Monday, December 27, 2021

RAIS SAMIA ATOA ZAIDI YA BILIONI 12 KUPUNGUZA KERO YA MAJI MKOANI SINGIDA

 Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Singida Mhandisi Lucas Japhary (kushoto) na Mhandisi na Mkurugenzi wa Mashauri T.C.L, Jonas Mwazyunga wakisaini mkataba  kwa jili ya ujenzi wa mradi wa Milade na Kaserya wenye gharama ya Sh.818,601,228 katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mkoa  Singida Dkt. Binilith Mahenge akishuhudia utiaji wa saini wa mikataba hiyo
Mkuu wa Mkoa     Singida Dkt. Binilith Mahenge akizungumza baada ya kushuhudia utiaji wa saini wa mikataba hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida  Juma Kilimba.
Watendaji wa RUWASA wakiwatayari kushiriki kutia saini mikataba hiyo na Wakandarasi.
Mmoja wa wakandarasi hao akijitambulisha.
Mkurugenzi wa kampuni ya Chakware Mhandisi Bagambo Bakari akishukuru kupata ujenzi wa mradi wa maji wilayani Ikungi na Manyoni wenye thamani ya Sh.4.9 Milioni.
Mkandarasi kutoka Mwanza akishukuru kupata kazi ya ujenzi wa mradi wa maji katika Wilaya ya Ikungi ambao utatekelezwa katika vijiji vya Ihanja, Iglanson na Irisya ambao utagharimu Sh. 9.8 Milioni.
Wakandarasi wakisubiri kutia saini mikataba yao.
 


Dotto Mwaibale na Godwin Myovela, Singida.


RAIS Samia Suluhu Hassan amekabidhi Shilingi Bilioni 12.1 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayolenga kupunguza kero ya maji kwa kiwango cha juu katika kipindi cha miezi sita kuanzia sasa kwa wananchi wa mkoa wa Singida.

Hafla ya utiaji saini mikataba ya maji vijijini yenye thamani ya fedha hizo baina ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) na wazabuni mbalimbali iliyofanyika mkoani hapa mwishoni mwa wiki ikishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa mkoani hapa Dkt. Binilith Mahenge na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida  Juma Kilimba.

Kwa mujibu wa Meneja wa RUWASA mkoa wa Singida Mhandisi Lucas Japhary alisema mikataba ya fedha hizo imegawanyika katika sehemu mbili ambazo mosi ni bajeti ya kawaida na pili ni fedha zinazotokana na miradi ya UVICO- 19.

“Kwa mwaka huu wa fedha tumetengewa fedha za miradi ya maji bilioni 12.1, na leo tunasaini mikataba ipatayo 6 ya sehemu ya hiyo bajeti yenye thamani ya shilingi bilioni 3.9, lakini sehemu ya pili tutasaini mikataba ya fedha zinazotokana na UVICO 19 ambayo kwa mkoa wetu wa Singida kwenye eneo la maji tumetengewa Bilioni 4.9,” alisema Japhary.

Alisema katika fedha hiyo ya Uvico wanatarajia kutumia shilingi bilioni 2.8 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji mijini chini ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani hapa (SUWASA) kwa maeneo ya Singida Mjini, Manyoni na Kiomboi, huku kwa upande wa vijijini miradi 3 inayotokana na fedha hiyo itakayohudumia vijiji 6 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.9 itasainiwa kwa maana ya kila mradi kwenda kuhudumu vijiji viwili.

Aidha, Meneja huyo wa RUWASA alimweleza Mkuu wa Mkoa kwamba kukamilika kwa miradi hiyo ipatayo 9 (kwa maana ya mitatu ya Uvico na sita bajeti ya kawaida) ambayo inatarajia kukamilika ndani ya muda wa kipindi cha miezi 6 kuanzia sasa inatarajia kupunguza kero kubwa ya maji kwa idadi ya wananchi zaidi ya laki tatu ndani ya mkoa wa Singida.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa SUWASA Mhandisi Patrick Nzamba alisema kuhusu hali halisi ya utekelezaji wa miradi ya maji mijini kwa sasa tayari wameshasaini mkataba wa kusambaza mabomba wenye thamani ya shilingi milioni 244, pia mkataba mwingine ni ununuzi na usambazaji wa pampu zinazotarajiwa kufungwa kwenye chanzo cha eneo la Mwankoko na visima ndani ya Manispaa wenye thamani ya shilingi milioni 150.

Pia Nzamba pia alimweleza Mkuu wa Mkoa kwamba mkataba wa tatu ambao wamesaini ni ule wa kuleta mita za malipo ya kabla-ambapo mamlaka hiyo inatarajia kupata Dira za malipo ya kabla zipatazo 300 kutoka moja ya Kampuni ya China-mkataba ambao una thamani ya shilingi milioni 142.

“Mkataba wa nne ambao tumesaini ni wa kuleta vifaa vya maunganisho ya bomba pamoja na bomba za chuma kwa ajili ya maunganisho mapya kwa wateja wapatao 1500-ambapo kati ya hao wateja 1000 watafanyiwa maunganisho  kwa miji ya Manyoni na Itigi na wateja 500 itakuwa ni kwa maeneo ya Singida Mjini pamoja na sehemu ya mji wa Kiomboi huku mikataba yote hiyo ikitarajiwa kukamilika mapema 2022,” alisema Nzamba.

Awali, Dkt Mahenge pamoja na kumpongeza Rais Samia na CCM kwa juhudi za makusudi katika utekelezaji wa miradi hiyo muhimu kwa jamii ikiwemo huduma hiyo ya maji, aliwataka wazabuni waliokabidhiwa dhamana ya kujenga miradi hiyo kuhakikisha wanazingatia ubora na viwango.

“Kajengeni miradi imara, yenye ubora, yenye viwango lakini mkajenge kwa wakati unaotakiwa ili wananchi waweze kupata huduma hii muhimu ya maji,” alisema Mahenge na kuongeza;

“Shabaha iliyopo kwa mkoa wa Singida ni kuhakikisha usambazaji wa huduma ya maji vijijini inakwenda kufikia zaidi ya asilimia 80 huku ile ya mijini ikifikia zaidi ya asilimia 90 muda mfupi baada ya kukamilika kwa utekelezaji wa mikataba hii.”

Mkazi wa Kijiji cha Mwankoko Neema Khambi aliishuku Serikali kwa namna inavyopambana kusogeza huduma hiyo muhimu kwa jamii ikizingatiwa maji ni kila kitu kwa ustawi wa afya,elimu na maendeleo kwa ujumla.

Sunday, December 26, 2021

SHIRIKA LA TAFEO NA SANT EGIDIO YATOA CHAKULA CHA KRISMASI KWA WATU KUTOKA MAKUNDI MAALUMU SINGIDA



Paroko wa  Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, Simion Gwanoga (kulia)  na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania for Equal Opportunity (TAFEO) na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya chakula cha Krismasi kwa watu wa makundi maalumu, Stella Mwagowa (katikati) na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Moses Msai wakikata keki maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya sherehe hiyo iliyofanyika  Ukumbi wa Social mjini hapa jana. Katikati ni mtoto kutoka kundi maalumu aliyewawakilisha wenzake katika tukio hilo la kukata keki.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Victorina Ludovick ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza kwenye hafla hiyo.

Saturday, December 25, 2021

ASKOFU DKT. ALEX MKUMBO WA KANISA LA KKKT DAYOSISI YA KATI AONGOZA IBADA YA KRISMASI SINGIDA

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzaia (KKKT) Dayosisi ya Kati, Dkt.Alex Mkumbo akisalimiana na waumini wa kanisa hilo baada ya kuongoza ibada ya Krismasi iliyofanyika Kanisa la Msalaba Mrefu mjini Singida leo. (Picha na Dotto Mwaibale)
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzaia (KKKT) Dayosisi ya Kati, Dkt.Alex Mkumbo akiwa na viongozi wengine wa kanisa hilo wakati akihitimisha ibada hiyo.
waumini wa kanisa hilo wakitoka kwenye ibada hiyo.
waumini wa kanisa hilo wakiwa nje ya baada ya kumalizika kwa ibada hiyo.
waumini wa kanisa hilo wakitoka kwenye ibada hiyo.
Kwaya Kuu ikitoa burudani baada ya kumalizika kwa ibada hiyo
Waumini wa kanisa hilo wakiwa nje ya kanisa hilo baadaya kumalizika kwa ibada hiyo ya Krismasi.
 

Friday, December 24, 2021

RC SINGIDA AWAKUMBUKA YATIMA SIKUKUU YA KRISMAS NA MWAKA MPYA

Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani (kulia) kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Singida akikabidhi msaada wa vyakula na vitu vingine mbalimbali vilivyotolewa na mkuu wa mkoa huo Dkt.Binilith Mahenge kwa ajili ya zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya kwa watoto  Yatima na waishio katika Mazingira magumu wa Kituo cha Amani Centre for Street Children kilichopo mkoani hapa.
 Mratibu wa kituo hicho Editruda Kifumo akitoa shukurani kwa mkuu wa mkoa kwa msaada huo.
Watoto wa kituo hicho wakitelemsha vitu mbalimbali vilivyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge.
Watoto hao wakiwa wamebeba msaada huo. Mbuzi aliyetolewa na mkuu wa mkoa kwa ajili ya kitoweo katika sherehe za sikukuu za mwishoni mwa mwaka.
Mtoto Emmanuel Frank akitoa shukurani kwa mkuu wa mkoa kwa msaada huo.
Mtoto Kaishi Gabriel akitoa shukurani kwa msaada huo.
Mtoto Baraka Isaka akishukuru baada ya kupokea msaada huo.
Muonekano wa Kituo cha Amani Centre for Street Children. 


Na Dotto Mwaibale, Singida


MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amekabidhi zawadi mbalimbali  kwa kituo cha kulelea watoto Yatima na waishio katika mazingira magumu cha Amani Centre for Street Children kilichopo Kata ya Mandewa Manispaa ya Singida.

Zawadi zilizokabidhiwa kwa Yatima na waishio katika Mazingira ni pamoja na mbuzi mmoja, mchele, mafuta ya kupikia,sukari, sabuni, unga na vitu vingine vidogo vidogo. 

Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wakati akikabidhi msaada huo alisema mkuu wa mkoa ametoa zawadi hizo ili watoto hao wapate chakula na kufurahia sikukuu za mwishoni mwa mwaka kwa kuwa anaguswa na kutambua uwepo wa watoto Yatima na waishio katika Mazingira magumu waliopo mkoani hapa.

Ndahani alisema kuwa mkuu wa mkoa amesisitiza kuwa lengo la Serikali kuweka Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali inayosimamia vituo hivyo,uanzishwaji na uendeshwaji wake ni kuhakikisha kuwa watoto wanaolelewa katika vituo hivyo wanalelewa kwa kuzingatia utaratibu.

Aidha Ndahani alisema ni muhimu kituo hicho kuwajenga watoto katika misingi ya maadili  ya  kiroho  kusudi watoto hao wakue katika misingi ya kumjua Mwenyezi Mungu na kwamba endapo suala hilo litatiliwa mkazo Taifa litakuwa na hazina ya Raia wenye  hofu ya Mungu jambo litakalopunguza na kuondoa kabisa changamoto ya mmomonyoko wa maadili katika Taifa.

Akishukuru kwa niaba ya watoto wenzake mtoto Emmanuel Frank alimshukuu Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Binilith Mahenge kwa msaada huo na akaomba msaada wa namna hiyo usiwe wa mwisho bali uwe endelevu kwani wanapopata wageni wanao watembelea wanafarijika na kujiona kama watoto wengine waliopo na familia zao.

“Tunawashukuru sana kuja kutuona na kutupatia msaada, lakini msiishie kuja kuleta misaada tu, hata kama hamna kitu msisite kuja kutusalimia na kuongea na sisi, tunaomba Mungu amzidishie mkuu wa mkoa pale alipotoa na siku nyingine tena mtukumbuke” alisema Frank.

Frank alisema watamkumbuka mkuu wa mkoa katika maombi yao ya kila siku kusudi Mwenyezi Mungu amjalie afya njema na maisha marefu na kumpa mafanikio katika safari yake ya uongozi na akawaomba wadau wengine kujitokeza kuwasaidi kama alivyofanya Dkt. Mahenge.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo mratibu wa kituo hicho Editruda Kifumo amemshukuru mkuu wa mkoa kwa msaadaa alioutoa kituoni hapo na kuahidi kumuombea kwa Mungu ili kusudi azidishiwe pale alipopunguza kusaidia watoto hao na kuwa msaada huo umewaongezea ari ya kuwalea watoto hao kwa nguvu na kasi mpya.

WALIOVAMIA KARANTINI YA MIFUGO MKOANI PWANI WATAKIWA KUONDOKA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (kulia) akikagua eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya kujenga Karantini mpya ya Kwala alipotembelea eneo hilo lililopo katika Wilaya ya Chalinze, mkoani Pwani jana. Akiwa katika eneo hilo alisema kuwa wananchi wote waliovamia eneo hilo waondoke kwa hiyari vinginevyo shughuli za ujenzi zitakapoanza wataondolewa kwa nguvu.

Wednesday, December 22, 2021

WAZIRI UMMY AWATAKA WANANCHI WILAYA YA MKALAMA KUTUNZA BARABARA ZINAZO JENGWA NA SERIKALI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu, akishiriki ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata Ilunda kilichopo wilayani Mkalama mkoani Singida kwa kuchanganya mchanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo aliyoifanya leo wilayani humo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Afya TAMISEMI, Dkt. Ntuli Kapologwe.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu, akikagua darasa la Uviko-19 la Shule ya Sekondari ya Gumanga.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge, akizungumza katika ziara hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo na Mbunge wa Iramba Mashariki, Francis Isack.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango TAMISEMI, John Cheyo, akiteta jambo na Waziri Ummy wakati wa ziara hiyo.
Mkurugenzi  wa Kikundi cha  Vijana cha Iguguno Youth Group kinachojishughulisha na ufyatuaji wa tofali na ufugaji wa kuku wa kienyeji, Vicky Mwaisakila akitoa taarifa ya kikundi hicho kwa Waziri Ummy Mwalimu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Vijana wa Kikundi cha  Iguguno Youth Group na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Singida.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijiji wa Wilaya ya Mkalama,  Edward Masola akitoa taarifa ya ujenzi wa miradi ya barabara wilayani humo.
Mbunge wa Iramba Mashariki, Francis Isack akimuelekeza jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu.
Diwani wa Kata ya Ilunda, Mohamed Imbele, akizungumza kwenye ziara hiyo.
Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Ilunda ukiendelea.
Wananchi wa Kata ya Ilunda wakiwa kwenye mkutano eneo kinapojengwa kituo cha afya ambapo walipata fursa ya kuzungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu.
Mkazi wa Kata ya Ilunda, Oscar Daudi akitoa shukurani kwa Serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa kituo hicho cha afya.
Mkazi wa Kata ya Ilunda Josephina Maige akizungumzia adha wanayoipata kwa kukosa kituo cha afya katika kata hiyo.
Mkazi wa Kata ya Ilunda, Hawa Gimbi akizungumzia furaha yake kwa Serikali kuanza kujenga kituo hicho cha afya kwani aliwahi kunususika kufariki alipokuwa mjamzito wakati akipelekwa hospitali kujifungua.
Mkazi wa Kata hiyo Omari Mkali akizungumzia umuhimu wa kituo hicho cha afya kwa wananchi wa eneo hilo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Messos (kulia) akizungumzia kuhusu ujenzi wa Zahanati ya Kisuluiga iliyopo Kata ya Gumanga ambapo Waziri Ummy ameagiza Halmashauri hiyo itoe Sh.60 milioni ili kukamilisha ujenzi wake.



Na Dotto Mwaibale, Mkalama


 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewataka Wananchi wa Wilaya ya Mkalama mkoani Singida kuzitunza barabara zilizojengwa na Serikali kwa gharama kubwa.

Ummy ametoa ombi hilo wakati akizungumza na wananchi hao wakati akikagua barabara ya Singa- Kinampundu-Ilunda iliyojengwa kwa kiwango cha changarawe katika ziara ya kikazi ya siku moja wilayani humo ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

"Jambo lililokubwa nawaomba wananchi mzitunze hizi barabara kwa sababu Serikali inazichonga lakini kunawananchi wanapitisha majembe ya kukokotwa na ng'ombe kwa hiyo niombe ulinzi wa barabara uwe ni jukumu letu sote kwa sababu fedha zilizotumika kuzitengeneza ni nyingi hivyo tunalitamani ziendelee kuwa na ubora na zisaidie kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi" alisema Waziri Ummy.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijiji wa Wilaya ya Mkalama,  Edward Masola alisema matengenezo ya barabara hiyo yatagharimu kiasi cha Sh.milioni 91,201,000.

Alisema barabara hiyo ambayo inaunganisha Kata za Ilunda na Kinampundu itakapokamilika itarahisisha usafiri kwa wananchi kufikia huduma za elimu, afya na masoko.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida kusaini mikataba yote ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Ilunda baada ya kuwepo madai ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo kugoma kuisaini kufuatia mgororo wa kugombea sehemu ya kujengwa kituo hicho ambapo baadhi ya madiwani walitaka kijengwe Nduguti.

Awali akitoa taarifa ya kituo hicho cha afya, Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Ibrahim Pazia alisema fedha za ujenzi wa kituo hicho ni Sh.250,000,000 zilizotokana na tozo na kuwa kitakuwa na majengo matatu jengo la wagonjwa wa nje (OPD) jengo la maabara na kiteketeza taka.

Alisema mradi huo utakapo kamilika utahudumia wananchi 12,000 wa vijiji vya Asanja, Nkungi, Ilunda na Iambi, Kinambili, Nduguti na vijiji jirani vya Mkunguru, Kidigida na Kata ya Kinampundu.

Waziri Ummy alitumia nafasi hiyo kuwaomba waheshimiwa madiwani kuacha mivutano ambayo haina tija ambayo inakwamisha maendeleo ya wananchi kama ilivyotokea katika kata hiyo.

Katika ziara hiyo Waziri Ummy alitembelea na kukagua kikundi cha Vijana cha Iguguno Youth Group kinachojishughulisha na ufyatuaji wa matofali na ufugaji wa kuku wa kienyeji ambapo aliwaunga mkono kwa kuwachangia Sh.2,000,0000 ambapo pia Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge aliwachangia kiasi hicho cha fedha.

Aidha Waziri Ummy alitembelea na kukagua darasa moja la Uviko-19 kati ya saba la Shule ya Sekondari ya Gumanga ambayo yamejengwa kwa Sh.140,000,000. 


Tuesday, December 21, 2021

WAZIRI UMMY ATOA SIKU SABA MANISPAA YA SINGIGA IKAMILISHE UJENZI CHUMBA CHA X-RAY HOSPITALI YA SOKOINE

  Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Manispaa ya Singida Mhandisi Lambert Bayona  (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu wakati akikagua ujenzi wa barabara ya mbadala ya Kindani-Mtamaa kwa kipande cha Ziwa Kindai ya kilomita 2.6  wakati wa  ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo iliyopo Manispaa ya Singida jana. Wengine ni viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akitoa maelezo kwa Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu kuhusu ujenzi wa barabara mbadala katika Manispaa ya Singida.