Friday, February 18, 2022

SHIRIKA LA SPRF LAFANYA MDAHALO KWA WANAFUNZI SINGIDA ILI KUJIFUNZA MBINU ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA


Mratibu wa Mradi kutoka Shirika  la Jiokoe na Umaskini yaani Stars of Poverty Rescue Foundation (SPRF)  Mwalimu Bernard Maira, akizungumza na Wanafunzi wa Shule za Sekondari ya Siuyu na Munkinya wilayani Ikungi Mkoani Singida jana katika mdahalo wa kujifunza mbinu bora za kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Ikungi, Haroun Yunus Haroun ambaye alikuwa ni mmoja wa majaji wa mdahalo huo akizungumza.

Tuesday, February 15, 2022

MAANDALIZI YA KONGAMANO LA SEKTA YA MADINI WILAYA YA IRAMBA YAPAMBA MOTO

Waziri wa Madini Dk. Doto Biteko, anayetarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la madini litakalofanyika Wilaya ya Iramba mkoani hapa Februari19, 2022.

Sunday, February 13, 2022

WAZIRI WA MADINI DK. DOTO BITEKO MGENI RASMI KONGAMANO LA MADINI WILAYA YA IRAMBA

 Waziri wa Madini Dk.Doto Biteko anayetarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la madini litakalofanyika Februari 19, 2022 wilayani Iramba mkoani Singida.

TAMUFO YAFANYA MAOMBI MAALUMU YA KUMUOMBEA PROFESA J

Wanamuziki wakiwa katika picha ya pamoja jijini Arusha kwenye moja ya matukio yao. Umoja wa Wanamuziki hawa unaweza kuwa chachu ya kusaidiana katika masuala mbalimbali hata mmoja kati yao anapokuwa mgonjwa. 
Mchungaji Mary Nyerere ambaye aliongoza maombi hayo.

Friday, February 11, 2022

SERIKALI KUU YAIIDHINISHIA WILAYA YA IKUNGI SH.10.5 BILIONI KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Justice Kijazi akitoa taarifa katika Kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani kilichoketi wilayani humo. mkoani Singida leo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Mwanga akizungumza kwenye baraza hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Peter Mtyana akitoa taarifa katika baraza hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Justice Kijazi (kulia) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Mwanga kwenye baraza hilo
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa akizungumza kwenye kikao hicho.
Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Singida, Adamu Kilongozi akitoa mada kwa madiwani hao kuhusu posho wanazostahili kulipwa.
Mratibu wa baraza hilo la Madiwani wilayani humo,  Peter Bahati akizungumza kwenye kikao hicho.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhandisi Paskas Mulagiri akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii wa Halmashauri hiyo Selestine Yunde akichangia jambo kwenye baraza hilo.
Madiwani Leonard Muna wa Kata ya Iseke (kushoto) na Diwani wa Viti Maalumu Kata ya Ihanja, Mariam Ntembo wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Diwani wa Kata ya Ihanja Mohamed Igae (kulia) na Abel Suri wa Kata ya Unyahati wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Diwani wa Kata ya Mwaru, Iddi Makangale na Deogratius Majige (kulia) wa Kata ya Mgungira wakiwa kwenye baraza hilo.
Baraza likiendelea.
Baadhi ya maafisa watendaji na wataalamu wa halmashauri hiyo wakiwa kwenye baraza hilo
Afisa Mtendaji wa Kata ya Dung'unyi, Yahaya Njiku (kushoto mbele) akiwa na watendaji wenzake kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Diwani wa Kata ya Mungaa Dulle Gabriel akichangia jambo kwenye baraza hilo.
Diwani wa Kata ya Unyahati Abel Suri akizungumza kwenye baraza hilo.
Baraza likiendelea.
Diwani wa Kata ya Mang'onyi, Innocent Makomelo akizungumza kwenye baraza hilo.
Diwani wa Kata ya Mtunduru Ramadhan Mpaki akichangia jambo.
Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.
Diwani pekee kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika halmashauri hiyo wa Kata ya Ntuntu, Athumani Toto akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Diwani wa Kata ya Issuna Stephen Misai (kushoto) na Diwani wa Kata ya Iglanson Yusuph Athuman yakipitia makabrasha kwenye kikao hicho. 
Madwani wa Viti Maalumu wakiwa kwenye kikao hicho.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Abubakar Muna akipitia kabrasha katika kikao hicho.

Wednesday, February 9, 2022

SHIRIKA LA INADES FORMATION TANZANIA (IFTz) LATOA MICHE YA MATUNDA KATIKA SHULE MKOANI SINGIDA

Mratibu wa Mradi wa Ustawi wa Mnyama Punda wa Shirika la  Inades Formation Tanzania (IFTz)  Fortunata Tarimo akimkabidhi mche wa matunda mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ghata ya Kata ya Maghojoa kwa ajili ya kuipanda shuleni hapo katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki wilayani Singida.
Mazungumzo yakifanyika kabla ya kupokelewa kwa miche hiyo.

Saturday, February 5, 2022

TAASISI YA TREES FOR THE FUTURE TANZANIA YATOA MICHE YA MITI 2000 SINGIDA KUHIFADHI MAZINGIRA

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini Mhandisi Paskas Muragili  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa  Singida Dk. Binilith Mahenge akipanda mche wa mti wakati wa zoezi la upandaji miti kimkoa lililofanyika eneo la maziwa ya Kindai na Munang lililoratibiwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Trees for the Future Tanzania hivi karibuni.
Miche ya miti iliyopandwa hivi karibuni katika eneo la Maziwa ya Kindai na Munang yaliyopo Manispaa ya Singida.
Uelekezaji wa namna ya upandaji wa miche hiyo ukifanyika.
Miche ikipandwa.
Safari ya kwenda kupanda miche hiyo ikifanyika.
Muonekano wa eneo lililopandwa miti hiyo.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Trees for The Future wakimuangalia Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida, Widege Mzalendo alivyokuwa akishiriki zoezi hilo la upandaji miche ya miti katika eneo hilo.
Wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakiwa eneo la tukio la upandaji miche ya miti.

 Wafanyakazi wa Taasisi ya Trees For Future Tanzania wakiwa eneo la tukio la upandaji miche ya miti.



Na Dotto Mwaibale, Singida


TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Trees for the Future Tanzania yenye makao yake makuu mkoani Singida imetoa miche ya miti 2000 kwa ajili ya kuboresha mazingira na kuufanya mkoa huo kuwa wa kijani.

Akizungumza hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa zoezi la upandaji miti kimkoa lililofanyika eneo la maziwa ya Kindai na Munang lililoratibiwa na Taasisi hiyo lenye lengo la kuhimiza watanzania kuongeza juhudi katika shughuli za uhifadhi wa mazingira Msimamizi wa miradi wa Taasisi hiyo Veliksi Haji alisema shabaha ya taasisi hiyo ni kutunza mazingira.

Alisema taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali pamoja na mambo mengine inajihusisha na uhamasishaji  wa kilimo endelevu kwa kutumia miti wameazimia kupanda takribani idadi ya zaidi ya miti milioni tatu ambayo ina uwezo wa kustahimili hali ya hewa ya eneo husika.

Haji alisema mazingira yanaharibiwa sana kutokana na shughuli za kibinadamu kama kukata miti kwa ajili ya kilimo, kujengea,malisho ya mifugo na shughuli mbalimbali imepelekea maeneo mengi kuwa wazi na kuharibu uoto wa asili hivyo wanashirikiana na uongozi wa Mkoa wa Singida kama juhudi zao za kuhamasisha wananchi kupanda miti kwa wingi ili waweze kurudisha uoto wa asili na hali ya hewa kurudi katika hali yake ya kawaida.

"Miaka ya nyuma Singida ilikuwa na mvua za kutosha na vyanzo vya maji vilikuwa vingi lakini sasa hali hiyo haipo tena ndio maana Taasisi yetu imekuwa ikifanya kazi ya kuhamasisha upandaji wa miti" alisema Haji. 

Alisema katika kutekeleza malengo yake ya kupanda miti taasisi hiyo inawawezesha kifedha wadau wa maendeleo mbalimbali wanaojihusisha na shughuli za za upandaji miti na uhifadhi wa mazingira nchini ikiwemo Magereza Tanzania kupitia Gereza la Uyui-Tabora, Ilagala-Kigoma, Msalato-Dodoma, Manyoni-Singida na Gereza la Shinyanga.

Aidha alisema taasisi hiyo inasaidia asasi za kiraia zinazofanyakazi na wakulima ambazo ni ADESE na WAENDELEE za Mkoa wa Singida, TaDeCaO na Frontie Friends of Environment za Mkoa wa Tabora, Women Against Poverty ya Mkoa wa Dar es Salaam, Twitange ya Mkoa wa Iringa, Environment Develepment Group na Life Securing and Relief Services za Mkoa wa Shinyanga na Friends of Lake Tanganyika ya Mkoa wa Kigoma na kuwa kwa kipee taasisi hiyo inashirikiana na Clinton Development Initiative (CDI) iliyoko Mkoa wa Iringa na HELVETAS ya Singida.

Alisema katika Mkoa wa Singida wanafanya kazi katika Halmashauri 4 ambazo ni Ikungi, Iramba, Mkalama na Singida.

Akizindua zoezi hilo Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini Mhandisi Paskas Muragili  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa  Singida Dk. Binilith Mahenge aliagiza Manispaa ya Singida kuhakikisha inawakamata watu wote watakaoacha mifugo yao ikizurura hovyo na kusababisha uharibifu wa mazingira kwa namna yoyote.

 " Ninaagiza mazingira yatunzwe na mifugo isiruhusiwe kuzurura hovyo-hivyo naagizawekeni utaratibu mzuri na muwe na tabia ya kupanda miti na kuitunza ili iwe endelevu kwa kizazi cha sasa na baadae" alisema Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili kwa niaba ya mkuu wa mkoa" 

Katika hatua nyingine Dk. Mahenge aliagiza kila kaya mkoani hapa kuhakikisha inalima ekari isiyo pungua moja ya zao la mtama aina ya serena ili kukabiliana na uhaba wa chakula ambao utaweza kutokea kutokana na changamoto zilizopo za mabadiliko ya hali ya hewa.

Kwa upande mwingine, Wizara ya Maji kupitia ofisi yake ya Bodi ya Maji Bonde la Kati ambayo imepewa dhamana ya kutunza vyanzo vya maji ikiwemo maziwa hayo imetahadharisha wananchi kuendelea kuchukua hatua za uhifadhi wa vyanzo vyote vya maji na kuvilinda ipasavyo ili kupendezesha mji, kuweka mandhari nzuri, kuzuia mmomonyoko wa ardhi na kuthibiti kuenea kwa jangwa ambako  kunaweza kupelekea kupungua kwa vina vya maji.

Kaimu Afisa wa Maji Bodi ya Maji Bonde la Kati, Danford Samson kwa niaba ya wizara alitoa angalizo hilo wakati wa kampeni hiyo ikiwa ni sehemu ya jitihada ya ofisi hiyo kuhakikisha kampeni ya kufanya Singida kuwa kijani inafanikiwa.