Thursday, May 19, 2022

DAS IKUNGI AONGOZA UZINDUZI WA KAMPENI YA CHANJO YA MATONE YA POLIO KWA WATOTO

Katibu Tawala (DAS) wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Winfrida Funto akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya utoaji wa chanjo ya polio kwa wilaya hiyo uliofanyia leo Mei 19, 2022. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Dk. Anthony Mwangolombe na kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Oliva Njoka.


Katibu Tawala (DAS) wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Winfrida Funto, akizungumza na wakina mama waliofika kwenye uzinduzi huo (hawapo pichani)

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Dk. Anthony Mwangolombe, akizungumza kwenye uzinduzi huo.

Wednesday, May 18, 2022

RC SINGIDA AONGOZA KAMPENI YA SIKU NNE YA CHANJO YA MATONE YA POLIO KWA WATOTO

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge akizungumza na wananchi wa Iguguno wilayani Mkalama wakati alipoongoza uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya polio uliofanyika leo Mei 18,2022
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge akiwa amempakata mtoto kabla ya mtoto huyo kupata chanjo hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge akiwa amempakata mtoto wakati mtoto huyo akipatiwa chanjo hiyo.
Wananchi wa Iguguno wakiwa kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa kampeni hiyo.
Kampeni hiyo ikizinduliwa.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Ibrahim Pazia akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ambapo aliwahimiza wananchi wa wilaya hiyo kuwapeleka watoto wao kupata chanjo hiyo.
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Victorina Ludovick  akiwa amembeba mtoto wakati akisubiri kupata chanjo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Asia Messos akiwa amempakata mtoto wakati akipatiwa chanjo hiyo.
Viongozi mbalimbali wakiwa wamewapakata watoto wakati wakisubiri kupatiwa chanjo hiyo. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala Wilaya ya Mkalama, Elizabeth Rwegasira, Diwani Viti Maalumu Kata ya Iguguno Mariam Hussein, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo na Dk.Ritha Willilo kutoaka Shirika la Afya Duniani (WHO)
 Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI) Cuthbert Kong'ola akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo.
Mwakilishi wa Wadau wa Sekta ya Afya Mkoa wa Singida Said Beleka akizungumza katika uzinduzi huo.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Honest Nyaki akichangia jambo wakati wa uzinduzi huo.

 

Na Dotto Mwaibale, Singida


MKUU wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge ameongoza uzinduzi wa kampeni ya siku nne ya chanjo ya matone ya polio kwa  watoto wenye umri wa  chini ya miaka mitano.

Kampeni hiyo ya siku nne ambayo imezinduliwa kimkoa Kata ya Iguguno wilayani Mkalama imeanza leo Mei 18 ambapo itamalizika Mei 21 mwaka huu.

Akizungumza wakati akizindua kampeni hiyo Mahenge alianza kwa kuelezea kazi kubwa iliyofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutenga bajeti kubwa kwa upande wa sekta ya afya ambapo kwa Mkoa wa Singida pekee kwa mwaka huu walipokea zaidi ya Sh.30 Bilioni huku hospitali za wilaya zikijengwa Ikungi, Manyoni, Mkalama na Singida DC kwa wakati mmoja na ndani ya mwaka mmoja.

Mahenge aliongeza kuwa katika mkoa huo katika sekta ya afya vinajengwa vituo vya afya  15 katika wilaya zote huku Iramba ikiwa na vituo vitano na kueleza kuwa hiyo sio kazi ndogo bali ni kazi kubwa anayoifanya Rais Samia Suluhu Hassan.

"Nimetangulia kuyasema haya ili kuonesha jinsi Rais wetu Samia Suluhu Hassan anavyo tujali watanzania na ndio maana leo tupo hapa tunazindua kampeni hii ya polio baada ya Serikali kutuwezesha" alisema Dk.Mahenge.

Alisema kazi kubwa ya serikali si kuangalia mienendo ya nchi pekee bali na ya nchi za jirani na ndio maana baada ya kugundua nchi ya Malawi kuna kirusi cha polia ndipo juhudi zilipoanza kuchukuliwa kwa kutoa kinga ya polia katika baadhi ya mikoa  inayopakana na nchi hiyo lakini ili tuwe na uhakika serikali imeagiza chanjo hiyo ifanyike mikoa yote.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Victorina Ludovick alisema kwa mkoa huo wanatarajia kuwafikia watoto waliochini ya miaka mitano 286,736 na kuwa maandalizi yote yamekamilika.

Dk.Ludovick alisema chanjo hiyo itatolewa kwa siku tatu na lengo ni kufika kwenye maeneo yote na kuwa itafanyika nyumba kwa nyumba .

"Madhara ya ugonjwa wa Polio ni ulemavu wa ghafla wa viungo na usiotibika kwa hiyo ni muhimu sana kwa kila mzazi na mlezi wawatoe watoto wao wenye umri tajwa wapate chanjo hii ambayo ni salama" alisema.

Dk. Ritha Willilo kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) aliwaomba wazazi kutoa ushirikiano wa kuwatoa watoto wao ili kupata chanjo hiyo na kusema kauli mbiu isemayo tone moja la chanjo  ya polio linatosha kabisa kuwakinga watoto wetu dhidi ya ugonjwa wa kupooza wa polio.

Diwani wa Viti Maalumu (CCM) Kata ya Iguguno Mariam Hussein akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo alishukuru Serikali kusogeza huduma hiyo ya chanjo hadi walipo wananchi hivyo itaweza itaweza kuwafikia watoto wengi.

Kampeni hii inafanyika nchi nzima baada ya Serikali ya Malawi kutoa tamko mapema mwaka huu la kuwepo mlipuko wa Polio katika nchi hiyo baada mtoto mmoja kudhibitika kuwa na Polio na hivyo kuwa  ni mara ya kwanza kwa bara ya Afrika kutokea changamoto hiyo baada ya kupita miaka mitano pasipo kuwepo na ugonjwa huo.


SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUWEKEZA KWENYE UBUNIFU NCHINI

Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Othman Masoud akitoa hotuba yake ya ufunguzi.
Prof. Gerald Misinzo akitoa maelezo kwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Othman Masoud alipotembelea banda la SUA.

 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Raphael Chibunda akitoa maelezo kwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Othman Masoud kuhusu panya wanavyoweza kutambua makohozi yenye TB sambamba na utambuzi wa mabomu.

Tuesday, May 17, 2022

SEMINA YA KUMUINUA MWANAMKE KISAIKOLOJIA KUPONYA NDOA ZILIZOTETELEKA IRAMBA

Mtaalamu wa Saikolojia Dk. Nkwabi Sabasaba kutoka jijini Dar es Salaam akiendesha Semina ya Kuwainua Wanawake Kisaikolojia iliyofanyika mwishoni mwa wiki Kata ya Kizaga wilayani Iramba mkoani Singida.

 Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Iramba, Jane Ng'ondi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi wa wilaya hiyo, Rudia Kidaila akizungumza kwenye semina hiyo.

RC SINGIDA AFUNGUA TAMASHA LA MICHEZO LA WANAFUNZI WA TAASISI YA UHASIBU SINGIDA

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo, akizungumza jana kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati akifungua wiki ya michezo ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida  iliyoanza juzi mkoani hapa. 

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa wiki hiyo ya michezo. 
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo, akipiga mpira wakati wa ufunguzi huo. 

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, akiwa na viongozi mbalimbali wa Taasisi hiyo. Kulia ni Meneja wa TIA Kampasi ya Singida Dk.James Mrema.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo, akikagua timu katika ufunguzi huo. 
Mazoezi ya viungo yakifanyika.
Mazoezi yakiendelea.
Mazoezi yakiendelea.
Mazoezi yakiendelea siku ya kwanza ya tamasha hilo la michezo.
Mazoezi yakifanyika.
Jogging ikifanyika.
Mashabiki wakifuatilia michezo iliyokuwa ikifanyika.
Michezo ikiendelea.
michezo ikiendelea.
Kivumbi kikitimka wakati wa michezo hiyo.

Mazoezi yakifanyika.
Timu    zikiingia uwanjani.
Picha ya pamoja.
Mchezo wa Netball ukifanyika.

SINGIDA GOLDEN MARATHON YAZINDULIWA RASMI

 Mwenyekiti wa Kamati ya Singida Golden Marathon ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Singida Golden Runners , Raymond Msangi akizunguza wakati wa uzinduzi wa Singida Golden Marathon uliofanyika juzi Viwanja vya Peoples mjini hapa  ambao ulifanyika sanjari na kuanza mazoezi ya Jogging kuelekea kilele cha mbio hizo zitakazofanyika Julai 23, 2022..
Katibu wa Singida Golden Mrathon Nemes Mushi akizungumza kwenye uzinduzi huo 
Washiriki wa mazoezi hayo wakijiandaa kwa kufanya jogging.
Wadau wakiwa viwanja vya Peoples wakati wa uzinduzi huo.
Mazoezi yakifanyika kabla ya kuanza kukimbia kilometa tano.

Monday, May 16, 2022

DC IKUNGI ATOA NENO LINALOWAHUSU WATUMISHI WA UMMA

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro.


NIMEONA niandike machache kwa leo yanayowahusu watumishi wa umma ambao ni walimu, watu wa sekta ya afya na kada mbalimbali katika utumishi wa umma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alitangaza kupunguza Kodi ya mishahara (PAYE) kwa 1% kwa watumishi wa umma, akaenda mbali akafuta tozo ya 6% kwa Watumishi wa umma wenye Mikopo ya Elimu ya Juu na kuondoa adhabu ya 10% kwa kuchelewa kulipa Mkopo huo.

Katika kuimarisha utawala bora na kutoa huduma bora kwa wananchi Rais Samia amewapandisha Vyeo na madaraja Watumishi 198,215 hili sio jambo dogo ni jambo linalohitaji ujasiri na haswa ukizingatia kuwa kila anaepandishwa daraja ana stahiki zake katika daraja husika.

Katika kipindi cha mwaka mmoja Rais Samia ameridhia kuajiriwa zaidi ya watumishi wapya 40,000 katika kada mbalimbali zikiwemo afya na elimu.

Katika eneo la utumishi wa umma, Mhe Rais Samia ameridhia pia kulipa malimbikizo ya mishahara kwa Wafanyakazi 75,000 ambayo ni zaidi ya  Bilioni 124.3 fedha ambazo sasa zimeingia katika mzunguko wa maisha ya watumishi hatua inayoongeza mzunguko wa fedha mitaani.