
Muonekano wa chumba cha kupumzikia wagonjwa wa figo wakati wakisubiri kupatiwa matibabu.
Muonekano wa jengo la wagonjwa wa dharura katika Hospitali hiyo.
Muonekano wa moja ya chumba chenye vifaa vya kuchujia damu katika Hospitali hiyo.
Na Mwandishi Wetu, Pwani
HOSPITALI ya Rufaa Mkoa wa Tumbi, wilayani Kibaha mkoani Pwani, inatarajia
kuanza kutoa huduma ya kusafisha damu kwa
wagonjwa wa figo kuanzia katikati ya mwezi Desemba mwaka huu.
Kuanza kwa huduma hiyo ni matokeo ya maboresho yaliyofanywa hospitalini
hapo na serikali ya awamu ya sita, ikiwemo ya kuiekeza Bohari ya Dawa (MSD)
kufunga vifaa tiba vya kisasa katika idara mbalimbali, ikiwemo idara ya
magonjwa ya figo ambako kumefungwa mashine 10 za kusafisha damu.
Daktari Bingwa wa Huduma za Ndani katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Tumbi
Dk. Adam Gembe, ambaye pia anasimamia Kitengo cha huduma ya kusafisha damu
amesema kwa sasa wamepata vifaa tiba vya kisasa kutoka Bohari ya Dawa na miongoni
mwa vifaa hivyo kuna mashine 10 za kusafisha damu.
“Tunaishukuru MSD, kwa kutuletea
mashine za kuchuja damu lakini tunaiomba kuendelea kuboresha huduma ya upatikanaji wa
vitendanishi na vifaa tiba, vitakavyotusaidia kutoa huduma bila kukwama na kwa
wakati,” alisema.
Kwa upande wake Afisa Huduma kwa Wateja MSD Kanda ya Dar es Salaam Diana Kimario alitoa rai kwa hospitali kujenga tamaduni za kuwasilisha maombi ya dawa na vifaa tiba mapema kabla kuisha, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki kwa wakati.



No comments:
Post a Comment