Monday, March 28, 2022
SHILINGI BILIONI 10 ZA RAIS SAMIA ZATEKELEZA MIRADI TARAFA YA NDAGO IRAMBA
Saturday, March 26, 2022
MREMA AFUNGUKA WANAOENEZA UVUMI MITANDAONI WANAPOTEZA MUDA WAO
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha TLP, Augostino Mrema akifunga ndoa na Doreen Kimbi.
Na Thobias Mwanakatwe, Moshi
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha TLP, Augostino Mrema, amesema anamshukru Mungu kwa sherehe ya ndoa yao kwenda vizuri na kwamba wanaoendelea kueneza uzushi na upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii wanapoteza muda wao.
Akizungumza na gazeti hili alisema anamshukru Mungu kwasababu taratibu zote za ndoa zilifuatwa hivyo mke wake Doreen Kimbi hajamuoa kinyemela.
Mrema alisema ndoa yake awali nilikuwa ifanyike Machi 8 mwaka huu lakini waliamua kuisogeza mbele hadi Machi 24 ili kutoa fursa kama kulikuwa na mtu ambaye angejitokeza kuweka pingamizi ndoa isiweze kufungwa.
" Ndoa imetangazwa kanisani mara tatu na hakuna mtu yeyote aliyejiyokeza kusema Doreen alikuwa mke wangu kwa hiyo uvumi wa mitandaoni hauna maana yeyote na wanaofanya hivyo wanadhani watavuruga ndoa yetu kumbe wanapoteza muda wao bure," alisema Mrema.
Alisema hadi kufikia Machi 23, mwaka huu ikiwa ni siku moja kabla ya kufungwa kwa ndoa hiyo hakuna mtu yeyote aliyejitokeza kutoa pingamizi hivyo wanaoeneza uvumi mbalimbali kwenye mitandao wanapoteza muda wao ndoa imeshafungwa na hivyo suala hill limeshapita.
Mrema alisema uvumi wa mambo yote hayo unatokana na kwamba watu hawajazoea mtu akipendwa kwa dhati na mtu mwingine,watu wamezoea rushwa wanahonga watu,wananunua watu,kwa hiyo wanafikiri kila mtu ananunulika.
Alisema mara baada ya mke wake kufariki Septemba mwaka jana, alimuacha katika mazingira magumu sana hivyo alimuomba Mungu amsaidie ili apate msaidizi mwingine.
"Mke wangu alipofariki aliniacha katika mazingira magumu sana afya ilikuwa imedorora hata hotuba yangu wakati wa kumzika sikuweza kusimama, nilimuomba Mungu na mke wangu atakapokuwa anisaidie nipate mtu atakayenitunza, atakayeniangalia," alisema.
Aliongeza kuwa kutokana na maombi yake hayo baraka za mwenyezi Mungu zilikuja na ndipo akajitokeza huyo binti (Doreen) akakubali kutumia maisha yake kwa ajili ya kunitunza.
Thursday, March 24, 2022
TANROADS RUKWA YAFANIKISHA UJENZI WA MADARAJA 13
Meneja wa TANROAD Rukwa Mhandisi Mgeni Mwanga (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa CCM Rukwa Ndugu Rainer Lukala (kushoto ) wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa daraja la Kisalala wilaya ya Sumbawanga lenye urefu wa mita 35 ambalo linajengwa kwa gharama za shilingi Bilioni 1.89 zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita.
Daraja la Kisalala katika barabara ya Laela- Mwimbi-Kizombwe wilaya ya Sumbawanga lenye urefu wa mita 35 linalojengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 1.89 chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara (TANROAD ) mkoa wa Rukwa.
Na. OMM Rukwa
SERIKALI ya Awamu ya Sita katika kipindi chake cha mwaka mmoja tangu kuingia madarakani kupitia Wakala wa Barabara (TANROADs) umefanikiwa kutekeleza kazi za matengenezo ya dharura ikiwemo madaraja 13 katika barabara za mkoa wa Rukwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa ukaguzi wa barabara katika kijiji cha Muze kilichopo katika Bonde la Ziwa Rukwa Wilaya Sumbawanga (22 Machi,2022) Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Rukwa Mhandisi Mgeni Mwanga alisema Serikali ilitoa shilingi 13,864,528,000/- katika mwaka wa fedha 2021/22.
Mafanikio hayo yamekuja ikiwa ni jitihada za serikali kufanya matengenezo ya dharura katika barabara za Rukwa ikiwemoile ya Kasansa –Muze –Kilyamatundu iliyopo ukanda wa Ziwa Rukwa yenye urefu wa kilometa 179 ambayo iko chini ya Wakala wa Barabara (TANROAD) hatua iliyofanya ipitike bila shida kipindi chote cha mwaka.
“Rais Samia Suluhu Hassan amefanikisha upatikanaji wa fedha katika bajeti ya mwaka 2021/22 kwa ajili ya matengenezo ya dharura ya miundombinu ya barabara ambapo tulifanikiwa kujenga madaraja 13 katika barabara za mkoa wa Rukwa” alisema Mhandisi Mgeni.
Mhandisi Mgeni aliongeza kusema miradi hiyo ya ujenzi imefanyika kwa kutumia wakandarasi wazawa hatua inayosaidia kukuza uchumi wa mkoa na Taifa.
Katika hatua nyingine TANROAD imesema serikali iko katika mpango wa ujenzi wa barabara ya Ntendo –Kazungu yenye umbali wa kilometa 25 na barabara ya Kazungu –Muze yenye urefu wa kilometa 12 kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi utaanza mwaka wa fedha 2022/23.
Akizungumzia umuhimu wa barabara ya ukanda wa Ziwa Rukwa Diwani wa Kata ya Zimba tarafa ya Mtowisa ,Ephraim Konta alisema kukamilika kwa miundombinu ya ikiwemo daraja la Lwanji kumesaidia kurahisisha shughuli za kiuchumi kwani mazao yanafika sokoni yakiwa katika ubora .
Diwani huyo aliongeza kusema anaomba serikali kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kutofanya shughuli za kilimo na Mifugo katika kingo za mito hatua itakayosaidia madaraja kuwa imara na mito kutokana hama.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Solola halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga,Godfrey Tanganyika alishukuru serikali kwa kujenga daraja lililokuwa kikwazo cha kuunganisha kijiji hicho na kijiji cha Ilemba kufuatia mvua kusababisha mto kuhama.
“Tunashukuru serikali kwa kujenga daraja hili pia tunamwomba Rais Samia atuwekee lami katika barabara hii ya ukanda wa Ziwa Rukwa kwani ndio barabara kubwa iliyobaki bila lami” alisema Tanganyika.
Nao wanafunzi Felista Zuberi na Elizabeth Nasri wa kidato cha nne shule ya sekondari Mazoka iliyopo kata ya Muze walisema kukamilika kwa ujenzi wadaraja la Muze kumesaidia waweze kuwa na uhakika wa kuhudhuria masomo muda wote ikiwemo kipindi cha masika.
“Tulikuwa tukikosa masomo kipindi mto huu ulipokuwa ukijaa na njia kukatika kwani tunaishi Muze na shule iko upande wa pili kijiji cha Mazoka kata ya Mbwilo” alisema Felista mwenye umri wa miaka 18.
Wakala wa Barabara (TANROAD) Mkoa wa Rukwa unaendelea na kazi ya kusimamia mtandao wa barabara Kuu za lami zenye urefu wa kilometa 415 .86 kati yake za lami kilometa 298.35 na za changarawe kilometa 117 huku ikisimamia barabara za mkoa zenye urefu wa kilometa 834.98 kati ya hizo za lami ni kilometa 76.83 na za changarawe ni kilometa 758.15.
SINGIDA KUFANYA MKUTANO WA KUPANGA BEI YA ZAO LA ALIZETI MSIMU WA 2021/2022
Ukaguzi wa mashamba hayo ukiendelea. Kutoka kushoto ni Diwani wa Kata hiyo Omari Mande, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Binilith Mahenge na Mkulima wa Kata ya Mudida, Fr Pasian Mwanga -Paroko Parokia ya Mtinko.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge amesema wanatarajia kuitisha mkutano utaowakutanisha wadau wote wa zao la alizeti na wakulima kwa ajili ya kupanga bei ilikuwaondelea wakulima changamoto ya kuuza zao hilo wakati msimu wa mauzo utakapo wadia.
Dk. Mahenge aliyasema hayo wakati alipokuwa katika ziara ya siku moja ya kutembelea mashamba ya wakulima ya zao hilo katika Kata ya Mudida iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Singida Vijijini.
Alisema Mkoa wa Singida katika msimu huu wa kilimo wa 2021/2022 unategemea kuvuna tani 580,000 za alizeti ikiwa ni ongezeko la zaidi ya mara tatu ikilinganishwa na msimu uliopita na hiyo imetokana na uhamasishaji wa wadau wa zao hilo na ukopeshwaji wa mbegu zenye ruzuku ya Serikali kwa wakulima.
Alisema kazi hiyo kubwa ya kuongeza zao hilo imetokana na makampuni mbalimbali kuwakopesha mbegu hizo wakulima na kuwa lengo la Serikali limefanikiwa kwa kiasi kubwa jambo litakalo saidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa mafuta ya kula ambayo yalikuwa yakiagizwa kutoka nje ya nchi.
"Kufuatia ongezeko hilo ni lazima tufanye mkutano na wadau wote wa kupanga bei yenye tija ili mkulima asipunjike kwani bila ya kufanya hivyo wanaweza kutokea wajanja wakaanza kununua zao hilo kwa bei ndogo na kumuangusha mkulima" alisema Mahenge.
Alisema muitikio wa wakulima wadogo na wakubwa wa kutumia mbegu hizo za ruzuku zilizotolewa na Serikali zimeleta tija na kutoa mavuno mengi msimu huu.
Dk. Mahenge alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wakulima na wadau mbalimbali wa zao hilo yakiwemo mashirika na makampuni mbalimbali yaliyojitolea kulima na kuwasaidia wakulima kupata mbegu baada ya ile iliyokuwa inatarajiwa kutoka izara ya Kilimo kutokidhi mahitaji.
Mkuu wa Wilaya hiyo Mhandisi Paskas Muragili alisema kwamba pamoja na kutofikia malengo ya kupata mbegu za kutosha wananchi na mashirika mbalimbali waliweza kuweka jitihada za upatikanaji wa mbegu kwa kununua sehemu mbalimbali jambo ambalo limesaidia kuongeza uzalishaji na kufanya wavuke malengo.
“Tangu wananchi wa Singida waanze kulima zao ili hawajawahi kulima mashamba makubwa kwa ufanisi kama kipindi hiki, na hii imetokana na uhamasishaji mkubwa uliofanywa na serikali pamoja na ugawaji wa mbegu kwa mkopo. Singida tutavuna alizeti nyingi kuliko miaka yote” alisema Muragili.
Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Stanslaus Choaji alisema Mkoa wa Singida ulipata mbegu za alizeti tani 469 kwa ajili ya kupanda ekari 239,700 jambo ambalo lilitekelezwa.
Alisema malengo ya mkoa ilikuwa ni kupata mbegu za alizeti tani 581.9 ambazo zingeweza kuwatosheleza wakulima wote na badala yake wakapata kiasi cha tani 469 ambazo hazikuweza kukidhi mahitaji ya wakulima wote.
Alisema Wilaya ya Singida Vijijini ilipata mbegu za alizeti tani 76.04 kutoka kwa Wakala wa Mbegu nchini (ASA) kupitia Wizara ya Kilimo ambazo zilisambazwa katika kata 21 za wilaya hiyo ambapo pia ilipata tani 3.8 za alizeti zilizotolewa na Shirika la IFARD ili kuwasaidia wakulima wa zao hilo na kuondoa changamoto ya upungufu wa mafuta ya kupikia hapa nchini.
Choaji alisema kutokana na mwitikio mkubwa wa wakulima pamoja na kwamba walipata mbegu pungufu lakini matokeo yatakuwa makubwa kwa kuvuka malengo ya kiasi walichotegemea kuzalisha.
Akitoa taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Singida, Afisa Kilimo wa wilaya hiyo Nathalia Mosha alisema Halmashauri hiyo ina eneo linalofaa kwa kilimo lipatalo hekta 321,400 ambapo 3, 400 zinafaa kilimo cha umwagiliaji.
Alisema katika msimu wa kilimo wa 2021/2022 wamelima hekta 38,936 na matarajio ni kuvuna tani 73,936 ambapo mbegu za alizeti zilizotumika ni standard seed, Hysun 33, supersun 66 na recod zilizozalishwa na wakulima wenyewe.
Wednesday, March 23, 2022
IKUNGI YATAJA MAFANIKIO LUKUKI MWAKA MMOJA WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN MADARAKANI
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Jerry Muro akizungumza na Wananchi na Wana CCM wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo katika hafla ya Mwaka Mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan iliyofanyika jana Viwanja vya Hospitali hiyo ambayo ujenzi wake unaelekea kukamilika hivi karibuni.
Muonekano wa baadhi ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Ikungi.
Na Dotto Mwaibale, Singida.
MACHI 19, 2022 Rais Samia Suluhu Hassan ametimiza mwaka mmoja tangu ale kiapo na kushika wadhifa wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli. Katika kipindi hiki Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Serikali ya awamu ya sita anayoiongoza ameendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 -2025 kwa kasi kubwa.
Mafanikio ya utekelezaji huo wa Ilani ni mengi na hapa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Jerry Muro anayataja baadhi wakati akihutubia katika hafla ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan iliyofanyika jana Viwanja vya Hospitali ya Wilaya ya Ikungi ambayo ujenzi wake unaelekea ukingoni akianza na sekta ya ulinzi.
ULINZI NA USALAMA WA TAIFA
Muro anasema katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 - 2025 Ibara 105 katika miaka mitano ijayo, Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kuhimiza Serikali zake kuimarisha Ulinzi na Usalama wa nchi yetu, raia wake na mali zao ili kudumisha umoja, mshikamano, amani na utulivu ambazo ni tunu kuu za Taifa letu.
Anasema uhakika wa amani, ulinzi na usalama ni nyenzo muhimu katika kuwawezesha wananchi kuishi na kuendelea na shughuli zao za maendeleo.
Anasema katika kipindi cha Mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan wilayani Ikungi imeendelea kuhakikisha Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinatekeleza majukumu yake katika mazingira yaliyoboreshwa hivyo kuhakikisha Wilaya ya Ikungi na Mkoa mzima wa Singida unakuwa salama na Wananchi wake wanatekeleza majukumu yao katika hali ya usalama, umoja, mshikamano na utulivu.
MUUNGANO
Akizungumzia Muungano Muro anasema katika kipindi cha mwaka mmoja Rais ameendeleza na Kudumisha Muungano wa Tanzania ambapo kero 11 za Muungano zimetatulika.
DIPLOMASIA YA SIASA NA UCHUMI
Muro akizungumzia Diplomasia anasema katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020/2025 Ibara 132 (a) katika Diplomasia Siasa Chama kinaelekeza Serikali kuboresha utekelezaji wa mipango ya kuimarisha Diplomasia ya Siasa ya kimkakati kwa ajili ya kulinda Amani, Uhuru, Masilahi ya Taifa na kuimarisha ujirani mwema.
Anasema katika kipindi cha Mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan Wilaya ya Ikungi wameendelea kunufaika na jitihada za Serikali kukuza mahusiano ya kiuchumi na Mataifa, Jumuiya za Kikanda na Taasisi za kimataifa ambapo Wilaya ya Ikungi wamefaidika na miradi mbalimbali iliyofadhiliwa na Taasisi ya KOICA pamoja na UN WOMEN kwa kuwawezesha baadhi ya Mabinti kutoka Wilaya ya Ikungi kupelekwa masomoni, baadhi ya Vikundi vya Wananchi kuanzisha Miradi ya Mbogamboga kupitia mashamba darasa yaliyoanzishwa katika Vijiji vya Kipumbwiko na Mnang’ana, kujenga Ghala la Alizeti katika Kijiji cha Mnang’ana, kupima na kutoa Hati Mililki za Kimila 6100 ambapo Hati 5050 zimeshagawiwa kwa Wananchi mbalimbali ambapo kati yake Hati 2030 zimegawiwa kwa Wanawake. Miradi yote hii imegharimu kiasi cha Sh. Bilioni 5.
Anasema Rais amefanya ziara mbalimbali katika Nchi tofauti tofauti kwa lengo la kukuza Diplomasia ya Siasa na Uchumi wenye lengo la kutunufaisha Wana Ikungi na Watanzania wote kwa ujumla.
Muro anasema Aprili 11, 2021 Rais alifanya ziara yake ya kwanza nje ya Tanzania na ziara hiyo ikiwa na lengo la kusaini makubaliano ya ujenzi wa bomba la mafuta. Ujenzi wa bomba hili unapita katika Mkoa wa Singida katika Wilaya za Iramba, Mkalama na Singida, Bomba hili kupita jirani na Wilaya yetu kunatengeneza ajira kubwa kwa watu wetu, utaongeza uchumi wa mtu mmoja mmoja na ni chanzo kingine cha uchumi wa Taifa letu baada ya Mradi huu kukamilika.
Anasema Mei 4 , 2021 Rais alifanya ziara nchi ya Jamhuri ya Kenya pamoja na mambo mengine akahutubia wananchi wa Kenya.
“ Ni ziara yenye tija kwa uchumi wa Nchi ambayo imeleta matokeo makubwa na zaidi ya vikwazo 46 kati 64 vya kibiashara baina yetu na nchi ya Kenya vimeondoka” anasema Muro.
Muro anaendelea kusema Novemba 10, 2022 Rais alifanya ziara ya siku tatu nchini Misri ambapo ulishuhudia utiwaji saini ya Nyaja za Uwekezaji baina ya nchi yetu na Misri baada ya ziara ile Nchi yetu imeendelea kupokea Wakezaji wengi kutoka Misri ambao watawekeza bilioni 460 katika ujenzi wa viwanda ambapo na Wananchi wa Ikungi wamejiandaa kuwapokea baadhi ya Wawekezaji watakaofika wilayani humo.
Mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro anasema Septemba 23, 2021,. Rais alifanya ziara Marekani na kuhutubia kwa mara ya kwanza mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo alilipatia Taifa letu heshima kubwa.
Anasema Februari 10, 2022 Rais alifanya Ziara Ufarasa na Ubeligiji pamoja na mambo mengine Ziara hiyo ilifanikisha kusainiwa kwa mikataba 6 na kiasi cha Euro milioni 178 mkopo wa masharti nafuu umepatikana kwa ajili ya kughalamia mradi wa ujenzi wa barabara wa mabasi yaendayo haraka. Pia kiasi cha Euro 80 kimepatikana ili kuimarisha Benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania ambayo tunaamini itanufaisha Wananchi wa Wilaya ya Ikungi.
Anasema Februari 25, 2022 Rais alifanya Ziara UAE- Dubai wakati wa mkutano wa Biashara na Uwekezaji Rais alishuhudia kutiwa saini kwa Hati (MoU) 36 za Kimaendeleo ambapo idadi ya Ajira zinazotarajiwa kupatikana kwa ujumla kutokana na makubaliano hayo ni zaidi ya Ajira 200,000 katika kipindi cha miaka 4 huku uwekezaji huo ukigharimu zaidi ya trilioni 17.35 za Tanzania.
“Tunamshukuru Mhe. Rais kwa kuendelea kufungua nchi kiuchumi na kuimarisha Diplomasia” anasema Muro.
KILIMO
Akizungumzia kuhusu sekta ya kilimo Muro anasema katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 - 2025 Ibara ya 37, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kusimamia mapinduzi ya kilimo ili kuhakikisha kinaendelea kuwa chenye tija na kinachotumia teknolojia ya kisasa.
Aidha, chama kitahakikisha kuwa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) inaendelea kutekelezwa na kutoa mchango mkubwa katika usalama wa chakula, pato la Taifa, maendeleo ya sekta ya viwanda.
Anasema katika kipindi cha Mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan ameiwezesha Wilaya ya Ikungi kuendeleza mashamba ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ya Mikorosho na Miparachichi katika Vijiji vya Mkiwa na Ulyampiti, ambapo katika kipindi hicho Halmashauri ya wilaya hiyo imepokea Sh. 4,500,000 kwa ajili ya kuendeleza mashamba hayo na Mradi huu bado unaendelea.
ELIMU
Muro anasema katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020/2025 Ibara ya 80 imesema Chama Cha Mapinduzi kinatambua umuhimu Sekta ya Elimu na mchango wake katika ajenda ya maendeleo kwa kuandaa mtaji watu wenye uwezo wa kutumia fursa za rasilimali zilizopo kujiletea maendeleo na kuchangia katika jitihada za nchi kufikia uchumi wa kati uliojikita katika misingi ya viwanda.
Anasema chama katika miaka mitano ijayo, kinalenga kuimarisha ubora wa elimu katika ngazi zote kwa kuzingatia falsafa ya kujitegemea yenye kuendana na mazingira ya nchi yetu, hususan elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi VETA.
Anasema katika kipindi cha Mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan Wilaya ya Ikungi wamefanikiwa kupata fedha zaidi za ukamilisha wa Chuo cha Ufundi VETA ambacho tunatarajia kitakamilika mwanzoni mwa mwezi Mei 2022.
Aidha, wamefanikiwa kujenga vyumba vya madarasa 79, vyoo na miundombinu ya maji 18 katika shule za msingi mbalimbali ambapo pia wamepokea jumla ya Sh. 628,002,811 kama fedha za Mpango wa Elimu Bila Malipo.
Anasema katika Elimu ya Sekondari wamepokea jumla ya Sh. 940,000,000 kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa Shule za Sekondari Matongo na Makilawa. Wamepokea kiasi cha Sh. 1,340,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba madarasa 67 katika shule za Sekondari.
“Tumepokea Sh. 81,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Utawala katika shule ya Sekondari ya Issuna na ujenzi wa miundombinu ya maji katika shule ya Sekondari Dadu. Tumepokea Sh. 100,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo Shule ya Sekondari Dr. Shein, ukamilishaji wa madarasa Shule ya Sekondari Lighwa, Ukamilishaji wa madarasa katika shule ya Sekondari Ntuntu, Ukamilishaji wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Sepuka na Ukamilishaji wa madarasa katika Shule ya Sekondari Utaho” anasema Muro.
Aidha Muro anasema jumla ya Sh. 367,851,448 zimepokelewa kama fedha za mpango wa Elimu Bila Malipo. Miradi hiyoi imewazesha kuwa na miundo mbinu mizuri ya Elimu kwa watoto hali iliyoongeza moyo wa kupenda shule kwa wanafunzi wanaoitumiai.
AFYA
Muro anasema kuwa katika Ilani ya CCM 2020/2025 Ibara ya 83 imeleza kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kutoa kipaumbele katika Sekta ya Afya kwa kuwa inagusa maisha ya Watanzania na ustawi wa Taifa letu. Lengo la Chama ni kuhakikisha Wananchi wanakuwa na afya na siha bora ili kuwawezesha kushiriki katika shughulli za ujenzi wa Taifa na kuboresha maisha yao.
Anasema katika kipindi cha Mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha kiasi cha zaidi ya Sh. Bilioni 2.8 ambazo zimetumika katika kutekeleza shughuli mbalimbali za Sekta ya Afya katika wilaya hiyo ambapo ujenzi wa Zahanati za Kinyampembee, Makotea, Misule, Mlandala, Mnang’ana, Mpugizi na Issuna unaendelea kufanyika.
Anasema ujenzi mwingine unaoendelea ni wa Vituo vya Afya vya Irisya, Iglansoni, Ntuntu na Iyumbu,Ukamilishaji wa Hospitali ya Wilaya, Ujenzi wa Nyumba ya Watumishi katika Hospitali ya Wilaya, ujenzi wa vyoo vya zahanati za Dung’unyi, Nkuwi, Matongo na Matyuku.
MAJI
DC Muro anasema katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020- 2025 ibala 100. katika miaka mitano ijayo, lengo la CCM ni kuona kuwa nchi inaendelea kuwa na usalama wa maji na kwamba huduma ya majisafi na salama inaendelea kuimarishwa na kuwafikia zaidi ya asilimia 85 ya wakazi wa vijijini na zaidi ya asilimia 95 kwa mijini ifikapo mwaka 2025. Aidha, CCM inalenga kuhakikisha kuwa Kaya nyingi zaidi mijini zinaunganishwa katika mtandao wa maji taka.
Anasema katika kipindi cha Mwaka Mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha kuanzia mwezi Machi 2021 hadi Machi 2022 Serikali ya awamu ya sita imetoa zaidi ya Sh. Bilioni 2.8 kwa ajili ya ujenzi ya miundombinu ya maji katika Vijiji vya Lighwa, Mtunduru, Ulyampiti, Ikungi, Matare, Ihanja, Irisya, Iglansoni na Igombwe.
Anasema Miradi inayoendelea ikikamilika itaongeza asilimia ya upatikanaji wa maji safi na salama kutoka asilimia 55 ya sasa hadi kufikia asilimia 65 ambayo ni sawa na wazi 219,640 kati ya Wakazi 337,907.
UJENZI NA UCHUKUZI
Muro anasema katika Ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 -2025 Ibara ya 55 inasema katika miaka mitano ijayo, Chama Cha Mapinduzi kitaelekeza Serikali kuendeleza shughuli za ujenzi wa miundombinu mbalimbali ili kuifanya Sekta ya Ujenzi ifikie malengo yake ya kuwezesha wananchi kuendelea na uzalishaji kwa ajili ya kuongeza kipato chao.
Anasema katika kipindi cha Mwaka Mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan Wilaya ya Ikungi wamepokea Nyongeza ya Bilioni 2 kwa ajili ya kufungua maeneo ambayo hayapitiki (hayana barabara) vijijini ambapo hadi sasa wameshapokea kiasi cha Sh. 828,361,074.14 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Utaho – Makiungu na Siuyu – Nali – Makotea yenye jumla ya Km 17.84, Mungaa – Ntuntu – Mang’onyi na Issuna – Ngongosoro – Ilolo yenye jumla ya Km 22.52. Barabara ya Igombwe – Makhonda – Mwaru yenye jumla ya Km 13.2 na ujenzi wa daraja la Mto Ngano katika barabara ya Mtamaa – Minyughe – Mtavile yenye jumla ya Km 4 na barabara ya Sepuka – Italala yenye urefu wa Km 2.75.
Aidha Muro anasema wameidhinishiwa kiasi cha Sh. Bilioni 1 kwa ajili ya Matengenezo ya barabara katika wilaya hiyo ikiwa ni miradi ya barabara kwa kila Jimbo Sh. milioni 500 ambapo mpaka sasa zimekwishapokelewa Sh. milioni 900 kwa ajili ya miradi hiyo ambapo wanatarajia zitumike kutekeleza barabara ya Misughaa – Msule – Sambaru yenye urefu wa Km 15.5 pamoja na ujenzi wa karavati sanduku 6 na kalavati misitari 13 pamoja na barabara za Mtunduru – Sepuka na Irisya – Unyinga zenye urefu wa Km. 24.3 kalavati sanduku 1, Kalavati misitari 11 na kivuko (driff) 1.
UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro anasema katika ilani ya uchaguzi ya CCM ibara 239, 241 na 243 Chama kina lengo la kuchochea na kuhamasisha na kuendeleza jamii Utanzania, kuburudisha, na kuongeza fursa za ajira kupitia Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Anasema katika kipindi cha Mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan katika wilaya hiyo wameweza kushirikiana na Wadau mbalimbali kuhamasisha shughuli za Utamaduni Sanaa na Michezo ambapo wamefanikiwa kuanzisha mashindano mbalimbali ya michezo ya Mpira wa Miguu kwa kushirikiana na Waheshimiwa Wabunge wa Majibo ya Singida Mashariki na Magharibi. Aidha, katika kudumisha mila na tamaduni zetu wamewawezesha na kushiriki usimikwaji wa Watemi katika Tarafa za Ihanja, Ikungi na Mungaa. Aidha, Vikundi mbalimbali vya Sanaa za Maonyesho wamewezeshwa kupitia vikundi vyao kuweza kufikia malengo waliyojipangia.
VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
Anasema katika ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 – 2025 ibala ya 46 na 49 Kwa kutambua umuhimu wa Sekta ya Viwanda na Biashara, Chama Cha Mapinduzi kitaelekeza Serikali kuendeleza mafanikio yaliyopatikana na kubuni mikakati zaidi ili kujenga uchumi wa viwanda jumuishi.
Muro anasema katika kipindi cha Mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan Wilaya ya Ikungi wameweza kuwaalika na kuwawezesha Wawekezaji mbalimbali waliofika wilaya humo kwa nia ya kuwekeza katika Kilimo, Viwanda na Uchimbaji madini akitolea mfano wamefungua shamba la Alizeti lenye ukubwa wa Hekari 4500 na kuwaalika Wawelezaji tofauti tofauti kutoka ndani ya wilaya na nje ili waweze kuwekeza katika kilimo cha Alizeti katika mashamba hayo, mwitikio ulikuwa chanya na umewashawishi kuufanya mpango huo kuwa endelevu kwa lengo la kuifungua Ikungi kiuchumi. Aidha, wamewezesha Kampuni ya Shanta Gold Mining kuendelea na Mradi wake wa uchimbaji dhahabu katika Kijiji cha Mang’onyi ambao una uwekezaji wa zaidi za Dola za Kimarekani Milioni 40, Uongozi wa Shanta umewahakikishia kuanza uzalishaji mwishoni mwa mwaka huu.
Aidha Muro anasema watumetengeneza mazingira wezeshi kwa wafanyabishara wadogo na wa kati kuweza kupata mazingira bora pamoja na vibali (Leseni) za kufungua na kufanyia biashara katika Wilaya ya Ikungi.
SEKTA YA HABARI
Muro anasema katika ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 – 2025 ibala ya 125, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuhakikisha Sekta ya Habari inaboreshwa ili kuwaongezea wananchi fursa ya kupata habari kwa kuongeza wigo wa upashanaji wa habari.
Anasema katika kipindi cha Mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan Wilaya ya Ikungi wamekuwa na uwanda mpana wa kujieleza na uhuru wa kutoa maoni. Aidha, kumekuwepo na ushirikiano kati ya Viongozi wa Serikali na Waandishi wa Habari hali inayopelekea wilaya hiyo kusikika na kufahamika zaidi kupitia vyombo vya Habari.
SEKTA MALIASILI
Anasema katika ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 – 2025 ibara ya 69, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuimalisha usimamizi, ulinzi na uhifadhi Maliasili kwa faida ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.
Muro anasema kuwa katika kipindi cha Mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan Wilaya ya Ikungi imeanzisha mchakato wa kuhifadhi msitu wa Minyughe kwa kuanzisha mchakato wa kuhamisha umiliki wa hifadhi ya Minyughe kutoka Halmashauri ya Wilaya na kuhamia Wakala wa Hudumu za Misitu Tanzania (TFS) ambapo mpaka sasa kiasi cha Sh.65,512,599 zimetolewa na Serikali kwa lengo la ukaguzi, upimaji na uelimishaji. Aidha, Wilaya imeendelea kusimamia Maliasili nyingine zilizopo Wilayani kwa lengo la kuhifadhi maliasili kwa kizaZi cha sasa na baadae. Jumla ya Sh. 204,277,787 zimekusanywa na Wakala wa Misitu (TFS) katika shughuli mbalimbali za uhifadhi wa Maliasili.
SEKTA YA NISHATA YA UMEME
DC Muro anasema katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 – 2025 ibara ya 63, Chama Cha Mapinduzi kinakusudia kuimalisha zaidi Sekta ya Nishati kuhakikisha kuwa Nchi inazalisha umeme wa kutosha ili kukidhi mahitaji ya uchumi wa viwanda na soko la nje.
Anasema katika kipindi cha Mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan Wilaya ya Ikungi imeendelea kusambaza umeme kwa Wananchi REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza ambapo walifanikiwa kupeleka umeme kwenye Vijiji 30.
Anasema Miradi jazilizi (Densification) jumla ya Vijiji 6 vya Issuna, Mahambe, Puma – Jimbo, Ighuka – Masenku, Inyang’ongo – Makiungu na Mnang’ana – Dung’unyi vilipelekewa umeme.
“Miradi inayotekelezwa na TANESCO kupitia bajeti za ndani, jumla ya Miradi 12 ilitekelezwa ndani ya kipindi hiki cha Machi 2021 mpaka Machi 2022 yenye thamani ya Sh. 375,662,883.86” anasema Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Mwanga amewaomba madiwani wa wilaya hiyo kuendelea kusimamia ukamilishwaji wa miradi hiyo badala ya kuiachia Serikali na kuwa miradi hiyo Serikali imetoa fedha nyingi hivyo wanakila sababu ya kuisimamia kwa nguvu zao zote katika maeneo yao na akatumia nafasi hiyo ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan kutoa wito kwa Wananchi wa Wilaya hiyo kuitunza miradi hiyo kwani inamanufaa makubwa.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo za miradi katika wilaya hiyo na akatumia nafasi hiyo kuwashukuru viongozi wote wa wilaya hiyo kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha katika kutekeleza miradi hiyo kwa uaminifu mkubwa kwa kuanzia na Mkurugenzi, Mkuu wa Wilaya, Watumishi, Wakuu wa Idara, Wataalamu pamoja na wananchi na Chama na akaomba ushirikiano huo uendelee ili Ikungi iwe mfano kwa maendeleo hapa nchini.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri katika hafla hiyo Leon Katanga alisema wataendelea kuwa tayari kusimamia sheria, taratibu na miongozo ya nchi yetu na kushiriki shughuli zote za kijamii na zile ambazo Chama na Serikali itaona zinaweza kufanywa na Halmashauri hiyo.
Tuesday, March 22, 2022
RENATUS MUABHI : TUME HURU YA UCHAGUZI NI MUHIMU KUANZA NAYO
Na Thobias Mwanakatwe, Arusha
VYAMA vya siasa nchini vimeshauriwa kusimamia mchakato wa kuundwa wa tume huru ya uchaguzi kwa kuwa ndio msingi mkubwa utakaowezesha upatikanaji haraka wa katiba mpya.
Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (pichani), alisema hayo jana katika mahojiano na gazeti jijini hapa kuhusu suala la katiba mpya ambalo vyama vya upinzani vimelishikia kidedea kutaka mchakato wake uanze.
"Vyama vya siasa na wadau wote wa kisiasa walione suala la kuwa na tume huru ya uchaguzi liwe ndio kipaumbele namba moja kwasababu tume huru ya uchaguzi ikipatikana itaharakisha upatikabaji wa katiba mpya kupitia wingi wa majority katika bunge ambacho ndio chombo kinachoweza kuisimamia serikali kwenye uanzishaji katiba mpya," alisema.
Muabhi alisema inashangaza kuona baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanasema hawaoni umuhimu wa tume huru ya uchaguzi kabla ya katiba mpya wakiamini katiba hiyo ndio inaweza kuvunja aina ya mifumo ya uchaguzi iliyopo hapa nchini wakati sio kweli.
Alisema katika mazingira kama haya ya kisiasa tuliyonayo hatuwezi kukaa na uona kwamba katiba ni muhimu kuliko tume huru ya uchaguzi ambayo ndio inasimamia haki na misingi yote ya amani na utulivu.
"Tume ya Uchaguzi ndio yenye kutoa maamuzi na kutangaza nafasi zote za uongozi wa kisiasa kuanzia ngazi ya chini hadi ya rais,kwa hiyo utekelezwaji wa haki na amani imebebwa kwa asilimia 80 na kutokuwa na tume huru ya uchaguzi kwasababu hapo ndio 'reaction' ya machafuko yanapoweza kuanza," alisema.
Aliongeza viongozi wa vyama vya siasa, wafuasi na wanachama wao inapofika wakati wa uchaguzi mkuu ambao husimamiwa na Tume ya Uchaguzi huwa wakiamini watafanya vizuri katika uchaguzi husika lakini matokeo yanapotangazwa na kuwa tofauti na matarajio yao wanaelekeza lawama kwa tume na hapo ndio unakuja umuhimu wa tume kuliko katiba mpya.
"Kutokuwa na Tume Huru ya Uchaguzi tulishawahi kushudia matokeo ya uchaguzi yakifutwa visiwani Zanzibar baada ya kubaini mgombea wa chama fulani ameshinda tofauti na mategemeo ya tume hali ambayo ilileta sintofahamu na kusababisha uvunjifu wa amani na kutopatikana kwa mwafaka wa kisiasa visiwani humo," alisema.
Alisema tukio hilo lililotokea Zanzibar limeleta somo zuri ya kuona ni namna gani tume huru ya uchaguzi inaweza kuwa ni suluhisho la migogoro ya kisiasa ambayo husababisha madhira kwa viongozi, wanachama na wananchi wa ujumla wa vyama vya siasa," alisema.
Sunday, March 20, 2022
CCM SINGIDA: FEDHA ZA MIRADI ZINAZOTOLEWA NA RAIS SAMIA ZIWE CHACHU YA MAENDELEO, AFANANISHWA NA MWANAMKE ESTHER KATIKA BIBLIA
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC, Eliya Digha akizungumza wakati akitoa taarifa ya fedha walizozipokea kutekeleza miradi ya maendeleo. |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi akizungumza wakati akitoa taarifa ya fedha walizozipokea kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa akizungumza kwenye hafla hiyo. |
Na Dotto Mwaibale, Singida
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah amesema fedha za kutekeleza miradi zilizoletwa mkoani hapa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika kipindi cha mwaka 2021/2022 kuanzia Julai 2021 hadi Februari 2022 ziwe chachu ya maendeleo kwa wananchi na wanachama wa chama hicho.
Killimbah aliyasema hayo katika hafla ya kuadhimisha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan iliyofanyika makao makuu ya chama hicho mkoani hapa jana.
“Fedha hizi zilizotetwa na Mama yetu katika mkoa wetu ziwe chachu ya maendeleo kwa mwaka huu unaokuja” alisema Killimbah huku akishangiliwa na mamia ya Wananchi na Wana CCM waliohudhuria hafla hiyo.
Alisema miradi inayokuja mahala popote fedha hizo zinatafutwa na Rais wetu kwa juhudi kubwa na wabunge wanasimamia bajeti ili ije Singida kwa ajili ya kuleta maendeleo.
Killimbah alitumia mkutano huo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa mambo makubwa ya maendeleo aliyoufanyia Mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla.
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Boniphace akizungumza kwenye hafla hiyo alisema kwa mwaka mmoja alioongoza Rais Samia Suluhu Hassan Mkoa wa Singida umepiga hatua kubwa ya kimaendeleo kwani wilaya zote wamepokea fedha nyingi za maendeleo.
Alisema sambamba na hilo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akikutana na makundi mbalimbali kwa lengo la kuwasikiliza na kupokea maoni yao kwa ajili ya kujenga nchi yetu na kuwa huo ni ukomavu mkubwa wa kisiasa na kujiamini katika utendaji wake wa kuongoza nchi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC, Eliya Digha akizungumza wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo alimfananisha Rais Samia Suluhu Hassan na mwanamke mmoja shujaa aliyetajwa kwenye Biblia aitwaye Esther ambaye alijulikana sana kwenye Taifa la Waisrael.
“Rais wetu Mama Samia amefanya mambo mema na makubwa katika nchi hii hivyo tunakila sababu ya kumpongeza” alisema Digha.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Mkoa wa Singida Yohana Msita alisema Rais Samia Suluhu Hassan hakika ameupiga mwingi hapa nchini kwa kazi kubwa aliyoifanya ndani ya mwaka mmoja tangu aingie madarakani.
Alisema Rais Samia hakuna sehemu aliyoiacha bila ya kuifikia kwa maendelea katika sekta zote na ameonesha uwezo mkubwa wa kuongoza nchi ambapo aliwaomba watanzania kuendelea kumuombea kwa Mungu na kuunga mkono jitihada zakezote za maendeleo anazozifanya.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Mjini Lusia Mwiru alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha mwaka mmoja ambapo alitumia nafasi hiyo kuwaomba Wana CCM wenye sifa ya kugombea nafasi mbalimbali kujitokeza kuchukua fomu ya kugombea katika uchaguzi wa ndani utaofanyika hivi karibuni.
Katika hafla hiyohiyo kila wilaya mkoani hapa ilitoa taarifa ya fedha walizopokea kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo walioifanya ambayo ziliwasilishwa na Wenyeviti wa Halmashauri husika ambapo katika Wlaya ya Ikungi Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ally Mwanga alisema walipokea Sh.11,263,030,397 ambazo zilitumika katika Elimu, Afya, Utawala, Mfuko wa Jimbo, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira (RUWASA), Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Singida (SUWASA).
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi alisema wao walipokea Sh.10,960,988,976 kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo huku Wilaya ya Itigi wakipokea Sh.7,435,318,522 na Manyoni Sh.10,505,419,366.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama walipokea Sh.7,811,623,781, Singida DC Sh.10,046,768,035, Singida Manispaa Sh.5,791,791,192, Sekretarieti ya Mkoa Sh.875,552,414, Tanesco Sh.63,507,622,522, Jumla Kuu ikiwa ni Sh.128,198,115,205.


