURI ZA WILAYA KUIGA UFANYAJI KAZI WA TASAF

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali wakati akikata utepe kuashiria kukabidhi magari 123 yenye thamani ya  Sh. 10.48 Bilioni kati ya 241 yaliyotolewa na Serikali kwa Mamlaka za maeneo ya utekelezaji kwa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa Tanzania Bara na Zanzibar katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama Jijini Dar es Salaam jana 

Mnufaika wa TASAF Khadija kutoka Kikundi cha Kwa Raha Zetu akimuonesha Rais Samia Suluhu Hassan bidhaa anazozitengeneza alipotembelea mabanda ya wanufaika.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)