Thursday, August 26, 2021

WANAMUZIKI WAANZA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA SIKU YAO KIMATAIFA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania  (TAMUFO) Stella Joel.
Stara Thomas
Komandoo Hamza Kalala.
Mwanamziki Mabisa.

 


Na Dotto Mwaibale 


WANAMUZIKI Nchini wameanza maandalizi kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Muziki Duniani yatakayoadhimishwa kitaifa jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa jana Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania  (TAMUFO) Stella Joel alisema tayari wameanza kuandaa maandalizi kwa ajili ya maadhimisho hayo.

"Tumeanza maandalizi ya Siku hiyo na tayari baadhi ya wanamuziki wamekwisha thibitisha kushiriki,". alisema Joel.

Alisema kuwa leo saa 4 asubuhi katika Hoteli ya Kibo Palace Jijini Arusha watakutana  na waandishi wa habari na kuzungumzia kwa kina maandalizi hayo.

 Joel aliwataja baadhi ya wanamuziki waliothibitisha kushiriki maadhimisho hayo  kuwa ni Komandoo Hamza Kalala, Stara Thomas na wengine wengi.

Alisema kilele cha maadhimisho hayo itakuwa ni  Oktoba 1,2021.

Saturday, August 21, 2021

CCM SINGIDA YAMPA TANO RAIS SAMIA KWENYE MABORESHO MIRADI YA AFYA


Mkuu wa Mkoa Singida, Dkt.Binilith Mahenge akisisitiza jambo wakati Wajumbe wa Kamati ya Siasa  Mkoa  wa Singida walipo kuwa wakikagua mradi wa Chuo cha Ufundi VETA jana unaojengwa wilayani Ikungi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Alhaji Juma Kilimba (wa tatu kushoto) akiongoza kamati hiyo kukagua mradi wa vyoo Zahanati ya Puma. Kulia ni Muuguzi Mkuu wa Zahanati hiyo Lucy Tathi.


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akizungumzia mradi wa ujenzi wa vyoo Zahanati ya Puma.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Puma, Samuel Mdimu akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi huo.
Wananchi wa Puma wakishuhudia ukaguzi wa mradi huo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida, Denis Nyiraha akizungumza wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa  vyoo vya Zahanati ya Puma. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Mkoa wa Singida, Yohana Msita, akichangia jambo kwenye ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa vyoo  vya Zahanati ya Puma. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa Singida, Dkt.Binilith Mahenge.


Muonekano wa baadhi ya majengo ya Zahanati ya Puma.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida, Iddi Maalim akichangia jambo wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa vyoo  vya Zahanati ya Puma.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida Diana Chilolo akichangia jambo kwenye ukaguzi wa miradi hiyo.
Ukaguzi wa mradi wa maji wa Kijiji cha Kipumbuiko ukiendelea.Mradi huo umegharimu Sh. 359 Milioni na wananchi wameanza kunufaika nao.
Kaimu Afisa Tarafa Ikungi, Yahaya Njiku (kulia) akiwaelekeza jambo Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kipumbuiko, Debora Malali (kushoto) na Afisa Tawala  Wilaya ya Ikungi Dijo Ndangeki wakati wa Ukaguzi wa mradi wa maji wa Kijiji hicho.

Ukaguzi wa mradi wa maji Kijiji cha Kipumbuiko ukiendelea. Kulia ni Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira (RUWASA) Wilaya ya Ikungi Mhandisi Hapeness Liundi.
Wananchi wa Kijiji cha Kipumbuiko wakishuhudia ukaguzi wa mradi wao wa maji.


Ukaguzi wa madarasa Shule ya Sekondari Ikungi ukiendelea.

Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Lucy Shee, akihimiza umuhimu wa kuchukua tahadhari ya kujikinga na Corona wakati wa ukaguzi ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Issuna.
Ukaguzi wa maabara Shule ya Sekondari Ikungi ukiendelea.
Ukaguzi wa madarasa Shule ya Msingi Ikungi ukiendelea.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ikungi akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa madarasa.
Ukaguzi ujenzi wa Chuo cha Ufundi  VETA  ukiendelea.
  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Gutete Mahava akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi ujenzi wa Zahanati Kata ya Issuna.
Fundi rangi akiwajibika kwenye mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Issuna.
Ukaguzi ujenzi wa ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Issuna  ukiendelea.
Wananchi wa Kata ya Issuna,watumishi wa Wilaya ya Ikungi na wajumbe wa kamati ya siasa wakiwa kwenye ukaguzi wa mradi ujenzi wa Zahanati ya kata hiyo.
        Mwenyekiti wa Kikundi cha Ufugaji Nyuki cha Save The Bee cha Issuna, Mrisho Amiry akisoma taarifa ya mradi huo mbele ya kamati hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akizungumzia mradi wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo mbele ya wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa kabla ya ukaguzi wa ujenzi wa hospitali hiyo.


Na Dotto Mwaibale, Singida


KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida imekagua miradi ya maendeleo wilayani Ikungi na kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo hususani eneo la maboresho makubwa yanayoendelea kufanyika chini ya Serikali ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya afya.

Pia kupitia ukaguzi wa utekelezaji wa miradi hiyo CCM kwa namna ya kipekee imeguswa na mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Issuna iliyopo Wilaya ya Ikungi ambao unakwenda kutatua changamoto za wananchi wa eneo hilo za kusafiri umbali mrefu kwenda kata zingine kufuata huduma za afya.

Akizungumza jana wakati wa ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa maagizo ya ilani ya CCM, Mwenyekiti wa kamati hiyo Alhaji Juma Kilimba alihimiza sekta hiyo na nyingine kuhakikisha inakamilisha miradi yote kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa.

"Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo nchini kote hivyo nawaomba wasimamizi wa ujenzi wa miradi hii kuwa wazalendo katika matumizi ya fedha hizo,". alisema Kilimba.

Katika hilo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Gutete Mahava akitoa taarifa ya ujenzi wa Zahanati hiyo alisema mradi huo ulibuniwa mwaka 2014 na upo Kijiji cha Issuna 'A'

Alisema zahanati hiyo ikikamilika itatoa huduma kwa wananchi wa vijiji vitano vya Issuna 'A, Issuna 'B', Ng'ongosoro, Nkuhi na Tumaini na kuwa ujenzi wake upo katika hatua za mwisho kukamilika.

Mahava alisema kuwa walipokea Sh.50 Milioni kutoka Serikali kuu na ununuzi wa vifaa vyote umefanyika na tayari Wizara ya Fedha imetenga Sh.8 Milioni kwa ajili ya dawa na vitendanishi.

Hata hivyo kamati hiyo imeomba hatua za haraka zichukuliwe ili kuharakisha ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo ambao bado mradi wake unasuasua kutokana na changamoto za kifedha -kutokana na umuhimu wake mkubwa kwa idadi kubwa ya watu wanaozunguka wilaya hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge akizungumza baada ya kukamilika kwa ziara hiyo aliwashukuru wakurugenzi na wakuu wote wa wilaya zote kwa kusimamia miradi hiyo.

"Niwashukuru wakurugenzi wote na wakuu wa wilaya kwa umoja wenu na kusimamia miradi hii ambayo inatumia fedha nyingi kutoka Serikalini,".  alisema Mahenge.

Akizungumzia mradi wa maji wa Kipumbuiko Dkt. Mahenge aliwata wahusika kutoangalia faida zaidi badala yake wazingatie utoaji wa huduma kwa wananchi na kuutunza.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro aliishukuru kamati hiyo na akatumia nafasi hiyo kuelezea mikakati ya maendeleo ya wilaya hiyo hususani katika sekta ya kilimo hasa cha zao la alizeti na mpunga ambao unalimwa kwa wingi maeneo ya Iyumbu.

Alitaja eneo lingine watakalo liangalia ili kupata mapato ni kwenye madini, ufugaji wa nyuki na miradi mingine.

Kamati hiyo katika wilaya hiyo ilikagua mradi wa ujenzi wa madarasa mawili na ofisi moja Shule ya Sekondari Ikungi, ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Msingi Ikungi, ukamilishaji wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo, ujenzi wa mradi wa maji Kipumbuiko, ujenzi wa matundu saba ya vyoo Zahanati ya Puma, ufugaji wa nyuki  (Kikundi cha Save The Bee Issuna, ukamilishaji wa ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Issuna, ujenzi wa Chuo cha Ufundi cha VETA na ukamilishaji wa ujenzi wa maabara Shule ya Sekondari Ikungi.

Friday, August 20, 2021

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AIPONGEZA BOHARI YA DAWA (MSD)



Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD)’ Meja Jenerali Dkt. Gabriel Saul Mhidze. akiwa ameongozana na Waziri wa Afya wa Zanzibar Mhe. Nassor Ahmend Mazrui wakati akimkaribisha  alipotembelea Bohari hiyo jana kujionea shughuli mbalimbali inazozifanya,

Waziri wa Afya wa Zanzibar Mhe. Nassor Ahmend Mazrui akipokea sampuli ya bidhaa za afya zinazo zalishwa na Bohari ya Dawa (MSD) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD’ Meja Jenerali Dkt. Gabriel Saul Mhidze.

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, akipokea maelezo ya uzalishaji wa dawa kutoka kwa mtaalamu wa Kiwanda cha dawa cha MSD- Keko (Keko Pharmaceutical)

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui,akiangalia uzalishaji wa Barakoa katika kiwanda hicho.
Msimamizi wa Kiwanda cha Barakoa cha MSD. Bw. Twahil Magooro, akitoa Maelezo ya mchakato wa uzalishaji Barakoa mbele ya Waziri wa Afya Zanzibar.


Na Mwandishi, Wetu

WAZIRI wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mzrui ameipongeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa hatua kubwa iliyochukua katika kuanzisha viwanda nchini, kwani itasaidia katika kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya nchini sambamba kuboresha afya za wananchi.

Mhe. Mazrui ametoa pongezi hizo leo tarehe 20/8/2021 baada ya kutembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa yaliyoko Keko jijini Dar es Salaam, ili kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na Bohari hiyo, mathalani mipango yake ya uzalishaji wa dawa na vifaa tiba.

“Nimevutiwa na hatua za MSD kuamua kuzalisha bidhaa za afya yenyewe, Mkurugenzi Mkuu na Menejimenti ya MSD nawapongeza sana, Sisi kama Serikali ya Mapinduzi Zanzibar tutaangalia namna tunaweza kushirikiana ili kupanua wigo wa kuboresha huduma za afya. Kiukweli naichukulia MSD kama sehemu ya Wizara ya Afya Zanzibar, “. alisema Mhe. Mazrui.

Katika hatua nyingine Mhe. Mazrui ametembelea viwanda vya MSD ikiwa ni pamoja na Keko Pharmaceuticals na kiwanda cha kuzalisha barakoa na kujionea hatua mbalimbali zilizofikiwa katika uzalishaji, na baadae alitembelea Kanda ya Dar es Salaam huku akipongeza uongozi kwa kazi kubwa zinazofayika na kuwataka kuendelea kujituma ili kuboresha sekta ya afya.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Meja Jenerali Dkt.Gabriel Saul Mhidze ameeleza jitihada mbalimbali alizozifanya toka ateuliwe kushika wadhifa huo, kwani zimesaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha huduma za afya nchini. 

“Toka nimeteuliwa tumeshirikiana vizuri na Menejimenti yangu kwa pamoja tumejitahidi kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba nchini, ujenzi wa viwanda na mageuzi ya kiutendaji, ninayo Imani kubwa kwamba siku si nyingi, ile adhima ya serikali ya kuboresha afya ya kila mtanzania inaenda kutimizwa kwa kiasi kikubwa kufuatia mageuzi makubwa tunayofanya” alisema Mhidze.

Aidha ameongeza kuwa, ifikapo mwezi wa 10 mwaka huu, Kiwanda cha Mipira ya Mikono, na pamoja na viwanda vingine vya dawa, vinavyojengwa Makambako mkoani Njombe vitaanza kufanya kazi, hivyo kuboresha huduma za upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

Ameongeza kuwa, kwa dawa na vifaa tiba ambavyo uchakataji wake ni mgumu, tayari MSD imenza kuingia mikataba ya ubia na wazalishaji wa huduma hizo, lengo likiwa ni kupunguza gharama za upatikanaji wa huduma hizo nchini, na kuleta unafuu kwa mwananchi wa kawaida ambalo ndio lengo hasa la serikali.

Thursday, August 19, 2021

KAZI NZURI YA MIRADI WILAYA YA MANYONI NA ITIGI YAKONGA NYOYO ZA WAJUMBE WA KAMATI YA SIASA MKOA WA SINGIDA.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Binilith Mahenge (kushoto) na viongozi wengine wakikagua mradi wa maji wa Kintinku Lusilile uliopo Manyoni mkoani hapa wakati Kamati ya Siasa ya mkoa huo ilipo kuwa ikikagua miradi hiyo jana.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge akipanda kukagua mradi wa maji wa Kintinku Lusilile uliopo wilayani  Manyoni.
Muonekano wa tenki la maji mradi wa maji Kintinku Lusilile uliopo wilayani  Manyoni.
Ukaguzi wa mradi wa maji Kintinku Lusilile uliopo wilayani  Manyoni ukiendelea.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Alhaji Juma Kilimba akizungumza wakati wa ukaguzi huo.

Ukaguzi wa madarasa Shule ya Msingi Heka ukiendelea.
Muonekano wa Vyoo vipya vilivyojengwa Shule ya Msingi Heka.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Heka Zamoyoni Mgumba akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa madarasa mawili.
Diwani wa Kata ya Heka, Haruna Thomas akizungumza wakati wa ukaguzi huo.
Ukaguzi wa mradi wa maji Kijiji cha Kitopeni Wilaya ya Itigi ukiendelea.
Meneja wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira (RUWASA) Wilaya ya Manyoni Mhandisi Gabriel Ngongi akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi wa maji  Kijiji cha Kitopeni uliopo Wilaya ya Itigi.
Taarifa ya ujenzi wa mradi wa maji  Kijiji cha Kitopeni ikitolewa,
Ukaguzi wa madarasa yaliyojengwa Shule ya Sekondari ya Itigi ukiendelea.

Taarifa ya ujenzi wa madarasa, Shule ya Sekondari Itigi ikitolewa.

Muonekano wa madarasa ya  Shule ya Msingi Mlowa yaliyojengwa.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mlowa, Isaya Ntandu akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa madarasa mawili.


Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida Diana Chilolo akichangia jambo kwenye ukaguzi wa Kituo cha Afya cha Chibumagwa.
Ukaguzi wa moja ya jengo la kituo cha Afya Chibumagwa ukiendelea.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida, Davis Nyiraha akizungumza wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa madarasa mawili ya Shule ya Msingi Mlowa iliyopo Itigi.


Na Dotto Mwaibale, Singida


KAZI nzuri ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na Itigi imekonga nyoyo za wajumbe wa Kamati  ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida wakati walipokuwa wakikagua miradi hiyo.

Miradi hiyo imetekelezwa na halmashauri hizo kwa wakati baada ya kupatiwa fedha na Serikali ili kujenga miundombinu ya maji, ujenzi wa zahanati, miradi ya maji, madarasa na maabara.

Wajumbe hao wakizungumza kwa nyakati tofauti jana wakati wakikagua miradi hiyo walisema wameliridhishwa na utekelezaji wake licha ya kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo.

Akizungumzia miradi hiyo Mjumbe wa Kamati hiyo Diana Chilolo alisema kazi kubwa imefanyika katika kutekeleza miradi hiyo katika wilaya zote hizo mbili.

"Tumetembelea miradi mbalimbali na tumeridhishwa na utekelezaji wake na kujenga imani kwa Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ," alisema Chilolo..

Mjumbe wa kamati hiyo Yohana Msita alisema miradi mingi iliyotekelezwa imelingana na fedha halisi walizopewa  na Serikali.

"Watekelezaji wa miradi hii wameonesha uaminifu mkubwa wa matumizi ya fedha walizopewa kwa ajili ya kuitekeleza," alisema Msita.

Martin Lissu mjumbe wa kamati hiyo alisema kasoro ndogo ndogo ambazo zimejitokeza wakati wa kujenga maabara katika baadhi ya shule za sekondari kama kuweka nondo kwenye madirisha na milango kufungukia ndani badala ya nje kwa ajili ya tahadhari ya majanga ya moto wametoa ushauri wa kuzirekebisha.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Alhaji Juma Kilimba alisema miradi hiyo inafanywa ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

 Kilimba  alisema ameridhishwa na utekelezwaji wa miradi hiyo iliyofanywa katika halmashauri hizo.

"Kwa kweli tunawapongeza kwa kuitendea haki miradi hii ambayo Serikali inatumia fedha nyingi kuitekeleza," alisema Kilimba.

Kilimba alitumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi ilipo miradi hiyo kuwahamasisha wananchi wao kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii badala ya kuisubiri Serikali.

Alisema Serikali inafanya kazi kubwa ya kutoa fedha za miradi na ni wajibu wa wananchi nao kuhamasika kuunga jitihada za serikali kwa kujitolea kufanya kazi zingine za maendeleo ambazo zipo ndani ya uwezo wao.

Aidha Kilimba akizungumza kwa nyakati tofauti aliwataka wananchi na viongozi waliofika kushuhudia ukaguzi huo kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa wa corona.

Aliwaomba wananchi kila ilipotekelezwa miradi hiyo kuitunza ili iendelee kuwa na manufaa kwao.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge aliomba miradi ambayo bado haijakamilika ikamilike haraka ili wananchi waanze kunufaika nayo kwani imetumia fedha nyingi kutoka Serikalini.

Miradi iliyokaguliwa na kamati hiyo katika Wilaya ya Manyoni ni ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Msingi Heka, ujenzi wa mradi wa maji Kintinku Lusilile, ukamilishaji wa maabara Shule ya Sekondari Mlewa, kutembelea mradi wa Kilimo cha umwagiliaji Kata ya Chikuyu na kuona changamoto ya mfumo wa maji kuacha njia badala  ya kwenda kwenye mashamba yana elekea maeneo mengine kutokana na mafuriko na ujenzi wa Kituo cha Afya Chibumagwa.

Katika Wilaya ya Itigi miradi iliyotekelezwa ni ukamilishaji wa maabara na vyoo Shule ya Sekondari Itigi,  ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa  Shule ya Msingi Mlowa na ujenzi wa mradi wa maji wa Kijiji cha Kitopeni. 

 Ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi hiyo iliwahusisha viongozi na wataalamu mbalimbali wa wilaya hizo. 

Leo kamati hiyo itahitimisha  ziara yake  kwa kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.