Thursday, October 21, 2021

WIZARA YA KILIMO YAWEKA MKAZO KWENYE KILIMO HAI NCHINI

Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akifungua mkutano wa pili wa Kilimo Hai unaofanyika Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa TOAM,Dkt. Mwatima Juma akitoa neno  la ukaribisho kwa wajumbe na waalikwa wa mkutano huo.

Waziri wa Kilimo,Umwagiliaji na Mifugo  wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Soud Hassan akitoa salamu za Zanzibar katika matumizi ya Kilimo Hai.

Wadau wa Kilimo Hai kutoka mikoa yote ya Tanzania nan je ya Tanzania wakifuatilia mawasilisho na ufunguzi wa mkutano huo.

Mkutano ukiendelea.
Wadau wa Kilimo Hai kutoka mikoa yote ya Tanzania nan je ya Tanzania wakifuatilia mawasilisho na ufunguzi wa mkutano huo.

Mkutano ukiendelea.
Wadau wa Kilimo Hai kutoka mikoa yote ya Tanzania nan je ya Tanzania wakifuatilia mawasilisho na ufunguzi wa mkutano huo.


Mkutano ukiendelea.
Wadau wa Kilimo Hai kutoka mikoa yote ya Tanzania nan je ya Tanzania wakifuatilia mawasilisho na ufunguzi wa mkutano huo.

Wadau wa Kilimo Hai kutoka mikoa yote ya Tanzania nan je ya Tanzania wakifuatilia mawasilisho na ufunguzi wa mkutano huo.

Mkutano ukiendelea,
Wadau wa Kilimo Hai kutoka mikoa yote ya Tanzania nan je ya Tanzania wakifuatilia mawasilisho na ufunguzi wa mkutano huo.


Na Calvin Gwabara - Dodoma


NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe  amewaahidi wadau wa Kilimo Hai nchini kuwa anakwenda kuanzisha Kitengo maalumu kwenye Wizara hiyo badala ya dawati lililopo sasa ili kuongeza msukumo utakaosaidia kukua kwa Kilimo hai ili kuchangia kuleta tija kwa Taifa tofauti na ilivyo sasa.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizfungua Kongamano la pili la kitaifa la Kilimo hai lililowakutanisha wadau wote kutoka ndani na nje ya Tanzania likijumuisha Wizara ya Kilimo,Mbalozi wa nchi mbalimbali,Wakulima wa Kilimo hai na wasndikaji,Mashirika ya Kimataifa,Sekta binafsi,Taasisi mbalimbali za Utafiti linalofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma.

“Najua kuwa kwa sasa pale wizarani tunalo dawati linaloshughulikia masuala mbalimbali ya kilimo Hai lakini kwa kutambua umuhimu wa kilimo hiki nawaahidi kuwa nakwenda kuanzisha Kitengo maalumu na sio dawati tena ambalo nguvu yake inaonekana sio kubwa na ninamini kupitia kitengo hiki kitasaidia kuweza kufikia malengo tnayoyakusudia”Alisema Mhe. Bashe.

Naibu Waziri huyo wa Kilimo amesema duniani kwa sasa watu wamekuwa wanzingatia sana swala la afya kutokana na vyakula wanavyokula lakini pia mazao yatokanayo na kilimo Hai yanabei nzuri kuliko yae mengine yasiyo ya kilimo hai hivyo kama wizara lazima ihamasishe na kuhimiza ukuaji wa Kilimo hai Nchini.

Bashe amesema pamoja na jitihada hizo ambazo Wizara yake inakwenda kuzichukua lakini pia kwa kushirikiana na wadau hao amedhamiria kuanzisha benki ya mbegu za asili nchini ambayo itakuwa na kila aina ya mbegu nzuri ambazo wazee wamekuwa wakizutumia kwa miaka mingi ambazo zitasafishwa vizuri ili ziweze kurudishwa mashambani.

 “Namuagiza mkurugenzi wa TARI nchini kama anavyohangaika kufanya tafiti za mbegu,mbolea na madawa sasa nataka awe na kitengo maalumu cha utafiti ambacho kitakuwa kinashughulika na maswala ya kilimo hai nchini kwa upana wake” aliagiza Bashe.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa TOAM,Dkt. Mwatima Juma alisema wakati sasa hivi kwenye kongamano hili hawazungumzii tena kuwa na kilimo hai bali wanazungumzia sasa nini kifanyike maana kuendelea na malumbano ya kufaa kwa mbolea na chumvichumvi na kutofaa au kuzungumzia dawah ii na ile ni jambo ambalo halikipeleki mbele kilimo hai nchini .

“Sasa hivi kote duniani imeshafahamika kwamba matatizo ya tabia nchi,matatizo ya kiuchumi,matatizo ya ajira yote yanatokana na mfumo usiofaa wa kupeleka mbele swala zima la kilimo hai kwahiyo tujaribu kuona ni namna gani na kuweka mkakati wa namna ya kuweka mfumo mwingine” alisisitiza Dkt. Mwatima.

Aliongeza Hivi sasa mkutano mzima utasikia mamswala ya tumefanikiwa wapi, nini kifanyike kupanuka zaidi kwa sababu kuna swala zima la utafiti,swala zima la Siasa ambayo yote yanatakiwa yaende sambamba ili kuona mambo ya kilimo endelevu na kilimo hai kinapofika.

“Sababu kubwa ya mimi binafsi ya kutaka tuelekee huko ni sababu ya kiafya kwani afya zetu zinaharibika sana kutokana na mfumo wa uzalishaji ambao umeharibika kwahiyo tunauchimbua kutoka kule ili tuweze kurekebisha maswala ya afya ili kupunguza matumizi ya rasilimali zetu kwenye matibabu, Tuna swala la mazingira,tuna swala la mabadiliko ya tabia nchi pamoja na swala la uchumi wa nchi,swala la kupatikana soko kwa mazao yetu,kuongeza thamani ya amzao yetu ambayo hapo utaona kuna kuongeza ajira kwa vijana” alibanisha Dkt. Mwatima.

Waziri wa Kilimo,Umwagiliaji na Mifugo  wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,  Soud Hassan alisema hivi sasa karibia asilimia 60 ya mazao ya Zanzibar ni Kilimo Hai maana walikuwa wakilima hivyo kwa muda mrefu bila kutambua kuwa ni kilimo Hai.

“Kama mnavyojua kuwa Zazibar tunalima sana viungo na kinawaingizia wakulima wetu fedha nyingi sana na kusaidia katika uchumi wao na Serikali lakini lazima tuseme ukweli kuwa kilimo Hai wafadhili wakubwa ni watu kutoka nje lakini niwahakikishie kuwa nitakaporudi Zanzibar wakati wa bajeti naiweka kilimo hai kwenye bajeti hiyo kwa lengo la kuendeleza kilimo hiki” alisisitiza Hassan.

Kongamano hilo la pili la Kilimo Hai linafanyika jijini Dodoma likiwa na kauli mbiu isemayo Kuchochea kilimo hai kwa mfumo endelevu ya Chakula.

WATAKAOCHEZEA RASILIAMLI ZA MISTU KILOSA MKOANI MOROGORO KUKIONA CHA MOTO

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaji Majid Hemed Mwanga (Katikati) akizungumza kwenye ziara hiyo katika Kijiji cha Kitunduweta .Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtedaji wa wilaya Kisena Mabula kushoto kwake ni Mwenyekiti Wa Halmashauri hiyo Mhe. Wilfred Sumari.

Meneja wa Mradi wa Mkaa endelevu, Charles Lyimo akieleza malengo ya Mradi huo mbele ya viongozi wa wilaya na madiwani.

Katibu wa kamati ya maaliasili ya Kijiji cha Kitunduweta, Leoti Msoloka aliyevaa nguo za kijani akieleza mafanikio ya mradi na namna wanavyofanya shughuli za uvunaji.
Katibu wa wachoma Mkaa katika Kijiji cha Kiotunduweta,Kulangwa Ganga akieleza namna wanavyopata eneo na wanavyochoma Mkaa kupitia matanuri hayo ya kisasa waliyofundishwa ya kuchomea mkaa.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaji Majid Hemed Mwanga akiwa amesimama juu ya Tanuri la mkaa ambalo linaendelea kupangwa.
Madiwani pamoja na viongozi wengine walioshiriki ziara hiyo wakifuatilia maelezo ya utekelezaji wa mradi pamoja na kuuliza maswali ili kupata ufafanuzi Zaidi kuhusu namna wanavyonufaika na mfumo huo.
Madiwani pamoja na viongozi wengine walioshiriki ziara hiyo wakifuatilia maelezo ya utekelezaji wa mradi pamoja na kuuliza maswali ili kupata ufafanuzi Zaidi kuhusu namna wanavyonufaika na mfumo huo.
Ziara ikiendelea.
Madiwani pamoja na viongozi wengine walioshiriki ziara hiyo wakifuatilia maelezo ya utekelezaji wa mradi pamoja na kuuliza maswali ili kupata ufafanuzi Zaidi kuhusu namna wanavyonufaika na mfumo huo.
 

Na Calvin Gwabara, Kilosa


MKUU wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro Alhaji Majid Hemed Mwanga amesema wilaya yake haitamvumilia wala kumfumbia macho kiongozi au Mwananchi yeyote atakayecheza na rasilimali za Misitu kwa kufanya kinyume na utaratibu uliowekwa kwenye vijiji vilivyo chini ya mpango wa usimamizi shirikishi wa Misitu ya Vijiji na vile ambavyo bado havijaingia kwenye mpango huo.

Wito huo ameutoa wakati wa ziara aliyoifanya na kamati ya Ulinzi Usalama,Madiwani na viongozi wa Mashirika ya TFCG na MJUMITA katika Kijiji cha Kitunduweta wilayani humo  ili kujionea namna mashirika hayo yanavyotekeleza mapango wa isimamizi shirikishi wa misitu kwenye vijiji 20 vya Wilaya hiyo na kusikia shuhuda na mafanikio na kazi kubwa zilizofanywa na mashirika hayo katika kufikia mafanikio hayo.

”Kwakweli kazi kubwa sana imefanywa na wadau wetu Shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii usimamizi wa misitu Tanzania (MJUMITA) na sasa kazi iliyobaki ni sisi kuhakikisha elimu tuliyoipata inaednelea kuleta matokeo chanya katika kutunza misitu yetu, na niseme tu kwamba fedha nyingi mnapata kwenye vijiji lakini naomba mtambue kuwa fedha hizo ni fedha za Umma zitumike kwa kufuata taratibu zote za matumizi ya fedha za Umma na Ssio vinginevyo maana ninaz taarifa kuwa baadhi ya viongozi wanatumia fedha hizo vibaya na kuna vijiji kamati zake kama Kijiji cha Ihombwe imeivunja” Alisisitiza Alhaj Mwanga.

Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka Wananchi kwenye vijiji hivyo kutowafumbia macho viongozi wanaovuruga utaratibu mzuri ulioanzishwa bali watoe taarifa kwenye ofisi yake na mamlaka zingine ili washughulikiwe na kuwasisitiza kuendelea kuhifadhi misitu hiyo ya vijiji na kuitumia kwa uendelevu na kwa maslahi mapata ya vijiji na Taifa.

“Nyinyi sasa ni Walimu maana tumeona wenzenu kutoka kwenye Wilaya ya Ruangwa anakotoka Waziri Mkuu wetu walikuja kujifunza kutoka kwenye Kijiji chenu sasa tuache kulalamika na kunedelea kulilia mafunzo Zaidi maana tunataka sasa hawa wadau wahamie kwenye vijiji vingine kwenye wilaya yet una mikoa mingine ili elimu hii ifike nchi nzima, tunachotaka sasa ni kuona nyinyi mnasonga mbele kama walimu” Aliongeza Mkuu huyo wa wilaya ya Kilosa.

 Alhaj Mwanga amewataka kuacha kusikiliza maneno ya baadhi ya watu wanaokuja kuharibu misitu na kuharibu taratibu zilizowekwa wakisingizia kuwa ni maagizo kutoka kwa wakubwa na kuwataka waache kuwasiliza maana hauna maagizo yoyote yanayotoka juu kwenye kuharibu misitu na akitokea mtu huyo watoe taarifa haraka ili watu hao wakamatwe na kuchukuliwa hatua.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Kilosa amewasisitiza viongozi wa Kijiji na kamati za maliasili kila mmoja kutambua majukumu yake na kuacha kuingilia kwenye majukumu ili kuondaa migogoro isiyo ya lazima ambayo inatokana na hela wanazozipata kutokana na mapatoa yanayokusanywa kwenye tozo na fedha za misitu.

Akieleza malengo ya Mradi huo Meneja wa Mradi wa Mkaa endelevu Charles Lyimo amesema lengo kuu ni kuhifadhi Misitu ya vijiji kikamilifu kutokana na tafiti kuonesha kuwa kwa mwaka Tanzania tunapoteza hekta 460,000 za misitu kutokana na shughuli mbalimbali za uchomaji Mkaa, Kuni,Kilimo na Mbao na kiasi kikubwa cha upotevu huo kinafanyika kwenye ardhi za vijiji katika maeneo ambayo hayajahifadhiwa.

Ameongeza kuwa katika kufanikisha hilo Mradi unawezesha vijiji pamoja na Wilaya kuweza kuziwekea mpango bora wa kusimamia rasilimali hizo za mistu vizuri ili kunufaika nazo kama vijiji lakini pia Serikali kwa ujumla.

Meneja huyo wa Mradi amesema lengo la pili ni kuchangia kwenye maendeleo ya Wananchi maana hiyo ndiyo sera ya Serikali kwamba wananchi wanaoishi pembeni mwa rasilimali za mistu waweze kunufaika nazo kwa njia endelevu nah ii ni katika kuwaonesha Wananchi kuona rasilimali hiyo ya misitu ni yao na wana jukumu la kuilinda na kuihifadh kwakuwa wanapata motisha.

”Kupitia program hii ya uhifadhi shrikishi wa misitu tunaona kwamba kuna haja ya kuzidi kuiendeleza na jukumu kubwa tulilonalo hasa katika awamu hii ya tatu ya mradi huu tayari tumeshaanza kuondoka kwenye vijiji vya awali na wilaya ya Kilosa sasa tunahamia kwenye wilaya zingine nje ya mkoa wa Morogoro na tumewaachia halmashauri ya Wilaya ili waweze kuwasimamia na kuratibu hivi vijiji”Alibainisha meneja wa Mradi.

Katibu wa kamati ya maaliasili ya Kijiji cha Kitunduweta, Leoti Msoloka amesema kupitia Usimaizi shirikishi wa Misitu ya Kijiji chao wamepata mafanikio makubwa ikiwemo ujenzi wa Ofisi ya Kijiji, Ukatabati wa vyumba vya madarasa,Ujenzi wa matundu ya vyoo pamoja na kuwakatia bima ya afya iliyoboreshwa Wanakijiji wote kijijini hapo ambapo sasa wamenza na ujenzi wa Zahanati ya Kijiji ili wapate huduma kijijini kwao.

“Faida kubwa ni kwamba hapo awali tulikuwa hatujui umuhimu wa kuhifadhi Msitu wa Kijiji lakini baada ya elimu na faida tulizozipata na sasa asilimia tisini ya mapato yatokanayo na misitu zinatumika kijijini tofauti nah apo awali ambapo asilimia hizo zilikuwa zinaenda wilayani na sasa tunaweza kuzitumia fedha hizo kulinda msitu na kunufaisha Kijiji chetu” Alifafanua bwana Msoloka.

Mradi huu wa uhifadhi shirikishi wa misitu ya vijiji unatekelezwa na shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii usimamizi wa misitu Tanzania (MJUMITA) kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo la USWISI (SDC).

 

Saturday, October 16, 2021

WILAYA YA HANANG KUWA NA WIKI YA MAENDELEO NOVEMBA 1 HADI NOVEMBA 5, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara,  Janeth Mayanja (katikati) akipokea mmoja wa mfuko wa saruji kati ya 200 iliyotolewa na Kampuni ya Bonanza Co.Ltd kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya Hospitali ya Tumaini iliyopo wilayani humo wakati wa hafla ya uzinduzi wa wiki ya maendeleo ambayo kilele chake kitakuwa kuanzia Novemba 1 hadi 5.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Janeth Mayanja akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Janeth Mayanja akipokea rangi  kwenye hafla hiyo iliyotolewa na Kampuni ya Ngano Limited.

Mkuu wa wilaya hiyo Mstaafu Mzee Mathew Sedoyeka akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang Rose Kamili akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Hanang, Yohana Leonie akizungumza kwenye hafla hiyo.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Hafla ikiendelea 
Saruji na rangi iliyotolewa na wadau wa maendeleo.
Hafla ikiendelea .



Na Dotto Mwaibale, Hanang

WILAYA ya Hanang mkoani Manyara itakuwa na Wiki ya Maendeleo kuanzia Novemba 1 hadi Novemba 5, 2021 ambapo utambulisho wake  umefanyika mapema wiki hii katika ofisi ya mkuu wa wilaya na  kuhudhuriwa na viongozi wa wilaya, Dini, Chama cha Mapinduzi (CCM) na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya hiyo Janeth Mayanja amepokea saruji mifuko 200 kutoka Kampuni ya Bonanza Co.Ltd, Rangi kutoka Kampuni ya Ngano Limited, Mchanga Tripu 73 kutoka Kampuni ya HLH. 

Mayanja  amesisitiza makampuni yote ya kibiashara wilayanj humo kutoa sehemu ya faida kwa jamii  kama sera ya   ushiriki wa jamii katika majukumu  inavyoelekeza kwa kuleta vifaa vya ujenzi kuanzia Novemba 1 hadi Novemba 5 mwaka huu.

Mayanja amewashukuru viongozi wote wa wilaya hiyo, wadau wa maendeleo na Wananchi kwa kuliunga mkono wazo hilo na kuliboresha toka Mwezi Julai 2021 baada tu ya kuliibua.

 Mkuu wa Wilaya hiyo Janeth Mayanja ametumia nafasi hiyo kuwaomba watu wote  waliopo ndani na  nje ya Hanang kushiriki kikamilifu katika  wiki hiyo ili kuunga jitihada za Selikali ya Rais Samia Suluhu Hassan za kuliletea Taifa maendeleo kwa vitendo.

Mayanja  alisema wanategemea kupokea saruji zaidi ya mifuko 2000 ,ndoo za rangi zaidi ya 300, vigae na vifaa vingine vya ujenzi katika wiki hiyo ya maendeleo wilayani Hanang.

MSIWABAGUE WATOTO WA KIUME; REPSSI TANZANIA

Mkurugenzi Mkazi wa REPSSI Tanzania, Edwick Mapalala akizungumza  kwenye Jukwaa la Kimataifa la Msaada wa Kisaikolojia (PSS FORUM) linalofanyika kwa njia ya mtandao, likiunganisha nchi 13 za Afrika ikiwemo Tanzania. 

Mwenyekiti wa Bodi ya REPPSI, Jeanne Ndyetabura akizungumza na wanahabari wakati Jukwaa la Msaada wa kisaikolojia likiendelea.

Watendaji wa REPSSI Tanzania wakielekezana Jambo wakati wa Jukwaa la Msaada wa kisaikolojia jijini Dar es Salaam.

Wadau wakifuatilia mada.


Tumaini Godwin, Dar es Salaam.


WADAU zikiwemo taasisi za serikali na zisizo za kiserikali zinazofanya kazi za watoto na vijana zimetakiwa kutowabagua badala yake, ziweke nguvu katika kuwasaidia watoto wa kiume kama ambavyo wanawasaidia wakike.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Kimataifa linalojihusisha na masuala ya malezi na msaada wa kisaikolojia  kwa watoto la  Regional Psychosocial Support Initiative (REPSSI) Jeanne Ndyetabura amesema ikiwa watoto wa kike watasaidiwa huku wakiume wakiendelea kuchwa wasitegemee matokeo wanayotarajia kupata.

Nyetabura alikuwa akizungumza  wakati akichangia mada kwenye Jukwaa la Kimataifa la Msaada wa Kisaikolojia (PSS FORUM) linalofanyika kwa njia ya mtandao, likiunganisha nchi 13 za Afrika ikiwemo Tanzania. 

“Watoto wa kiume mnamwachia nani? Hivi mnadhani watoto wote wa kike wanaopewa mafunzo wanaweza kuruka vihunzi vya watoto wa kiume ambao hawajasaidiwa?” alisema Ndyetabura.

Alisema kukosa taarifa sahihi kuhusu makuzi yao na watu wa kutatua changamoto zao kumewafanya watoto wa kiume watafute sehemu mbalimbali ikiwamo kwenye mitandao ya kijamii, jambo ambalo ni hatari.

Awali Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Darius Kaijongo alisisitiza suala la malezi ya watoto kwa usawa.

Mkurugenzi Mkazi wa REPSSI Tanzania, Edwick Mapalala amesema Jukwaa la Kimataifa la Msaada wa Kisaikolojia linalenga kujadili changamoto za watoto na kuandaa mikakati ya namna ya kuziondoa ikiwemo masuala ya kisaikolojilia.

Thursday, October 14, 2021

NYERERE DAY 2022 WANAFUNZI IKUNGI KUPIGWA MSASA MAENDELEO YA TAIFA


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza na Wanafunzi katika Bonanza la michezo mbalimbali ikiwa ni Maadhimisho ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere ambayo yalifanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Ikungi mkoani Singida.

Afisa Michezo wa wilaya hiyo Rachel Maliwa, akiongoza kufanya mazoezi.

Mwanafunzi Rehema Peter wa Shule ya Sekondari Ikungi akizungumza kwenye bonanza hilo.

Mwanafunzi Glory Malecela wa  Shule ya Sekondari Ikungi akizungumza kwenye bonanza hilo.
Jogging ikifanyika.
Mazoezi yakiendelea.

Mazoezi yakiendelea.
Afisa Ustawi wa Jamii wa wilaya hiyo Haruni Yasin Haruni akiongoza kufanya mazoezi.
Mazoezi yakiendelea.
Wanafunzi wakisakata rhumba.
Wanafunzi wakisakata rhumba.
Wanafunzi wakiwa kwenye bonanza hilo.

Michezo ikiendelea
Michezo ikiendelea
Mashabiki wakifuatilia michezo.
Wanafunzi wakiwa katika foleni ya kupima afya.
Upimaji  afya ukiendelea.
Upimaji  afya ukiendelea.
Michezo ikiendelea.

 Wanafunzi wakiangalia michezo.




Na Dotto Mwaibale,  Ikungi


SERIKALI wilayani Ikungi mkoani Singida imesema Maadhimisho  ya Siku ya Kumbukizi ya Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere yatakayofanyika mwakani  yatakuwa ya kipekee ambapo midahalo ya kuwafundisha wanafunzi kuhusu maendeleo ya Taifa itatolewa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Bonanza la michezo mbalimbali ikiwa ni Maadhimisho ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere ambayo yalifanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Ikungi.

" Ndugu zangu  niwashukuru ninyi nyote mliojitokeza kuja kushiriki michezo mbalimbali tangu asubuhi kwa ajili ya kumbukizi hii ya kuadhimisha siku ambayo mhasisi wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifariki," alisema Muro.

Muro aliwashukuru washiriki wote wa bonanza hilo wakiwemo viongozi wa wilaya hiyo, wanafunzi pamoja na Afisa Michezo wa wilaya hiyo Rachel Maliwa kwa kuratibu bonanza hilo.

Alisema wanapo maliza kumbukizi hiyo wao kama Serikali ndio mwanzo wa maandalizi mapya ya kuandaa Tamasha lingine la mwaka ujao kwani alifika kwenye bonanza hilo kuona na kujifunza.

Alisema maandalizi ya kumbukizi nyingine ya Mwalimu Nyerere inayokuja wataanza maandalizi yake mapema na kwa muda mrefu wakisaidiana na Walimu, Afisa Utumishi, Afisa Michezo, Afisa Elimu Sekondari na Msingi.

Alisema katika tamasha hilo itafanyika midahalo ya kitaaluma baada ya kutengeneza mada mbalimbali watakazopewa wanafunzi ambazo zitaelezea mtazamo na maendeleo ya Taifa na kuzishindanisha shule zote za Sekondari zilizopo kwenye wilaya hiyo na washindi watapatiwa zawadi zitakazopendekezwa.

Alisema michezo itaanza wiki mbili kabla ya siku ya maadhimisho hayo kwa kuzishindanisha timu za shule na za mitaani na siku ya kilele watatoa vikombe, zawadi na kwa wanafunzi watapatiwa vyeti na kwa shule itakayofanya vizuri sana itapatiwa zawadi nono na ya kipekee ambayo ni siri yake na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo.

Muro alitumia nafasi hiyo kuwataka wanafunzi kuzingatia masomo na kuacha mambo mengine yote yatakayoweza kuwakwamisha wasiweze kumaliza masomo yao na kushindwa kutimiza ndoto za maisha yao.

Afisa michezo wa wilaya hiyo Rachel Maliwa alisema katika kumbukizi ya Mwalimu Nyerere waliona wafanye bonanza la michezo mbalimbali kukimbia (Jogging)  kilometa mbili, mazoezi ya viungo, mpira wa miguu, kikapu, Netball na mingine mingi ambayo ilichezwa na Watumishi wa Serikali Kuu, Halmashauri na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ikungi.

 Alisema bonanza hilo lilifanyika sambamba  na upimaji wa afya kama kupima uzito, urefu, damu, Ukimwi,  uchangiaji wa damu salama na chanjo ya Uviko 19.

Alisema kazi hiyo ya upimaji wa afya ilifanywa na Wafanyakazi kutoka Idara ya Afya wilaya humo.

Wanafunzi wa Sekondari ya Ikungi Glory Malecela na Rehema Peter wakizungumza kwa nyakati tofauti katika bonanza hilo walisema michezo inawafanya wafurahi, kujumuika na watu mbalimbali, inawafanya kuwa vizuri katika masomo na wakatoa shukurani zao kwa waandaaji wa bonanza hilo.