Sunday, October 11, 2020

RC NCHIMBI: TUTACHUKUA HATUA KWA YEYOTE ATAKAYE HATARISHA AMANI YA NCHi

Mkuu wa  wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi  akihutubia wananchi, wazazi na wanafunzi wakati wa sherehe za mahafali ya kuhitimu kidato cha nne kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari.Mandewa wanaosali  Kanisa la Tanzania Assemblies of God la Evangelistic Christian Centre (ECC), mkoani hapa jana. 

Wanafunzi, wananchi na wazazi wakiwa kwenye mahafali hayo. 
Wananchi na wazazi wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mahafali yakiendelea.
Watoto wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wake wa wachungaji wa kanisa hilo wakiwa kwenye mahafali hayo.
Askofu wa kanisa hilo, Gasper Mdimi (kushoto) Mchungaji Abeli Manupa na Mwalimu Mkwiye Emmanuel (kulia) wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mahafali yakiendelea.
Wahitimu hao wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mkuu wa  wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, akimkabidhi cheti Mhitimu, Faraja Nyambi.
Mkuu wa  wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, akimkabidhi cheti Mhitimu, Betha Isaya.
Mkuu wa  wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, akimkabidhi cheti Mhitimu, Alex Stephano.
Mahafali yakiendelea.
Wahitimu hao wakiombewa.
Mgeni rasmi Mkuu wa  wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi na  viongozi wa kanisa hilo wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao. 

 Mkuu wa  wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi na viongozi wa kanisa hilo wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa kiislamu waliofika kanisani hapo kushiriki na wenzao kwenye mahafali hayo. 


Na Dotto Mwaibale, Singida


MKUU wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi amesema serikali haitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayehatarisha amani katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu. 

Nchimbi ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyasema hayo alipohutubia wananchi, wazazi na wanafunzi wakati wa sherehe za mahafali ya kuhitimu kidato cha nne kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mandewa wanaosali Kanisa la Tanzania Assemblies of God la Evangelistic Christian Centre (ECC), mjini hapa jana. 

"Kuna watu fulani fulani wanazungumza maneno yenye kila aina ya viashiria vya uvunjifu wa amani wakidhani huenda kipindi hiki cha kampeni serikali haipo kazini. Niwatahadharishe kamwe wasithubutu kufanya hivyo wataishia kwenye mkono wa sheria," alisema na kuongeza:"Mpaka mda huu serikali ipo, na Rais wetu sote bado ni Dk. John Pombe Magufuli. 

Katika hatua nyingine, 'Mama' Nchimbi alimpongeza Rais kwa ujasiri,na maono yake kwa namna ya pekee alipofanikiwa kulivusha salama Taifa dhidi ya janga hatari la Corona.

"Haya maamuzi sio mepesi mepesi tazameni nchi nyingine zinavyoendelea kuteseka mpka sasa...kwakweli tunamshukuru sana Rais na Mwenyezi Mungu aendelee kumuongoza na kumjalia hekima na busara ili mapenzi yake ya dhati kwa watanzania wenzake yazidi kushamiri." 

Aidha, katika mahafali hayo yaliyofanyika kwenye Kanisa la Tanzania Assemblies of God la Evangelistic Christian Centre (ECC), Nchimbi aliwakumbusha wazazi kuepuka kuwapa simu watoto wawapo masomoni ili kuwajengea nidhamu ambayo itakuwa ni msingi wa ufaulu na mafanikio yao kwenye tafakari ya masomo. 

Akizungumzia maisha ya wahitimu hao baada ya kidato cha nne, aliwaasa kuwa waangalifu na kuepuka mitego na vishawishi vya kidunia ambavyo vinaweza kuwatumbukiza katika mashimo ya dhambi na kuharibikiwa, ikiwemo kupoteza ndoto zao njema za maisha walizonazo. 

Kwa upande wake, Askofu wa kanisa hilo, Gasper Mdimi aliwataka wahitimu hao kutafakari sambamba na kuchukulia mahafali hayo na malezi waliyopewa kwa kipindi chote kama kiapo chao kwa Mungu cha kutotenda dhambi wala kurudia kutenda dhambi na wasisahau kila mmoja kuendelea kulinda usafi wa moyo popote pale watakapokuwepo.

Saturday, October 10, 2020

JUMUIYA YA WATUMIA MAJI WA BWAWA LA NHUMBU MKOANI SHINYANGA YAPATA VIONGOZI

Viongozi wa Jumuiya ya Watumia Maji wa Bwawa la Nhumbu Mkoa wa  Shinyanga waliochaguliwa juzi mkoani humo wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka kulia ni  Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Ndoshi Magadula, Mwenyekiti Msaidizi, Ndula Maboma, Katibu, John Boniphace, Mtunza Hazina,  Eunice Machiya, Mjumbe, Anastazia Mihambo na Mjumbe, Majiku Salumu. 

Afisa Maendeleo  ya Jamii Mkuu Bodi ya Maji Bonde la Kati, Halima  Faraji, akizungumza katika uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya ya Watumia Maji wa Bwawa la Nhumbu Mkoa wa  Shinyanga waliochaguliwa juzi mkoani humo.

Afisa Maendeleo  ya Jamii Mwandamizi wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, Nelea Bundala, akizungumza katika uchaguzi huo.

Kura zikihesabiwa.

Kura zikihesabiwa.
Mchakato wa uchaguzi ukiendelea. Kulia ni Afisa Maendeleo  ya Jamii Mwandamizi wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, Hhau Sarwatt, akishiriki uchaguzi huo. Kutoka kushoto ni Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni Afisa Uvuvi kutoka Wilaya ya Kishapu. Moses Zacharia, Afisa Mazingira kutoka Kampuni ya Williamson Diamonds Limited, Queen Tizeba na Fundi Sanifu kutoka Ofisi Ndogo ya Bonde la Kati- Shinyanga, Israel Chafumbwe.
Uchaguzi ukiendelea.
Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni Afisa Uvuvi kutoka Wilaya ya Kishapu. Moses Zacharia, akitangaza matokeo. .
Watendaji wa kata na wenyeviti wa vijiji wakiwa kwenye uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwigumbi Kata ya Mondo, Sospeter Mapinda, akizungumza kwenye uchaguzi huo.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Seseko, Hamis Ndege, akizungumza kwenye uchaguzi huo.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Mondo, Masanja Said, akizungumza kwenye uchaguzi huo.
Mhandisi kutoka Kampuni ya Williamson Diamonds Limited, Raphael Matola akizungumza kwenye 
uchaguzi huo.
Afisa Kilimo kutoka Manispaa ya Shinyanga Daniel Nsanzugwanko, akizungumza kwenye uchaguzi huo.
Fundi Sanifu wa Umeme na Vifaa vya Umeme wa Wakala wa Maji Safi na Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kishapu, Christopher Damas, akizungumza kwenye uchaguzi huo.
Picha ya pamoja baada ya uchaguzi huo.
Picha ya pamoja baada ya uchaguzi huo.


Dotto Mwaibale na Godwin Myovela, Shinyanga.


JUMUIYA ya Watumia Maji wa Bwawa la Nhumbu Mkoa wa  Shinyanga imepata viongozi wake kwa mara ya kwanza baada ya kufanyika uchaguzi  ambapo watahudumu katika nafasi zao kwa muda wa miaka mitatu.

Uchaguzi huo ulifanyika juzi eneo la Songwa nje kidogo ya Manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na watendaji wa kata na wenyeviti wa vijiji wanaotumia maji ya Bwawa hilo ambalo jumuiya hiyo itakuwa na jukumu la kulilinda.

Uchaguzi huo uliandaliwa na Bodi ya Maji Bonde la Kati ambao walitembelea vijiji nane na kufanya mikutano ya hadhara ya kuwapata wajumbe watatu kutoka katika kila kijiji ambao wameunda jumuiya hiyo kwa kuzingatia jinsia na makundi ya wafugaji, wakulima na watumiaji wa maji.

Baada ya mikutano hiyo Bodi ya Maji Bonde la Kati ilitoa mafunzo ya siku tatu kwa wajumbe hao na kuunda jumuiya hiyo yenye lengo la kujua wajibu wao na namna ya kulinda rasilimali za maji.

Katika uchaguzi huo Ndoshi Magadula alichaguliwa kuwa Mwenyekiti kwa kupata kura 16 sawa na asilimia 7 huku nafasi ya Mwenyekiti Msaidizi ikichukuliwa na Ndula Maboma ambaye alipata kura 5 sawa na asilimia 20.8.

Nafasi ya Katibu ilikwenda kwa John Boniphace ambaye alipata kura 22 sawa na asilimia 91.7 huku Eunice Machiya akichaguliwa kuwa Mtunza Hazina  kwa kupata kura 16 sawa na asilimia 66.7.

Katika uchaguzi huo walichaguliwa wajumbe wawili ambao ni Anastazia Mihambo ambaye alipata kura 15 sawa na asilimia 62.5 na Majiku Salumu aliyepata kura 16 sawa na asilimia 66.7.

Akizungunza kwa niaba ya wenzake Magadula alisema watashirikiana na wana jumuiya hiyo na kuhakikisha kila kilichokusudiwa kinakwenda sawa ikiwa ni pamoja na kulinda rasilimali  za maji katika eneo hilo hasa Bwawa la Nhumbu. 

Friday, October 9, 2020

WANAO VIBEZA VITAMBURISHO VYA WAJASIRIAMALI WAMEKOSA UZALENDO WA NCHI

Mfanyabiashara wa Matunda wa Kata ya Ihanja Robert, akizungumzia umuhimu wa vitambulisho hivyo.
Mama Lishe Pili Juma wa Puma, akizungumzia umuhimu wa vitambulisho hivyo.
Vitunguu na viazi vitamu vikiwa sokono/


Rehem Said,  Mfanyabiashara wa Nkhunikana akizungumzia umuhimu wa vitambulisho hivyo na alimpa pongezi nyingi Rais Magufuli kwa kutoa vitambulisho hivyo.

Nyanya zikiwa sokoni.
Mfanyabiashara Martina Michael, akizungumzia vitambulisho hivyo.
Gaudensia Paul mkazi wa Kideka, akizungumzia vitambulisho hivyo.
Baraka Paul kutoka Kijiji cha Kideka alisema vitambulisho vimepanua wigo wa kufanya biashara.
Mfanyabiashara  Sebastian Mathias, akizungumzia vitambulisho hivyo.
Issa Salum, Mfanyabiashara wa Samaki, Ikungi Mjini,  akizungumzia vitambulisho hivyo.



Na Dotto Mwaibale, Ikungi


WAFANYABIASHARA wadogo katika Wilaya ya Ikungi mkoani Singida , wamesema watu wanao vibeza vitambulisho vya wajasiriamali hawana uzalendo wa nchi yetu na kuwa wanawashangaa wanaopotosha umuhimu wa vitambulisho hivyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wilayani hapa wananchi hao walisema wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John  Magufuli, kwa kuwapa vitambulisho hivyo ambavyo vimewafanya wawe huru na kuwa pungumzia gharama kubwa iliyotokana na ulipaji wa ushuru mkubwa.


Akizungumzia vitambulisho hivyo Mfanyabiashara wa Matunda wa Kata ya Ihanja aliyejitambulisha kwa jina moja la Robert alisema hivi sasa wapo huru baada ya kuanza kutumia  vitambulisho hivyo.

“Sasa hivi adha ya kufukuzana na mgambo walikuwa wakipita kudai fedha za ushuru haipo tena na zile Sh. 200 tulizo kuwa tukilipa kila siku ambapo kwa mwezi ilikuwa ni Sh.60,000 hazipo kwani tukilipa Sh. 20,000 hakuna malipo mengine kwa mwaka mzima" alisema Robert.

Mama Lishe Pili Juma wa Puma alisema tangu aanze kutumia vitambulisho hivyo amekuwa huru na amewaomba wafanyabiashara wenzake kutodanganyika na wanaodai vitambulisho hivyo kuwa havina tija.

Rehema Said Mfanyabiashara wa Nkhunikana alisema anampa pongezi nyingi Rais Magufuli kwa kutoa vitambulisho hivyo ambavyo vimewafanya waheshimike na kuwa zawadi pekee ni kumpa kura nyingi ifikapo Oktoba 28.

Mfanyabiashara Martina Michael wa Kijiji cha Nkhunikana alisema Sh.500 waliokuwa wakilipa kila siku sawa na Sh.150,000 kwa mwezi zilikuwa ni nyingi ukilinganisha na Sh.20,000 wanayoitoa sasa kwa mwezi na kuwa wanafurahia kufanya biashara.

Kwa upande wake Gaudensia Paul mkazi wa Kideka, aliomba kiasi hicho cha Sh.20,000 wanacho kitoa kipunguzwe na wale wanaobeza vitambulisho hivyo wapuuzwe na kuwa hawana uzalendo wa nchi yetu.

Baraka Paul Mfanyabiashara kutoka Kijiji cha Kideka alisema vitambulisho hivyo vimepanua wigo wa kufanya biashara kwani hivi sasa wanapeleka biashara zao hadi mikoa mingine bila ya kubugudhiwa.

Wafanyabiashara hao walimpongeza  Rais Magufuli kwa kuwaletea vitambulisho hivyo kwa Sh. 20,000 tu kwa mwaka na kuondokana na changamoto za kukimbizana na mgambo na kuwa sasa biashara zao zimeimarika zaidi na kipato chao kimeongezeka huku baadhi yao wakifanikiwa kununua ardhi, kusomesha watoto na kujenga nyumba.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Mpogolo alisema kwa mwaka jana vitambulisho 7,800 vilitolewa kwa wafanyabiashara hao na kuwa mwaka huu vimetolewa 3,600 sawa na asilimia 58 na bado vinaendelea kutolewa.

"Vitambulisho hivi vimesaidia kuongeza mapato ya wilaya yetu kwani hapo awali fedha nyingi zilizokuwa zikipatikana kutokana na ushuru ziliishia mikononi mwa wajanja." alisema Mpogolo.

Mpogolo alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Dkt.John Magufuli kwa kuwa na maono makubwa ya kuanzisha mpango huo ambao umekuwa ni mkombozi kwa wafanyabiashara ndogondogo kote nchini.

Hivi karibuni baadhi ya wanasiasa wakiwa kwenye kampeni waliibuka na kuanza kupotosha umma kuhusu vitambulisho hivyo vya wajasiriamali 'maarufu kama vya wamachinga'  kuwa haviwanufaishi na badala yake wanaibiwa, kauli ambayo Rais John Magufuli ambaye ni Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliwataka wafanyabiashara hao kuwapuuza badala yake waunge juhudi za serikali za kuwaletea maendeleo.

IRAMBA YAJIPANGA KUANZA KUZALISHA KOROSHO KWA TIJA


Mratibu wa zao la Korosho Kitaifa, Dkt. Geradina Mzena akisisitiza faida za kulima zao hilo alipokutana na wakulima na maafisa ugani wa Wilaya ya Iramba jana, kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya hiyo Emmanuel Luhahula (wa pili kushoto) kufungua mafunzo ya Kilimo Bora cha Korosho, wengine pichani ni DAICO Iramba, Marietha Kasongo na DAICO Mkalama, Seleman Musunga.

Wakulima na Maafisa Ugani wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa.
Mafunzo ya Agronomia ya Korosho yakiendelea.
Wakulima na Maafisa Ugani wakishiriki mafunzo hayo kwa vitendo.

Mafunzo yakiendelea.

Mafunzo ya namna bora ya kupogolea mkorosho.

Mafunzo yakiendelea.
-Afisa Kilimo Wilaya ya Iramba, Marietha Kasongo (aliyechuchumaa) akiweka alama kuhakikisha mstari .

Mafunzo yakiendelea.

Mafunzo ya namna bora ya kupogolea mkorosho.

Thursday, October 8, 2020

Benki ya I&M yasheherekea wiki ya huduma kwa wateja

 

 Wafanyakazi wa I&M Benki wakisherehekea pamoja na wateja maadhimisho ya wiki ya wateja huku wakiwa katika mavazi ya utamaduni ambapo siku ya Jumatano oktoba 7 ndio maadhimisho rasmi ya utamaduni wa Afrika.


Wafanyakazi wa I&M Benki wakisherehekea pamoja na wateja maadhimisho ya wiki ya wateja huku wakiwa katika mavazi ya utamaduni ambapo siku ya Jumatano oktoba 7 ndio maadhimisho rasmi ya utamaduni wa Afrika.
Wafanyakazi wa I&M Benki wakisherehekea pamoja na wateja maadhimisho ya wiki ya wateja huku wakiwa katika mavazi ya utamaduni ambapo siku ya Jumatano oktoba 7 ndio maadhimisho rasmi ya utamaduni wa Afrika.

Wafanyakazi wakiwa pamoja na wateja wa benki ya I&M siku ya Jumaatano ambapo benki hiyo iliadhimisha kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kukata keki na wateja wao waliotembelea benki siku hiyo. Licha ya kukata keki pia benki ilichukua fursa ya kutembelea wateja wa kila ngazi, kutoa zawadi kama shukrani kwa wateja pamoja na kuvaa mavazi ya aina mbalimbali kuonyesha utofauti na furaha ya kuhudumia 

Wafanyakazi wa Benki ya I&M wakitoa zawadi kwa mteja wa benki hiyo kama moja ya njia ya kuwashukuru wateja kwa kuendelea kuitumia na kuiamini Benki ya I&M kwa huduma bora inazotoa kwa wateja wake na jamii kwa ujumla.


Wafanyakazi wa I&M Benki wakisherehekea pamoja na wateja maadhimisho ya wiki ya wateja huku wakiwa katika mavazi ya utamaduni ambapo siku ya Jumatano oktoba 7 ndio maadhimisho rasmi ya utamaduni wa Afrika.
Wafanyakazi wa Benki ya I&M wakiwa katika mavazi ya udaktari wakionyesha kuwapatia wateja suluhisho la changamoto za kifedha kwa kuwapatia wateja huduma bora kibenki ili kufanikisha shughuli za kibiashara na uchumi. Haya yote yamefanyika katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 

Wafanyakazi wa Benki ya I&M wakiwa katika mavazi ya udaktari wakionyesha kuwapatia wateja suluhisho la changamoto za kifedha kwa kuwapatia wateja huduma bora za kibenki ili kufanikisha shughuli za kibiashara na uchumi. Haya yote yamefanyika katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 
Mfanyakazi wa Benki ya I&M katika mavazi ya udaktari akiwa anatoa huduma kwa mmoja kati ya wateja waliotembelea tawi la benki hiyo katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja
 

                                                      ...........................................

Dar es Salaam

BENKI ya I&M Tanzania imeadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, kwa kutambua mchango muhimu unaotolewa na fanyakazi wake katika kuwahudumia wateja wao kwa viwango vya juu na kuhakikisha kuwa wanakuwa wenye furaha wakati wote.

Hafla hiyo ilifanyika leo maktaba square  jijini Dar es Salaam katika makao makuu ya benki hiyo, ikiambatana na shughuli mbalimbali kwa wateja kama ishara ya shukrani kwa wateja wanaothaminiwa na pia wafanyakazi wake ambao wamekuwa wakitekeleza jukumu muhimu la kutoa huduma bora kwa wateja wakati wote.

Miongoni mwa shughuli za kusherehesha hafla hiyo na wiki ya huduma kwa wateja zilizofanywa na benki hiyo ni pamoja na Maofisa wa juu na waandamizi wa benki hiyo akiwamo Afisa Mtendaji  Mkuu, walichukua jukumu la kuhudumia wateja katika matawi mbalimbali kwa siku ya leo.

Sheherehe hiyo ya wiki nzima ni matokeo ya kujitolea kwa benki hiyo ya I&M katika kuongeza ushiriki wa wafanyakazi katika kuunga mkono kaulimbiu ya mwaka huu ya siku hiyo inayosema kuwa, ‘Timu ya ndoto’.

Mbali na ushiriki wa watendaji wakuu, maafisa waandamizi katika kufanya jukumu la huduma kwa wateja, pia wafanyakazi wote wa benki hiyo walipokea barua binafsi za shukurani kwa bidii yao na kujitolea kwao katika kuleta matokeo chanya na furaha kwa wateja katika benki hiyo.

Mkuu wa Mauzo ya rejareja wa benki hiyo, Lilian Mtali alisema katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja wanataka onyesha thamani ya watoa huduma kwa wateja.

“Sisi benki ya I&M tunataka kutumia wiki hii ya huduma kwa wateja kuhakikisha kuwa tunawaonyesha thamani na ukarimu wateja wetu,lakini pia kuunga mkono na kutambua kazi nzuri na kubwa inayofanywa na maafisa wa huduma kwa wateja kama dawati namba moja ambalo ni nembo na kilelezo cha huduma bora za benki.

“Kwani sote tunatambua kuwa dawati la huduma kwa wateja ndilo limebeba sura na kilelezo cha huduma bora zinazotolewa na benki, wamekuwa wakaifanyakazi kwa bidi kwani hata pale wateja wanapokuwa na jazba, wao wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha kuwa wanakamilisha mahitaji yao na kuwaacha wakiwa na furaha jambo ambalo ni kipaumbele cha benki,” alisema Lilian.

Wiki ya Huduma kwa Wateja ni maadhimisho ya umuhimu wa huduma kwa wateja na ya watu ambao wanahudumia na kusaidia wateja kila siku. 

Hafla hiyo huadhimishwa kila mwaka wakati wa wiki ya kwanza ya Oktoba na wafanyabiashara wote na mashirika yanayolenga huduma kote ulimwenguni, ambayo hutambua umuhimu wa kutoa huduma bora kwa wateja.