Wednesday, March 15, 2023

MAFUNDI 1800 KUKUTANA KWENYE KONGAMANO MJINI IRINGA MACHI 17, 2023

Mafundi umeme wakiwajibika sehemu ya mafunzo.


Na Mwandishi Wetu, Iringa

ZAIDI ya mafundi 1800 wa aina mbalimbali wanatarajia kukutana pamoja katika kongamano kubwa litakalo fanyika Mjini Iringa lengo kubwa likiwa kupanua wigo wa ajira na kuongeza fursa kwenye kundi hilo muhimu kwenye jamii.

Meneja wa FundiSmart, Fabian Mwiga amesema kongamano hilo litafanyika Machi 17, 2023 katika ukumbi wa Masiti, Manispaa ya Iringa.

Kiuhalisia, mafundi ni kati ya kundi lililoachwa pembeni licha ya kuwa vitu vingi zinavyoizunguka dunia vinatokana na uwepo wa fundi.

 “Tunawakutanisha mafundi mbalimbali bila kujali aina ya ufundi wao, mpaka sasa tunao mafundi 1800 waliojiandikisha,” amesema Mwiga.

Amesema kwenye kongamano hilo mafundi watapata fursa ya kujua umuhimu na thamani ya kazi yao, elimu ya afya na bima, fedha, sheria, akiba na huduma bora kwa wateja.

“Sekta ya ufundi ni nyeti na mafundi wanazo ndoto zao, sasa wanaweza kufikia ndoto zao ikiwa tutawaonyesha mlango wa kupita, FundiSmart imekuja kwa ajili hiyo,” amesema Mwiga.

Amesema kwa sababu kundi hilo limekuwa likilalamikiwa zaidi na wateja hasa kwenye suala la uaminifu, elimu kuhusu sheria na huduma kwa wateja itawasaidia zaidi.

Kwa upande wao baadhi ya mafunzi wamesema hakuna siku waliketi pamoja na kutambuliwa kama sekta nyeti.

‘Hata tukifanya kazi mtu anakulipa atakavyo bila kujali kazi kubwa unayofanya, naamini hii ni fursa kwetu kutambua kazi yetu na kuipatia kipaumbele,” amesema.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo.

Fundi Washi akiwajibika.
Mafundi Washi wakiendelea na kazi.
Fundi magari akiwa kazini
Fundi Seremala, Joseph Msoffe wa mkoani Morogoro akitengeneza milango katika Workshop yake.
 

Sunday, March 12, 2023

TACAIDS YAWASILISHA TAARIFA KUHUSU MUUNDO NA MAJUKUMU YAKE KWA KAMATI YA BUNGE AFYA NA UKIMWI

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu, Mhe George Simbachawene  akizungumza na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI walipokutana na TACAIDS wakati wa wasilisho la muundo na majukumu ya TACAIDS kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI katika Ukumbi wa Ofisi za Bunge jijini Dodoma, Leo Machi,12, 2023.

Na Nadhifa Omar, Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe.George Simbachawene amesema Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kutoa ushirikiano unaostahiki kwa kamati ya Afya na masuala ya UKIMWI kutekeleza majukumu kwa kufuata miongozo,maoni na ushauri unaotolewa na kamati hiyo.

Kauli hiyo amaitoa leo Machi12 ,2023 baada ya Tume ya kudhibiti UKMWI Tanzania (TACAIDS) kuwasilisha Taarifa kuhusu muundo na majukumu yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI katika Ukumbi wa Ofisi za Bunge jijini Dodoma.

Awali akiwasilisha taarifa hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko amesema TACAIDS ni Idara inayojitegemea chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na imeanzishwa kwa mujibu wa sheria Na.22 ya mwaka 2001 na Marekebisho yake Na.6 ya mwaka 2015, sheria hiyo ni kwa ajili ya Tanzania Bara pekee. Zanzibar ipo Tume ya UKIMWI Zanzibar (ZAC).

Dkt. Maboko ameyataja majukumu ya TACAIDS kuwa ni kuandaa sera na miongozo kwa ajili ya mwitikio wa UKIMWI nchini pamoja na kusimamia athari zake, kusimamia mpango mkakati kwa ajili ya mipango ya programu za UKIMWI pamoja na masuala mtambuka yahusuyo virusi vya UKIMWI na UKIMWI.

Kujenga mahusiano ya kitaifa na kimataifa kwa watu wote wenye UKIMWI kwa kufanya uratibu wa masuala ya UKIMWI,kutafuta raslimali fedha ,kuzigawa na kuzifuatilia katika programu za Mwitikio wa UKIMWI,kusambaza taarifa kuhusu UKIMWI na madhara yake na programu za kuzuia na kudhibiti.

Kukuza tafiti ,upashanaji taarifa na kutunza kumbukumbu zinazohusiana na udhibiti wa UKIMWI nchini,kukuza uraghibishi na utoaji wa elimu kwa ngazi ya juu kuhusu kuzuia na kudhibiti UKIMWI, kufuatilia na kutathimini shughuli zote za UKIMWI zinazotekelezwa nchini.

Aidha ameongeza kuwa shughuli nyingine ni Kuratibu shughuli zote za UKIMWI na kuzisimamia kwa mujibu wa mkakati wa Taifa wa UKIMWI, kwa kushirikiana na sekta binafsi husika kuwezesha juhudi za upatikanaji wa tiba na kuhamasisha upatikanaji wa tiba na matunzo na chanjo.

Jukumu lingine ni kuhamasisha haki na wajibu kwa watu wanaoishi na VVU ,kuhamasisha WAVIU kuishi kwa matumaini na kushauri serikali kuhusu masuala yote yanayohusu kuzuia na kudhibiti UKIMWI ,kutambua vikwazo katika utekelezaji wa kuzuia na kudhibiti katika sera na programu ,kusimamia shughuli zote zinazohusiana na kuzuia na kudhibiti maambukizi ya VVU na UKIMWI,pamoja na kushirikiana na sekta nyingine husika,kufanya shughuli nyingine za kuzuia na kudhibiti VVU na UKIMWI.

Dkt. Maboko amesema utekelezaji wa majukumu ya TACAIDS unaongozwa na sera ,sheria ,kanuni ,mikakati na miongozo ikiwa ni pamoja na sheria ya tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania Na,22 ya mwaka 2001na marekebisho yake Na6 ya mwaka 2015,Sera ya Taifa ya UKIMWI ya mwaka 2001.

Mwongozo wa uraghibishi na mabadiliko ya tabia,Mwongozo wa VVu na UKIMWI  na magonjwa sugu yasiyoambukiza, mwongozo wa kusshughulikia makundi maalum kuhusu UKIMWI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ,mwongozo wa jinsia na UKIMWI

,Mwongozo wa UKIMWI na haki za binadamu ,Mwongozo wa kufundishia kamati za kudhibiti UKIMWI ngazi za Halmashauri,kata na vijiji, pamoja na mwongozo wa kuunda kamati za kudhibiti UKIMWI kwenye mikoa,mwongozo wa kuunda kamati za kudhibti UKIMWI kwenye Halmashauri.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe Stanslaus Nyongo iliipongeza TACAIDS kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kudhibiti na kupunguza maambukizi ya VVU nchini na kuagiza kuendelea kufanyia kazi ushauri na maekezo yaliyotolewa na kamati hiyo,ikiwa ni pamoja na kufanya ufatiliaji wa utekelezaji wa majukumu ya kamati za kudhibiti UKIMWI ngazi za chini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Stanslaus Nyongo akizungumza na wajumbe pamoja na watendaji wa TACAIDS na Ofisi ya Waziri Mkuu waliohdhuria kikao cha kamati hiyo walipokutana leo jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt Leonard Maboko akiwasilisha Muundo, na Majukumu ya TACAIDS kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI wakati wakikaokilichfanyika leo jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene na Katibu Mkuu Dkt. Jimmy Yonaz (kulia) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt Leonard Maboko alipokuwa anawasilisha Muundo na Majukumu kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Mhe. Seif Salum Seif akichangia wakati wa kikao cha kamati hiyo na TACAIDS kuhusu kubadilisha jumbe zinazotumika kwenye vibao vya ujenzi vinavyo tumia maneno ya Unyanyapaa.

Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya  na masuala ya UKIMWI Mhe Hassan Mtega akichangia wakati wa kikao cha kamati hiyo umuhimu wa TACAIDS kufatilia utekelezaji wa majukumu ya kamati za UKIMWI za ngazi za chini. 

Friday, March 10, 2023

KATAMBI: HALMASHAURI ACHENI URASIMU MIKOPO MNAYOTOA KWA VIJANA, WANAWAKE NA WALEMAVU

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi, akiwa ameshika keki maalumu aliyoandaliwa na Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa watu wenye Ulemavu Sabasaba-Singida  wakati wa ziara yake mkoani hapa ya kukagua shughuli mbalimbali zilizo chini ya wizara yake.

Na Dotto Mwaibale, Singida

NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi, amezitaka Halmashauri za Wilaya na Manispaa nchini kuacha urasimu wa kutoa fedha zilizotolewa kwa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu zinazotokana na asilimia 10 ya mapato ya halmashauri hizo.
Katambi alitoa maagizo hayo juzi katika ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa inayotokana na asilimia 10 za mapato ya halmashauri wakati akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani hapa.
Hatua ya Katambi kutoa maagizo hayo ilifuatia baada ya Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana Chapa Kazi, Mwanahamisi Omari, kulalanikia kucheleweshewa kupatiwa fedha za kulipia tripu 50 za mchanga wanaotumia kufyatua matofali baada ya halmashauri hiyo kuwapa mkopo wa Sh. Milioni 25.
“ Mheshimiwa Naibu Waziri tunachangamoto kubwa ambayo inatukwamisha na kushindwa kuendelea na ufyatuaji wa matofali fedha yetu tuliopewa awali imekwisha sasa ni siku ya tatu kila tukienda pale halmashauri tunapigwa danadana hasa pale ofisi ya Maendeleo ya Jamii mara tunaambiwa hela hizo zitatolewa mpaka mhandisi aje kwenye mradi kuhakikisha kama mchanga huo upo, mara tumsubiri mkurugenzi jambo ambalo linatuchelewesha,” alisema Omari.
Katambi baada ya kupokea malalamiko hayo akazitaka halmashauri zote kuacha kufanya urasimu huo ukizingatia kuwa fedha hizo zinatolewa na halmashauri kwa lengo la kuyasaidia makundi hayo na unapojitokeza urasimu huo unarudisha nyuma maendeleo ya walengwa hao.
Aidha, Katambi aliagiza taasisi zote za Serikali zinapotekeleza miradi ikiwemo ya maji na ujenzi wa madarasa na miundombinu mbalimbali itoe kazi hizo kwa kununua matofali, vifaa vya chuma  na vifaa vingine kutoka katika vikundi hivyo ili vikuze mitaji yao.
Katambi alisema taasisi hizo zinapofanya sherehe zao hasa katika mikoa ambayo ina vyuo vya ufundi ziwe zinakwenda kununua keki, upambaji na sare zinazotengezwa na wanafunzi wa vyuo hivyo zikiwemo za Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na bendera ya Taifa ili kuviinua kiuchumi badala ya kwenda kuagiza nje.
Aliwaomba wataalamu waliopo inapotekelezwa miradi hiyo kujenga tabia ya kuvitembelea vikundi hivyo na kutoa elimu ya namna ya matumizi ya fedha hizo jambo litakalosaidia kupata bidhaa bora zinazozalishwa pamoja na kuondoa matumizi mabaya ya fedha zilizotolewa kwenye vikundi.
Akizungumzia kukua kiuchumi kwa vyuo hivyo, aliwataka walengwa hao kuondoa dhana ya kuwa wajasiriamali badala yake wawe wafanyabiashara wa kati na hata kufikia hatua ya kufungua makampuni yao makubwa kutokana na kazi zao wanazo zifanya na kuziomba halmashauri kutoa maeneo kwa bei nafuu kwa makundi hayo ili wajenge ofisi zao na kufungua viwanda.
Katambi pia aliziagiza halamashauri kuviongezea vikundi vinavyofanya vizuri kurejesha mikopo inayokopeshwa akikitolea mafano kikundi cha vijana cha St.Vidicon Manyoni Computer Workshop ambacho kilianzishwa Julai 2020 chini ya umoja wa mafundi wenye ujuzi wa fani mbalimbali waliokubaliana kufanya kazi kwa kushirikiana.
Aliongeza kuwa wanafunzi wanaopata fursa ya mafunzo ya miezi mitatu yanayowezeshwa bure na Ofisi ya Waziri Mkuu wanapomaliza mafunzo yao halmashauri iwe inawapa mikopo kwa ajili ya kufungua viwanda vidogo vidogo badala ya kukaa mitaani na ujuzi wao.
Katika ziara hiyo Katambi alitembelea miradi ya vijana hao katika wilaya za Manyoni, Ikungi, Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa watu wenye Ulemavu Sabasaba kilichopo Manispaa ya Singida, Shamba Kitalu Nyumba lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Singida Ilongero na kukagua ujenzi wa ukumbi wa CCM unaojengwa wilayani Manyoni.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi, akimlisha keki mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi, akisalimiana na Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani mara alipowasili wilayani Manyoni kuanza ziara yake hiyo juzi mkoani hapa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi,  akikagua ujenzi wa ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni.
Ukaguzi wa ukumbi huo ukiendelea. Kushoto ni Mjumbe wa Halimashauri Kuu CCM Wilaya ya Manyoni, Mjumbe wa Baraza  UVCCM Mkoa wa Singida na Mjumbe wa Kamati ya Ujenzi wa Ukumbi wa CCM Wilaya ya Manyoni,  Ngwigula Shigela.
Afisa Maendeleo ya Jamii, Wilaya ya Manyoni, Flavia Kiwango (kulia) akisoma taarifa ya miradi ya maendeleo ya Vijana wilayani humo mbele ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi (kushoto), Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa wilaya hiyo, Elias Mollel na wa pili kulia ni Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani.
Mwenyekiti wa kikundi cha vijana cha St.Vidicon Manyoni Computer Workshop, Fidel Timoth (kulia) akisoma taarifa ya kikundi hicho kwa Naibu Waziri Katambi.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi, akikagua vifaa vinavyotengenezwa kwa chuma na kikundi cha vijana cha St.Vidicon Manyoni Computer Workshop, 
   Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi, akiwa amekaa na msafara wake na maofisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Singida kwenye sofa zilizotengenezwa na kikundi cha Vijana cha St.Vidicon Manyoni Computer Workshop wakati wa ukaguzi wa shughuli za vijana waliopata mkopo kutoka halmashauri. 

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi, akielekeza jambo baada ya kuangalia majiko yaliyotekenezwa na vijana wa kikundi cha St.Vidicon Manyoni.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi, akisalimiana na mmoja wa WanaKikundi cha Vijana cha Chapakazi cha Wilaya ya Ikungi, Ashura Abubakari baada ya kuwasili wilayani hapo juzi katika ziara yake hiyo ya kikazi.
Vijana wa Kikundi cha Chapa Kazi cha Ikungi, wakinyoosha mikono mbele ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi, kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fedha nyingi kwa ajili ya kuendesha miradiya maendeleo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi, akikagua matofali yanayofyatuliwa na Vijana wa Kikundi cha Chapakazi cha Wilaya ya Ikungi. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa kikundi hicho, Mwanahamisi Omari. Na kushoto ni Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi katika shughuli hiyo, Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Dijovson Ntangeki.


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi (kulia)  akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Ikungi na Vijana wa Kikundi cha Chapakazi wakati akikagua Shamba la Kitalu Nyumba lililopo nje ya Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,  Richard Rwehumbiza
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi, akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu cha Sabasaba, Fatuma Malenga baada ya kufika chuoni hapo wakati wa ziara yake hiyo ya kikazi. Katikati ni Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Singida, Ally Mwendo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi, akizungumza na mwanafunzi wa fani ya ushonaji nguo wa chuo hicho.Janeth Lucas.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi, akiangalia nguo za CCM zilizoshonwa na wanafunzi wa chuo hicho.
Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani, akimlisha keki mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho wakati wa ziara ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi, 
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Patrobas Katambi, akizungumza na Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana na Wanagenzi cha Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Ilongero, Frida Dastan, baada ya kutembelea Shamba Kitatu cha zao la nyanya zinazilimwa na vijana hao baada ya kupatiwa mkopo wa Sh.Milioni 10. 
 

Tuesday, March 7, 2023

WANAWAKE TANESCO, SUWASA SINGIDA WAPANDA MITI KUELEKEA KILELE CHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Wanawake watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Singida wakionesha furaha yao kabla ya kwenda kupanda miti kwenye chanzo cha maji cha Mwankoko kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Singida ikiwa ni shamra shamra kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, kesho Machi 08,2023. 

Na Dotto Mwaibale, Singida

 

WANAWAKE watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na wenzao wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 08, 2023, wamepanda miti katika chanzo za maji cha Mwankoko kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Singida ikiwa ni moja ya kazi ya upandaji miti ili kuimarisha uoto wa asili utakaosaidia upatikanaji wa mvua na hivyo kuimarisha vyanzo vya maji kwa ajili ya kuzalisha umeme mwingi.

Mbali na upandaji miti wanawake hao wa TANESCO wametoa msaada wa unga, mafuta ya kula, sabuni na vitu vingine kwa watoto yatima wa Kituo cha Upendo Home for Street Children, ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku hiyo ambayo duniani kote yatafanyika kesho.

Zoezi hilo la upandaji miti limefanyika leo Machi 7, 2023 kwa kuwashirikisha wakuu wa idara wa taasisi hizo mbili za Serikali mkoani hapa. 

Akizungumza katika zoezi hilo la upandaji miti Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa  Shirika hilo, Lulu Silungwe alisema TANESCO imekuwa ikitegemea mvua inayotokana na miti kwa ajili ya kusambaza huduma ya umeme hivyo zoezi hilo la upandaji wa miti litasaidia kukabiliana na athari za kimazingira na mvua kuwa nyingi. 

“Tumekutana hapa leo na wenzetu kutoka SUWASA kwa ajili ya kupanda miti chanzo cha maji Mwankoko chini ya kauli mbiyu yetu isemayo Panda Miti, Mvua Ndi, Umeme Ndindindi ikiwa ni moja ya kazi yetu kuelekea maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wanawake Duniani ambayo ni kesho” alisema Silungwe. 

Alisema mbali ya kupanda miti pia watawatembelea watoto Yatima wanaolelewa Kituo cha Upendo Home for Street Children, kwa ajili ya kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwa ni kazi yao nyingine kuelekea maadhimisho hayo. 

Neema Ntandu ambaye ni mfanyakazi wa shirika hilo alisema wamepanda miti 150 ya aina mbalimbali na kuwa watahakikisha inakuwa na kuimarisha chanzo hicho cha maji cha Mwankoko. 

Mwenyekiti wa Wanawake wa Shirika hilo Mkoa wa Singida, Asiatu Mnanura akizungumza wakati wa kutoa msaada kwa watoto wa kituo hicho alisema wamefurahi kuwatembelea ukizingatia kuwa wao ni wazazi hivyo waliona vizuri jambo hilo liwe ni sehemu ya moja ya kazi yao kuelekea maadhimisho hayo. 

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa SUWASA, Fatina Mbaga alisema ni wajibu kwa kila mwana Singida kupanda miti kwa wingi ili kuhifadhi mazingira jambo litakalosaidi kuhifadhi mazingira na kuwepo kwa mvua nyingi na hivyo kuwa na maji ya kutosha. 

Mratibu wa kituo hicho Afesso Ogenga alishukuru kwa msaada huo na kueleza kuwa kituo hicho kinawapokea watoto kutoka mitaani na majumbani lakini ni baada ya kufanyika utaratibu wa kuwatambua na kujua historia zao kwa kushirikiana na watu wa ustawi wa jamii.

Furaha ikiendelea kutamalaki kwa wanawake hao watumishi wa Tanesco Mkoa wa Singida.

Wanawake watumishi wa Tanesco Mkoa wa Singida wakifanya maandamano kuelekea katika zoezi hilo la kupanda miti.

 Mratibu wa Kituo cha  Home for Street Children, Afesso Ogenga akizungumza baada ya kukabidhiwa msaada huo.

Wanawake watumishi wa Suwasa Mkoa wa Singida wakipanda ngazi kuingia kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda kupanda miti.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Suwasa, Fatina Mbaga, akizungumzia kuhusu zoezi hilo la upandaji miti.
Wanawake watumishi wa shirika hilo wakiwa wameshika miche ya miti tayari kwa kuipanda.
Kaimu Meneja wa Tanesco Mkoa wa Singida, Mhandisi , Ramadhan Mwanga akipanda mche wa mti eneo la chanzo cha maji Mwankoko.
Miche ya miti ikipandwa kwenye chanzo hicho cha maji.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Suwasa, Fatina Mbaga, akipanda mche wa mti.
Afisa Rasilimali Watu wa Tanesco Mkoa wa Singida, Angelina Kaarata (kulia) na Afisa wa shirika hilo, Neema Ndaskoy wakipanda mche wa mti katika eneo hilo., 
Yusra Nicholaus akipanda mche wa mti.
Salama Juma akipanda mche wa mti kwenye chanzo hicho cha maji.
Neema Ntandu ambaye ni mfanyakazi wa shirika hilo, akizungumzia umuhimu wa kupanda miti katika vyanzo vya maji.
Picha ya pamoja wakati wa kukabidhi msaada kwa watoto Yatima wa Kituo cha 
Zawadi kwa kituo hicho cha Yatima zikitolewa.
 

Monday, March 6, 2023

VYANZO VYA MAJI BONDE LA RUFIJI KULINDWA

Mhaidrolojia wa Bodi ya Maji Bonde la Rufiji (RBWB), Ally Diwani akiwaelezea waandishi wa habari namna wanavyopima kiwango cha maji kwenye bonde hilo.

Na Selemani Msuya, Iringa

BODI   ya   Maji   Bonde   la   Rufiji   (RBWB)   imesema   ilikuhakikisha uwekezaji mkubwa wa miradi mbalimbali yauzalishaji  inakuwa endelevu wanatarajia  kuajiri walinzi50 ambao watalinda vyanzo mbalimbali vinavyotiririshamaji eneo hilo. 

Hayo   yamesemwa   na   Mkurugenzi   Mkuu   wa   RBWB,Florence   Mahay   wakati   akizungumza   na   waandishi   wahabari   kutoka   katika   vyombo   vya   habari   mbalimbaliambao wapo kwenye ziara ya kutembelea bodi hiyo.

Mahay alisema bonde hilo  linapokea  maji   kutoka  mitomikubwa   minne   ambayo   ni   Ruaha   Mkuu,   Kilombero,Luwegu na Rufiji.Mkurugenzi   huyo   amesema   kutokana   na   faida   ambazozimeonekana   na   zinaendelea   kuonekana   wamejipangakuongeza   ulinzi   kwenye   bonde   hilo   ambapo   katikamwaka   wa   bajeti   wa   2023/2024   wanatarajia   kuajiriwalinzi 50 ambao watalinda vyanzo vilivyopo.

Amesema   wamejipanga   kulinda   vyanzo   vya   majivinavyoingiza   maji   katika   bonde   hilo,   ili   kuhakikisha shughuli za kiuchumi zilizopo zinakuwa endelevu, kwakuwa zinachangia ukuaji wa uchumi.

Mahay   amesema   bodi   hiyo   ina   kazi   moja   kuu   yausimamizi   wa   rasilimali   za   maji,   kwa   kuhakikishawanatambua kiasi cha rasalimali maji kwenye bonde hilo,kugawa   maji,   kutunza   vyanzo   vya   maji   na   kuzuiauchafuzi.

Mkurugenzi   huyo   amesema   wamelazimika   kuwapitishawaandishi wa habari katika maeneo ya Bonde la Rufiji, ilikuhakikisha umma unapata taarifa sahihi katika eneo hilo.

“Serikali imewekeza katika Bonde la Rufiji kwa kujuengamiradi   ya   kuzalisha   umeme,   kama   Bwawa   la   Mtera,Kidatu   na   Kihansi   na   kwa   sasa   Mradi   wa   UzalishajiUmeme wa Mwalimu Nyerere (JNHPP). Miradi yote hiyoina   mchango   katika   uchumi   wa   nchi   kama   unavyoonaasilimia 80 ya umeme wa maji unatokea hapo.Lakini pia ukubwa wa bonde hili unachangia asilimia 50 ya miradi kilimo cha umwagiliaji, kama chai na sukari,hivyo tunakuwa na usalama wa chakula na tuna mbuga zawanyama takribani sita,” amesema.

Mahay amesema kwa sasa Bonde la Rufiji lina maji yakutosha ambapo kuna mita za ujazo bilioni 40, mita za ujazo bilioni 31 juu ya ardhi na bilioni 9 ni chini ya ardhi,huku   maji   yanatumika kwa kutolewa vibali ni mita zaujazo bilioni 2.4.

Amesema kwa sasa bodi hiyo imesitisha utoaji wa vibalivya maji ikiwa ni maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan,ili kuhakikisha maji yanajaa kwenye Bwawa la Nyerereambalo linatarajiwa kuzalisha megawati 2,115.

Mahay   amesema   bodi   hiyo   haitasita   kubomoamiundombinu ya wale ambao watabainika kutumia majibila kupewa vibali, hivyo wataka wananchi hasa jumuiyaza watumiaji maji kutoa taarifa pale wanapobaina.“Naomba   nisisitize   kuwa   bodi   hii   haitamvumilia   mtu yoyote   anashiriki   kutumia   maji   bila   kibali,   jumuiya   zawatumia maji tunaziomba ziendelee kutoa ushirikiano, ilikuhakikisha uwekezaji unaofanywa na serikali unakuwaendelevu,” amesema.

Kwa upande wake Mhaidrolojia wa RBWD Ally Diwani,amesema kitengo chao kina vituo 137 ambapo vituo 59vinapima maji juu ya ardhi, 29 chini ya ardhi na 49 vyahali ya hewa.Amesema katika eneo hilo wana changamoto ya uharibifuwa vituo, wizi na uvunjaji wa vifaa vinasaidia kuchukua takwimu kwa ajili ya tathminj ya rasilimali maji kwenyebonde.

Naye   Msimamizi   wa   Kitengo   cha   Ugawaji   RasilimaliMaji wa Bodi, Mhandisi Gallus Ndunguru amesema hadisasa wametoa vibali 2005 kwa watumiaji maji mbalimbaliwalioko katika eneo la bonde.“

Pia   tumetoa   vibali   10   vya   kutiririsha   maji   taka   kwataasisi   mbalimbali   ambao   wanatoa   huduma   zao   kwakutumia maji. Ila kwa sasa tumesitisha kutoa vibali vyawawekezaji   wakubwa   hasa   katika   maeneo   ambayoyameathirika,” amesema.

Ofisa   Maendeleo   ya   Jamii   RBWB,   Upendo   Lugallaamesema   katika   kuhakikisha   bonde   hilo   linakuwaendelevu wanataerajia kupata miti 200,000 rafiki na maji.Amesema   pia   kupitia   idara   yao   wamefanikiwa   kuundajumuiya 42 za watumiaji maji ambao wanashiriki kulindavyanzo vya maji katika bonde hilo. 


Mhandisi wa Maji, Bodi ya Maji Bonde la Rufiji (RBWB), Gallus Ndunguru,  akiwaelezea waandishi wa habari namna wanavyotoa vibali vya maji kwenye bonde hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Maji Bonde la  Rufiji (RBWB), Florence Mahay akifafua jambo mbele ya waandishi wa habari waliotembeleofisi za bonde hilo mkoani Iringa.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Maji Bonde la Rufiji (RBWB), Florence Mahay akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati yao ya kulinda bonde hilo, ili liwe endelevu.
Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Bodi ya Maji Bonde la Rufiji (RBWB), Upendo Lugalla akielezea namna idara yao inavyotoa elimu ya utunzaji rasilimali maji