Monday, January 25, 2021

NGURUWE WENYE THAMANI YA MIL. 370 WAMEKUFA KWA HOMA, SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KUDHIBITI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kudhibiti ugonjwa wa homa ya Nguruwe kwenye Mkutano uliofanyika jijini Dodoma juzi.

 Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Hezron Nonga (kushoto) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu ugonjwa wa homa ya Nguruwe katika Mkutano uliofanyika jijini Dodoma juzi. Kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki.


Na Mbaraka Kambona,

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema Serikali imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha ugonjwa wa homa ya Nguruwe ulioikumba Mikoa ya Kanda ya Ziwa hivi karibuni unadhibitiwa, huku akisema kuwa tangu ugonjwa huo uanze mpaka sasa umeshasababisha vifo vya Nguruwe 1500 wenye thamani ya shilingi milioni 375. 

Ndaki aliyasema hayo juzi jijini Dodoma alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kuudhibiti ugonjwa huo uliokumba Mikoa ya Kanda ya Ziwa. 

Alisema kuwa vifo hivyo vimesababisha hasara ya moja kwa moja kwa wafugaji kwa sababu kipato hicho kilichopotea ilikuwa wakipate wafugaji huku akiwataka wafugaji hao kuwa watulivu na kufuata maelekezo ya serikali ili ugonjwa huo uweze kudhibitiwa kwa haraka. 

Aliongeza kuwa  ugonjwa huo unaosababishwa na virusi unahama kutoka kwa nguruwe pori na  Ngiri na unasambaa kupitia  njia ya Maji, Damu au Kinyesi. 

Ndaki alisema kuwa Halmashauri zilizoathirika mpaka sasa ni Mbogwe, Kyerwa, Geita, Sengerema, Kahama na Misungwi na alibainisha kuwa serikali imeshachukua hatua kadhaa za kudhibiti ugonjwa huo. 

Alisema kuwa mpaka sasa serikali imeshachukua hatua mbalimbali za kuhakikisha ugonjwa huo unadhibitiwa ikiwemo kuweka karantini za mifugo hiyo ili kudhibiti ugonjwa huo usisambae zaidi. 

“Tumeongeza Wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wakala ya Maabara ya Veterinari (TVLA), Wataalamu kutoka Chuo cha Sokoine (SUA) na Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO) kwenda kuungana na wataalamu wa Halmashauri ili kuongeza nguvu ya kudhibiti ugonjwa huo,” alisema Ndaki. 

Ndaki alisisitiza kuwa ugonjwa huo hauna chanjo wala tiba huku akiwahimiza wananchi kuhakikisha wanazingatia maelekezo wanayopewa na wataalamu ikiwemo kupulizia dawa za kuua wadudu Kupe katika mabanda ili kuzuia ugonjwa huo usisambae zaidi. 

“Niwaombe wananchi waache kula nyama ya Nguruwe, hatua hizi tunazochukua lengo lake ni kudhibiti ugonjwa usiendelee kuleta madhara zaidi katika maeneo mengine,”alisema Ndaki. 

Aidha, Ndaki amewataka Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi katika maeneo yaliyoathirika kuhakikikisha wanasimamia kikamilifu karantini zilizowekwa na wataalamu ili ugonjwa huo kuzuiwa kusambaa katika maeneo mengine  huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano ili hatua hizo zinazochukuliwa na serikali ziweze kuzaa matunda. 

Naye, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Hezron Nonga alisema kuwa ili ugonjwa huo usisambae zaidi ni muhimu wafugaji kuhakikisha kuwa mifugo yao inakuwa katika mabanda wakati wote na kuacha kusafirisha mifugo na mazao yake kutoka sehemu moja kwenda nyingine kabla ya kupimwa na Daktari. 


Friday, January 22, 2021

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WATAFITI KUBORESHA TIBA ASILI NCHINI


1.     Mratibu wa Tiba asili Mkoa wa Morogoro Dkt. Ngalula Wille akizungumza katika uzinduzi wa Maonesho ya siku moja ya wadau wa tiba asili na bidhaa zake yaliyofanyika mkoani Morogoro kwa niaba ya  Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Amandus Mhairwa,  akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua maonesho hayo kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda.

1.     Muwakilishi wa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Taaluma,  Prof. Samweli Kabote akitoa shukrani kwa mgeni rasmi mara baada ya hutuba yake ya ufunguzi,

Mkuu wa Mradi wa GRILI, Dkt. Faith Mabiki ambao ndio waandaaji wa maonesho akieleza malengo ya maonesho hayo na uzinduzi wa jukwaa la Ubunifu wa Tiba Asili Tanzania.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na viongozi wa meza kuu mara baada ya kufungua maonesho hayo.

Mgeni rasmi na ujumbe aliofuatana nao wakitembelea mabanda ya maonesho ya waganga wa tiba asili kuona bidhaa mbalimbali waliozokuja kuonesha kwenye maonesho hayo toka mikoa mbalimbali nchini.

Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu Mhe, Fredirick Sumaye akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa waoneshaji kutoka shirika la SAT bwana Allen alipotembelea maonesho hayo kuona bidhaa mbalimbali za wataalamu wa Tiba Asili.

 


Na Calvin Gwabara,  Morogoro


SERIKALI Mkoa wa Morogoro, na hasa vitengo vya Uchumi na Mali Asili vimewahakikishia wadau wa tiba asili kuwa wakotayari kushirikiana nao kikamilifu ili kuona kuwa mimea dawa nchini inatumika kwa uangalifu na kwa mpango endelevu.  

Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo kwa niaba yake na Mratibu wa Tiba asili mkoa wa Morogoro Dkt. Ngalula Wille wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya siku moja ya wadau wa tiba asilina bidhaa zake yaliyofanyika mkoani Morogoro na kuandaliwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kupitia Mradi wa GRILI. 

Mratibu huyo wa tiba asili mkoa wa Morogoro amewataka wazalishaji wa bidhaa hzo za mimea dawa kipindi hiki ambacho kuna ugonjwa wa mlipuko kama COVID-19, waone namna gani watatengeneza dawa ilikusaidia jamii kukabiliana na majanga kama haya yanayiweza kujitokeza. 

"Nimefurahishwa sana na taarifa kwamba maonesho haya yamendaliwa na Chuo chetucha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia Kurugenzi yake ya Uzamili kitengo chake cha Uhaulishaji wa tekinolojia pamoja na mradi wa utafiti wa GRILI Hii inatokana na uzoefu na ueledi walionao kwenye masuala ya utafiti na Biashara za aina hii zikiwemo za bidhaa zinazotokana na mimea dawa hivyo ni matumaini yangu kuwa maonesho haya yataangalia pia namna yakupunguza changamoto za uzalishaji na za kibiashara zilizopo na zinazoweza kujitokeza katika biashara nzima ya bidhaa za mimea dawa" alisema Dkt. Ngalula.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua maonesho hayo Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Amandus Mhairwa kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda alisema kuwa  ingawa kwenye kanuni za biashara ya madawa kuna mitizamo tofauti kuhusu kutangaza dawa za mimea zitokanazona mimea tiba, lakini ukweli ni kwamba bilikujitangaza, wateja hawatatambua biashara za bidhaa na soko. 

“Biashara hii iko pia kwenye biashara ya huduma zinakuzwa sana na watoa huduma wenyewe hivyo hii sio tu yatatangaza biashara zao bali pia yatatangaza watoa huuma wenyewe na kauli zao kwa wateja ni muhimu sana ili waweze kupata masoko ya bidhaa na huduma zao hvyo lengo la maonesho haya nikuwakutanisha wazalishaji, wasambazaji, watengenezaji na wanunuzi wa bidhaa za mimea dawa” alifafanua Prof Mhairwa.

 

Aliongeza "Napenda niwahakikishie wadau hawawanaozalisha dawa zinazotokana na mimeadawa kwamba, Chuo Chetu chaSUA, kupitia kurugenzi ya Uzamili, Utafiti,Uhaulishaji waTekinolojia na Ushauri wa Kitaalaamu, kwakushirikiana na Watafiti tulionao na wamasuala ya kisayansi na tekinolojia, na wale wa masuala ya biashara, tutaendelakushirikiana bega kwa bega na wajasiriamalihawa ili kuboresha bidhaa wanazozalishatukishirikiana na wadau wengine katika sektahii kwa kadri uwezo wetu utakavyoturuhusu". 

Akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Ras wa Ndaki ya Sayansi za Jamii na Insia Prof. Samweli Kabote kwa niaba ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Maulid Mwatawala amesema wamepokea ushauri na maelekezo yote aliyoyatoa mgeni rasmi na kuahidi kutafanyia kazi na kushirikiana nao zaidi katika kuboresha bidhaa za tiba asili kufikia viwango vya kimataifa ili kuinua uchumi wao na taifa sambamba na kuboresha afya za jamii. 

Alisema maonesho hayo ni mwanzo wa maonesho ya fursa nyingi za katika tafiti za mimea dawa na tiba asili na kuwataka wataalamu wa tiba asili kuwatumia watafiti wa SUA kwenye mambo mbalimbali yanayohitaji sayansi zaidi. 

Kwa pande wake Mkuu wa Mradi wa GRILI ambao ndio waandaaji wa maonesho hayo Dkt. Faith Mabiki amesema tafiti nyingi zimefanywa na watafiti wa SUA kwenye Mradi huo kwenye masuala ya miti dawa na kupata matokeo mazuri ambayo yatassidia kwenye kuongeza thamani na kuboresha tiba asili na uendelevu wake. 

Dkt. Mabiki ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wadau wote wa Tiba asili nchini kushiriki kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Ubunifu katika tiba asili na bidhaa zake litakalofanyika kwenye Ndaki ya Solomon Mahlangu ya Sayansi na Elimu kwenye kampasi ya Mazimbu kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 7:00 Mchana. 

Amesema uzinduzi wa jukwaa hilo utakuwa mwanzo mzuri wa kupata jukwaa la pamoja kati ya wadau wote wa tuba asili na wasimamaizi wa tiba asili upande wa serikali kujadiliana kwa pamoja mambo muhimu ya kuendeleza sekta hiyo ambayo imeshika kasi sana ikilinganishwa na huko nyuma kabla ya Ugonjwa wa Covid-19.


Thursday, January 21, 2021

WAGANGA WA TIBA ASILI WATUMIE SUA NA WATAFITI WAKE KUBORESHA BIDHAA ZILIZOPO NA KUANZISHA MPYA.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Utawala na Fedha  Prof. Amandus Muhairwa akifungua kongamano kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda wakati akifungua Kongamano la siku moja la Watalaamu wa Tiba asili na kutoka maeneo mbalimbali nchini lililofanyika Chuoni kabla ya maonesho na uzinduzi wa jukwaa la ubunifu wa bidhaa za mimea dawa kwa maendeleo ya taifa lililoandaliwa na Mradi wa GRILI.

Mratibu wa Utafiti na machapisho katika kurugenzi ya shahada za uzamili,utafiti,uhaulishaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalamu ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Japhet Kashaigiri akitoa salamu za kurugenzi yake kwenye kongamano hilo la wadau wa tiba asili nchini.

Mtafiti Mkuu wa mradi wa GRILI Dkt. Faith MabikiAkileza malengo ya mradi huo wa GRILI na malengo ya Kongamano hilo la wadau wa tiba asili nchini. 

Mkuu wa Ndaki ya Solomoni Mahlangu ya Sayansi na Elimu Dkt. Geofrey  akitoa salamu za Ndaki yake na kuwakaribisha wageni hao Chuoni hapo. 

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Utawala na Fedha  Prof. Amandus Muhairwa (Katikati) akisikiliza maelezo toka kwa viongozi wa mradi, Prof. Samweli Kabote amabye ni Muwakilishi wa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na fedha  (Wa kwanza Kushoto) Akifuatilia hotuba ya ufunguzi, W KWANZA Kushoto ni Dkt. Geofrey Kalugila Rasi wa ndaki ya Solomon Mahlangu ya sayansi na Elimu. 

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Utawala na Fedha  Prof. Amandus Muhairwa akiangalia maonesho ya bidhaa mbalimbali za tiba asili zilizoletwa kwenye kongamano hilo kabla ya maonesho rasmi siku ya ijumaa.
Washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia ufunguzi wa Kongamono hilo na mada mbalimbali.
Washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia ufunguzi wa Kongamono hilo na mada mbalimbali.
Washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia ufunguzi wa Kongamono hilo na mada mbalimbali.


Na Calvin Gwabara,  Morogoro.


WAGANGA wa Tiba Asili nchini wametakiwa kuangalia kwa undani namna ya kutumia matokeo ya tafiti zinazofanywa na watafiti wa Chou Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Taasisi zingine ili kuboresha bidhaa zilizopo na kuanzisha bidhaa mpya ili kuendana na mahitaji ya jamii kwa wakati sahihi.

Wito huo ulitolewa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Utawala na Fedha  Prof. Amandus Muhairwa kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda wakati akifungua Kongamano la siku moja la Watalaamu wa Tiba asili na kutoka maeneo mbalimbali nchini lililofanyika Chuoni kabla ya maonesho na uzinduzi wa jukwaa la ubunifu wa bidhaa za mimea dawa kwa maendeleo ya taifa lililoandaliwa na Mradi wa GRILI.

Prof. Mhairwa alisema kuwa njia hiyo ni muhimu sana hasa katika wakati huu ambao dunia inahangaika kutafuta chanjo na tiba ya ugonjwa wa COVID 19 ambapo dawa za mimea zimeonekana kufanya vizuri Zaidi kuliko za hospitalini,

” Wanasayansi na waganga wa tiba ya asili sio kama vyama viwili vya upinzani, sisi tunafanya kazi kwa kutegemeana, sisi tunavitu tunavumbua kisayansi lakini pia kuna vitu vingine tunavifanyia utafiti vile ambavyo mmevianzisha nyinyi ili kuweza kupata udani Zaidi wa dawa mnazogundua kwahiyo hatupingi kazi zenu wala msituone kama vile maadui sisi tufanye kazi kwa pamoja kwa faida ya jamii na taifa letu” Alisisitiza Prof. Mhairwa.

Alisema bidaa za mimea dawa zinakabiliwa na changamoto zinazohusiana na uzalishaji,uvunaji,utengenezaji,uuzaji na upatikanaji endelevu wa malighafi hivyo ili kupunguza changamoto hizo na kuzindoa kabisa kunahitajika utafiti Zaidi wa kisayansi,ubunifu Zaidi katika masoko,uzingatiaji wa hali ya juu wa vigezo vya ubora vinavyotakiwa na kufuata taratibu za biashara zenye tija.

Lakini pia aliwataka Wataalamu hao wa Tiba asili kuangalia masuala ya kisera yanayoleta changamoto katika kuhaulisha teknolojia hizi ili ziweze kutumika kibiashara na kuanzisha viwanda vya uzalishaji wa mimea dawa na hasa katika kipindi hiki ambapo sera ya serikali ni kusukuma uanzishwaji wa viwanda kwenye sekta hii.

Naibu Makamu huyo wa Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha aliwahakikishia kuwa SUA na hasa kurugenzi ya uzamili,Utafiti,Uhaulishaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalamu kwa kushirikiana na serikali wataendelea kuwa nao bega kwa bega kwa kusaidia jitihada za wadau wote kwenye sekta hii katika kuboresha tafiti za oaina hii kwa kadri mazingira yatakavyoruhusu.

Akitoa salamu kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua kongamano hilo Mratibu wa Utafiti na machapisho katika kurugenzi ya shahada za uzamili,utafiti,uhaulishaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalamu ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Japhet Kashaigiri alisema kuwa kurugenzi hiyo na vitengo vingne vya SUA vimekuwa na utaratibu wa kuandaa makongamano ya aina hiyo ili kujaribu kuboresha biashara za mazao ya Kilimo,Ufugaji na Misitu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika sekta hizo.

“Katika makongamano haya SUA imekuwa ikishirikisha wasimamizi na wakaguziwa ubora wa biashara hizi pamoja na watunga sera kwa ujumla na utaratibu huu umeongeza mchango mkubwa wa chou chetu katika kutatua changamoto mbalimbali na kuboresha biashara za mazao nah ii ni muhimu hasa katika awamu hii ya serikali ya tano ambayo mwelekeo wake ni kuwa uchumi wa viwanda.

Prof. Kashaigili alisema Vyuo Vikuu kote duniani ni vitovu vya maendeleo ya kitaaluma na Tafiti mbalimbali na kwa muktadha huo kurugenzi ya uzamili kupitia kitengo chake cha uhaulishaji wa teknolojia pamoja na mradi wa GRILI zimeona ni vyema kutumia uzoefu wake wa ndani na kwa kushirikiana na wadau wengine kuandaa kongamano hili hapa SUA ili kuwaleta wadau wote pamoja na kujadili namna ya kukuza uelewa na kutatua changamoto hizo.

Akileza malengo ya mradi huo wa GRILI na malengo ya Kongamano hilo Mtafiti mkuu wa mradi huo Dkt. Faith Mabiki amesema Utekelezaji wa mradi huu ulianza mwaka 2018 ukiwa na lengo la kuchangia katika kuongeza ubora wa bidhaa za miti dawa ili kuboresha Maisha ya watengenezaji,afya za watumiaji na kuchangia katika pato la taifa.

Dkt. Mabiki alisema ili kufikia malengo hayo ya muda mrefu mradi huo unajenga uwezo wa kitafiti wa kitafiti kwa wanafunzi wa shahada za uzamivu 5 na shahada za uzamili 2 katika maeno muhimu ya kemikali,usugu wa dawa na masoko na unategemea kutoa matokeo ya kitafiti yatakayo tumika na wadau muhimu wa kuboresha biadhaa hizi.

“Kongamano hili la kitaalamu la wadau likiwa ni moja ya shughuli za uzinduzi wa Jukwaa la ubunifu wa bidhaa za mimea dawa kwa maendeleo ya taifa litajikita Zaidi kwenye kujadili Uboredhaji wa uzalishaji,uchakataji,ufungsdhsji na uuzaji wa bidhaa zinazotokana na mimea dawa hapa Tanzania na namna ya kutatua changamoto hizo” Alisema Dkt. Mabiki.

Kwa upande wake Mkuu wa Ndaki ya Solomoni Mahlangu ya Sayansi na Elimu Dkt. Geofrey  alisema kwa upande wa utafiti ndaki hiyo ni ya pekee inayotoa shahada ya uzamili ambazo zinajikita moja kwa moja katika utafiti wa mazao ya mimea dawa ambayo mojawapo inahusika katika tukio hili na ina miradi Zaidi ya tisa ambayo kwa namna moja au nyingine zinagusa bidhaa hizi za mimea dawa.

“Kwa sababu hiyo tunategemea kuchangia juhudi za SUA na Taifa katika kuongeza ubora wa bidhaa hizi ili zipate Masoko” Alisisitiza Dkt. Kalugila.

 Pia Dkt. Geofrey Kalugila aliwashukuru wadau hao kutoka maeneo yote nchini kufiki akushiriki kwenye kongamano hilo,maonesho na uzinduzi wa Jukwaa la ubunifu na kuwataka watumia siku chache watakazokuwa SUA kujifunza na kujionea mambo mbalimbali ya kistoria kwenye kampasi hiyo ambayo ilikuwa kambi ya wapigania uhuru wa Afrika kusini.

Kongamano hilo litafuatiwa na Maonesho makubwa ya Tiba asili na bidhaa zake litakalofanyika kwenye viwanja vya soko kuu la mkoa wa Morogoro tarehe 22/01/2021 na baada siku ya jumamosi kutakuwa na uzinduzi wa Jukwaa la ubunifu wa bidhaa za tiba asili litakalofanyika kwenye kampasi ya Solomon Mahlangu Mazumbu tarehe 23/01/2021 zilizoandaliwa na Mradi wa GRILi.

Tuesday, January 19, 2021

SKAUTI MBEYA WATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO KATA YA KALOBE

Muathirika wa mafuriko Bibi, Tamali Mwalukunga Mkazi wa Kata ya Kalobe jijini Mbeya akiwashukuru Vijana  wa Skauti baada ya kumjengea choo kilicho sombwa na mafuriko. Wa pili kushoto ni Kamishna wa Skauti Mkoa wa Mbeya, Sadock  Ntole na kulia ni Mratibu wa Majanga wa  chama hicho mkoani humo, Lusajo Exaud Sanga.

Vijana wa Skauti wakizibua mtaro.



Diwani wa Kata ya Kalobe, akiwapongeza vijana wa Skauti kwa kazi hiyo.
Vijana wa Skauti wakiwa katika picha ya pamoja.
Kazi ya uchimbaji choo cha Bibi Tamari Mwalukunga ikiendelea.
Choo cha Bibi Tamari Mwalukunga kikichimbwa.
Kazi ikiendelea.
Kazi ikiendelea..



Na Dotto Mwaibale.


CHAMA cha Skauti Mkoa wa Mbeya kimetoa msaada kwa kuwasaidia waathirika wa mafuriko katika Kata ya Kalobe jijini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Kamishna wa Skauti wa mkoa huo Mratibu wa Majanga wa  chama hicho mkoani humo, Lusajo Sanga alisema eneo lililoathiriwa zaidi na mafuriko hayo ni Mtaa wa Maendeleo A katika kata hiyo.

Alisema mafuriko hayo yalitokea Januari 8 mwaka huu kufuata mvua kubwa iliyonyesha.

" Eneo hilo liliathiriwa zaidi na mafuriko hayo kutokana na mifereji ya maji kuziba hivyo maji ya mvua kukosa muelekeo na kwenda kwenye makazi ya watu" alisema Sanga.

Alisema baada ya kutokea mafuriko hayo walisaidia na Kamishna wa Skauti Mkoa huo, Sadock Ntole, kuratibu namna ya kwenda eneo la tukio kutoa msaada wa kibinadamu kwa waathirika ikiwa ni pamoja na kuchimba vyoo vilivyosombwa na maji, kuzibua mitaro na kuwafariji waathirika kwa kushirikiana na diwani wa kata hiyo na viongozi wengine. 

Sanga alisema mafuriko hayo yaliathiri nyumba tano katika mtaa huo ambapo nyumba ya mkazi mmoja wa eneo hilo  aliyefahamika kwa jina la Mama Muro na Bibi Tamali Mwalukunga ziliathiriwa zaidi  kwani sehemu ya nyumba yake na choo  vilibomoka ambapo walilazimika kumjengea choo kingine cha muda.

Kamishna wa Skauti Mkoa wa Mbeya, Sadock  Ntole alisema wao kama skauti wamekuwa wakitoa msaada kwa jamii pale yanapotokea majanga ya namna hiyo hivyo baada ya kutokea mafuriko hayo walienda eneo la tukio kutoa msaada huo. 

Monday, January 18, 2021

SPRF YAKUTANISHA ZAIDI YA WANAWAKE 100 KUJADILI UKATILI

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Justice Kijazi, akizungumza kwenye kikao kazi cha tathmini ya hali ya matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto wilayani humo jana kilichoshirikisha wanawake 120 waliokutanishwa na Shirika la SPRF chini ya ufadhili wa FCS ili kujadili namna bora ya kutokomeza matukio hayo kwa mujibu wa sheria.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Stars of Poverty Rescue Foundation (SPRF) Dkt. Suleiman Muttani  akizungumza kwenye mkutano huo ulioshirikisha wanawake 120 kutoka vijiji 12 kuzunguka wilaya ya Ikungi, Singida. 

Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali zilizojikita katika kuwajengea uwezo na kuwaimarisha katika mapambano dhidi ya matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani humo.

Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali zilizojikita katika kuwajengea uwezo na kuwaimarisha katika mapambano dhidi ya matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani humo.

Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali zilizojikita katika kuwajengea uwezo na kuwaimarisha katika mapambano dhidi ya matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani humo.

Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali zilizojikita katika kuwajengea uwezo na kuwaimarisha katika mapambano dhidi ya matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani humo.

Kikao kazi cha vikundi vya uhamasishaji kwa Sauti Ya Mwanamke na Sauti ya Mwanafunzi  kikiendelea.

Maafisa Watendaji wa Shirika la SPRF wakifuatilia matukio yanayoendelea kwenye kikao hicho.

Jeshi la Polisi likishiriki ipasavyo kikao hicho.

Mmoja wa waratibu wa mradi wa Aware, Bernard Maira akizungumza kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa Sauti ya Mwanamke kwenye moja ya makundi ya uhamasishaji akizungumza.

Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Ikungi, Beatrice Maeda akizungumza.

Kikao kikiendelea.
Moja ya kikundi cha Uhamasishaji cha Sauti ya Mwanamke wilayani  Ikungi  wakieleza moja ya tukio la ukatili wa kijinsia walilofanikiwa kuliibua.



Na Dotto Mwaibale, Singida


SHIRIKA lisilo la Kiserikali linalojikita zaidi katika mlengo wa shughuli za kupunguza umaskini kwa afya na ustawi nchini (SPRF) kupitia mradi wake wa  ‘Aware’ jana limewakutanisha wanawake 120 kutoka vijiji 12 vya wilaya ya Ikungi, mkoani hapa kwa lengo la kuwaimarisha kuweza kukabiliana ipasavyo na  matukio ya ukatili.

 Jumla ya matukio ya ukatili wa kijinsia 104 yameripotiwa kufanyika ndani ya Wilaya ya Ikungi  kwa kipindi cha kati ya Julai 2019 hadi Novemba 2020, ambapo kati ya matukio hayo 56 yalijitokeza katika kipindi cha Julai 2019 hadi Februari 2020, huku matukio mengine 48 ya aina hiyo hiyo yakijitokeza  kipindi cha Machi hadi Novemba 2020.

Kwa mujibu wa SPRF chini ya ufadhili wa Shirika la Foundation for Civil Society (FCS) imebainika kuwa kati ya matukio hayo 56 yaliyoripotiwa kutoka vijiji 12 vya mradi huo kwa kipindi hicho cha Julai 2019 hadi Februari 2020 ni kesi 2 ndizo zilizofikishwa kwenye ngazi ya mahakama, na kati ya hizo kesi moja pekee ndiyo iliyotolewa hukumu.

Matukio mengine 7 ya ukatili yaliyoripotiwa yaliishia kwenye Kituo cha Polisi Ikungi kutokana na kukosa vielelezo na ushahidi shawishi, huku kesi 4 zikikomea kwenye vituo vidogo vya polisi, 7 kwenye ngazi za kata, 16 ngazi ya vijiji, 5 ngazi ya vitongoji na 14 zikiishia kutatuliwa kindugu kwenye ngazi ya familia.

Aidha, kwa upande wa matukio 48 yaliyojitokeza  kwenye kipindi cha Machi hadi Novemba 2020 ni kesi 2 pekee ndizo zilizofikishwa na kuamriwa kwenye ngazi ya mahakama, huku matukio mengine 11 yakiishia Kituo cha Polisi Ikungi, 5 vituo vidogo vya polisi kwenye maeneo hayo, 1 ngazi ya kata, 12 vijiji, 6 Ustawi wa Jmii Wilaya, 2 Vitongoji na  7 zikiishia kutatuliwa kindugu kwenye ngazi ya familia.

Wakichangia ripoti hiyo kabla ya kufikia maazimio, baadhi ya wanawake kutoka kwenye majukwaa ya Sauti za wanawake na Sauti za Wanafunzi wilayani hapo walisema bado kuna udhaifu mkubwa katika kushughulikia utekelezaji wa sheria zinazopinga  vitendo vya ukatili.

“Suala hili limeendelea kuwa sugu na linalochochea  ongezeko la matukio ya kufedhehesha, undugu, ujamaa na urafiki ndio chanzo kikubwa kinachoathiri mwenendo wa mashauri haya ya ubakaji, ndoa za utotoni na mimba za umri mdogo hasa pale tunaporuhusu yamalizwe kwenye ngazi za familia,” alisema mmoja wa washiriki wa mkutano huo, Anna Heneriko.

Mwingine Pili Hussein alisema kesi nyingi zimekuwa zikimalizwa kwenye ngazi ya vituo vya polisi na kwa maaafisa watendaji. Lakini kubwa zaidi kuna uvujishaji mkubwa wa siri kwa watoa taarifa jambo ambalo linafifisha hamasa ya mapambano dhidi ya vitendo hivyo. 

Kupitia mkutano huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Justice Kijazi aliwataka maafisa wa ustawi wa Jamii na Jeshi la Polisi kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria katika kuhakikisha mashauri yote yanayoripotiwa yanafikishwa kwenye ngazi za utatuzi wa kisheria.

“Niwahakikishieni mama zangu wote mliopo hapa serikali yenu chini ya Rais John Pombe Magufuli ni sikivu sana, na inakwazwa sana na aina yoyote ya uhalifu na uvunjifu wa sheria kwa makusudi. Nimeguswa sana na matukio haya yanayofedhehesha mama zetu na watoto wetu…chukueni namba zangu za simu ili yeyote kati yenu atakayeona tukio lolote la ukatili likitendeka anijulishe,” alisema Kijazi

Aidha, Kijazi aliwataka aliwataka maafisa Ustawi wa Jamii na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanashughulikia kikamilifu kesi za matukio yote ya ukatili yanaripotiwa kwa utimilifu unaozingatia matakwa ya kisheria kwa minajiri ya kutokomeza kabisa vitendo hivyo, sambamba na kuwezesha haki kuonekana kutendeka.

 Hata hivyo, Jeshi la Polisi Ikungi kupitia mkutano huo liliwataka wananchi wa wilaya hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha pindi matukio hayo yanapojitokeza, na hasa kutoharibu wala kuwashawishi wahanga kuficha ushahidi ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe pindi matukio hayo yanapojitokeza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa SPRF, Dkt. Suleiman Muttani  alisema lengo la kikao hicho ni kutaka kuyaimarisha kiutendaji majukwaa ya vikundi vyote vya uhamasishaji dhidi ya matukio ya ukatili, ikiwemo kundi la Sauti ya Mwanamke katika kuendelea kushirikiana na majukwaa mengine kutetea haki za wanawake na watoto.

“Azma ya mradi huu wa ‘Aware’ ni kuona mifumo ya serikali za mitaa imeimarika kwa kupokea na kuitikia kwa haraka utekelezaji wa mahitaji ya jamii hasa matakwa ya wanawake, watoto na makundi mengine athirika kuona wanatambua suala la ukeketaji, ndoa za utotoni, ukatili kwa wanawake na unyanyasaji kwa watoto haukubaliki,” alisema Muttani 

mpaka sasa kati ya matukio yote hayo yaliyoibuliwa kwa ushirikiano wa majukwaa yake mbalimbali ikiwemo Sauti ya Mwanamke, Sauti ya Mwanafunzi, Kamati za Mtakuwa na Wanaume Washawishi ndani ya Vitongoji na Vijiji ni kesi 48 pekee ndizo zilizofika kwenye ngazi za utatuzi huku nyingine utatuzi wake ukiishia kwenye ngazi za familia.

Sunday, January 17, 2021

TARURA SINGIDA YAOKOA ZAIDI YA BILIONI 1.8 UJENZI WA DARAJA WILAYANI MANYONI



Watendaji wa  Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Manyoni wakikagua daraja hilo.

Wananchi na vyombo vyao wakivuka mto Nkonjigwe kwa kutumia daraja hilo.
Wananchi wanaozunguka maeneo ya daraja Nkonjigwe wakifurahia kutokana na kujengewa daraja hilo.


Na Dotto Mwaibale, Singida.


SERIKALI ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk. John Magufuli kupitia watendaji waaminifu wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) imeokoa zaidi ya bilioni 1.8 kwenye ujenzi ambao tayari umekamilika wa daraja la Mto Nkonjigwe Wilayani Manyoni mkoani hapa.

Kabla ya kuanza kwa ujenzi huo kati ya Juni na Septemba upembuzi yakinifu wa mradi huo kupitia wazabuni mbalimbali ulikadiriwa kufikia zaidi ya shilingi bilioni 2, kabla ya Tarura kufanya maamuzi magumu ya kutumia mfumo wa Force Account.

Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo kunakwenda kufungua fursa za uhakika wa upatikanaji wa huduma za afya hususani kwa akina mama wajawazito sambamba na kuimarisha wigo wa kibiashara kwa wakazi wa kata takribani tano zinazotumia njia inayounganishwa na daraja hilo yenye urefu wa km 76.2.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wanaozunguka eneo hilo akiwemo Halima Abdallah mkazi wa Kijiji cha Chikuyu alisema wamefurahishwa na ujenzi wa daraja hilo ambalo litawasaidia akina mama wajawazito kuvuka na kwenda kujifungua kwenye Zahanati za Kilimatinde na Chikuyu kwani awali wengi walikatisha maisha yao kwa kushindwa kuvuka mto huo.

Halima alisema walikuwa wanatoa shilingi elfu 2 hadi elfu 3 kuvushwa kwenye Mto huo na watu wenye uzoefu wa kuogelea jambo ambalo halikuwa salama kwao kwani kuna wakati licha ya uzoefu wao hushindwa kuvuka na kupelekwa na maji pamoja na aliyekuwa anavushwa.

"Tulikuwa tukifika hapa tunavua nguo halafu ndio tunavushwa, tunatoa shilingi elfu 2 za mtu kuvushwa na shilingi elfu 3 za nguo.watu wamekufa wengi sana hapa hasa Wanawake wajawazito." alisema  Halima.

Thomas Minaloganawenda mkazi wa Kijiji cha Chinyika kilichopo Kata ya Sasajila alisema moja ya shughuli kubwa ya kiuchumi kwenye maeneo haya ni uchimbaji wa chumvi lakini kuna wakati ilikuwa ikiharibikia kwenye mto kutokana na kukosa daraja.

Alisema amefanya kazi ya kuwavusha watu kwenye mto huo kwa muda mrefu licha ya kujipatia ujira lakini ilikuwa inaumiza anapoona wengi wakipoteza maisha hakuwa anafanya kazi hiyo kwa raha ila ni katika kujaribu kuokoa maisha ya watu waliokuwa wanafika hapo na kuhitaji kuvuka kwenda kupata huduma.

Awali Mratibu wa TARURA Mkoa wa Singida Mhandisi Boniphace William alisema ujenzi wa daraja hilo umegharimu shilingi milioni 122,415,500 hadi kukamilika kwake ambapo limetumia mfumo wa raslimali za ndani 'Force Account' 

Aidha, William alisema daraja hilo linatoa fursa ya upatikanaji wa huduma mbalimbali kuzunguka Vijiji vya Chikuyu,Chibumagwa, Sasajila, Majiri na Sanza.

"Nawaomba wananchi wanaohudumiwa na daraja hili na miradi mingine sehemu mbalimbali kutambua miradi hiyo ni kwa ajili yao, hivyo ni wajibu wao kuitunza na sio suala la Tarura pekee, wakijenga tabia hiyo miradi mingi itadumu kwa muda mrefu." alisema William.

Kwa upande wake Meneja wa Tarura Wilaya ya Manyoni Mhandisi Yose Mushi alisema daraja hilo ambalo lina urefu wa mita 53 na mita 25 eneo la kupitisha maji, kadhalika lenye tuta mita 28 linatarajia kuchagiza kasi ya ustawi wa uchumi kwa wakazi wanaozunguka maeneo hayo. 

Friday, January 15, 2021

MAAFISA WATENDAJI KATA NA VIJIJI WAPEWA MENO SEKTA YA ARDHI

Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Singida, Shamim Hoza (kulia) akiwasilisha taarifa ya mpango wa usimamizi wa matumizi ya ardhi kimkoa na hatua za utekelezaji wake wakati Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alipofanya ziara ya kikazi kutembelea mkoa huo.

Mkuu wa Wilaya ya Singida, anayesimamia Halmashauri za Singida Manispaa na Singida Vijijini, Mhandisi Paskas Muragiri akizungumzia mambo kadhaa yanayohusu maboresho kwenye sekta ya ardhi mbele ya Waziri Lukuvi.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akikagua mafaili na nyaraka zote zilizohifadhiwa ndani yake kwenye Masijala ya Ardhi Singida Vijijini alipofanya ziara kwenye eneo hilo, sanjari na kutoa maelekezo ya namna bora ya utunzaji wa kumbukumbu hizo kwa faida ya wananchi.
Waziri Lukuvi akitoa maelekezo juu ya maboresho kadhaa yanayopaswa kufanywa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, alipofanya ziara kwenye ofisi za ardhi ndani ya halmashauri hiyo. Kushoto ni Afisa Ardhi na Kaimu Mkuu wa Idara hiyo, Ambroce Ngonyani
Waziri Lukuvi akitoa maelekezo juu ya maboresho kadhaa yanayopaswa kufanywa ndani ya Manispaa ya Singida, alipofanya ziara kwenye ofisi za ardhi ndani ya Manispaa hiyo. Kulia ni Afisa Ardhi Mteule, Christian Kasambala.
Ziara ikiendelea.
Ziara ikiendelea.

Waziri Lukuvi akiwa kwenye ziara ya kukagua mashamba makubwa ya mradi wa Kilimo cha Pamoja cha Korosho ‘Block Farming’ yaliyopo eneo la Masigati Wilaya ya Manyoni. Kupitia ziara hiyo aliagiza wakulima wote kwenye maeneo hayo wapatiwe hati kwa ustawi zaidi wa maisha yao.

Ziara kwenye mashamba hayo ikiendelea.

Baadhi ya Watendaji Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Singida wakiwa na Waziri Lukuvi (hayupo pichani) kwenye ziara hiyo. Kutoka kushoto ni Naibu Kamishna wa wa ofisi hiyo Shamim Hoza, Msajili wa Hati Msaidizi Jamila Awadhi, Mpima Ardhi Mkoa Sesaria Lusingu na Afisa Mthamini Angelina Bauleni..

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Mdogo wa Manyoni, Charles Fussi (kulia) akizungumza na Waziri Lukuvi kwenye ziara hiyo eneo la masigati, Manyoni.

Ziara ikiendelea.

Ziara ikiendelea.



Na Dotto Mwaibale, Singida


WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameagiza Wakurugenzi nchini kuanza mara moja kuwapa wajibu Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji kufanya kazi ya kuratibu na kusimamia masuala yote yanayohusu shughuli za uendelezaji ardhi kwenye maeneo yao-isipokuwa kugawa na kuuza, ili kupunguza changamoto ya migogoro na kurahisisha ukusanyaji wa kodi na taarifa.

Lukuvi aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani hapa juzi, alipotembelea ofisi zote za ardhi kwenye Halmashauri za wilaya Singida Vijijini, Singida Manispaa, Ikungi na Manyoni.

“Nataka Wakurugenzi wote muwape wajibu kwa maandishi Maafisa Watendaji wote wa Mitaa na Vijiji kufanya kazi kama ‘Land Administrators’ kwenye maeneo yao. Na lazima tushirikiane nao kwa karibu kama jicho letu kule chini, fanyeni haraka jitihada ya kuwakutanisha pamoja na kuwapa uelewa kujua mambo gani ya kwenda kusimamia, hii itasaidia sana katika usimamizi wa pamoja wa ardhi,” alisema Lukuvi na kuongeza:

“Nataka ieleweke huyu Mtendaji wa Mtaa sio jukumu lake kumilikisha wala kugawa ardhi, sababu hilo ni jukumu la kamati ya wilaya ya Manispaa. Yeye atahusika tu katika usimamizi wa kila kitakachofanyika na kwa kufanya hivyo tutapokea taarifa nyingi na kwa haraka sana juu ya uendelezaji holela, ukwepaji kodi na uvunjifu wa sheria. Tukiheshimu na kufuata utaratibu huu tutapiga hatua kubwa kwenye makusanyo.

Aidha, aliwataka wananchi wote kutofanya chochote kinachohusiana na uendelezaji wa shughuli yoyote ya ardhi bila kwanza kuripoti kwa Afisa Mtendaji wa Mtaa au Kijiji hata kama umepewa kibali toka wilayani lengo ni kwanza kumfanya Mtendaji ajue ni kitu gani kinataka kufanywa kwenye mtaa wake lakini pia kama kweli kina baraka zote kisheria.

“Makamishna wa mikoa simamieni hili sababu lengo la serikali hapa ni kutaka kudhibiti ujenzi holela ndani ya miji na kuhakikisha kila kinachoendelezwa kipo kwenye taratibu za michoro ya mipango miji na kimefuata sheria hata kama eneo ni lake. Na hao watendaji watengeneze mtandao na wajumbe wao ndani ya serikali za mitaa ili kupeana taarifa nani anajenga wapi na kwa wakati gani,” alisisitiza Lukuvi.

Katika hilo aliagiza kila Mtendaji wa Mtaa apatiwe jedwali maalumu litakalokuwa na orodha ya kutambua wangapi kwenye mtaa wake wamemilikishwa ardhi kwa hati, na wanamiliki nini, nani anastahili kulipa kodi ya pango la ardhi, na zile hati wanazomiliki wameendeleza nini ijulikane!-azma ni kusaidia namna ya kuwakumbusha na kuchukua kodi kwenye maeneo hayo.

Hata hivyo, Lukuvi aliwataka maafisa ardhi wa wilaya kutoficha taarifa badala yake wahakikishe kila mmilikaji mpya wa ardhi anayepatikana ndani ya wilaya basi taarifa zote zinamfikia Mtendaji wa Mtaa husika, lengo ni pamoja na mambo mengine, kurahisisha uhakiki wa taarifa na utunzaji kumbukumbu katika muktadha wa kuwatambua wote wanaomiliki ardhi kwenye mitaa mbalimbali nchini.

Hata hivyo, Waziri alishauri vitolewe vipande vidogo-vidogo ndani ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi (Masterplan)kwa kila Manispaa na Halmashauri ‘Final Draft’ vinavyohusu mpango wa kila mtaa na akabidhiwe Mtendaji ili kumwezesha kuoanisha kama kinachoendelezwa kwenye ardhi kinafanana na mpango uliopo.

“Agizo na maelekezo haya nataka kabla ya bajeti yawe yametekelezwa na taarifa hizi ziwe mitaani kwa maana ya taarifa za wamilikishwaji wote kwenye mitaa ziwe zimeshapatikana na zipo kwa watendaji wa mitaa nchi nzima. Makamishna simamieni hili nitapita kukagua,” alisisitiza Lukuvi.

Katika hatua nyingine, akiwa wilayani Manyoni  mbali ya kupongeza juhudi kubwa zilizofanyika katika mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye eneo la Masigati na Kinangali unapotekelezwa Mradi wa Kilimo cha Pamoja cha zao la Korosho kupitia mashamba makubwa (Block Farming), aliagiza wakulima wote wanaotekeleza mradi huo wapatiwe hati mara moja ili ziwasaidie kuweza kukopesheka.