Saturday, December 3, 2022

PROFESA NDUNGURU AANZA ZIARA YA KIKAZI KAGERA KWA KUZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA KITUO CHA UTAFITI WA KILIMO TARI MARUKU

Wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI)  wa Kituo cha Maruku mkoani Kagera wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Utafiti na Ubunifu wa TARI Dkt Joseph Ndunguru (wa nne kutoka kushoto) baada ya kikao kilichofanyika leo katika ziara yake ya kikazi ya vituo vya ukanda wa ziwa. 

Na Junior Mwemezi, TARI

TAASISI ya Utafiti wa Kilimo   Tanzania -TARI imesema itaendelea na utaratibu wa kuwajengea uwezo watumishi wake wa idara tofauti juu uandikaji wa maandiko ya miradi  itakayoweza kuongeza ufanisi katika maswala ya kiutafiti.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Utafiti na Ubunifu wa TARI Dkt Joseph Ndunguru katika kikao chake na watumishi wa kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera  ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi katika vituo vya ukanda wa ziwa.

Dkt Ndunguru amesema wafadhili wengi wamekuwa wakishindwa kutoa pesa katika miradi mbali mbali kutokana na waandaaji wa maandiko ya miradi hiyo kutoainisha mambo muhimu ,ambayo yanaweza kuwashawishi wafadili .

Aidha Dkt Ndunguru amewaeleza wafanyakazi wa TARI Maruku  kuwa njia pekee ya kufikia mafanikio ni kuepukabhana makundi,ubinafsi na kujenga umoja na kutambua wote wanajenga nyumba moja ambayo ni Tanzania.

Mkurugenzi wa Utafiti na Ubunifu wa TARI Dkt Joseph Ndunguru akizungumza na watumishi wa TARI wa kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera.

Watumishi wa TARI Kituo cha Maruku Kagera wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Watumishi wa TARI  Kiruo cha Maruku wakiwa kwenye kikao hicho.

Kikao kikiendelea.


Kikao kikiendelea.
 

Friday, December 2, 2022

TARI UKIRIGURU KUFANYIA MABORESHO ZANA YAKE RAHISI YA KUPANDIA PAMBA

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Masoud Othman akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo (TARI) Ukiriguru Dauson Malela ya namna bunifu bora na ya kipekee ya zana rahisi ya kupandia pamba maarufu 'Rafiki Planter' inavyofanya kazi. Tukio hilo lilitokea kwenye Maonesho ya Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo (TARI) Ukiriguru na Mratibu wa zao la pamba Tanzania Dk. Paul Saidia akielezea sababu zilizopelekea watafiti wa kituo hicho kubuni teknolojia hiyo rahisi na rafiki ya kupandia pamba maarufu 'rafiki planter.' 

Mtaalamu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo (TARI) Ukiriguru Dauson Malela akionyesha zana hiyo waandishi wa habari waliofika kituoni hapo (hawapo pichani) 

Mwonekano wa zana hiyo.

Mwonekano wa zana hiyo na namna inavyotumika ikiwa shambani.

Mwonekano wa zana hiyo na namna inavyotumika ikiwa shambani.

Mwonekano wa zana hiyo na namna inavyotumika ikiwa shambani.

Mwonekano wa zana hiyo na namna inavyotumika ikiwa shambani.

Mwonekano wa zana hiyo na namna inavyotumika ikiwa shambani.

Mwonekano wa zana hiyo na namna inavyotumika ikiwa shambani

Kabla ya ugunduzi wa zana hiyo hali halisi ni kama inavyoonekana pichani kwa wakulima wa pamba kutumia muda mrefu kutengeneza kamba, kunyoosha mstari, kuweka alama na vipimo, kuchimba mashimo, kudondosha mbegu na kuzifukia kwa kutumia jembe la mkono jambo lililopelekea vijana wengi, wanawake na wazee kukata tamaa na kutafuta shughuli nyingine. Hivyo bunifu hiyo sasa ni mwarobaini wa changamoto hizo.

Na Godwin Myovela 

WATAFITI kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo (TARI) Ukiriguru wapo kwenye mchakato wa maboresho ya bunifu yao ya zana rahisi na ya kipekee ya kupandia pamba maarufu 'Rafiki Planter' kutoka hatua ya kukokotwa na wanyama na kuvutwa na binadamu na sasa kuwekewa viongeza mwendo (motorised machines) ili kuongeza ufanisi.

Zana hiyo ambayo imegeuka mkombozi kwa wakulima wa pamba kwa kurahisisha shughuli zote za upandaji, ina uwezo wa kutumia kati ya saa moja mpaka masaa 3 kupanda eneo la ekari moja, ikilinganishwa na wastani wa masaa kati ya 10 na 11 ambayo hutumika kama zao hilo litapandwa kwa mkono.

Aidha, zana hiyo inapokuwa inakokotwa au kuvutwa na binadamu kupitia sehemu maalum ya kufunga mnyororo  au mkono wake wa kuvuta, ina uwezo wa kudondosha mbegu kutoka shimo hadi shimo kwa cm 30, na kutoka mstari hadi mstari cm 60, sanjari na uwezo wa kubeba mbegu kati ya kilo 3 mpaka  6 kupitia vibeba mbegu maalum kwa wakati mmoja.

Pia ugunduzi huo, umeiwezesha zana hiyo kuwa na uwezo mahsusi ya kutengeneza yenyewe mashimo ya mbegu na vifukia udongo ambavyo hufanya kazi yake punde tu mbegu inapodondoshwa.

Kwa mujibu wa Tari, teknolojia ya zana hiyo imewekewa mfumo wa vifungua ardhi ambavyo kadiri zana hiyo itakavyokuwa inasogea vifungua ardhi hivyo vinachimba mashimo  kwa maana ya kutengeneza mifereji kwa umbali wa cm 60 kutoka kimoja hadi kingine.

Mkurugenzi wa kituo hicho, ambaye pia ni mratibu wa zao la pamba nchini, Dk. Paul Saidia alisema ugunduzi huo na maboresho yake vitahusisha, kushawishi na kuvutia idadi kubwa ya makundi mbalimbali wakiwemo vijana, wanawake na wazee kuingia katika kilimo tofauti na ilivyokuwa awali, na hivyo kuongeza tija zaidi ya mara mbili kwenye uzalishaji wa pamba.

Akizungumza jijini hapa, wakati akishiriki utekelezaji wa mradi wa kuinua thamani kwenye mnyororo wa zao la pamba unaojulikana kama 'Beyond Cotton,' Saidia alisema kabla ya uwepo wa zana hiyo, na baada ya kufanya majaribio walibaini nguvu kazi ya wakulima kati ya 12 na 14 ilitumika kupanda ekari moja kwa siku 1 kwa wastani wa masaa 10 hadi 11.

Aidha, alisema hali hiyo hata hivyo ilipelekea usumbufu kwa wakulima walio wengi kutumia muda mrefu kutengeneza kamba, kunyoosha mstari na kuweka vipimo kwa kutumia zana duni za jembe la mkono sambamba na kuinama kwa muda mrefu, hususan wakati wa kudondosha mbegu na kufukia, hali iliyosababisha ugumu kwenye kufikia azma ya uzalishaji wa pamba kwa tija.

"Sasa naamini bunifu hii ni mkombozi  sababu inafanya kazi zote tatu; kwa maana ya kuchimba mashimo yenyewe, kuweka mbegu na kufukia. Pia kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Tume ya Sayansi Teknolojia Bodi ya Pamba nchini  tupo kwenye mchakato wa kuifanyia maboresho kwa kuifungia 'motorised machine' itakayotumia mafuta ya petrol ili kuipa ufanisi zaidi," alisema Dk. Saidia.

Zaidi alisisitiza; "Kilichopelekea wazo la uvumbuzi huu ilikuwa ni baada ya tafiti nyingi za kubadilisha namna ya upandaji pamba kutoka kwenye cm 90 kwa 40 wa hapo awali kuja kwenye huu mpya wa sasa wa  cm 60 kwa 30 kufanywa kupitia mradi wa 'Cotton Victoria' katika azimio lililofanyika kwenye mkutano wa wadau mkoani Simiyu mwaka 2020."

Ikimbukwe, katika mkutano huo ilionekana upandaji mpya wa cm 60/30 pamoja na uzuri wake lakini bado ulikuwa na changamoto ya matumizi makubwa ya muda, ongezeko la nguvukazi na idadi ya mimea. Mathalani upandaji wa cm 90/40 ililazimika kuwa na mashimo yapatayo 11,111 kwa ekari, wakati 60/30 idadi ya mashimo ya kupandia mbegu ni 22,222.

Kwa mantiki hiyo, kwenye kila shimo au mashimo zinapopandwa zaidi ya mbegu 2 kitaalamu inashauriwa mkulima ang'olee ili ibakie mimea 2; na kwa kufanya hivyo, idadi ya upandaji wa awali wa cm 90/40 kwa mashimo 11,111 mimea itakuwa 22,222, na upandaji wa sasa ulioidhinishwa nao mimea itaongezeka mara mbili zaidi kutoka 22,222 hadi idadi mpya ya 44, 444 kama itang'olewa na kubakizwa miwili kwa kila shimo.

Kwa upande wake mmoja wa wataalamu kutoka Idara ya Uhaulishaji Teknolojia ambaye pia ni miongoni watafiti wavumbuzi wa zana hiyo kutokaTari Ukiriguru, Dauson Malela alipongeza Taasisi za Bodi ya Pamba nchini (TCB), Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) , Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) pamoja na  kiwanda cha kuchambulia pamba cha Biosustain mkoani Singida kwa ushirikiano mkubwa walioutoa katika kufanikisha uvumbuzi wa zana hiyo.

Kwasasa Costech kwa kushirikiana na Tari wapo kwenye mchakato wa majaribio kadhaa ya kuboresha zana hiyo kutoka kwenye mfumo wa sasa kwenda kwenye hatua kubwa zaidi ya kufungia mashine itakayowezesha kujikokota yenyewe, ili hatimaye iwe  rahisi zaidi na rafiki kwa wakulima wasio na mifugo na wazee wasioweza kuivuta.

Uvumbuzi wa zana hiyo unakwenda sambamba na falsafa ya sasa ya Wizara ya Kilimo na Taasisi ya Utafiti nchini chini ya Waziri mwenye dhamana Hussein Bashe ambaye mara kadhaa amekuwa akitoa maelekezo mahususi kwa wataalam wa kilimo kuhakikisha wanaongeza kasi ya kiutendaji na tafiti ili kuleta mageuzi chanya ndani ya sekta hiyo katika kufanikisha ajenda ya 10/30.

"Mchakato wa maboresho kwenye zana hii mali ya TARI ambayo imegunduliwa na watafiti watatu Dk. Paul Saidia, Dauson Malela na Robert Chaleo unaendelea, pia tunakaribisha wadau wengine kujitokeza ili kwa pamoja tuweze kuinua tija ya kilimo cha pamba," alisema Malela.

Thursday, December 1, 2022

ORYX YAKABIDHI MITUNGI YA GESI 600 KWA WAKE WA VIONGOZI SONGEA

Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menemjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma(wa pili kushoto) akipokea jiko la gesi kati ya majiko 600 ambayo yametolewa Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Limited Araman Benoite(wa pili kulia) kwa ajili ya wake wa viongozi wa Halmashauri ya Songea Vijijini ikiwa ni mkakati wa kuhamasisha nishati safi ya kupikia kama hatua ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menemjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama(kushoto) na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Limited Araman Benoite(katikati) wakimkabidhi mtungi wa gesi wa Oryx Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini Juma Nambaila.

 Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Limited Araman Benoite(kushoto)akimkabidhi mtungi wa gesi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini Menasi Komba (kulia).Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menemjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama.

Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Limited Araman Benoite(kushoto) akimkabidhi mtungi wa gesi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Vijijini Neema Maghembe(kulia).Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menemjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama.Mtungi huo ni kati ya mitungi 600 iliyotolewa na Oryx Gas Tanzania kwa ajili ya kuwapatia wake wa viongozi kwenye halmashauri hiyo kama mkakati wa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kutunza na kulinda mazingira.

Matukio mbalimbali katika picha baada ya mitungi ya Oryx kukabidhiwa kwa wake wa viongozi wa ngazi mbalimbali katika Halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma .Mitungi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Ltd Araman Benoite leo.

Mitungi ya gesiikikabidhiwa.
Mitungi ya gesi ikiendelea kukabidhiwa.

Matukio mbalimbali katika picha baada ya mitungi ya Oryx kukabidhiwa kwa wake wa viongozi wa ngazi mbalimbali katika Halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma .Mitungi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Ltd Araman Benoite leo.

Wanawake wakiondoka na mitungi ya gesi baada ya kukabidhiwa.

Matukio mbalimbali katika picha baada ya mitungi ya Oryx kukabidhiwa kwa wake wa viongozi wa ngazi mbalimbali katika Halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma .Mitungi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Ltd Araman Benoite leo.

Kijana akifunga mtungi wa gesi kwenye pikipiki baada ya kukabidhiwa.
Wanawake wakiondoka na mitungi yao baada ya kukabidhiwa.
Viongozi wakiwa katikapicha ya pamoja baada ya hafla hiyo ya kugawa mitungi ya gesi.

Na Mwandishi Wetu,Ruvuma

WAKE wa viongozi wa ngazi mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma wamepatiwa mitungi ya gesi 600 pamoja na majiko yake kutoka Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Ltd  ikiwa ni mkakati wa kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini huku pia mwanamke wa Tanzania akiendelea kuondolewa changamoto ya kutafuta kuni na mkaa kwa ajli ya kupikia.

Majiko hayo yamekabidhiwa leo Novemba 30 mwaka 2022 na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Limited Araman Benoite mbele ya viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvua wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menemjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama.

Akizungumza baada ya kupokea majiko hayo kwa niaba ya wake wa viongozi ,Waziri Mhagama amesema katika  kampuni ambazo zinatoa huduma ya gesi ya kupikia majumbani Oryx inaongoza kwa kubadilisha maisha ya wanawake wa maeneo mbalimbali nchini kwa kuwapatia majiko ya gesi na lengo kubwa ni kuhifadhi mazingira na kuongeza Mkurugenzi wa Oryx sio mtanzania lakini amemsikiliza Rais Samia na ameona haja ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kulinda na kuhifadhi mazingira.

Amesema uharibifu wa mazingira umekuwa chanzo cha madiliko ya tabianchi ambayo yanasababisha mvua kuwa chache kutokana na miti kuendelea kukatwa, hivyo kupitia majiko ya gesi yaliyotolewa na Oryx yanakwenda  kusaidia kuihifadhi mazingira na hivyo mvua kuendelea kunyesha na wananchi kupata mazao.

“Dawa ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira ni kutunza misitu na dawa ya kutunza mazingira ni moja tu ambayo ni kutumia nishati ya gesi , mtungi ambao thamani yake ni zaidi ya Sh.70,000 lakini kwa wanawake wa Peramiho imetolewa bure tena mtungi ukiwa na gesi iliyojaa.Mitungi na majiko ya gesi ambayo imetolewa leo ndio zawadi ya Kristmass kwa wanawake wa viongozi,amesema Waziri Mhagama.

Ameongeza siri mojawapo ya kuonekana maisha yako mazuri ni pamoja na kutumia gesi, jambo la msingi tu ni kuweka fedha kidogo kidogo ili gesi inapoisha inanunuliwa nyingine huku akisisitiza kanawapenda sana wanawake wa viongozi wa Jimbo la Peramiho na ndio maana ameamua kuwatafutia majiko hayo ili nao wawe wanapika kwa raha.

“Tunawashukuru sana Oryx kwa zawadi hii ya kwa wanawake wa viongozi.Zawadi hii ambayo tumepewa inakwenda kubadilisha maisha yako,”amesema Waziri Mhagama huku akitumia nafasi hiyo kueleza baada ya Rais Samia kuupiga mwingi kwenye maeneo mbalimbali kwa kuimarisha uchumi yeye kama mbunge wa jimbo la Peramiho lengo lake sasa ni kuona wanaimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na hivyo ametoa rai kwa wadau  kuendelea kushirikiana na wananchi wa Peramiho kujenga uchumi kwani huo ndio mpango wake kwa sasa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Limited Araman Benoite alisema wataendelea kufanya uwekezaji mkubwa nchini Tanzania kwa makundi mbalimbali ya wananchi ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhamasisha matumizi ya gesi safi ya LPG ambayo ni suluhisho la kuondoa matumizi ya kunina mkaa, hivyo basi kuboresha afya ya jamii na kulinda mazingira.

“Wakati wa kongamano la nishati safi kwa wote lililoandaliwa na Wizara ya Nishati na kufanyika jijini Dar es Salaam Mwezi wa Novemba 1 na 2, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alieleza wazi lengo lake la kuona asilimia 80 hadi 90 ya idadi ya watu wa Tanzania kupatiwa ufumbuzi wa kupika kwa nishati safi ndani ya miaka 10 ijayo.

“Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Ltd, katika kuunga mkono lengo hilo adhimu, imeongeza juhudizake kwa kusaidia jamii mbalimbali kubadilisha matumizi yasiyo ya kiafya ya kuni na mkaa kwakutumia LPG ambayo ni rafiki kwa mazingira na afya. OGTL inaendelea kuwekeza katika uagizaji, uhifadhi, ujazaji wa gesi kwenye mitungi na usambazaji wa LPG Tanzania nzima, pamoja na Visiwa vyake,”amesema Benoite.

Aidha amesema OGTL huwekeza kila mwaka mamilioni kadhaa ya dola kwenye mitungi mipya inayoingizwa sokoni kila siku na kwamba inatoa . mitungi hii kwa punguzo kubwa, ikigharimia kwa kiasi kikubwa vifaa vya kuanzia vya LPG (Silinda, Gesi, Burner, Trivet) ili kuwezesha wananchi kubadili kutoka kwa nishati za kuni na mkaa hadi kwagesi safi na kufanya gesi ipatikane kote nchini.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma Mwalimu Neema Maghembe alisema wanamshukuru Mkurugenzi wa Oryx Gas kwa kuwaona akina mama na kusikia kilio chao kwa kuwapatia mitungi na majiko ya gesi kwa ajili ya kupikia.

“Yaani kupika kwa kutumia kuni na mkaa sasa basi tena, Mbunge wetu na Waziri wetu hili ni jambo kubwa na la kihistoria , kwa wanawake wa songea Vijiji kwenye Jimbo la Peramiho akina mama watatuma majiko ya gesi, yale mambo ya umetoka shamba umechoka halafu unahangaika na kuni sasa basi, ni mwendo wa gesi,”alisema Maghembe.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Songea Vijijini Thomas Masolwa amesema kitendo cha Waziri Mhagama kuhakikisha Oryx Gas wanatoa majiko hayo kwa wake wa viongozi ndani ya wilaya hiyo kunakwenda kufanya wake hao sasa wawe wanapika chakula kisasa zaidi na hawatakula tena chakula chenye harufu ya moshi wa kuni na mkaa.

“Mbunge wa jimbo letu la Peramiho na Waziri wetu Jenista Mhagama CCM tunasema wewe chapa kazi, hakuna mbadala wako kwa sasa, tunakuomba endelea kupeleka salamu zetu kwa Mkurugenzi wa Oryx umwabie tunamshukuru sana na jambo hili kubwa ambalo umelifanya linaonesha uhusiano mzuri ulionao kati yako na Oryx pamoja na wadau wengine wa maendeleo.” 

MSD YAPOKEA VIPIMO VYA KUCHUNGUZA UKIMWI NA KASWENDE

Muonekano wa vifaa vilivyopokelewa na Bohari ya Dawa (MSD) 
Moja ya kifaa kilichopokelewa.
Vifaa hivyo vikiwa kwenye maboksi

Na Mwandishi Wetu 

Katika kuadhimisha Siku ya UKIMWI Duniani MSD imeendelea kupokea na  kusambaza bidhaa mbalimbali za afya za kupambana na kudhibiti maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai ameeleza kuwa miongoni mwa bidhaa za afya ambazo kwa sasa inauhitaji mkubwa na inaendelea kusambazwa na MSD kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ni vipimo vya kupima maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na gonjwa la zinaa la Kaswende ( HIV/ Syphilis Duo).

Vipimo hivyo vinafadhiliwa na Mfuko wa Dunia wa  kupambana UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria  (The Global Fund) na pia hutumika kupima akina mama wajawazito kutambua maambukizi ya magonjwa yote mawili kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa Dr. Ibadi Kaondo wa MSD, vipimo hivyo vinamsaidia mama mjamzito kutambua hali ya afya mapema, na endapo maambukizi yamegundulika inarahisisha  kuanza matibabu  mapema ili kufubaza makali ya virusi vya ukimwi na kutibu kaswende kwa ajili kuimarisha afya ya mzazi na kumkinga mtoto dhidi ya Maambukizi ya VVU, Kaswende ama kujifungua mtoto mfu.

Hapo awali vipimo hivi kila kimoja kilikuwa kinajitegemea, ambapo vilitumia muda mrefu kutoa  majibu.  MSD kwa sasa ina shehena ya kutosha ya vipimo hivyo ambavyo tayari  baadhi vilishaanza kusambazwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

MRADI BEYOND COTTON WASHIKA KASI MISUNGWI MWANZA

Mtaalamu wa zao la pamba kutoka Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP,) Joelcio Carvalho akiwaelekeza wakulima wa Kijiji cha Nguge kilichopo Kata ya Mwaniko wilayani Misungwi mkoani Mwanza namna ya kutumia teknolojia ya kuchanganya udongo kwa kutumia mashine maalumu wakati wa mafunzo kwa vitendo kupitia mradi wa Beyond Cotton unaofadhiliwa na Serikali ya nchi ya Brazili kwa kushirikiana na Tanzania chini ya WFP, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) na Bodi ya Pamba (TCB) unaolenga kuinua tija ya zao la pamba kwa wilaya za Magu, Kwimba na Misungwi mkoani hapa. Katikati mwenye kofia ya blue anaye shuhudia mafunzo hayo ni Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango Wizara ya Kilimo, Gungu Mibavu.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Benson Mihayo akijifunza kutumia mashine maalumu ya kuchanganya udongo wakati wa mafunzo hayo.
Mkulima wa Kijiji cha Nyashani Kata ya Mwaniko, Hellena Mane (70) akijifunza kutumia mashine maalum ya kuchanganya udongo wakati wa mafunzo hayo.
Afisa Kilimo wa Kata ya Nguge, Sostenis Rwalukaba akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

Mratibu wa zao la pamba nchini Dk. Paul Saidia alitoa hamasa kwa wananchi wakati akishiriki utekelezaji wa mradi huo. Kata ya Nguge wilayani Misungwi mkoani hapa.

Afisa Kilimo na Umwagiliaji wa Wilaya ya Misungwi, Dk. Chrispine Shami akizungumza na wakulima wakati wa mafunzo hayo. Kushoto ni  Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango Wizara ya Kilimo, Gungu Mibavu.
Ujenzi wa tenki la kuvunia maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji linalojengwa Shule ya Msingi Nguge ukiendelea.
Mtaalamu wa zao la Pamba kutoka WFP, Joelcio Carvalho akiwaelekeza wakulima wa Kijiji cha Nguge kilichopo Kata ya Mwaniko wilayani Misungwi mkoani Mwanza namna ya upandaji mbegu za pamba kwa kuzingatia vipimo.

 Mtaalamu wa zao la pamba kutoka WFP, Joelcio Carvalho akiwaelekeza wakulima wa Kijiji cha Nguge kilichopo Kata yaMwaniko wilayani Misungwi mkoani Mwanza namna bora ya kupima hali ya hewa kwa kutumia kifaa maalumu cha kupima kiasi cha mvua kabla ya kupanda pamba maarufu 'rain gauge'

Mratibu wa Lishe kutoka Wizara ya Kilimo Magreth Matai akitoa mafunzo kwa akinama wa Kata ya Nguge kupitia mradi huo.

Mtaalamu Mwandamizi wa masuala ya lishe na virutubishi kutoka TARI Ukirigulu Dk. Calesma Chuwa akisimamia utekelezaji wa mafunzo kupitia mradi wa 'Beyond Cotton' kwenye eneo la kuboresha lishe kwa wakulima wa kata hiyo..

Ukaguzi wa ujenzi wa tenki la kuvunia maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji linalojengwa Shule ya Msingi Nguge wilayani Misungwi mkoani Mwanza ukifanyika. (Picha zote na Dotto Mwaibale