Monday, October 17, 2022

WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUJILINDA NA UHALIFU WA MTANDAO

Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama Mtandao wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Stephen Wangwe akiwasilisha mada ya kuwajengea uelewa juu ya Elimu ya Usalama Mtandao Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha jana  Oktoba 17, 2022.

Elimu ya usalama mtandao kwa Menejimenti ya Chuo cha Ufundi cha Arusha ikitolewa. 

Mtaalam wa Usalama Mtandao na Uchunguzi wa Kidijitali, Bw. Yusuph Kileo akiwasilisha mada ya kuwajengea uelewa juu ya Elimu ya Usalama Mtandao Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha jana  Oktoba 17, 2022. 

Matukio mbalimbali katika picha wakati wa mafunzo ya elimu ya Usalama Mtandao kwa Menejimenti ya Chuo cha Ufundi cha Arusha.

Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama Mtandao wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Stephen Wangwe (kulia) akimkabidhi tshirt Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Dkt. Cairo  P.  Mwaitete mara baada ya semina ya Usalama Mtandao kwa wanafunzi wanaojiunga na Chuo hiko jana Oktoba 17, 2022, jijini Arusha.

Matukio mbalimbali katika picha wakati wa mafunzo hayo.
Picha ya pamoja.
Taswira ya mafunzo hayo.
Michango mbalimbali ikitolewa wakati wa mafunzo hayo.
Wawezeshaji wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja.
Mafunzo yakiendelea.
Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama Mtandao wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Stephen Wangwe (kulia) akimkabidhi tshirt Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Dkt. Cairo  P.  Mwaitete mara baada ya semina ya Usalama Mtandao kwa wanafunzi wanaojiunga na Chuo hiko jana Oktoba 17, 2022, jijini Arusha.
 

Na Mwandishi Wetu, WHMTH, Arusha. 

Watumishi wa umma na binafsi wametakiwa kuwa makini na chochote wanachofanya mtandaoni ili kujilinda na changamoto za uhalifu wa mtandao ambapo katika zama hizi za kidijiti taarifa binafsi au za taasisi zimegeuka kuwa malighafi muhimu kwa wahalifu wa mtandao.

Vifaa na mifumo ya TEHAMA ambayo hutumika kupitisha taarifa binafsi au za taasisi vimekuwa vikishambuliwa zaidi na wahalifu kwa njia mbalimbali lengo likiwa ni kupata taarifa za kibenki, nywila n.k.

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama Mtandao wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Stephen Wangwe wakati akitoa elimu ya usalama mtandao kwa Menejimenti ya Chuo cha Ufundi cha Arusha jana  Oktoba 17, 2022, jijini Arusha.

Mhandisi Wangwe amesema kuwa suala la usalama mtandao ni changamoto ya kidunia ambapo takwimu zinaonesha kila siku majaribio milioni 156 ya uhalifu kwa njia ya barua pepe au tovuti hutokea na majaribio milioni 16 hufanikiwa.

Ameongeza kuwa Serikali kupitia Wizara hiyo imeendelea kuimarisha usalama wa mtandao kwa kujenga mazingira wezeshi na mifumo imara ya kusimamia sera, sheria, kanuni na miongozo ya usalama wa mtandao pamoja na kutoa elimu kwa makundi yote katika jamii ili kupunguza mianya ya uhalifu wa mtandaoni.

“Usalama wa mtandao huanza na mtu binafsi, pamoja na juhudi nyingi zinazofanywa na Serikali, bado kila mtu analo jukumu la kuchukua tahadhari na kujilinda na uhalifu unaofanywa kwa njia ya mtandao”, Amesema Wangwe.

Naye Mtaalamu wa Masuala ya Usalama Mtandao na Uchunguzi wa Kidijiti wa African ICT Alliance (AfICTA) kutoka Tanzania, Bw. Yusuph Kileo amesema kuwa, namba ya siri imara na madhubuti ni kitu cha kwanza na cha msingi za kujilinda na uhalifu wa mtandao lakini pia umakini na kuchukua tahadhari kutawaepusha watumiaji kuwa wahanga wa uhalifu wa mtandao.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Wangwe amewataka wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu cha Arusha (IAA) kutafakari mara mbili kabla ya kuweka chochote mtandaoni ili kujiepusha na matukio ya udhalilishaji na utapeli ambayo yanaweza kuathiri maisha yao ya baadae.

Akijibu maswali mbalimbali ya wanafunzi chuoni hap oleo oktoba 17, Mhandisi Wangwe ametolea ufafanuzi masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na huduma ya bure ya kutafuta simu iliyoibiwa na umakini wa Serikali wa kujiridhisha kabla ya kuzifungia namba za simu zilizoripotiwa kufanya uhalifu kupitia namba 15040.

Mapokeo ya Elimu ya Usalama mtandao kwa Menejimenti ya Chuo cha Ufundi cha Arusha na wanafunzi wa Chuo cha IAA yamekuwa ni mapokeo chanya ambapo kwa nyakati tofauti wamekiri kuwa elimu iliyotolea imewafungua katika maeneo mengi sana na matamanio yao ni Wizara kuendelea kutoa mafunzo haya mara kwa mara na kuyafikia makundi yote ya kijamii. 

Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

ESTL YAANZA RASMI KUTOKOMEZA MATUKIO YA UKATILI WILAYA YA IKUNGI

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Richard Rwehumbiza,  akifungua kikao cha tathmini na uzinduzi wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia, ikiwemo ukeketaji, na mila potofu mbele ya Kamati ya MTAKUWWA ngazi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kupitia ufadhili wa Shirika la Foundation Civil Society (FCS). Kutoka kushoto ni  Mkurugenzi wa ESTL Joshua Ntandu Lisu na kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya hiyo, Mariam Mwandikile ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho.  

 Mkurugenzi wa ESTL Joshua Ntandu  Lisu, akitoa taarifa ya mradi waliofanya kwa kipindi cha miaka minne katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC na Singida Manispaa. Katikati ni Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Margaret Kapolesya .
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ikungi, Mariam Mwandikile akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mganga wa Shirika la ESTL, Getrude Liberatus akizungumzia mbinu mpya zinazotumika kuwafanyia ukatili wa kijinsia watoto.
 Mkaguzi wa Uhamiaji Wilaya ya Ikungi Abel Shindayi  akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ikungi (OCD) Suzana Kidiku (kulia) na  Mkaguzi wa Uhamiaji Wilaya ya Ikungi Abel Shindayi wakiwa kwenye kikao hicho.

 Afisa Mawasiliano na Vijana wa shirika hilo Edna Mtui (kushoto) akiteta jambo na Ofisa wa shirika hilo, Aisha Msuya.

Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Margaret Kapolesya .akisisitiza jambo kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Wadau wakiwa kwenye kikao hicho.

Muhudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wa shirika hilo, Hawa Njolo akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Afisa Miradi wa Shirika hilo, John Nzungu akielezea utekelezaji wa mradi huo wilayani Ikungi.
Sheikh wa Kata ya Ikungi, Salum Ngaa akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Wilaya ya Ikungi, Joyce Madadi akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ombeni Komba akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Msimamizi wa Miradi wa shirika hilo, Chrian Zimbaiya akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Taswira ya kikao hicho.
Picha ya pamoja.
Wafanyakaziwa ESTL wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao hicho. 

 Na Dotto Mwaibale,Singida. 

SHIRIKA la Empower Society Transform Lives (ESTL) linalojihusisha na masuala ya kupinga ukatili wa kijinsia  limezindua rasmi huduma za elimu na uwezeshaji jamii kwenye wilaya ya Ikungi mkoani hapa ambazo pamoja na mambo mengine zitajikita katika kuhakikisha elimu ya kutosha inatolewa kwa wana Ikungi hususani kwenye kata mbili za Kikio na Misughaa katika muktadha wa dhana hasi ya kuondokana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.

Kabla ya huduma hizo kutolewa wilayani Ikungi shirika hilo lisilo la kiserikali kwa udhamini wa Ubalozi wa Finland,Uholanzi na Shirika la Foundation Civil Society (FCS)  katika kipindi cha miaka minne (2018/2022 limefanikiwa kuzifikia takribani kata 28 ndani ya Wilaya za Singida Manispaa na Singida Vijijini kwa utekelezajiwa huduma kama hizo.

Kwa mujibu wa shirika hilo huduma nyingine walizofanikiwa kuzitoa kwenye maeneo hayo ni pamoja na uanzishwaji wa utaratibu wa utoaji huduma mbalimbali ndani ya eneo moja (One Stop Centre), uundaji wa kamati za MTAKUWWA zipatazo 39 sambamba na uanzishaji wa mfumo maalumu wa TEHAMA ambao umekuwa ukifanya kazi ya kufuatilia kesi za matukio ya ukatili-ambapo kwasasa shirika lina mpango wa kuuwezesha mfumo huo kufanya kitaifa.

Akizungumza wakati akifungua kikao cha tathmini na uzinduzi wa mradi huo, mbele ya kamati ya MTAKUWWA ngazi ya halmashauri ya wilaya ya Ikungi kupitia ufadhili wa Shirika la Foundation Civil Society (FCS) , Mkurugenzi wa ESTL Joshua Ntandu Lisu alisema wilaya hiyo ina vihatarishi vikubwa vya matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto kutokana na jiografia yake ya mipaka na wilaya za jamii ya wafugaji za Hanang (Manyara) na Kondoa (Dodoma) zilizopo kwenye bonde la ufa ambazo kwa kiwango kikubwa zimegubikwa na matukio ya ukeketaji.

Hata hivyo, mjumbe wa kamati ya mtakuwwa ambaye ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ikungi (OCD) Suzana Kidiku alisema jeshi hilo limekuwa kwenye harakati mbalimbali za kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia kwa nyakati tofauti, ambapo kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu limefanikiwa kunusuru kwa kuwarejesha shuleni wanafunzi watatu ambao walikuwa hatarini kukatisha masomo yao kutokana na matukio ya ukatili.

Pia Kidiku alisema jeshi hilo wilayani hapa katika kipindi hicho limefanikiwa kufikisha kesi tatu za matukio ya ukatili wa kijinsia kwenye vyombo vya sheria, ambapo hata hivyo, mahakama iliwakuta watuhumiwa wakiwa na hatia, na wawili walihukumiwa vifungo vya hadi miaka 30 huku mmoja akiadhibiwa kifungo cha maisha.

Aidha, Mkaguzi wa Uhamiaji Wilaya ya Ikungi Abel Shindayi alisema kuna haja ya mamlaka za elimu kufanya marekebisho ya mfumo wa mtaala wa elimu uliopo kwa kuongeza kipengele cha somo la ukatili wa kijinsia, athari zake na namna bora ya kukabiliana na matukio hayo kuanzia ngazi za shule za msingi hadi vyuo ili kuwafanya wanafunzi kuwa na uelewa mpana wa masuala hayo.

Awali, akifungua kikao cha tathmini na uzinduzi wa mradi huo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Richard Rwehumbiza aliwasihi viongozi wa shirika hilo kutofanya kazi kwenye kata mbili pekee bali wasambae kwenye kata zote ili kusaidia kuelimisha jamii hiyo kuachana na unyanyasaji wa aina zote hasa ukeketaji-ambao kwa sasa umeanza kuathiri hadi watoto wenye umri wa chini ya siku saba.

Sunday, October 16, 2022

MWANDISHI WA HABARI MWANDAMIZI AFARIKI DUNIA

Mwanahabari Frank Mbunda, enzi za uhai wake
 

Na Dotto Mwaibale 

Mwandishi wa Habari Mwandamizi, Frank Mbunda amefariki dunia leo Oktoba 16, 2022 Hospitali ya Mkoa General Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kufikishwa jana jioni.

Mtoto wa Marehemu Ashery Mbunda amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuwa taratibu za maziko zinafanyika Makole Dodoma nyumbani kwa mlezi wake wa Kiroho.

Mke wa marehemu, Yunice Mbunda amesema kesho Oktoba 17 itafanyika Misa ya kumuombea marehemu katika Kanisa la Anglikana Makole Dodoma na kesho kutwa Oktoba 18, 2022 mwili wake utasafirishwa kwenda nyumbani kwake jijini Dar es Salaa ambako taratibu za mazishi yake zitafanyika.

Marehemu Frank Mbunda ameacha mjane na watoto wanne, wakike wawili na wakiume wawili.

Frank Mbunda enzi za uhai wake amewahi kuandikia magazeti mbalimbali na hadi kifo chake alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kinarani Co.General Publishers and Priting iliyokuwa ikichapisha gazeti la Tanganyika Tanzania.

RC KILIMANJARO AONGOZA KONGAMANO KUJADILI MAONO YA MWALIMU NYERERE


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu akiongoza Kongamano la kumbukizi ya miaka 23 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa ,Mwalim Julius Nyerere lililofanyika wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo akizungumza katika Kongomano la kumbukizi ya miaka 23 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa ,Mwalim Julius Nyerere lililofanyika wilayani humo..
Askofu Mstaafu wa Kanisa Katoliki ,Jacob Koda akichangia jambo kwenye kongamano hilo.

Kongamano likiendelea. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Abdallah Mwaipaya, Mkuu wa Wilaya ya Siha, Thomas Abson, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maige na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Same, Abdillah Mnyambo.

Mada zikitolewa.
Kongamano likiendelea.

Mada zikiendelea kutolewa kwenye kongamano hilo.

Kongamano likiendelea 

Na Mwandishi Wetu, Same Kilimanjaro. 

MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo amefungua Kongomano la kumbukizi ya miaka 23 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa ,Mwalim Julius Nyerere ambalo pamoja na mambo mengine limejadili maono mbalimbali ambayo baba wa taifa aliyoyafanya enzi za uhai wake.

Mpogoro wakati akifungua kongamano hilo ametumia nafasi hiyo kuelezea kwa kina jitihada ambazo zilifanywa na Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuwa wamoja na kudumisha mshikamano huku akipenda kuona watu wake wanapiga hatua kimaendeleo.Askofu Mstaafu wa Kanisa Katoliki,Jacob Koda ameiomba Serikali kufufua Viwanda vyote vilivyokuwa vikifanya uzalishaji enzi za Mwalimu Nyerere ikiwa kama njia mojawapo ya kumuenzi Mwalimu.

Kwa upande wake Askofu Koda aliyasema hayo wakati akitoa mada kuhusu Mchango wa Mwalimu katika kukuza uchumi na Maendeleo endelevu ambapo alisema Nyerere alijitahidi kuanzisha viwanda katika mikoa mbalimbali ili kukuza uchumi.

Alisema Baba wa Taifa alitambua ili nchi iweze kuwa na Maendeleo endelevu lazima kuwe na viwanda na ndipo alipoanzisha viwanda vya nguo kwenye mikoa karibu yote,kulikuwepo na viwanda vya ngozi vikitengeneza viatu,mabegi,kulikuwepo na viwanda vya magunia na kiwanda Cha General Tyre cha Arusha ambacho kilikuwa kinaaaminika kwa matairi bora Afrika Mashariki.

Wakati huo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ambaye  alikuwa mgeni rasmi katika Kongamano hilo aliahidi kuuchukua ushauri wa Askofu na kuufanyia kazi.

Katika kongamano hilo mada mbalimbali zilitolewa na watoa mada wabobezi waliopata bahati ya kumjua Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Saturday, October 15, 2022

MAKALA YA WIKI LA VIJANA MKOANI KAGERA PAMOJA NA KILELE CHA KUZIMA MWENGE WA UHURU 2022

Mjasiriamali Saimon Sirilo.

 

Kwa kushirikiana na Shirika la Restless Development  linalofanya kazi na Vijana tumeshiriki katika maadhimisho ya wiki la vijana na kuweza kubadilishana mawazo na vijana wengi wa Kitanzania mkoani kagera kwa kuwajengea uwezo katika mambo kadhaa ikiwemo namna ya kujiajiri,Afya na makuzi pia.

Kupitia mambo mtambuka yanayowahusu kujenga uchumi wa vijana nilifanikiwa kuwa moja ya wanajopo walioendesha mdahalo uliojikita katika kuzungumzia hatma ya uchumi wa vijana kupitia mafaniko,changamoto na mapendekezo kwa serikali.

Binafsi,nilitoa mawazo yangu kama ifuatavyo

1:Vijana kuwa na uthubutu na kuanzisha mambo/miradi japo kwa kidogo ili kuweza kuiaminisha serikali kuwa vijana tunao uwezo,maarifa,nguvu na ari ya kufanya kazi...hapa ndipo serikali itawashika mikono kupitia zile fedha asilimia 4 za vijana kutoka halmashauri.

Uthubutu huleta kuaminika zaidi kuliko maneno matupu,kijana mwenye uthubutu huaminika zaidi kuliko asiyeanza kabisa.

2: Vijana tujitahidi kutafsiri  fursa zinazotuzunguka katika jamii zetu ili kuifanya serikali ione fursa  hizo zina tija katika jamii zetu na kutupatia fedha kama mtaji.

Fursa zipo nyingi sana ila zinapaswa kutafsiriwa  kwa umuhimu wake, mfano, jamii moja inaweza ona fursa zaidi ya moja kwa kitu kile kile...Mti waweza kuwa na fursa nyingi kadiri atakavyoutafsiri mtu,mwingine anaona mti ni fursa ya mbao, mwingine fursa ya dawa,mwingine  fursa ya kiganga,mwingine fursa ya mazingira nk...hivyo ukienda kwa hoja hii ya tafsiri na kuelezea faida yake utaaminika zaidi.

Fursa zipo nyingi sana ila zinapaswa kutafsiriwa kwa umuhimu wake na hapa ndio hoja ya kusema vijana tubadili taaluma zetu kuwa fedha na ziendane na matumizi ama mahitaji ya jamii husika.

 *Changamoto zinazowakabili vijana na kushindwa kufikia malengo yao*

1: Ukosefu wa mtaji,hii ni kutokana na kutumia muda mwingi  masomoni na kurudi mtaani wakiwa hawana kitu kabisa.

2: Jamii kuwa na kasumba y kutowaani kulingana na sifa za vijana wachache kutoridhisha.

3: Vijana wasomi wamejengewa uwezo wa kuajiriwa zaidi kuliko kujiajiri,jambo hili huwapa changamoto vijana pale wanapokosa ajira walizozisotea kwa muda mrefu.Vijana wengi hujikatia tamaa ya kupambana baada ya kukumbana na ugumu wa maisha.

 *Mapendekezo*

1:Vijana waanzishe mawazo na kuunda vikundi wakapewe fedha halmashuri pamoja na mfuko wa vijana kutoka wizara  inayohusika na vijana na watu wenye ulemavu ambapo hata kijana mmoja mmoja huweza kukopesheka kwa masharti nafuu.

2: serikali iwaamini vijana na kuendelea kutengeneza miundombinu wezeshi ili kuwawezesha vijana kufikia malengo yao.

3: serikali ibadili mfumo kwa wasomi wanaopata fedha za mkopo kwaajili ya masomo yao basi ikifaa kiasi kidogo cha asilimia anachopata mnufaika basi atunziwe ili punde amalizapo masomo yake akabidhiwe fedha yake na iwe kama kiinua mgongo cha kumsaidia kuanza  biashara wakati akisubiria ajira na hii itamsaidia kuanza kurejesha huo mkopo aliopewa chuoni.

Mfano, kama mtu amepewa mkopo asilimia 100 basi wakati wa masomo yake akabidhiwe asilimia 80 kwa mwaka na asilimia 20 aitunziwe kila mwaka ili amalizapo masomo yake akabidhiwe ili iwe kama mtaji wake wa kuanzia maisha wakati anasubiria ajira yake kwani serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi sana kwa wanafunzi lakn hazirudi kutokana na vijana hao kukosa ajira.

 *Mwisho*

Sisi vijana tunaendelea kupambana na kujengeana uwezo sisi kwa sisi, pia tunaipongeza sana serikali ya awamu ya sita chini ya mama samia kwa mambo makubwa inayofanya kwa vijana kwa mustakabali wa Taifa letu na tupo bega kwa bega na Mh. Rais kuhakikisha tunalijenga Taifa letu pendwa. 

Imeandaliwa na SAIMON SIRILO

MJASIRIAMALI


TAMUFO YAPONGEZWA KWA KUANDAA KWA MARA YA PILI SIKU YA MUZIKI DUNIANI

Wanamuziki wakitumbuiza katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Muziki Duniani yaliyofanyika wilayani Karatu mkoani Arusha Oktoba 1, 2022..
Wasanii wa kikundi cha Ngoma  cha Mahahaha wilayani Karatu wakitoa burudani wakati wa maadhimisho hayo.

Mlezi wa maadhimisho haya hapa nchini, Toriano Salamba

Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel. 
Mlezi wa TAMUFO, Dk.Frank Richard akizungumza wakati wa maadhimisho hayo.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho hayo.

Na Dotto Mwaibale, Arusha. 

UMOJA wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) umepongezwa kwa kuandaa kwa mara ya pili Siku ya  Muziki Duniani (International Music Day 2022) hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stellah Joel alisema wamepokea pongezi nyingi kutoka kwa wadau wa muziki kuhusu maandalizi na maadhimisho ya siku hiyo.

Alisem maadhimisho ya siku hiyo yanafanyika kila mwaka ambapo wanamuziki hapa nchini wanaungana na wenzao duniani kote kufurahia siku hiyo.

Alisem  maadhimisho hayo  yalianzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) miaka mingi iliyopita lakini kwa Tanzania TAMUFO ndio waanzilishi na kuwa lengo lao likiwa ni kupanua wigo kwa wanamuziki hapa nchini  kuweza kuungana na wenzao  kimataifa na kuinua hadhi ya muziki duniani na Tanzania kwa ujumla.

Alisem maadhimisho hayo kila mwaka hufanyika Oktoba 1 na kuwa hapa nchini yalianzishwa tangu mwaka 2021 na kitaifa yanafanyika jijini Arusha ambayo mwaka huu yalifanyika katika Uwanja wa Makumbusho ya Elimu Viumbe kuanzia Septemba 28  hadi kilele chake kilifanyika Oktoba 1, 2022, wilayani Karatu na kuhusisha wanamuziki wa kada zote.

Akizungumzia kwa nini maadhimisho hayo yanafanyika Arusha alisema sababu Arusha inaanza na herufi  A na ni katikati ya Afrika na hata harakati nyingi za kudai uhuru zilifanyika Arusha na ndio maana na wao wakaona wafanyie hapo lakini.baadae wataweza kuadhimisha katika mikoa mingine.

Mlezi wa TAMUFO na mmoja aa waanzilishi wa Dk. Frank Richard alisema wataendelea kuadhimisha siku hiyo kila  mwaka na akawaomba wadau wamaendeleo kutoa ushirikiano katika kuunga mkono juhudi hizi ili kuleta Maendeleo katika Tasnia ya Muziki  kwa ujumla

Dk. Richard aliishukuru Serikali, viongozi  wa Mkoa,  Wilaya,  Taasisi, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Cosota na Makumbusho ya Taifa kwa ushirikiano waliutoa na kuhakikisha maadhimisho hayo yanafanyinka vizuri huku pia akilishuru jeshi la polisi.

Mlezi wa maadhimisho haya hapa nchini, Toriano Salamba alisema watafanya maboresho makubwa katika maadhimisho haya kuhakikisha yanakuwa katika ubora wa kimataifa. 

Tuesday, October 4, 2022

NSSF SINGIDA YAKAMILISHA MAANDALIZI WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA DUNIANI

Meneja  wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Singida, Oscar Kalimilwa akizungumzia maandalizi ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani ambapo kilele chake ni Octoba 7, 2022.
Kazi zikiendelea ofisi za mfuko huo.
Kazi ikiendelea.
Muonekano wa maandalizi kuelekea kilele cha wiki hiyo.

 

Dotto  Mwaibale na Philemon Mazalla Singida

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Singida umekamilisha maandalizi ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani ambapo kilele chake ni Octoba 7, 2022 siku ya Ijumaa.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Meneja wa NSSF Mkoa wa Singida, Oscar Kalimilwa alisema na wao wanaadhimisha siku hiyo kuonesha kuwajali wateja wao chini ya kauli mbiu isemayo ‘Huduma bora ndio kipaumbele chetu’

Alisema katika maadhimisho hayo wameandaa baadhi ya shughuli ambazo watazifanya siku hiyo ya kilele ambapo watachangia damu, kutoa msaada wa vitu mbalimbali Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida ya Mandewa.

Alisema siku hiyo ya kilele wameandaa keki maalumu ambayo itakatwa na wataila pamoja na wateja wao ikiwa ni ishara ya kuwathamini kwani ndio wanaowafanya waendelee kuwepo na kuwa wamejipanga vilivyo kuifanya siku hiyo kuwa ya mafanikio kwao na wanachama wao.

Aidha Kalimilwa alisema wataitumia siku hiyo kutoa elimu kwa wanachama ambao hawana elimu kuhusu mifuko hiyo ya jamii na akatoa wito kwa wananchi na wanachama wao waendelee kuiamini NSSF kwani kuwepo kwake kunasaidia kupambana na majanga yanayomtokea binadamu.