Mwakilishi wa Benki ya Dunia
nchini Bi. Xiayon Liang (kulia) akipata maelezo wakati wa ziara ya siku moja ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Kuendeleza
Ujuzi (SDF) unaoendeshwa na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia na kuratibiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Wa pili
kulia ni Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi Bahati Geuzye.
Thursday, September 23, 2021
WAWAKILISHI WA BENKI YA DUNIA (WB) WATEMBELEA MIRADI YA KUENDELEZA UJUZI JIJINI DAR ES SALAAM
RAIS SAMIA AMWAGA MABILIONI UJENZI WA OFISI ZA SANAA NA MICHEZO
Katibu Mkuu wa Sanaa, utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi akionesha picha ya jenhgo jipya la Wizara hiyo mara baada ya kusaini Mkataba wa ujenzi wa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Septemba 22,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Sanaa, utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi(kulia) wakikabidhiana Mikataba ya Ujenzi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani.
Picha ya pamoja baina ya Katibu Mkuu na Menejimenti ya Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo katika pamoja na viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)
……………………………………………………………………………
Na John Mapepele- WSUM, Dodoma
Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kujengewa jengo la TZS Bilioni 22.843 makao makuu jijini Dodoma na mkataba wa ujenzi tayari umesainiwa kati ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani.
Akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji saini Septemba 22, 2021 jijini Dodoma, Dkt. Abbasi amesema jengo hilo litakuwa na ofisi za kisasa pamoja zenye mahitaji yote yanayohusika katika sekta za Sanaa, Utamaduni na Michezo.
“Hakika hii ni thamani kubwa kwa sekta hizi na jengo hili ni la kwanza kubwa na la thamani zaidi na kali zaidi tangu kuasisiwa kwa sekta hizi kabla na baada ya Uhuru”. Amefafanua Dkt Abbasi
Aidha, Dkt. Abbasi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa jengo hilo ambapo amesema Mhe. Rais amefanya maamuzi magumu na makini katika kuboresha sekta hizi ambazo ni nguvu laini ya nchi.
Ameongeza kuwa tayari serikali imetenga fedha hizo na zitatolewa kulingana na taratibu za Serikali ambapo linatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24 sawa na miaka miwili kuanzia sasa.
Amewahimiza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambao ni watekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo pamoja Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambao ni wasanifu na wabunifu wa majengo hayo kukamilisha mradi huo kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa kwa kuwa wao ni mabingwa na wameaminiwa kwa uzoefu wao katika masuala ya ujenzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani ameishukuru Wizara na Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwaamini na kuwapa kazi ya ujenzi wa majengo ya Serikali kwa kuwa waliomba na wamepewa kazi hiyo na kuahidi kuitekeleza kwa ubora na kwa wakati kama ilivyopangwa kulingana na bajeti waliyopewa.
Naye Katibu wa Kuratibu Serikali Kuhamia Dodoma Bw. Meshaki Bandawe amesema Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo inakuwa Wizara ya nane kukamilisha taratibu za utiaji wa Saini Mkataba wa ujenzi ambapo ameipongeza kwa hatua hiyo.
Amefafanua kuwa mpango wa Serikali kuhamia Dodoma umerahisisha wizara kuwa na majengo yao na zipo katika eneo moja hatua inayorahisisha wananchi kupata huduma kwa wakati.
Bw. Bandawe ameongeza kuwa majengo ya Wizara yanayojengwa katika awamu ya pili yapo 24 ambapo hadi sasa Wizara nane ikiwemo ya Sanaa, Utamaduni na Michezo zimekamilisha taratibu za ujenzi huo, hivyo zimetekeleza agizo la Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alilotoa Septemba 08, 2021 la Wizara zote zikamilishe taratibu za ujenzi wa awamu ya pili ifikapo Septemba 30, 2021.
Wednesday, September 22, 2021
RC SINGIDA AITISHA KIKAO KUNUSURU MRADI WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI ITAGATA ITIGI
Afisa Kilimo Wilaya ya Itigi Mkinguzi Mgalula akitoa taarifa ya mradi huo kwa mkuu wa mkoa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi John Mgalula akizungumza katika ziara hiyo.
Na Dotto Mwaibale, Itigi.
MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge ameagiza uongozi wa wilaya ya Itigi kuitisha kikao cha viongozi wa Kijiji cha Itagata, wananchi na wadau wa kilimo ili kunusuru mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa kijiji hicho ambao Serikali ilitoa Sh. 2 Bilioni kwa ajili ya kuanzisha mradi huo ulioridhiwa na wananchi lakini haufanyi kazi kwa sababu mbalimbali.
Dkt.Mahenge alitoa agizo hilo jana wakati alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi na kuzungumza na wananchi.
" Ninaagiza muitishe kikao hicho haraka sana na mimi mwenyewe nitakuja, nilipokuwa nasikiliza takwimu za mradi huu za Sh.2.1 Bilioni za ambao haufanyi kazi nimesikitika sana kwani kuna maeneo wanalia kukosa fursa ya namna hiyo nawaambia kwa uvivu wenu huo mtaendelea kulalamika na kuwa maskini ". alisema Mahenge.
Alisema baada ya kikao hicho ndipo watakapoamua kuona cha kufanya ikiwa ni pamoja na kuwapatia mashamba hayo watu wengine wenye uwezo ya kuyaendeleza baada ya wananchi wanachama wa kilimo cha umwagiliaji waliopewa kushindwa kuyafanyia kazi.
Afisa Kilimo Wilaya ya Itigi Mkinguzi Mgalula akitoa taarifa ya mradi huo kwa mkuu wa mkoa alisema mradi wa kilimo cha umwagiliaji Itagata una jumla la eneo la hekta 160 linalofaa kwa kilimo sawa na ekari 400 na kuwa eneo linalofikiwa na miundombinu ya umwagiliaji ni hekta 83.6 sawa na ekari 209.
Alisema mradi huo ni matokeo ya wazo lililobuniwa na wananchi wa kijiji hicho wakati wa zoezi la kubaini fursa na vikwazo vya maendeleo na hatimaye kuingizwa kwenye mpango wa maendeleo ya kilimo cha Kijiji cha Itagata mwaka 2008/ 2009.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kuhusu mradi huo ambao umekwaka kuendelea viongozi mbalimbali wananchi na wadau wengine waliunga mkono agizo la mkuu wa mkoa la kuitisha kikao hicho ili kitoe maamuzi ya kuyachukua mashamba hayo na kuwapa watu wengine ambao watakuwa na uwezo ya kuyaendeleza.
Baadhi ya viongozi waliotoa maoni hayo ni pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji cha Itagata Salum Mbesi, Diwani wa Kata hiyo Martin Kapona, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni Jumanne Muhanda, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo pamoja na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho akiwepo Makamo Mwenyekiti wa Umoja wa Kilimo hicho cha umwagiliaji Itagata, Rashid Mfaume, Zena Matonya na Mussa Lupia.
Walitaja baadhi ya sababu za mradi huo kukwama ni uvivu, ubinafsi na watu kukumbatia mashamba ambayo wanashindwa kuyaendeleza huku wengine wakiyakodisha kwa bei kubwa.
Mussa Lupia alisema Tume ya Taifa ya Umwagiliaji itoa kipaumbele kwa kuwapa kwanza mashamba wananchi wa kijiji hicho walioibua mradi huo lakini wameshindwa kuyaendeleza hivyo analiunga mkono wazo la mkuu wa mkoa la kuitisha kikao hicho ili kitoe maamuzi ya kuwapa watu wengine watakaokuwa na uwezo wa kuyaendeleza kutoka ndani ya kijiji hicho na nje.
Katika ziara hiyo Dkt.Mahenge alitembelea Hospitali ya St Gaspar iliyopo Itigi mjini na kuona huduma kubwa za matibabu zonazofanyika zikiwemo za upasuaji na akatoa wito kwa wananchi mbalimbali kutoka mikoa jirani na Singida kwenda kupata huduma za upasuaji na matibabu mengine badala ya kukimbilia Hospitali zingine kubwa za hapa nchini na kutumia gharama kubwa ambapo pia alizungumza na Viongozi na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi na kusisitiza ukusanyaji wa mapato na kutenga asilimia 10 ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Tuesday, September 21, 2021
JITIHADA ZINAHITAJIKA KUNUSURU BONDE LA MTO RUFIJI NA FAIDA ZAKE KIUCHUMI
Mratibu wa Utafiti na Machapisho kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA na Mkuu wa Mradi wa UMFULA Prof. Japhen Kashaigili akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu Matokeo ya utafiti huo mara baada ya kumaliza kuyawasilisha kwa wadau wote waliohudhuria kwa njia mbalimbali duniani ikiwemo Zoom.
Na Calvin Gwabara, Iringa
WADAU wa Bonde la Mto rufiji wametakiwa kuendelea kujizatiti katika kudhibiti shughuli za kibinadamu ambazo zinachangia katika kuharibu mtiririko wa maji ili kuepukana na athari zinazoweza kutokea na kuathiri mahitaji ya maji ya wadau wote wanaotegemea maji hayo.
Wito huo umetolewa na Prof. Japhet Kashaigili ambaye ni Msimamizi na Mratibu wa Mradi wa utafiti wa kutathimini ya mabadiliko ya tabia nchi kwenye bonde la mto Rufiji na kuangalia athari zake katika mtiririko wa maji na utengenezaji wa vielelezo vya kusaidia kupanga mipango ya kimaendeleo katika bonde hilo (UMFULA) wakati wa Mkutano wa kuwasilisha matokeo ya mwisho ya Utafiti huo na kufunga mradi.
“ Kutumia Modeli 34 zinazotumiwa na IPCC zimeonesha kuwa mfumo wa mvua ni wa kubadilika sana na kwamba huko mbeleni kunaweza kuwepo kwa mvua nyingi au mvua chache hasa kwenye maeneo ya kusini mwa Bonde hilo hivyo taarifa hizi zinaisaidia nchi katika kujipanga ikitokea mvua zimeongezeka nini kifanyike na zikipungua nini kifanyike na hivyo mradi umeainisha mambo ya kufanya katika hayo yote” Alifafanua Prof. Kashaigili.
Aliongeza “ Lakini kubwa kabisa tunaangalia Mvua ikipungua nini kifanyike maana sasa hivi tunatambua nchi ipo katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama vile Mradi wa umeme wa Mwl Nyerere ( JNHPP) hivyo ni lazima kuwe na mipango ya kuhakikisha kunakuwa na maji ya kutekeleza mradi huo ili uweze kuzalisha umeme kama ulivyopangwa hivyo Modeli hizo zinazoonyesha kunaweza kuwa na upungufu wa mvua zinatupa kiashiria cha kuweza kujipanga zaidi”.
Amesema kuwa pamoja na matokeo hayo ya kupanda au kushuka kwa mvua lakini matokeo ya jumla yanaonesha kuna kila sababu ya wadau wote kujipanga katika kukabiliana na hali hiyo hasa kutokana na viashiria vikubwa kabisa kuonesha vinatokana na shughuli za kibinadamu hasa maeneo ambayo kuna ukataji mkubwa wa miti.
“Tumeona maeneo yaliyokatwa miti sana mvua zikinyesha maji yanakaa kwa muda mfupi na kukauka na hii maana yake ni kwamba kipindi cha kiangazi ambapo maji yanahitajika kuwepo ili kutunza baionuai kwenye mito na kuwezesha mabwawa kuendelea kupata maji yanayoingia kupungua hivyo jitihada lazima zifanyike ili kuendeleza mtiririko huo wakati wote kwa kutunza maeneo yote ya bonde.
Mratibu na Msimamizi huyo wa Mradi huo wa Utafiti upande wa Tanzania ameongeza kuwa kupitia Modeli hizo wameona pia kuwa kuna uzalishaji mkubwa wa mchanga unaoingia kwenye maeneo ya mabwawa kwa sababu maeneo mengi ya dakio hilo au Bonde yenye ardhi oevu ambazo husaidia kupunguza mchanga usiende kwenye mabwawa zimelimwa na kubadilishwa matumizi hivyo utafiti huo pia umeeleza kinachopaswa kufanyika ili kunusuru mabwawa ya kuzalisha Umeme kujaa mchanga.
Prof. Kashaigili amesema matokeo mengine waliyoyapata ni kwenye kuangalia upunguaji wa maji kwa sasa na tangu kuanzishwa kwa vituo vya kupimia maji miaka 40 iliyopita wamebaini kuwa mabadiliko sio makubwa lakini tofauti inaonekana wakati wa kiangazi kwamba maji yanaendelea kupungua kadri siku zinazoenda hali ambayo haikuwepo zamani nankiashiria kikubwa na hali iliyopo sasa kwenye Mto Ruaha Mkuu kukauka Mara kwa mara kuanzia miaka ya 1990.
“ Pia swala la ugawaji wa maji ni swala muhimu ambalo linahitaji kuwa na vifaa maalumu wa kuwezesha kufanya ugawaji kwa usahihi na Mradi umeweza kutengeneza Modeli nzuri na ya kisasa ambayo itapatikana kwenye mtandao na hii itasaidia watu wa Bonde kugawa maji kwa utaratibu mzuri ili kupunguza changamoto za ugawaji wa maji bila kufanya tathimini kwanza na hii itasaidia maeneo mengi hata wizara na tutaendelea kuifanya iwe rahisi zaidi kutumia wadau” Alieleza Prof. Kashaigili.
Akizungumzia faida za matokeo ya utafiti huo Mkurugenzi wa Bodi ya maji ya Bonde la Mto Rufiji Mhandisi Florence Mahay amesema yanawasaidia katika kufanya maamuzi na kupanga mikakati ya namna ya kutekeleza majukumu yao na kuwa na mipango endelevu ya matumizi ya Bonde hilo ambalo asilimia 80% ya umeme wa maji unategemea bonde hilo katika maji kuzalisha umeme.
“50% ya maeneo ya kilimo yanayomwagiliwa yapo katika bonde la mto Rufiji kwahiyo ni muhimu kujua kama upatikani wa maji katika maeneo hayo kutaathirika na mabadiliko ya tabia nchi basi ni kwa namna gani na kiasi gani na hasa hayo mabwawa ambayo yakikosa maji yataathiri uchumi wa nchi sambamba na maeneo yaliyohifadhiwa kama vile hifadhi za taifa” Alisema Mhandisi Mahay.
Mkurugenzi huyo amesema changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni namna ya kuweka uwiano kati ya kilimo na miradi ya umeme kwani Miradi ya Umeme ipo chini wakati Kilimo kinafanyika juu ingawa Mradi wa umeme hauli maji kama kilimo bali ubayatumia tu na kuyaacha yatiririke lakini inazuia Miradi ya kilimo inayotumia maji ambayo ipo juu kutotumia maji hayo ili yafike kwenye mabwawa kwa wingi.
“ Tunaendelea sasa kuhamasisha Miradi mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji ifanyike chini baada ya miradi ya Umeme ili kuweza kutumia maji ambayo yanatoka kwenye miradi ya umeme nankutiririka bila matumizi na kwenda Baharini hii itaongeza tija maana maji yanakuwa mengi yanakwenda bure au kutumiwa kidogo sana kwa kilimo” Alibainisha Mkurugenzi wa Bodi ya Maji ya Bonde Mhandisi Mahay.
Mradi huo wa miaka mitano umefanikiwa kusomesha wanafunzi kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili na Uzamivu, Kutengeneza Modeli mbili pamoja na kuzalisha machapisho mbalimbali ya kisayansi na Majarida na Taarifa mbalimbali zkwa lugha rahisi kwaajili ya Wadau wote hasa Wakulima.
DKT. MAHENGE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MANYONI AWAPONGEZA WANANCHI
Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Binilith Mahenge (katikati) akikata
utepe kuashiria ufunguzi wa Zahanati ya
Kijiji cha Maweni wilayani Manyoni
katika Hafla iliyofanyika kijijini hapo jana wakati wa zaira yake ya kukagua miradi ya maendeleo. Wengine ni viongozi
mbalimbali wa wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa akizungumza wakati wa hafla ya kuwakabidhi
vifaa vijana Wajasriamali walivyowezeshwa na Shirika la Compassion International
Tanzania (CIT)
Dkt. Mahenge akimkabidhi Kadi ya Bima ya Afya iCHF
iliyoboreshwa Mzee Godwin Nguluga.
Makabidhiano yakiendelea.
Makabidhiano yakiendelea.
Makabidhiano yakiendelea.






















