JAMII YETU BLOG
Thursday, April 18, 2024
Tuesday, April 9, 2024
MSD YAKUTANA NA WADAU WAKE KANDA YA IRINGA, RC RUVUMA ATAKA WELEDI SEKTA YA AFYA
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali. Ahmed Abbas Ahmed (kushoto) akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji wa Bohari ya Dawa (MSD), Victor Sungusia wakati wa mkutano mkuu wa MSD na wadau wake wa Mkoa wa Ruvuma uliofanyika Aprili 8, 2024,
Na Mwandishi Wetu, Ruvuma
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali. Ahmed Abbas Ahmed, amewataka watumishi wa sekta ya afya Mkoani Ruvuma, kuzingatia weledi na kutoa huduma bora kwa wananchi, ili kuakisi maboresho na uwekezaji mkubwa uliofanywa kwenye sekta ya afya, chini ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita.
Kanali Ahmed amesisitiza kuwa, serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa fedha nyingi kwa ajili ya maboresho na ujenzi wa miundombinu ya afya mathalani majengo, ununuzi wa bidhaa za afya
na kuwezesha ajira za kutosha, lengo likiwa kuinua hadhi ya huduma zinazotolewa nchini, hasa zinazomgusa mtanzania wa kawaida.
Kanali Ahmed ametoa rai hiyo hii leo, wakati wa akifungua kikao kazi baina ya MSD Kanda ya Iringa na wadau wake kutoka halmashauri saba za mkoa wa Ruvuma (Madaba Tc, Madaba Dc, Songea MC, Songea DC, Nyasa DC, Mbinga TC na Mbinga DC), kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ruwiko, ulioko Manispaa ya mji wa Songea.
Mkuu huyo wa Mkoa amewakumbusha viongozi hao wa sekta ya afya Mkoani humo, kufanya maoteo yao ya bidhaa za afya kwa usahihi, umakini na kwa wakati ili kuiwezesha Bohari ya Dawa (MSD) kutekeleza majukumu yake ya ugavi wa bidhaa za afya kwa weledi.
Mhe. Ahmed amewataka pia watendaji hao kusimamia ukusanyaji wa mapato, na kutumia vyema vyanzo vyao vingine vya mapato katika kulipa madeni ya MSD, huku akiwakumbusha pia kuhakiki taarifa sahihihi za utunzaji na utoaji wa bidhaa za afya, ili kuepuka upotevu wa bidhaa hizo.
Katika hatua nyigine, Mkuu huyo wa mkoa ameipongeza MSD kwa utendaji wake katika kuboresha hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya, huku akiwapongeza kwa kuitisha mkutano huo wa wadau kwani utasaidia kuboresha mahusiano na mawasiliano.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ugavi na uendeshaji wa MSD Victor Sungusia, amebainisha maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanywa na MSD katika nyanja mbalimbali kupitia majukumu yake makuu ya uzalishaji, ununuzi, utunzaji na usambazaji.
Bw. Sungusia amebainisha jinsi MSD ilivyojizatiti katika utekelezaji wa majukumu yake kupitia mifumo ya kisasa ya kidigitali, ugatuzi wa majukumu ya Kanda, ujenzi wa viwanda mbalimbali vya dawa na vifaa tiba, maboresho ya mfumo wa usambazaji wa bidhaa, upanuzi wa maeneo ya uhifadhi na kuwajengea uwezo watumishi wake.
Naye Meneja wa MSD Kanda ya Iringa Bw. Robert Lugembe akiwakiribisha wajumbe wa kikao hicho, alibainnisha kuongezeka kwa uwezo wa MSD kuwahudumia wateja wake na kukidhi mahitaji, sambamba na maboresho ya upatikanaji wa bidhaa za afya mathalani vifaa tiba, mkoani humo.Meneja wa MSD Kanda ya Iringa Bw. Robert Lugembe akizungumza kwenye mkutano huo.
Friday, March 22, 2024
WADAU WA MSD WAHIMIZWA KUSIMAMIA MATUMIZI SAHIHI YA TAKWIMU BIDHAA ZA AFYA
Mkuu wa Wilaya ya Masasi Lauteri Kanoni, akifungua kikao cha wadau na wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Mtwara Machi 22, 2024.
...........................
Na Mwandishi Wetu, Mtwara
WADAU wa Afya wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Mtwara
wamehimizwa kusimamia matumizi sahihi ya takwimu za mnyororo wa ugavi wa bidhaa
za afya, ili ziwawezeshe kufanya maamuzi sahihi juu ya bidhaa hizo katika
maeneo yao.
Akifungua kikao cha wadau na wateja wa MSD kanda
ya Mtwara, Mkuu wa Wilaya ya Masasi Lauteri Kanoni amesema uwepo wa takwimu
sahihi unaiwezesha MSD kuagiza kwa usahihi bidhaa za afya na kuboresha
upatikanaji wa bidhaa hizo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
Aidha, amewashauri MSD kuhakikisha utaratibu wa
vikao vya mwaka vya wadau ni muhimu kwa
pande zote mbili, yaani Bohari ya Dawa (MSD) yenyewe na wadau ili kwa pamoja
kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya, kwa kujadili changamoto na kuzitafutia
utatuzi.
Kwa upande wake Meneja wa MSD Kanda ya Mtwara Tea Malay
ameeleza kuwa kwa sasa kanda ya MSD Mtwara inahudumia vituo vya kutolea huduma
za afya 631, na inasambaza bidhaa za afya kila baada miezi miwili.
Naye Meneja Huduma kwa Wateja na Miradi Dkt.
Pamella Sawa ameeleza kuwa vikao vya MSD na wadau wake kuanzia sasa vitakuwa
endelevu kila mwaka.
MSD Kanda ya Mtwara inahudumia mikoa ya Lindi,Mtwara na Wilaya ya Tunduru.Meneja wa MSD Kanda ya Mtwara Tea Malay, akizungumza kwenye kikao hicho
Tuesday, March 19, 2024
Sunday, March 17, 2024
UBALOZI WA UHOLANZI, SERIKALI WAZINDUA KITABU CHA MWONGOZO WA ULIMAJI VIAZI
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TANZANIA kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi wamezindua kitabu cha
mwongozo wa usajili wa aina za mbegu za viazi kwa lengo la kuimarisha ustawi wa
kilimo cha viazi na usalama wa chakula hapa nchini.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho wiki iliyopita
jijini Dar es Salaam,Balozi wa Ufalme wa Uholanzi hapa nchini, Wiebe de Boer
aliwaambia viongozi waalikwa na wageni mbalimbali kuwa hiyo ilikuwa hatua kubwa
katika safari yao ya kuimarisha sekta na kilimo cha viazi hapa nchini.
"Safari ambayo imechangiwa na ushirikiano wa miaka kumi kati ya
Tanzania na Uholanzi,katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, ushirikiano huu
umewavutia wakulima wa viazi wa Uholanzi kusajili aina zao za viazi nchini
Tanzania," aliongeza.
Alisisitiza kwamba si hivyo tu bali pia kuvutia uwekezaji kuongeza na
kupanua mnyororo wa thamani wa viazi na sasa wanatambua kwamba viazi kama
chakula kikuu cha kuhakikisha usalama wa chakula, kuzalisha kipato kwa wakulima
na kutengeneza fursa za ajira.
Balozi Boer alisema kuwa ufanisi na tija katika kilimo cha viazi unahitaji
matumizi ya mbegubora sambamba na kanuni bora za kilimo zilizochochea ukuaji wa
sekta ya kilimo.
Alisema nchini Uholanzi kuna aina zaidi ya 250 za viazi zinazolimwa kwa
matumizi mbalimbali,ikiwa ni pamoja na kuchemsha, kukaanga, krisps, kuoka,
kuzalisha mbegu na usindikaji wa wanga.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu
Tanzania(TOSCI), Dk Patrick Ngwediagi alisema kitabu hicho kitatumika kama
mwongozo kwa wagunduzi wa mbegu za viazi , wakulima na wawekezaji wa ndani na
nje ya nchini wanaovutiwa kuwekeza kwenye sekta ya viazi hapa nchini.
"Kwa kweli leo ni hatua muhimu kwa sababu kitabu hiki kitasaidia
wakulima kuwa na taarifa za kutosha kuhusu sera, sheria zinazosimamia sekta ya
kilimo pamoja na kuangalia changamoto na fursa zilizopo nchini kwenye kilimo
cha viazi," alisistiza Dr Ngwediagi.
Dk Ngwediagi alisema kuwa kitabu hicho kitawapa wakulima na wagunduzi hatua
kwa hatuajinsi ya kusajili mbegu zao nchini na mchakato wa kuzalisha mbegu bora
ili kuhakikisha ukuaji wa sekta hiyo.
“Jinsi hizi zote ni taratibu za hapa nchini katika kuimarisha ukuaji wa
sekta na mbegu zote lazima zisajiliwe kwenye Daftari la Taifa la mbegu katika
juhudi za serikali kuimarisha usalama wa vyakula kwa watanzania,” aliongeza.
Mshauri wa Kilimo wa Ubalozi wa Uholanzi, Bart Pauwels alisema kuwa Ubalozi
wa Uholanzi hpa nchini utaendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya
Tanzania, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na sekta binafsi kwa ujumla ili
kuhakikisha inakuza ukuaji wa sekta ya viazi.
“Kilimo bora ni injini ya ukuaji wa sekta, Ubalozi wa Uholanzi utaendelea
kutoa msaada wasekta hii kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika
kuboresha kilimo kwa kuleta piateknoloji na ujuzi mwingine wa kitaalamu,”
aliongeza.
Kwa miaka 10 sasa, Tanzania na Uholanzi zimekuwa na ushirikiano mzuri
katika sekta ya viazi.Kupitia ushirikiano huu, jumla ya aina 16 za viazi
zilisajiliwa na kati ya hizo 12 ni aina za Kiholanzi zinazotoa mavuno mengi,
kustahimili ukame na wadudu.
Maendeleo haya yalivutia biashara zaidi kwenye mnyororo wa viazi kutoka kwa
ufugaji, kukua hadi usindikaji. Ili kusaidia sekta hii zaidi, Ubalozi
uliiwezesha TOSCI kutoa mwongozo wa hatua kwa hatua kuhusu taratibu za kuchukua
iwapo mwekezaji anataka kusajili aina ya viazi nchini Tanzania kwa ajili ya
biashara. Kitabu hiki kimeidhinishwa na TOSCI kwa matumizi ya Tanzania.
ujumbe wa wafugaji 30 wa viazi vya Uholanzi, watafiti, wakulima wanaojihusisha na uendelezaji wa aina za viazi hivyo wametembelea Tanzania. Lengo ni kufahamiana na mahitaji ya soko, upendeleo na kupokea maoni kutoka kwa wakulima. Taarifa hizi zitatumika katikautafiti na ukuzaji wa aina mpya kwa Tanzania.
Saturday, March 16, 2024
MAAFISA WATENDAJI WATAKIWA AJENDA YAO KUWA ANWANI ZA MAKAZI, KUHAKIKI TAARIFA ZA WANANCHI
Na Dotto Mwaibale, (Singidani Blog)
MAAFISA Watendaji wa Mitaa kote nchini wametakiwa katika vikao vyao vyote
vya msingi ajenda yao kubwa iwe ni anwani za makazi pamoja na uhakiki wa taarifa
za wananchi.
Ombi hilo limetolewa Machi 15, 2024 na Mtaalamu wa Mfumo wa Anwani za Makazi kutoka Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (WHMTH), Innocent Jacob wakati wa siku ya pili ya mafunzo ya siku 14 kwa watendaji wa kata, mitaa, wenyeviti wa Serikali za mitaa na vijiji yanayohusu namna ya kukusanya taarifa za Anwani za Makazi Manispaa ya Singida yaliyoanza Machi 14, 2024 ambayo yameandaliwa na wizara hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kuwa siku mbili kati ya hizo 14 zitatumika kwa ajili ya kuhakiki taarifa. .
Jacob alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwawzesha wenyeviti hao ili waweze
kutoa taarifa kwa wanananchi za zoezi hilo ndani ya siku hizo na wananchi nao
waweze kutoa za kwao kama NIDA, namba ya simu, Tin namba ya biashara na taarifa
nyingine za majengo, makazi kama walivyoelekezwa watendaji wa mitaa jinsi ya
kulifanya zoezi hilo.
"Watendaji wa mitaa ndio watakao kwenda kukusanya taarifa hizi kwa
wakazi wao kwa sababu katika maeneo yote ya utawala wao ndio wahusika wakubwa
na watashirikiana na wenyeviti wa mitaa kufanya kazi hiyo," alisema Jacob.
Alisema Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (WHMTH), kwa
kushirikiana na TAMISEMI, wameandaa zoezi hilo kwa lengo la kuhakiki taarifa za
makazi kwa awamu ya pili baada ya awali kufanyika kwa njia ya operesheni ambapo
huenda kuna baadhi ya wakazi hawakuweza kupata fursa ya kuingia katika
kanzidata ya Anwani za Makazi.
Alitaja baadhi ya vitu ambavyo viliweza kusahulika kuwekwa kwenye kanzidata
kuwa ni taarifa ya majengo, viwanja, majina katika vibao vya mitaa hivyo
kurudiwa tena katika zoezi hilo la awamu ya pili la uhakiki.
Jacob alisema umuhimu wa Anwani za Makazi zitarahisisha utambuzi kwa wakazi
wa eneo husika na kuweza kupata huduma mbalimbali kwa kufikiwa kiurahisi mahala
walipo kwa kutumia programu tumizi kwa ajili ya umma inayoitwa NAPA ambayo
inapakuliwa kupitia simu janja ambapo wananchi wote hapa nchini wakiwemo wa
Manispaa ya Singida wataweza kuingia katika mfumo huo kwa kuandika NAPA
Tanzania.
Alisema mafunzo hayo yanafanyika Manispaa ya Kigoma, Iringa na Singida na
yatakuwa endelevu kwa kufanyika katika mikoa mingine.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Dkt. Adrianus
Kalekezi alisema katika mafunzo hayo wataalamu wanaelekeza namna ya kuingiza
taarifa katika mfumo wa Anwani za Makazi na kuwa hivi sasa wanauhisha taarifa
za awali baada ya kazi hiyo kufanyika awamu ya kwanza.
Dkt. Kalekezi alisema suala hilo la Anwani za Makazi ni la muhimu katika
manispaa hiyo kwani wananchi watapata huduma kwa urahisi na alitumia nafasi
hiyo kuwaomba wananchi kuilinda miundombinu ya Anwani za Makazi iliyowekwa kama
vibao vinavyoonesha majina ya mitaa na barabara na kueleza kuwa ni lazima
ilindwe ili waweze kunufaika na zoezi hilo kwani bila miundombinu hiyo inakuwa
vigumu kwao kuelekezwa na kuitambua mitaa na barabara.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mwankoko, Habiba Juma akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo alisema zoezi hilo litawarahisishia kutoa huduma kwa wananchi na kupunguza gharama ya fedha na muda kutoka sehemu moja kwenda nyingine na wananchi wataweza kupata huduma kupitia anuani za makazi.Mtaalamu wa Mfumo wa Anwani za Makazi kutoka WHMTH, George Leonard, akitoa mafunzo kwa watendaji hao.Mtaalamu wa Mfumo wa Anwani za Makazi kutoka WHMTH, Janeth Peter , akiwajibika wakati wa mafunzo hayo.Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Dkt. Adrianus Kalekezi, akizungumzia zoezi hilo.
Wednesday, March 13, 2024
SINGIDA HAWAPO TAYARI KUWA DAMPO LA DAWA, VIFAA TIBA VISIVYO BORA
Katibu Tawala Msaidizi wa Huduma za Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Singida, Stanslaus Choaji ambaye alikuwa mgeni rasmi akifungua mafunzo hayo............................Na Dotto Mwaibale, (Singidani Blog)
MKOA wa Singida hautakuwa tayari kuwa dampo la matumizi ya dawa, vitendanishi na vifaa tiba ambavyo havina havina ubora.
Katibu Tawala Msaidizi wa Huduma za Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Singida, Stanslaus Choaji aliyasema hayo Machi 12, 2024 wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya wataalamu, wakaguzi na wafamasia wa Halmashauri za wilaya ambao wanakagua dawa, vifaa tiba na vitendanishi yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA)
Choaji alisema jukumu la Serikali ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora za afya na kuweza kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali na kukuza uchumi wa Taifa.
"Hilo ni jukumu kubwa la Serikali na mtaona jinsi inavyofanya kila jitihada kadili itakavyowezekana kwa kutumia rasilimali mbalimbali ili kuwawezesha na kuona wananchi wanapata huduma bora za afya," alisema Choaji.
Alisema kutokana na jitihada hizo zinazofanywa na Serikali wakaguzi hao na watendaji kwenye eneo lao wanaweza kuonesha jinsi ambavyo wanashiriki kwenye hizo jitihada za Serikali kwa kutekeleza majukumu hayo kama vile inavyotakiwa.
Choaji alisema majukumu ya wataalamu hao ni ya msingi kwa sababu yanahusisha maisha ya binadamu hivyo kutekeleza jukumu hilo la kusaidia binadamu ni kutekeleza jukumu la Mungu aliye tuumba.
Alisema kutenda tofauti na majukumu hayo na kuhakikisha dawa, vifaa tiba na vitendanishi vinavyotumika na binadamu ni kwenda kinyume kabisa na kusudio la Mungu la kumuumba binadamu na mifugo ambayo nayo ni viumbe hai.
Aliwaomba kufanya kaguzi zao kwa kuzingatia kanuni na maadili kwa lengo la kulinda afya za jamii na kuwahakikishi uwepo wa bidhaa salama
"Tusingependa sisi Mkoa wa Singida tuwe na changamoto ya matumizi ya vifaa hivyo ambavyo havina sifa," alisema Choaji.
Kwa upande wake Meneja wa TMDA Kanda ya Kati, Sonia Mkumbwa alisema kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanalinda afya ya jamii kwa kuhakikisha bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi ni bora salama na zenye ufanisi.
Alisema ili jukumu hilo liweze kutekelezeka kwa kuzingatia ukubwa na upana wa nchi yetu yenye halmashauri za wilaya na mikoa mingi takribani 26 kwa upande wa Tanzania Bara TDMA kwa kuzingatia uchache wa watumishi wake waliona haitakuwa rahisi kufika kila kona ya nchi ndipo kanuni ya kukasimu baadhi ya majukumu na madaraka ya TMDA iliandaliwa na kupitishwa ili majukumu hayo yaweze kukasimiwa kwa halmashauri za wilaya.
Alisema majukumu hayo yamepelekwa katika halmashauri hizo ili ziweze kusaidia kufanya baadhi ya majukumu ya TMDA kwa kufanya ukaguzi na kuhakikisha wanafuatilia bidhaa ziwe bora na salama katika soko pia kufanya usajili wa maeneo ya kutolea huduma ambayo yapo chini ya TMDA.
"Leo tumewaalika wakaguzi kutoka halmashauri saba za Mkoa wa Singida tumejumuika kwa pamoja ili tuweze kupeana ABC jinsi ya kufanya kazi hizo ambazo zimekasimiwa katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa tupo hapa na wataalamu wakaguzi wa mifugo, wafamasia, wataalamu wa maabara na dawa na wote hawa wanahusika kwa namna moja ama nyingine kuhakikisha hizo bidhaa zinawafikia walengwa ambao ni wananchi.
Washiriki wa mafunzo hayo Upendo Kiula ambaye ni Mratibu wa Huduma za Maabara kutoka Wilaya ya Itigi na Alfred Rwamtoga Mfamasia kutoka Wilaya ya Manyoni wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kwani yamewajengea uwezo wa kukagua na kutambua bidhaa ambazo hazina ubora.Meneja wa TMDA Kanda ya Kati, Sonia Mkumbwa pamoja na mambo mengine akizungumzia kuhusu baadhi ya majukumu ya TMDA kukasimishwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa TAMISEMI.
Mshiriki wa mafunzo hayo Upendo Kiula ambaye ni Mratibu wa Huduma za Maabara kutoka Wilaya ya Itigi, akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo.
Mshiriki wa mafunzo hayo Alfred Rwamtoga Mfamasia kutoka Wilaya ya Manyoni akizungumza kuhusu mafunzo hayo
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.Taswira ya mafunzo hayo.
Afisa wa TMDA, Neema Debwe akichukua moja ya matukio wakati wa mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo hayo na mgeni rasmi